• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • China yaipa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) magari 12 2019-11-13

  CHINA imeahidi kuipa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) magari 12 yenye thamani ya dola za Marekani US$400,000 ili kutumika katika programu mbalimbali za kuwajengea jamii uwezo.

  • China yawapa wanakijiji mbegu kompyuta 2019-11-11

  BALOZI wa China nchini Tanzania Bibi Wang Ke amekabidhi msaada wa mbegu za Alizeti, Choroko na Mahindi zenye uzito wa kilo 4800 ambazo zitagaiwa kwa wananchi wa kijiji Mhenda kilicho jirani na Hifadhi ya Taifa Mikumi mkoani Morogoro.

  • Tanzania inathamini mchango wa China-Balozi Mahiga 2019-10-24

  WAZIRI wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga amesema Tanzania itaendelea kuthamini mchango unaotolewa na Jamhuri ya Watu wa China huku akisisitiza kuwa masuala yanayoendelea hivi sasa ambapo Hong Kong inataka kujitenga, yanapaswa kushughulikiwa na China yenyewe.

  • Ujumbe toka jimbo la Hebei China kuwekeza mkoani Pwani 2019-10-24

  UJUMBE kutoka China ukishirikisha wawekezaji na maofisa wa serikali uMEwasili mkoani Pwani kusaka maeneo ya uwekezaji huku wakitembelea maonesho ya viwanda yanayoendelea mkoani hapa.

  • China Academy of Building Research yaanza upembuzi yakinifu mradi wa upanuzi Taasisi ya Moyo ya JKCI Mloganzila 2019-09-17

  UJUMBE wa wawakilishi kutoka China Academy of Building Research wamefika nchini kwa ajili ya kupata taarifa zinazohusiana na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa upanuzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), awamu ya pili katika eneo la Mloganzila Jijini Dar es Salaam.

  • Jeshi China lamkabidhi Rais Magufuli magari 40 ya JWTZ 2019-09-16

  JESHI la Ukombozi wa watu wa China (PLA) limekabidhi Jeshi la Ulinzi la wananachi wa Tanzania (JWTZ) magari 40.

  • UDSM yajivunia uhusiano Tanzania na China kuleta manufaa ya kielimu 2019-09-16

  CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimejivunia manufaa ya kielimu waliyopata kutokana na wahadhili na wanafunzi wake kwenda kusoma nchini China katika fani mblimbali.

  • China yatoa mafunzo ya Upishi na ukarimu Zanzibar 2019-09-16
  • Kampuni ya Kimataifa ya Hongwei toka China yaajiri vijana 514 kuchakata mazao ya misitu Mufindi 2019-08-30
  • Madaktari bingwa waliosoma China Wafanya kampeni ya  upimaji magonjwa yasiyoambukiza Kisarawe 2019-08-30
  WAKAZI wa Kisarawe mkoani Pwani, takribani 1,000 watanufaika na kambi ya kwanza ya kampeni ya uchunguzi na matibabu dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza, inayotolewa na madaktari bingwa wa Jumuiya ya Watanzania Waliosoma China (DCAT).
  Mwenyekiti wa DCAT, Dk. Liggyle Vumilia anasema katika siku hizo tatu, watachunguza afya watu 600 hadi 1,000 wa magonjwa ya saratani, moyo, kisukari na mengineyo.
  • Vijana 20 Tanzania wajiunga na sanaa ya Wing Chun toka China 2019-08-30

  VIJANA 20 kutoka eneo la Murieti jijini Arusha wamejiunga katika Sanaa mpya ya mapigano iliyoanzishwa ijulikanayo Kama 'Wing Chun'.

  Mwanzilishi na mkufunzi was Sanaa hiyo Rashid Said amesema kuwa ni mchezo mpya umeingia kwa Kasi nchini kutokana na vijana kuuelewa haraka.

  Alisema asili ya Wing Chun ni nchini China na unaendelea kusambaa maeneo mbalimbali ni miongoni mwa michezo ambayo inafundishwa kihalali na umesashasajiliwa.

  • China yaweka rekodi kwa kutokuwa na maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa miaka mitatu 2019-08-23

  China, nchi inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu duniani, ikiwa na watu zaidi ya bilioni 1.4, huku ikiwa nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani, imefanikiwa kwa miaka mitatu kuhakikisha hakuna maambukizi ya malaria nchini humo, na itafikia malengo ya milenia ya kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo hadi kufikia mwaka 2020.

  • China yaongeza ufadhili kwa wanafunzi wa fani mbalimbali Tanzania kufikia 259 kwa mwaka 2019-08-22

  UFADHILI kutoka nchini China kwa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma fani mbalimbali nchini humo imeongezeka mara mbili zaidi mwaka huu kutoka wanafunzi 120 mpaka 259 mwaka jana .

  • Balozi wa China nchini Tanzania ataka taasisi za Confucius kufundisha Kiswahili 2019-08-22

  LUGHA ni muhimu katika mawasiliano ikiwemo kubadilishana tamaduni za aina mbalimbali,biashara,utalii na muingiliano wa watu katika dunia hii ambayo kwa sasa imekuwa kama kijiji kwa mtu wa eneo moja kwenda kuishi au kufanya shughuli mbalimbali katika eneo lingine.

  • China yatoa samani za Ofisini kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) huku Balozi wake akipongeza serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji 2019-08-19

  BALOZI wa China nchini Wang Ke amepongeza jitihada za serikali katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kueleza kuwa mwaka huu mambo mengi yamefanyiwa kazi hivyo anatarajia wawekezaji zaidi nchini hususan kutoka nchini China.

  • Vigae "Tiles" za Tanzania zinazozalishwa na mwekezaji toka China zakamata soko Afrika Mashariki 2019-08-16

  KIWANDA cha kutengeneza vigae "Tiles" nchini cha Goodwill Tanzania Ceramic Limited kilichopo katika Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani,kinachomilikiwa na mwekezaji toka China kimeshika soko katika ukanda wa Afrika Mashariki.

  • China yaipa Tanzania Milioni 217 kusaidia shughuli za kiofisi wakati wa mkutano wa SADC 2019-08-16

  CHINA imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ofisini vyenye thamani ya zaidi ya milioni 217 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za ofisini wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa afrika (SADC).

  • Zanzibar yanunua meli mpya ya Mafuta iliyowasili kutoka Shanghai China 2019-08-09

  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetimiza ahadi yake kwa wananchi wake ya kununua meli mpya ya mafuta MT Mkombozi II, baada ya meli hiyo kuwasili katika Bandari ya Zanzibar ikitokea Shanghai nchini China.

  • Kampuni ya CHICO kutoka China yasaini mkataba ujenzi barabara Tanga-Pangani 2019-08-05

  KAMPUNI ya China Henan International Company Limited (CHICO) imesaini mkataba wa ujenzi sehemu ya barabara ya Tanga- Pangani yenye urefu wa kilometa 50.

  • Tanzania yapokea watalii 120 toka Hong Kong, China 2019-08-01

  SEKTA ya utalii nchini Tanzania inazidi kukua baada ya kupokea watalii 120 kutoka Hong kong, China kuwasili nchini kwa ajili ya kutembelea hifadhi mbalimbali za Taifa na maeneo mbalimbali yenye vivutio vya utalii nchini.

  • Chama cha Waajiri Tanzania watoa elimu Sheria za Kazi na Ajira kwa Wafanyabiashara toka China 2019-07-30

  Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) wamefanya mkutano na wafanyabiashara toka China kwa lengo la kujadili fursa za uwekezaji nchini pamoja na sheria ya kazi na ajira pamoja na kujadili changamoto za kibiashara wanazokutana katika uwekezaji wao.

  • Wafanyabiashara Tanzania kufanya ziara ya mafunzo China 2019-07-29

  HUKU uhusiano wa kibishara na uwekezaji ukizidi kukukua na kuimarika kati ya Tanzania na China, wafanyabiashara kutoka Mkoani Mtwara, kusini mwa nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki, wanatarajia kutembelea China hivi karibuni ili kujifunza fursa mbalimbali za kibiashara zikiwemo za uwekezaji wa viwanda ili kuendana na kasi ya Tanzania ya viwanda.

  • China yawezesha Tanzania kuwa ya kwanza Afrika Mashariki kutibu moyo unaokwenda mbio kwa kuipatia mashine yenye thamani ya Shilingi milioni 500 2019-07-29

  CHINA imewezesha Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kutibu wagonjwa wa moyo ambao unakwenda mbio baada ya mfumo wa umeme wa moyo kuharibika, tatizo ambalo wagonjwa walikua wakipelekwa nje kupata matibabu .

  • Balozi mdogo wa China Zanzibar asema Misaada ya China Zanzibar inalenga kuimarisha uchumi na huduma za jamii kwa wananchi 2019-07-29

  SERIKALI ya Jamhuri ya Watu wa China imesema misaada yake inayotoa inalenga katika kuimarisha uchumi na huduma za jamii kwa wananchi wa Zanzibar.

  • Tanzania yaanza kutumia mbinu ya kutokomeza Malaria iliyotumika China kutokomeza ugonjwa huo mikoa ya Kusini 2019-07-27
  TANZANIA imeanza kutekeleza mradi wa kutokomeza malaria kwenye mikoa ya kusini kwa kutumia mbinu iliyotumika kuutokomeza nchini China.
  • Rais Magufuli ahaidi kuboresha utendaji kazi wa Reli ya kihistoria Ushirikiano Afrika na China ya TAZARA 2019-07-27
  RAIS John Magufuli amesema Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) halitakufa kwa sababu wazo la shirika hilo ni la kihistoria baina ya nchi husika.
  • Kampuni ya China yasaini mkataba kuongeza watalii na uwekezaji Zanzibar 2019-07-23

  WIZARA ya habari Utalii na Mambo ya kale imetiliana saini makubaliano ya kuimarisha uhusiano katika sekta ya utalii na kampuni ya kimataifa ya touchroad kutoka jimbo la Zhejiang ya China yenye lengo la kuongeza idadi ya wa watalii wanaokuja zanzibar kutoka nchi hiyo.

  • Wafanyabiashara 25, kutoka Kampuni 15 za Jimbo la Zhejiang China kufanya ziara ya siku tatu kusaka fursa za biashara Tanzania 2019-07-22

  UWEKEZAJI wa China kwa anzania mwaka jana umefikia dola za Marekani Bilioni saba na kufanya nchi hiyo kuendelea kuongoza kwa uwekezaji nchini kwa kuwa na kampuni 200 zilizowekeza na kutoa huduma nchini hadi sasa,ambazo wawakilishi wake walipata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo.

  • Xinhua, TSN wakubaliana kudumisha ushirikiano na kukuza Kiswahili 2019-07-22

  USHIRIKIANO baina ya Vyombo vya habari China na Tanzania unazidi kushika kasi baada ya Shirika la Habari la China, Xinhua na Kampuni ya Magazeti ya Serikali Daily News, Habari Leo (TSN), zimezidi kudumisha ushirikano ikiwa ni pamoja na kuendeleza programu ya lugha ya Kiswahili kwa Wachina.

  • Sekta ya Utalii China inavyobebwa na Wachina Wenyewe 2019-07-16

  UTALII nchini China ni sekta muhimu kwa maendeleo ,unaochangiwa na raia wenyewe wa nchi hiyo kutokana na kuwa na vivutio vya kila aina ikiwemo maeneo ya historia mbalimbali kuanzia dini,siasa,maendeleo ukuaji wa miji na mengineo imekuwa vivutio katika miji mbalimbali nchini humo huku idadi kubwa ya watalii wakiwa ni kutoka ndani ya nchi hiyo tofauti na nchi nyingine.

  1  2  3  4  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako