• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • China kufadhili utafiti zaidi juu ya Afrika katika juhudi za kuimarisha ushirikiano 2017-10-11

  Serikali ya China sasa inasema itaingiza rasilimali na fedha zaidi katika miradi ya utafiti ili kuelewa mahitaji ya wananchi barani Afrika. Utawala huo wenye makao yake jijini Beijing unasema kuwa ufahamu mwafaka kuhusu bara hilo lilatoa nafasi nzuri kwa taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Asia kutoa mchango wake na msaada dhabiti katika jitihada zake za kusaidia hali ya maisha katika Afrika.

  • China yaadhimisha tamasha la mbalamwezi 2017-10-07

  China inafahamika kwa uaminifu wake kwa mila za tangu jadi. Taifa hilo kubwa zaidi barani Asia kwa kweli imesifika kwa utajiri wa tamaduni. Mila hizi kwa njia nyingi zimezidi zile za nchi nyingine. Sifa mojawapo ya kipekee ya watu wa China, ni kujitolea kwao kuhadhimisha sherehe za mabadiliko ya hali ya hewa. Tamaduni hizi zimekuzwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

  • BRICS yaelekeza macho yake kwa mataifa yanayoendelea Afrika 2017-09-04

  Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayoshiriki mkutano wa BRICS unaoendelea Mkoani Fujian, eneo la Xiamen nchini China. Nchi hiyo kutoka Afrika Mashariki ilialikwa kushiriki katika mkutano huo kwa mara ya kwanza kabisa huku ikidhihirika kwamba kongamano hilo linabadili mwelekeo na kutaka kuvutia mataifa yanayoendelea barani Afrika.

  • Hifadhi ya Summer Palace, kivutio cha Utamaduni na Utalii  2017-07-24

  Hifadhi ya Summer Palace mjini Beijing inajumuisha ziwa kubwa bandia, kisiwa na kilima vilivyotengenezwa na binadamu.

  • Taasisi zaungana kuzuia kuenea kwa maradhi ya Ukimwi Afrika 2017-07-14
  Juhudi za kimataifa za kuzuia maambukizi na kuenea kwa maradhi ya ukimwi unashika kasi. Jicho la dunia sasa linaangazia juhudi za kuwashawishi watu wengi iwezekanavyo ili kujua hali zao.
  • China inakuza sekta ya nishati mbadala kupigana na uchafuzi wa mazingira 2017-07-12

  China inazidi kupunguza utegemezi wake juu ya makaa ya mawe kama nguvu ya nishati, badala yake inaendeleza miradi ya vyanzo vya umeme mbadala. Ujenzi wa mitambo ya upepo na umeme wa jua kwa sasa inafanyika katika karibu mikoa yote ya taifa hilo ya mashariki ya mbali. Utegemezi wa nishati inayotokana na makaa ya mawe imetajwa kama moja ya sababu kuu ya uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi kama inavyoshuhudia nchini China. Viwanda vya uzalishaji wa umeme kupitia makaa ya mawe kwa sasa vinapunguzwa kwa kasi kubwa.

  • Inner Mongolia yapanua biashara na Afrika huku China ikitafuta mahusiano zaidi 2017-07-03

  Jimbo la Mongolia ya ndani ipo kaskazini mashariki mwa China katika mpaka wa Mongolia na Urusi. Si mengi yametangazwa kuhusu mkoa huu lakini umesajili maendeleo makubwa tangu kiongozi Deng Xiaoping kuweka mageuzi ya kiuchumi China mwaka 1978.

  • Mafanikio na uzoefu wa China katika kupunguza umaskini 2017-06-20

  "LAZIMA tuondoe umaskini ambao upo katika akili zetu kabla ya kuuondoa ndani ya maeneo tunaotawala, kabla ya kusaidia raia na taifa kutoka kwenye minyororo ya umaskini na kuanza barabara ya mafanikio." Haya ni maneno ya kiongozi wa China Xi Jinping katika kitabu chake maarufu "Kuondokana na Umaskini." Kitabu hiki kinatoa maelezo ya kina kuhusu jinsi yeye alifanikiwa kukabiliana na kushinda vita dhidi ya umaskini kama kiongozi katika Ningde, moja ya sehemu ya Mkoa wa Fujian iliyokuwa na umaskini zaidi katika miaka ya 1980.

  • Maendeleo na ujenzi wa kihistoria China baada ya tetemeko la ardhi 2017-06-16

  JE, utafanya nini iwapo tetemeko la ardhi wenye ukubwa wa 8.0 kwenye Richter utazuka na kufanya uharibifu mkubwa na kuleta pigo mijini na vijijini? Mbaya zaidi, unaweza kufanya nini wakati vitetemeko zaidi vinaendelea kwa maeneo yaliyokaribu kwa miezi kadhaa baada ya tetemeko hilo kuu na kusababisha majeruhi zaidi na uharibifu?

  • China yasema mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja ni njia rahisi ya kusaidia nchi wanachama 2017-06-15
  Beijing imesisitiza kuwa mpango wa kiuchumi wa karne ya 21 wa Ukanda Mmoja na Njia Moja ni mfumo bora mno ambayo China itatumia kutoa msaada wake kwa nchi zinazoendelea ambazo zimeamua kushirikiana na taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Asia.
  • Kenya kutafuta fursa ya biashara zaidi na China kupitia mpango wa Mkanda Mmoja Njia Moja 2017-06-09
  Nairobi imetangaza kuwa itaanza kuwinda nafasi za biashara zaidi na Beijing kupitia mpango wa kiuchumi uliozinduliwa karibuni wa Mkanda Mmoja Njia Moja. Waziri wa biashara na viwanda wa Kenya Adan Mohamed anasema mfumo huu unaofuata barabara ya kale ya Silk ambao una mizizi yake China utahusisha matrilioni ya dola ya uwekezaji na miradi mikubwa muhimu katika kila moja ya nchi husika.
  • Makampuni kutoka China yaahidi fursa zaidi Afrika kupitia mfumo wa Mkanda Mmoja Njia Moja 2017-06-06
  Wiki tatu tu baada ya kumalizika kwa kongamano la kwanza kabisa kuhusu Mkanda Mmoja Njia Moja mjini Beijing, makampuni makubwa ya Kichina yameelezea utayari wao wa kuongeza uwekezaji katika nchi ambazo hadi sasa yamejiunga katika mpango huo.
  • Wachina Waadhimisha tamasha la Duanwu 2017-05-31

  Wachina wanaadhimisha sherehe ya siku tatu kwa kuandaa tamasha la Duanwu maarufu kama Dragon Boat Festival. Tamasha hili linaandaliwa kukumbuka mshairi mkubwa tajika ambaye alipigana dhidi ya mateso ya raia maelfu ya miaka iliyopita.

  • Mchango wa dola milioni 20 kutoka China wa Uhifadhi Mazingira na Wanyamapori Afrika 2017-05-26

  Serikali ya China imedhihirisha nia yake kubwa ya kuhifadhi mazingira na wanyamapori kwa kuongeza fedha kwa sekta hii Afrika kwa dola milioni 20 za Marekani. Toleo hili ni mara mbili ya kiasi cha fedha zilizoahidiwa mwaka wa 2014 na nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi barani Asia.

  • Waziri wa Usafiri Kenya asema matunda ya Mkanda Mmoja Njia Moja tayari yanaonekana 2017-05-22

  Mwezi Mei, duniani yote ilielekeza macho yake kuelekea Mjini Beijing kwa sababu ya tukio kubwa ya kihistoria iliyokuwa ikiendelea katika mji huo mkuu wa China. Serikali mbalimbali na mashirika ya kimataifa yalikuwa hapa kushuhudia kuzaliwa kwa mpango wa maendeleo wa Mkanda Mmoja Njia Moja.

  • Afrika yajiunga na China wakati dunia umeweka uhai ndoto ya Mkanda Mmoja Njia Moja 2017-05-19

  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ni miongoni mwa viongozi 29 wa nchi zilizokongamana Beijing kupumulia uhai pendekezo la Mkanda Mmoja Njia Moja.

  • Afrika itafanya vyema kuukumbatia pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja 2017-05-12

  Rais wa China Xi Jinping alipendekeza na kukuza pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja (One Belt One Road) miaka 3 iliyopita, akiutangaza kama kielelezo mpya ya ushirikiano ambayo itachochea maendeleo ya pamoja na mafanikio. Dhahiri, hii imekuwa kipengele muhimu zaidi ya sera za kigeni ya China. Wengi wanautambua kama mchango wa China kwa utaratibu mpya wa dunia.

  • Ushawishi wa Kiuchumi unaonawiri wa Mkoa wa Guangdong kwa Mataifa ya Afrika 2017-05-05

  China imebarikiwa na kanda maalum ambayo imeiweka kwenye kilele cha uchumi duniani. Lakini jimbo la Guangdong kwa wepesi yaonekana kama kichocheo kikuu cha ushawishi wake.

  • Huawei: Utafiti na Ubora ni nguzo yetu 2017-05-04

  Katika mfululizo wa mipango ya 13 ya China ndani ya miaka mitano (2016-2020), serikali ya China imeweka bayana kwamba inategemea uvumbuzi kuongeza ukuaji wake. Kwa mujibu wa utawala huo wenye makao makuu Beijing, hii itakuza nguvu mpya katika utekelezaji wake wa mikakati ya maendeleo yanayotokana na msukumo wa uvumbuzi.

  • Droni za Kilimo kutoka China kunufaisha wakulima 2017-04-26

  Sekta ya kilimo inaendelea kupitia mabadiliko mengi. Kuongezeka kwa idadi ya watu duniani inatoa wito wa kuongeza uzalishaji wa chakula. Hata hivyo ahadi hii inaandamwa na vikwazo chungu nzima.

  • Mashirika ya kijamii yaliyojitolea kusaidia Waafrika Kuishi China 2017-04-24

  Ni jinsi gani Waafrika ambao husafiri nje ya nchi katika kutafuta malisho mazuri hufanikiwa kuishi kati ya watu wageni kutoka asili mbalimbali pamoja na tamaduni tofauti?

  • Beijing yatetea ubora wa bidhaa Kutoka China 2017-04-20

  Ubora wa bidhaa zinazotengenezwa kutoka China na kusafirishwa sehemu nyingi duniani, daima zimepokelewa kwa miitikio tofauti. Kwa mara nyingi bidhaa hizo zimedaiwa kuwa na ubora wa hali duni. Afrika kwa upande mwingine imetajwa kuwa mahala ambapo bidhaa hizo zinarundikwa.

  • China yakiri changamoto nyingi katika uwekezaji wake kwenye baadhi ya mataifa ya Afrika 2017-04-14

  Beijing imetangaza kuwa imeboresha ushirikiano wake na Afrika kufikia kiwango cha kina kimkakati. Hii hoja ya karibuni kulingana na maafisa wakuu wa serikali ya China itaharakisha utekelezaji wa malengo muhimu yaliyoandaliwa hasa kuwezesha mataifa ya Africa kuwa bora kiuchumi na kujitegemea.

  • Wachina wakaribisha majira ya machipuko kwa maadhimisho 2017-04-04

  Mwanzo wa Aprili inadhihirisha mwisho wa majira ya baridi, lakini la muhimu zaidi ni kwamba inatoa fursa kwa msimu mpya wa majira ya machipuko, ambalo ni tukio la kihistoria kwa idadi kubwa ya mataifa duniani.

  • Kampuni Maarufu ya uchapishaji ya China ya Phoenix yatafuta washirika Afrika 2017-03-31

  Kampuni maarufu ya uchapishaji kutoka China sasa inanuia kupanua shughuli zake barani Afrika kuanzia mwaka huu. Kampuni hiyo ya Phoenix Publishing Media Group imetangaza kuwa inatafuta makampuni kutoka bara hilo ili kushirikiana katika sekta ya uchapishaji.

  • China yataka mataifa ya Africa yatoe habari zaidi kuhusu nafasi za uwekezaji 2017-03-30

  Serikali ya China imefichua kuwa iko tayari kuwekeza zaidi katika bara la Africa. Wizara ya biashara ya nchi hiyo hata hivyo inasema ni wajibu wa nchi za Afrika kutoa taarifa za kutosha kuhusu maeneo ya uwekezaji ambayo usimamizi wa Beijing utaingiza rasilimali zaidi.

  • Maofisa wa Kenya na China kukamilisha makubaliano ya ujenzi wa barabara mpya 2017-03-29
  Kikosi cha maafisa wa serikali ya Kenya wako China kukamilisha mikataba kuhusiana na sheheni ya mwisho ya makocha ya abiria na mizigo zitakazotumika karibuni mara tu reli ya kisasa inayojengwa kutoka Mombasa kuelekea Naivasha itakapozinduliwa
  • Kuondoa mkanganyo wa tiba ya jadi ya kichina 2017-03-27
  Sehemu kubwa ya maisha ya watu wa China yakini ni ya kipekee na tofauti ikilinganishwa na mataifa mengine duniani. Mfumo wa afya katika taifa la China ni mojawapo. Tofauti na aina nyingine za dawa za jadi ambazo kwa kiasi kikubwa yaonekana kutokomea, tiba asilia ya Kichina maarufu TCM inaendelea kunawiri.
  • Makampuni ya biashara ya nyumba ya China yapanua biashara zao Afrika 2017-03-24
  Kampuni ya China Jiangsu International Economic and Cooperation Group, CJI, sasa inataka kupanua shughuli zake ndani ya bara la Afrika katika sekta ya mali isiyohamishika.
  • China inavyothamini utamaduni wa jadi wa okestra na kuutumia kuleta umoja 2017-03-22
  Ni utamadauni wa kufana, ambao umekuwepo kwa vizazi vingi na bado ni maarufu miongoni mwa watu wa China. Utamaduni wa okestra ya jadi kwa kichina huheshimiwa na wengi, vijana kwa wazee pamoja. Lakini kinachofanya uwe wa kipekee, ni jinsi ulivyo na mvuto kwa watu. Mengi yamesemwa kuhusu utamaduni huu, lakini ukibahatika kujionea mwenyewe maonyesho yake, ndio unaweza kuelewa zaidi.
  1  2  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako