![]() Ndege zisizo na rubani juzi zilishambulia maeneo ya Abqaiq na Khurais ya Shirika la mafuta la Saudi Arabia, ambapo shambulizi hilo limesababisha kupungua kwa takriban nusu ya uzalishaji wa mafuta nchini humo. |
![]() Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema nchi yake itachukua hatua zaidi za kusitisha utekelezaji wa ahadi ilizotoa kwenye Makubaliano ya Nyuklia ya Iran (JCPOA) yaliyofikiwa mwaka 2015 kama inahitajika. |
![]() Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF imetangaza kuwa itafikiria kumteua Kristalina Georgieva kutoka Bulgaria ambaye sasa ni ofisa mkuu mtendaji wa Benki ya Dunia kuwa mkurugenzi mkuu wa IMF. |
![]() Wabunge wa Uingereza wamekataa hoja ya waziri mkuu Boris Johnson ya kufanya uchaguzi Oktoba 15, ambaye ameapa kuiondoa nchi yake kwenye Umoja wa Ulaya Oktoba 31 yafikiwe ama yasifikiwe makubaliano. |
![]() Waziri mkuu wa Uingereza jana usiku alitangaza kuwa ataitisha uchaguzi mkuu kama wabunge leo watapiga kura ya kupinga Brexit isiyo na makubaliano. |
![]() Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu ICRC limesema, wafungwa takriban 130 wanahofiwa kuuawa katika shambulizi la anga lililoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya gereza la mkoani Dhamar, Yemen. |
![]() Banda la China katika maonesho ya kimataifa ya shughuli za anga ya MAKS-2019 yanayofanyika huko Moscow, Russia limezinduliwa, na litaonesha mafanikio ya hivi karibuni ya makampuni yanayoongoza ya China, pamoja na matokeo ya ushirikiano kati ya China na Russia. |
![]() Mkutano wa kilele wa mwaka 2019 wa kundi la nchi 7 (G7) umemalizika jana mjini Biarritz nchini Ufaransa. Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano imesema masuala kadhaa yalijadiliwa ikiwemo masuala ya biashara, Iran, Ukraine na Libya, lakini haukupata matokeo halisi. |
![]() Waziri mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson ambaye yupo ziarani nchini Uingereza, amefanya mazungumzo na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, ajenda kuu ikiwa ni suala la mpaka wa Ireland lililopo kwenye Mpango wa Uingereza wa kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya, Brexit. |
![]() Rais Vladimir Putin wa Russia amesema nchi yake itatumia makombora ya aina kadhaa kukabiliana na tishio linalotokana na Marekani kujitoa kwenye mkataba wa makombora ya masafa ya kati. |
![]() Waziri mkuu mpya wa Uingereza Boris Johnson ameteua mawaziri wa awamu ya mwanzo jana usiku, saa chache baada ya kushika wadhifa huo. |
![]() Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Juu ya Marekani NASA imetangaza kupitia majukwaa mbalimbali video kuhusu mwanaanga Neil Armstrong wa "APOLLO 11" kutua kwenye sayari ya Mwezi miaka 50 iliyopita, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu binadamu kutua kwenye sayari hiyo. |
![]() Balozi wa Uingereza nchini Marekani Bw. Kim Darroch amejiuzulu wakati mgogoro wa kidiplomasia ukiendelea kutokana na kuvuja kwa ujumbe wa kumkosoa rais Donald Trump wa Marekani. |
![]() Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif ametangaza mjini Natanz kuwa akiba ya Iran ya madini ya uranimu yaliyosafishwa imezidi kilogramu 300. |
![]() 2019-06-26 Mkoa unaojiendesha wa kabila la wa-uygur wa Xinjiang umepata maendeleo makubwa kuhusu ulinzi wa haki za binadamu na kutoa elimu ya mafunzo kazi ili "kuwalinda na kuwaokoa" watu walioshawishiwa na msimamo mkali wa kidini. |
![]() Kampuni ya kusafirisha vifurushi ya Marekani FedEx imeifungulia mashtaka wizara ya biashara ya Marekani kuhusiana agizo la kuitaka kampuni hiyo iweke vizuizi dhidi ya kampuni ya Huawei. |
![]() Mkurugenzi wa Shirika la fedha la kimataifa IMF Bibi Christine Lagarde amesema mvutano wa kibiashara kati ya Marekani na China hautakuwa na manufaa ya muda mrefu kwa yoyote. |
![]() Mkurugenzi wa Shirika la fedha la kimataifa IMF amesema mvutano wa kibiashara kati ya Marekani na China hautakuwa na manufaa ya muda mrefu kwa yoyote. |
![]() Mkutano wa mawaziri wa biashara na uchumi wa kidigitali wa nchi za kundi la nchi 20 ulifunguliwa jana huko Tsukuba, nchini Japan. Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo imesema ni muhimu sana kulinda mazingira ya uhuru na usawa wa kibiashara, na kundi la nchi 20 linapaswa kufanya juhudi kuhimiza mageuzi ya shirika la biashara la dunia. |
![]() Kutokana na waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda baraza la mawaziri kama ilivyopangwa, bunge la nchi hiyo jana limepiga kura na kupitisha mswada uliotolewa na chama cha Likud kinachoongozwa na Bw. Netanyahu kuhusu kuvunja bunge la 21 na kuitisha uchaguzi mpya. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |