• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Umoja wa Mataifa wahimiza kupunguza kiwango cha vifo vya watoto 2017-10-20

  Umoja wa Mataifa umetoa ripoti ikisema, ingawa idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano waliofariki kote duniani imekuwa chini zaidi katika historia, lakini kiwango cha vifo vya watoto wachanga kimeongezeka kutoka asilimia 41 ya mwaka 2000 hadi asilimia 46 ya mwaka 2016.

  • Askari 43 wa Afghanistan wauawa na kundi la Taliban kwenye kambi yao
   2017-10-19

  Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imetoa taarifa ikisema askari 43 wa jeshi lake wameuawa na wengine tisa kujeruhiwa kwenye shambulizi lililofanywa na waasi wa Taliban kwenye wilaya ya Maywand mkoa wa Kandahar.

  • Serikali ya Hispania yasema hali ya kujiendesha ya Catalan inaweza kusimamishwa
   2017-10-18

  Waziri mkuu wa Hispania na naibu wake, wamesema serikali ya Hispania imejiandaa kutumia kipengeleza cha 155 cha katiba kusimamisha hali ya kujiendesha ya jimbo la Catalan.

  • Jeshi la serikali ya Iraq ladhibiti mji wa Kirkuk 2017-10-17

  Jeshi la serikali limetwa udhibiti kamili wa mji wa Kirkuk, na wapiganaji wa kundi la Kikurdi wameondoka.

  • Wajumbe wa Umoja wa Ulaya wasema hakuna maendeleo yaliyopatikana kwenye duru ya tano ya mazungumzo ya Brexit 2017-10-13
  Duru ya tano ya maungumzo ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya imemalizika jana mjini Brussels, Ubelgiji.
  • IMF yapandisha makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia katika mwaka huu na mwaka kesho 2017-10-11

  Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limepandisha makadirio yake kuhusu ongezeko la uchumi wa dunia katika mwaka huu na mwaka kesho kwa asilimia 0.1 na kufikia asilimia 3.6 na asilimia 3.7 mtawalia.

  • Watu 12 wafariki katika ajali ya mashua kwenye mto kati ya Bangladesh na Myanmar 2017-10-09

  Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya mashua iliyobeba Warohingya wanaotoka Myanmar kuelekea Bangladesh imefikia 12, na wengine kadhaa bado hawajulikani walipo.

  • Watu 50 wauawa kwa kupigwa risasi nchini Marekani
   2017-10-02

  Watu wasiopungua 50 wameuawa na wengine 200 kujeruhiwa kwa kupigwa risasi katika mji wa Las Vegas magharibi mwa Marekani.

  • Watu 15 wafariki na wengine 50 wajeruhiwa katika tukio la kukanyagana nchini India 2017-09-29

  Watu 15 wamefariki na wengine 50 kujeruhiwa, baadhi yao vibaya, mapema leo katika tukio la kukanyagana lililotokea kwenye daraja la waenda kwa miguu karibu na kituo cha treni mjini Mumbai, India.

  • Mjadala wa wazi wa baraza kuu la 72 la Umoja wa Mataifa wafungwa 2017-09-26

  Mjadala wa wazi wa Baraza kuu la awamu ya 72 la Umoja wa Mataifa umefungwa katika makao makuu ya umoja huo mjini New York.

  • Wakurdi nchini Iraq waanza kupiga kura ya kihistoria ya maoni kutaka uhuru
   2017-09-25

  Wakurdi nchini Iraq leo wamepiga kura ya maoni ambayo itaamua uhuru wa mkoa a Kurdi na maeneo mengine ambayo yanakaliwa na jeshi lililoasi la Wakurdi.

  • Mkuu wa jimbo la Wakurdi athibitisha upigaji kura utaendelea leo 2017-09-25
  Mkuu wa jimbo la Wakurdi Bw Masoud Barzani amethibitisha kuwa upigaji kura utaendelea leo na hawatarudi nyuma, kwani wamefikia hitimisho kuwa kujitenga kutawafanya wasirejee tena kwenye madhila yaliyowakumba katika siku nyuma.
  • Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi Mexico yafikia 273 2017-09-22
  Taarifa iliyotolewa na idara ya ulinzi wa kiraia ya Mexico, imesema idadi ya vifo vinavyotokana na tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.1 kwenye kipimo cha Richter, lililotokea jumanne katikati ya nchi hiyo, imeongezeka hadi 273.
  • Vikundi vya uongozi vinafanya juhudi kutafuta watu walionusurika kwenye tetemeko la ardhi Mexico 2017-09-21

  Idara ya ulinzi wa kiraia ya Mexico imesema zaidi ya watu 230, ikiwa ni pamoja na 100 mjini Mexico City, wamepoteza maisha yao kwenye tetemeko lenye nguvu ya 7.1 kwenye kipimo cha Richter lililotokea jumanne.

  • Mjadala kwenye mkutano wa 72 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa wafunguliwa 2017-09-20

  Mjadala kwenye mkutano wa 72 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa umefunguliwa mjini New York, ambapo washiriki zaidi ya 100 watajadiliana kuhusu ufumbuzi wa matishio na changamoto zinazoikabili dunia.

  • Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa, na Rais wa Marekani watoa mwito wa kubadilishwa kwa urasimu umoja wa mataifa 2017-09-19

  Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Antonio Geterres na Rais Donald Trump wa Marekani wametoa mwito wa kubadilishwa kwa urasimu kwenye umoja wa mataifa.

  • Uingereza yashusha ngazi ya tishio la kigaidi 2017-09-18
  Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Bibi Amber Rudd amesema ngazi ya hatari ya tishio la shambulizi nchini humo imepunguzwa, baada ya kutajwa kuwa ya juu kabisa kufuatia mlipuko uliotokea kwenye kituo cha subway.
  • Polisi Russia wasumbuliwa na matishio feki ya mabomu 2017-09-14

  Polisi wa miji kadhaa mikubwa nchini Russia, ikiwemo Moscow, wamesumbuliwa na ripoti nyingi feki za matishio ya mabomu. Hadi sasa operesheni za kutafuta mabomu bado zinaendelea kwenye sehemu 190 za miji mikubwa 17 nchini humo.

  • Mkutano wa 72 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa wafunguliwa 2017-09-13

  Mkutano wa 72 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa umeanza rasmi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York. Kaulimbiu ya mkutano huo ni "Kuzingatia maslahi ya watu: Kujenga amani na maisha bora kwa binadamu wote katika dunia yenye maendeleo endelevu".

  • Dhoruba Irma yasababisha vifo vya watu 10 Cuba 2017-09-12
  Ripoti iliyotolewa na idara ya ulinzi wa kiraia nchini Cuba inasema dhoruba ya Irma imesababisha vifo vya watu 10 katika mikoa mbalimbali ya nchi hiyo.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako