![]() 2019-05-27 Viongozi wa Japan na Marekani wamesema wanakubaliana katika mambo mengi muhimu baada ya kumaliza mazungumzo yao mjini Tokyo. |
![]() Mwanzilishi wa maabara ya vyombo vya habari vya chuo cha Teknolojia cha Massachusetts MIT Bw. Nicholas Negroponte hivi karibuni ameandika makala akisema sera za mawasiliano ya habari zinapaswa kufuata kigezo cha bila kupendelea, na wala si masuala ya siasa za kijiografia. |
![]() Ofisi ya Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Jumatano ilitangaza kupanga kuinua kiwango cha ushuru wa forodha dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 hadi asilimia 25 kutoka asilimia 10 ya awali, hatua ambayo itatekelezwa kuanzia Mei 10. Kuhusu uamuzi huo wa Marekani, China imetoa taarifa ikisema kuwa kuongeza mgogoro wa kibiashara kati ya pande hizo mbili hakuendi na maslahi ya watu wa nchi hizo mbili na dunia nzima, China imesikitishwa na uamuzi huo, na kama Marekani ikitekeleza hatua hiyo, China italazimika kuchukua hatua za lazima za kujibu. |
![]() 2019-05-02 Mbunge wa Uingereza Bw. Faisal Rashid, ambaye pia ni mwenyekiti wa kikundi cha wabunge wa vyama tofauti cha pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na "njia ya uchumi ya China na Pakistan" anafuatilia ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kutetea ushirikiano kati ya China, Uingereza na Pakistan kufuatia pendekezo hilo. |
![]() Kiongozi wa juu wa kundi la IS Abu Bakr al-Baghdadi ametoa video yake ya dakika 18 kwenye mtandao na kutambua kushindwa kwa wapiganaji wake katika wilaya ya al-Baghouz, Syria na kupongeza mashambulizi ya mabomu nchini Sri Lanka. |
![]() Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang, mwenyekiti wa Kamati ya Ulaya Bw. Donald Tusk na mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Mataifa Bw. Jean-Claude Juncker jana huko Brussels wameendesha kwa pamoja mkutano wa 21 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya. Viongozi hao wamekubaliana kuhimiza mazungumzo kuhusu makubaliano ya uwekezaji kati ya pande hizo mbili kupata mafanikio ndani ya mwaka huu, na kufikia makubaliano ya kiwango cha juu ndani ya mwaka kesho. |
![]() Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May jana ameuomba Umoja wa Ulaya kuahirisha muda wa Brexit mpaka tarehe 30 Juni. |
![]() Mkuu wa kampuni ya Boeing ya Marekani Bw. Dennis Muilenburg amekiri kuwa katika ajali za ndege mbili za Boeing 737-8, mfumo wa kuongoza kasi ya ndege MCAS ulikuwa na matatizo, na kampuni hiyo itaboresha program husika katika wiki zijazo. |
![]() 2019-04-04 Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi (NATO) wamekutana mjini Washington, Marekani jana kwa mkutano wa siku mbili katika kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ya kijeshi, huku Russia ikiwa ajenda kuu ya mkutano huo. |
![]() 2019-04-03 Waziri wa Uingereza anayeshughulika na Wales Bw. Nigel Adams amejiuzulu wadhifa wake baada ya waziri mkuu wa nchi hiyo Bi. Theresa May kutangaza mpango wake wa kuongea na kiongozi wa chama cha upinzani cha Labor Bw. Jeremy Corbyn ili kumaliza mvutano kuhusu suala la Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya. |
![]() Rais Xi Jinping wa China ametoa pongezi kwa uzinduzi wa Mwaka wa Utalii wa China na Nchi za Visiwa vya Bahari ya Pacifiki uliofanyika leo mjini Apia nchini Samoa. |
![]() 2019-03-27 |
![]() Rais Donald Trump wa Marekani jana huko Washington alikutana na kiongozi wa ujumbe wa China wa mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani Bw. Liu He, akisema duru hii ya mazungumzo imepita hatua kubwa, lakini bado kuna kazi nyingi, hivyo pande hizo mbili zimeamua kurefusha mazungumzo hayo kwa siku mbili. |
![]() Mjumbe maalumu wa rais wa China Bw. Liu He na mjumbe wa biashara wa Marekani Bw. Robert Lighthizer, pamoja na waziri wa fedha Bw. Steven Mnuchin wameongoza ufunguzi wa duru ya saba ya mazungumzo ya ngazi ya juu ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani katika ikulu ya Marekani huko Washington. |
![]() Waziri wa maendeleo ya uchumi wa Russia Bw. Maksim Oreshki amesema, pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" la China linaisaidia Russia kutekeleza miradi ya taifa, na kupungua vikwazo dhidi ya kuunganisha Umoja wa Uchumi wa Asia na Ulaya na pendekezo hilo kunasaidia kuendeleza uchumi wa Ulaya na Asia. |
![]() Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya Yemen Bw. Martin Griffiths amesema, tangu pande zinazopambana nchini Yemen zifikie makubaliano mwezi wa Desemba mwaka jana, hali nchini humo imekuwa na mabadiliko mazuri. |
![]() Mnadhimu Mkuu wa jeshi la Iran Meja Jenerali Mohammad Bagheri amesema, Iran ina haki ya kuvuka mpaka na kuchukua hatua za kijeshi kama ikihitajika, ili kukomesha kambi za makundi ya ugaidi nchini Pakistan. |
![]() Baraza la juu la bunge la Marekani limezuia miswada miwili inayojaribu kufungua idara za serikali, huku vyama vyote vya siasa vikijitahidi kufikia mwafaka wa kumaliza kufungwa kwa idara hizo ambako kumechukua muda mrefu zaidi katika historia ya nchi hiyo. |
![]() 2019-01-24 Rais Donald Trump wa Marekani atalihutubia bunge kuhusu hali ya taifa baada ya idara za serikali kufunguliwa tena. |
![]() Rais Vladmir Putin wa Russia amezungumza na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na kusema, makubaliano ya amani kati ya nchi hizo yanahitaji maandalizi ya muda mrefu ili kupata utauzi bora zaidi utakaoridhisha pande zote mbili. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |