Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
v Mtunzi wa muziki wa kabila la Wa-mongolia Bwana Yong Rubu 2007/05/23
Bwana Yong Rubu alizaliwa kwenye mbuga mzuri wa Kerqin wa mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani, ambako ni maskani maarufu ya nyimbo na ngoma ya kabila la wamongolia. Kutokana na kuathiriwa na muziki wa huko, Bwana Yong Rubu alikuwa anapenda sana muziki tangu utotoni mwake, alipokuwa na umri wa miaka 14 alijiunga na jeshi na kuwa askari wa michezo ya sanaa
v Moja kati ya vipindi 24 katika kalenda ya kilimo ya China, "Siku ya Kuanza kwa Majira ya Joto"  2007/05/14
Kugawa vipindi 24 katika kalenda ya kilimo ya China ni busara za Wachina wa kale kutokana na uzoefu wao wa muda mrefu kuhusu hali ya hewa na unajimu, vipindi hivyo vinasaidia sana kwenye shughuli za kilimo. Kwa mujibu wa historia, mapema mwaka 104 K.K. watu wa China walikuwa wamepata vipindi hivyo 24.
v Vitu vya sanaa za mikono vya makabila madogo madogo mkoani Qinghai  2007/05/09
Katika mkoa wa Qinghai, kaskazini magharibi mwa China, wanaishi watu wa makabila mengi yakiwemo Wa-han, Wa-tibet, Wa-hui, Wa-tu, Wa-sala na Wa-mongolia. Watu wa makabila hayo wanapojitahidi kujiendeleza kiuchumi, pia wamevumbua utamaduni wenye umaalum wa kikabila. Hadi baadhi ya ustadi wa kutengeneza vitu vya sanaa kwa mkono bado unaenea.
v Beijing yaimarisha hifadhi ya majengo ya kale kuchangia mazingira ya "Olimpiki ya utamaduni" 2007/04/30
Kutokana na michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 kukaribia siku baada ya siku, maandalizi yamekuwa yakiendelea haraka ikiwa ni pamoja na juhudi za kuimarisha hifadhi ya majengo ya kale mjini Beijing. Katika miaka ya hivi karibuni juhudi hizo zimekuwa kubwa kadiri miaka inavyozidi kwenda.
v China yaimarisha hifadhi ya vitabu vya kale 2007/04/16
Hivi karibuni serikali ya China ilitangaza rasmi kuanzisha mradi wa miaka mitano wa kuchunguza na kuweka orodha ya vitabu vya kale kote nchini ili kupata idadi halisi, kupima thamani ya vitabu hivyo na kufahamu mazingira ya kuhifadhi vitabu hivyo, kuchapisha orodha ya vitabu hivyo na kuandaa wataalamu wa kukarabati vitabu hivyo.
v Mwigizaji mashuhuri wa tamthilia ya kuchekesha Huang Hong 2007/04/02
Mwigizaji wa tamthilia ya kuchekesha Bw. Huang Hong anajulikana sana kwa sababu ya kuzingatia sana haki na maslahi ya wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini, na anasifiwa kuwa ni "msemaji wa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini".
v Kongamano la nne kuhusu uzalishaji kwenye sekta ya utamaduni wamalizika  2007/03/20

Uzaishaji katika sekta ya utamaduni umepata maendeleo ya haraka tokea mwaka 2000, na kutokana na sera nzuri za serikali makampuni husika yamestawi haraka. Mchango wa uzalishaji katika sekta ya utamaduni kwa pato la taifa unaongezeka.

v Mwanamuziki Tan Dun 2007/03/12
Bw. Tan Dun ni mwanamuziki mashuhuri wa China. Muziki alioutunga kwa ajili ya filamu ya "Mahali Penye Watu Hodari" ulipata tuzo ya Oscar mwaka 2001, ambayo ni mwanamuziki wa kwanza wa China kupata tuzo hiyo. Bw. Tan Dun anazingatia sana kuunganisha mtindo wa Kichina na wa Kimagharibi na kuufanya muziki wake kuwa wa aina mpya, na unaopokelewa na watu wa magharibi kwa furaha.
v Watibet wazungumzia filamu inayoonesha hali halisi ya zamani ya Tibet  2007/02/26
Hivi karibuni filamu inayoonesha hali halisi ya zamani ya Tibet imekuwa ikioneshwa mjini Beijing. Filamu hiyo inaonesha hali ilivyokuwa kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kabla ya mkoa wa Tibet kufanyiwa mageuzi ya kidemokrasia mwaka 1959. Filamu hiyo ilisababisha hisia kali miongoni mwa Watibet
v Sikukuu ya Spring ya China  2007/02/19
Tarehe 18 Februari ni sikukuu ya Spring ya China yaani sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China. Siku hiyo ni sikukuu kubwa kabisa kwa Wachina katika mwaka mzima ambayo ni kama siku ya Krismasi katika nchi za Magharibi
v Filamu za kibiashara na za kisanaa zote zaongoza katika soko la filamu nchini China 2007/02/12
Filamu ya "Askari Wenye Deraya Kote Mjini" iliyopigwa chini ya uelekezaji wa Zhang Yimou, mwongoza filamu maarufu wa China, imepata mapato makubwa katika mwezi mmoja tokea ianze kuoneshwa nchini China na nchi za nje, na filamu nyingine za kuonesha maisha halisi ya wakazi wa China ingawa bado hazijapata mafanikio kama filamu ya "Deraya" lakini pia zinasifiwa sana na watazamaji. Filamu za kibiashara na za kisanaa zote zimekuwa zinaongoza katika soko la filamu nchini China.
v Mwigizaji mashuhuri wa filamu Bi. Gong Li 2007/01/29
Katika siku za karibuni filamu inayoitwa "Askari Wenye Deraya Kote Mjini" ambayo iliongozwa na Zhang Yimou na kuigizwa na Bi. Gong Li inaoneshwa katika majumba yote ya filamu mjini Beijing.
v Msomi mashuhuri wa China Yu Qiuyu 2007/01/15
Bw. Yu Qiuyu aliwahi kuwa kijana kabisa kati ya maprofesa wa sanaa na sayansi za jamii nchini China, aliwahi kuwa mkuu wa chuo kikuu na baadaye alikuwa mwandishi anayejitegemea. Amewahi kutembelea sehemu nyingi zenye kumbukumbu za kihistoria na kitabu alichoandika mkusanyiko wa makala zinazoeleza hisia zake kuhusu matembezi yake ni kitabu kinachonunuliwa kwa wingi kabisa kati ya vitabu vinavyosomwa sana nchini China
v Mtu mashuhuri katika historia ya China, Lin Zexu  2007/01/01
Katika historia ya karibu ya China, Lin Zexu ni shujaa wa taifa la China anayefahamika kwa Wachina wengi, na hadithi yake ya kuteketeza kasumba ni moja ya makala zake zilizoko katika kitabu cha historia ya China katika shule za msingi na sekondari.
v Mtaalamu wa kuhifadhi Ukuta Mkuu nchini China Bw. Dong Yaohui 2006/12/25
Tangu tarehe mosi Desemba Sheria ya Kuhifadhi Ukuta Mkuu ilipoanza kutekelezwa rasmi, vitendo vyote vya kuchukua udongo, matofali au mawe, kupanda mimea, kuendesha vyombo vya usafiri kwenye Ukuta Mkuu vimepigwa marufuku. Sheria hiyo ilimfanya Bw. Dong Yaohui aliyejishughulisha na hifadhi ya Ukuta Mkuu kwa zaidi ya miaka 20 aone faraja kubwa.
1 2 3 4 5 6 7 8 9