![]() Wizara ya sheria ya Israel imesema, kesi ya rushwa inayomkabili waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Benjamin Netanyahu itasikilizwa tarehe 17, mwezi wa Machi, wiki mbili baada ya uchaguzi mkuu wa tatu. |
![]() Mkuu wa Tume ya uchaguzi ya Afghanistan Hawa Alam Nuristani ametangaza kuwa rais wa sasa Mohammad Ashraf Ghani amepata asilimia 50.64 ya kura kwenye uchaguzi mkuu, na kuwa rais wa nchi hiyo kwa muhula wa pili. |
![]() China itaanza kupokea maombi ya ya ushuru kwa uagizaji wa baadhi ya bidhaa kutoka Marekani, ikiwa ni pamoja na vifaa vya matibabu kuanzia tarehe 2 Machi. |
![]() Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ambaye yuko ziarani nchini Pakistan, amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua zaidi kuwasaidia wakimbizi wa Afghanistan. |
![]() Mkutano wa 56 wa usalama wa Munich MSC umefungwa jana ambapo waliohudhuria mkutano huo wameshindwa kufikia makubaliano kuhusu "ukosefu wa nchi za magharibi". |
![]() Wizara ya biashara ya Marekani jana imesema, serikali ya nchi hiyo inairuhusu kampuni ya Huawei ya China inunue bidhaa na huduma za Marekani kwa siku 45 nyingine, ili kupunguza athari mbaya kwa makampuni na wateja wa Marekani. |
![]() Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wamekubaliana kupanua muungano wa mafunzo wa NATO nchini Iraq, ikiwa ni kujibu amri ya rais wa Marekani Donald Trump kwa jumuiya hiyo kufanya kazi zaidi katika Mashariki ya Kati. |
![]() Askari 51 wa Syria wameuawa katika shambulizi lililofanywa na Jeshi la Uturuki kaskazini magharibi mwa Syria, na kusababisha mvutano kati ya serikali za Syria na Uturuki kuwa mbaya zaidi jana. |
![]() Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Ghebreyesus amesema, shirika hilo linachukua hatua mbalimbali kuratibu nguvu za kisayansi duniani, ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona kwa njia ya kisayansi. Aidha amehimiza kuongezwa kwa ushirkiano wa kimataifa. |
Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya kunamaanisha nini? 2020-02-01 Saa tano usiku jana kwa saa za London, Uingereza ilijitoa rasmi kwenye Umoja wa Ulaya. Tukio hili kubwa la kisiasa baada ya cita baridi linamaanisha nini kwa hali ya siasa nchini Uingereza, uhusiano kati ya Uingereza na Ulaya, na mchakato wa utandawazi barani Ulaya? |
![]() Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza mpango wake wenye utata wa amani ya Mashariki ya Kati uliosubiriwa kwa muda mrefu, akitoa wito wa kuwepo kwa suluhu ya nchi mbili huku akiitambua Jerusalem kuwa mji mkuu usiogawanyika wa Israel. |
![]() Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuwa maambukizi ya virusi vipya vya nimonia aina ya 2019-nCoV nchini China, hayajawa tukio la dharura la afya ya umma linalofuatiliwa na dunia PHEIC. |
![]() 2020-01-21 Tarehe rasmi ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya inakaribia, na katika muda huo, serikali ya Uingereza inaangalia fursa zake za biashara ya kimataifa katika siku zijazo baada ya Brexit. Januari 20, Uingereza iliwakaribisha wajumbe wa Afrika katika mkutano wa kilele wa Uingereza na Afrika uliofanyika mjini London. Kutokana na habari zilizotolewa na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, serikali ya nchi hiyo inaona fursa nzuri ya kibiashara na nchi za Afrika baada ya Brexit. |
![]() Wizara ya mambo ya Ulaya na mambo ya nje ya Ufaransa imetoa taarifa ya pamoja ikisema serikali za Ubelgiji, Denmark, Ufaransa, Ujerumani, Greece, Italia, Uholanzi and Ureno zimeahidi kuunga mkono kuanzishwa kwa tume ya usimamizi wa mambo ya majini inayoongozwa na Ulaya kwenye Mlangobahari wa Hormuz. |
![]() Rais Vladimir Putin wa Russia amemteua Mikhail Mishustin kuwa waziri mkuu mpya wa Russia. Mapema jana baraza la chini la bunge la Russia lilipitisha uteuzi huo kupitia upigaji wa kura. |
![]() Mwanadiplomasia wa wizara ya mambo ya nje ya China, Balozi Qi Qianjin alipokutana na wanahabari wa China na Israel mjini Tel Aviv, Israel, amefafanua maoni ya China kuhusu uhusiano kati yake na Israel na masuala yanayofuatiliwa zaidi ya Mashariki ya Kati. Amesema China inatumai kuwa kanda hiyo inaweza kudumisha amani na utulivu, na uhusiano kati ya China na Israel utaendelea kwa utulivu. |
![]() Baraza la chini la Bunge la Marekani limepitisha azimio linalolenga kumzuia rais wa nchi hiyo Donald Trump kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran bila idhini ya Bunge. Baraza hilo limepitisha azimio hilo kwa kura 224 za ndio dhidi ya 194 za hapana. |
![]() Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yupo ziarani barani Afrika jana huko Cairo alipokutana na wanahabari pamoja na mwenzake wa Misri Sameh Shoukry, alifafanua msimamo wa China kuhusu masuala ya Mashariki ya Kati. |
![]() 2020-01-08 Vikosi vya Ulinzi vya Mapinduzi ya Kiislamu vya Iran IRGC leo alfajiri vimerusha makombora kulenga vituo visivyopungua viwili vya kijeshi vya Iraq vyenye askari wa Marekani. |
Serikali ya Trump yaendelea kuwa imara dhidi ya Iran licha ya ukosoaji wa wabunge 2020-01-06 Serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani jana iliendelea kutetea nia yake ya kuizuia Iran kuchukua hatua za mashambulizi ya kujibu kwa kauli za vitisho, wakati wabunge wa Marekani wanamlaumu Rais Trump kwa kutoa habari kupitia mitandao ya kijamii kuipeleka nchi kwenye eneo la hatari. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |