|
|
|||
| Serikali ya Marekani haina sababu ya kuzusha ugomvi dhidi ya China kwa lengo la kupanua uuzaji wa bidhaa zake nchi za nje Tangu mwanzoni mwa mwaka huu serikali ya Obama ya Marekani imeendelea kusisitiza umuhimu wa uuzaji wa bidhaa zake nje ili kuhimiza kuongeza nafasi za ajira na kufufua uchumi wa nchi hiyo, na kwa mara ya kwanza katika historia imetoa mpango wa taifa kuhusu kuhimiza uuzaji wa bidhaa nje. Muhimu zaidi ni kuwa baadhi ya maudhui ya mpango huo yanailenga China. Kuhusu hali hiyo baadhi ya wasomi wa Marekani walitumia takwimu na utafiti wao wakithibitisha kuwa mashaka, lawama na ukosoaji huo dhidi ya China hauna msingi wowote.
|
| Wabunge wa Marekani kupigia kelele suala la kiwango cha ubadilishaji wa fedha za RMB ni "mchezo wa siasa" Hivi karibuni baadhi ya wabunge wa Marekani walianza tena kupigia kelele suala la kiwango cha ubadilishaji wa fedha za RMB, wakitaka kuilazimisha serikali ya Marekani kuichukulia China kuwa ni "nchi inayoendesha kiwango cha ubadilishaji wa fedha".
|
| Umoja wa Ulaya wazuia kuenea kwa msukosuko wa madeni wa Ugiriki Mkutano wa mawaziri wa fedha wa nchi za sehemu inayotumia Euro tarehe 15 ulikubali kutoa msaada kwa Ugiriki katika wakati wa lazima. Waziri mkuu wa Ugiriki Bw. George Papandreou tarehe 16 alisema, hii ni hatua kubwa ya Umoja wa Ulaya katika utatuzi wa msukosuko wa madeni wa Ugiriki, pia alisisitiza kuwa Ugiriki inahitaji muda wa kutimiza mageuzi ili kutuliza hali ya mambo ya fedha, lakini haihitaji kutegemea misaada ya Umoja wa Ulaya. Wachambuzi wanasema lengo la taarifa ya mkutano huu na jibu la Bw. Papandreou ni kuimarisha imani za wawekezaji kwa uwezo wa serikali ya Ugiriki wa kulipa madeni, ili kuzuia msukosuko wa madeni usienee katika sehemu nzima inayotumia Euro.
|
| Utatuzi wa msukosuko wa Ugiriki unaitaka nchi hiyo "ijikwamue" yenyewe Mkutano wa mawaziri wa fedha wa nchi wanachama wa sehemu inayotumia Euro ulifanyika tarehe 15 huko Brussels, pande mbalimbali ziliafikiana kuhusu njia ya kiufundi itakayotumiwa katika hatua ya kuisaidia Ugiriki, na kueleza kuwa zitachukua hatua kwa haraka kama ikihitajika.
|
| Mpango wa Israel wa kujenga makazi mapya katika sehemu ya Jerusalem ya mashariki wakasirisha Marekani Habari zilizotolewa tarehe 14 na vyombo vya habari vya Israel zinasema, waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Benjamin Netanyahu hivi karibuni alikosolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Hillary Clinton kutokana na mpango wa kujenga makazi mapya ya wayahudi katika sehemu ya Jerusalemu ya mashariki, na hali hii inamaanisha kuwa mgongano kati ya Marekani na Israel kuhusu mpango huo bado haujaondolewa kama alivyosema Bw. Netanyahu, hata unaongezeka siku hadi siku.
|
| Ripoti ya Umoja wa Mataifa yadhihirisha kashfa ya utoaji misaada ya chakula nchini Somalia Hali ya usalama wa chakula nchini Somalia ni mbaya kwa muda mrefu, na watu milioni 3 nchini humo wanahitaji msaada wa chakula kutoka kwa jumuiya ya kimataifa. Lakini ripoti iliyotolewa hivi karibuni na idara ya Umoja wa Mataifa inasema, chakula cha msaada kinachotolewa kwa Somalia "kinaibiwa na maofisa mara kwa mara", wakati fulani kiasi hicho kimefikia asilimia 50 hivi.
|
| Rais wa Iran afanya ziara nchini Afghanistan Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran tarehe 10 aliwasili mjini Kabul na kuanza ziara yake nchini Afghanistan, ambapo alifanya mazungumzo na rais Hamid Karzai wa nchi hiyo. Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Karzai kufanya ziara nchini humo tangu achaguliwe tena kuwa rais mwezi Agosti mwaka jana. Wachambuzi wanaona kuwa katika ziara hiyo rais Ahmadinejad atajitahidi kuihimiza serikali ya Afghanistan ifanye mazungumzo ya amani na kundi la Taliban, ili kupinga mkakati wa Marekani wa kuangamiza kundi la Taliban kwa njia ya kijeshi.
|
| Makamu wa rais wa Marekani azuru Israel na kusisitiza suala la nyuklia la Iran Makamu wa rais wa Marekani Bw. Joe Biden, ambaye yuko ziarani nchini Israel tarehe 9 alisisitiza tena ahadi ya Marekani ya kuhakikisha usalama wa Israel, pia alisema Marekani itaizuia kabisa Iran kupata silaha za nyuklia. Wachambuzi wanaona lengo kuu la ziara ya Bw. Biden nchini Israel ni kuionya Israel, isichukue vitendo vya kijeshi dhidi ya Iran, ama sivyo matokeo yatakuwa mabaya zaidi.
|
| Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa azungumzia mustakabali wa kufufuka kwa uchumi wa Afrika Msukosuko wa fedha ulienea duniani mwaka jana, na kuathiri maendeleo ya uchumi wa dunia. Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Doinique Strauss Khan tarehe 8 alisema Afrika ni sehemu iliyoathiriwa zaidi na msukosuko wa fedha wakati hazikufanya makosa yoyote, na hivi sasa uchumi wake umeonesha dalili ya kufufuka.
|
| Uchaguzi wa wabunge wa Iraq ni hatua ya mwanzo ya kuchora upya ramani ya kisiasa nchini Iraq Uchaguzi wa wabunge wa Iraq ulianza kufanyika tarehe 7. Hii ni mara ya pili kwa uchaguzi huo kufanyika rasmi nchini Iraq tangu Marekani ianzishe vita dhidi ya Iraq na kupindua serikali ya Saddam Hussein mwaka 2003. Ingawa kazi ya kupiga kura ilimalizika usiku wa siku hiyo, lakini bado haijulikani kama matokeo ya uchaguzi yatakayotangzwa yatakubaliwa na makundi mbalimbali ya kisiasa, na kama viti vya ubunge vitagawanywa bila matatizo na serikali mpya itafanikiwa kuunda baraza la mawaziri.
|
| Maonesho ya 80 ya magari ya Geneva yafunguliwa Maonesho ya 80 ya magari ya Geneva yalifunguliwa rasmi tarehe 4 Machi kwa saa za huko. Maonesho hayo si kama tu yameonesha dalili za kufufuka kwa sekta ya magari, na bali pia yameonesha mustakabali mkubwa wa magari yanayotumia nishati mpya.
|
| Nchi za Afrika zatakiwa kutumia soko lake la kuifanya misitu yake isaidie kutimiza lengo la kupunguza utoaji wa carbon dioxide Mkutano wa pili wa Baraza la Afrika kuhusu kupunguza hewa ya carbon ulifunguliwa tarehe 3 huko Nairobi, ambapo utajadili ajenda kuhusu jinsi nchi za Afrika zitakavyotimiza lengo la kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto kwa kutumia soko lake la kuifanya misitu yake isaidie kupunguza carbon dioxide.
|
| Rwanda kuandaa maadhimisho ya "siku ya mazingira duniani" Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa hivi karibuni lilitangaza kuwa, nchi ya Afrika ya mashariki Rwanda imechaguliwa kuwa nchi itayoandaa shughuli za maadhimisho ya "siku ya mazingira duniani" kwa mwaka 2010, kutokana na mafanikio yake katika maeneo mengi yakiwemo wazo la hifadhi ya mazingira, uchumi usio na uchafuzi kwa mazingira, matumizi ya nishati mpya na kuweko kwa aina nyingi za viumbe.
|
| Pilikapilika za uokoaji zaendelea nchini Chile Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa tarehe 1 na ofisi ya hali ya dharura ya Chile, tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 27 Februari nchini humo limesababisha vifo vya watu 723. |
| Hali ya sasa ya Chile baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi Tetemeko kubwa la ardhi lililotokea siku ya Jumamosi nchini Chile limesababisha vifo vya watu wasiopungua 708. Rais Michele Bachelet wa Chile ametangaza hali ya hatari katika sehemu 6 za nchi hiyo zilizoathirika vibaya zaidi. Waandishi wa habari wa Radio China Kimataifa walifika Chile Jumapili kuwatembelea waathirika wa maafa hayo na kutuletea maelezo haya.
|
| Amani yaonekana Darfur, lakini bado kuna changamoto mbalimbali Serikali ya Sudan na kundi la upinzani la JEM la Darfur tarehe 23 usiku zilisaini makubaliano ya kusimamisha vita huko Doha, Qatar. Wachambuzi wanasema, kusainiwa kwa makubaliano hayo ni hatua ya kwanza ya kuifanya Darfur iwe na amani, lakini namna ya kutekeleza makubaliano hayo utakuwa mchakato mgumu.
|
| Mgogoro wa kidiplomasia kati ya Libya na Uswisi kuhusu mateka wapata maendeleo Wizara ya mambo ya nje ya Uswisi tarehe 24 ilithibitisha kuwa, mfanyabiashara mwenye uraia wa Uswisi Bw. Rashid Hamdani, ambaye alishikiliwa nchini Libya kwa miezi 19 tarehe 23 alirudi nchini Uswisi, na Mswisi mwingine Bw. Max Goldi anatumika kifungo nchini Libya. Baadhi ya vyombo vya habari vinaona kuwa, mgogoro wa kidiplomasia kati ya Libya na Uswisi uliodumu kwa mwaka mmoja na nusu umepata maendeleo baada ya Umoja wa Ulaya kuingilia kati, lakini utatuzi wa mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili bado unahitaji nguvu kubwa ya usuluhishi wa Umoja wa Ulaya.
|
| Wazimbabwe wajivunia urafiki kati yao na China Kutokana na mwaliko wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Yang Jiechi, waziri wa mambo ya nje wa Zimbabwe Bw. Simbarashe Mumbengegwi anafanya ziara nchini China kuanzia tarehe 23 Feburari hadi tarehe 2 Machi. Alipohojiwa na waandishi wetu wa habari kabla ya kuondoka Zimbabwe, alisema Zimbabwe inathamini uhusiano wa kirafiki wa muda mrefu kati yake na China. Lengo la ziara yake nchini China ni kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali.
|
| Hafla ya Zimbabwe kuanza kushiriki Maonesho ya kimataifa ya Shanghai yafanyika Maonesho ya kimataifa ya Shanghai yatafunguliwa tarehe 1 Mei mwaka huu, hivi sasa nchi mbalimbali zinazoshiriki kwenye maonesho hayo ziko kwenye pilikapilika za maandalizi. Tarehe 22 usiku hafla ya Zimbabwe kuanza kushiriki kwenye Maonesho ya kimataifa ya Shanghai ilifanyika huko Harare.
|
| Jumuiya ya kimataifa yafuatilia uasi wa kijeshi wa Niger na kuchunguza sababu za uasi huo Tarehe 18 uasi wa kijeshi ulitokea nchini Niger. Sasa hali ya nchi hiyo kwa jumla ni shwari. Tarehe 21 wajumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika walikwenda Niger na kufanya usuluhishi wa kidiplomasia, kutathimini hali ya nchi hiyo na kufanya mazungumzo na wanajeshi waasi. Kabla ya hapo, wajumbe wa nchi 15 wanachama wa jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS walifanya mazungumzo na wanajeshi waasi, pia wanataka wanajeshi hao waitishe uchaguzi mkuu ulio wazi na wenye kuaminika. Kutokana na shinikizo la kimataifa, wanajeshi hao wamesema wataitisha uchaguzi mkuu, lakini ni lini wataitisha uchaguzi na kama wao wenyewe watashiriki kwenye uchaguzi huo au la, mpaka sasa bado haijajulikana.
|
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |