• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Russia yatarajia kuiuzia India mfumo wa kuzuia makombora wa S-400 2018-05-30

  Russia imemaliza mazungumzo na India kuhusu kuiuzia nchi hiyo mfumo wa kuzuia makombora wa S-400, na makubaliano hayo yatasainiwa siku zijazo.

  • Qatar yazuia uingizaji wa bidhaa kutoka UAE, Saudi Arabia, Bahrain na Misri baada ya mwaka mmoja wa kuwekewa vikwazo
   2018-05-28

  Qatar imesema itazuia bidhaa zinazotoka kwenye nchi za Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia, Bahrain na Misri, ikiwa ni karibia mwaka mmoja tangu nchi hizo nne kuiwekea vikwazo.

  • Ripoti ya Umoja wa Mataifa yakadiria ongezeko la uchumi wa dunia kuzidi asilimia 3 katika mwaka huu na mwaka kesho 2018-05-18

  Ripoti iliyotolewa jana na Umoja wa Mataifa imekadiria kuwa, uchumi wa dunia utaongezeka kwa asilimia 3 katika mwaka 2018 na mwaka 2019, ambao umezidi makadirio ya awali, sababu kuu ikiwa ni nguvu kubwa ya ongezeko la uchumi la nchi zilizoendelea na mazingira mazuriya uwekezaji.

  • Naibu waziri mkuu wa China awasili Marekani kwa ajili ya majadiliano ya kiuchumi na kibiashara 2018-05-16

  Mjumbe maalum wa rais wa China ambaye pia ni naibu waziri mkuu wa China Liu He amewasili mjini Washington, Marekani kwa ajili ya majadiliano ya kiuchumi na kibiashara na upande wa Marekani.

  • Marekani kuondoa vikwazo vya uchumi dhidi ya Korea Kaskazini kama nchi hyo ikiacha silaha za nyuklia 2018-05-14

  Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo amesema kama Korea Kaskazini ikiweza kutimiza kutokuwa na silaha za nyuklia, Marekani itaondoa vikwazo dhidi ya nchi hiyo na kuyaruhusu makampuni binafsi ya Marekani kuwekeza nchini humo.

  • Mawaziri wa fedha kutoka China, Japan, na Korea Kusini wasisitiza kujizuia na vitendo vya kujilinda
   2018-05-04

  Mawaziri wa fedha na magavana wa Benki Kuu za China, Japan, na Korea Kusini wamesisitiza haja ya kuzuia aina zote za kujilinda, na kukubaliana kuhakikisha mfumo wa wazi wa biashara na uwekezaji wa pande nyingi.

  • Kundi la IS latangaza kuwajibika na shambulizi dhidi ya tume ya uchaguzi Libya 2018-05-03

  Kundi la Islamic State limekiri kufanya shambulizi la kujitoa mhanga dhidi ya makao makuu ya tume ya uchaguzi ya Libya mjini Tripoli. Kundi hilo pia limesema shambulizi hilo linatokana na amri ya msemaji wa kundi hilo Abu Hassan al-Muhajir, na limesababisha vifo vya wanausalama na wafanyakazi zaidi ya 15 wa tume hiyo.

  • Mtu mmoja auawa na mwingine kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la risasi jijini London 2018-05-02

  Vyombo vya habari mjini London, Uingereza, vimesema mtu mmoja ameuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la risasi lililotokea jana usiku kaskazini magharibi mwa mji wa London.

  • Rais wa korea Kusini autaka Umoja wa Mataifa kufuatilia mpango wa Korea Kaskazini wa kufunga vituo vya majaribio ya nyuklia
   2018-05-01

  Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini ameutaka Umoja wa Mataifa kufuatilia mpango wa Korea Kaskazini wa kufunga vituo vyake vya majaribio ya nyuklia.

  • Idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi mawili ya mabomu nchini Afghanistan yafikia 23
   2018-04-30

  Watu 23 wameuawa wakiwemo washambuliaji wawili na wengine 27 kujeruhiwa katika mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotokea kwenye eneo lenye ofisi za balozi za nchi za nje katikati ya mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, leo asubuhi.

  • Pendekezo la Ukanda moja na Njia moja linasaidia ongezeko la uchumi la nchi husika 2018-04-19

  Zaidi ya asilimia 90 ya benki kuu za nchi 26 zilizoko kwenye Ukanda Mmoja na Njia Moja zinaona kuwa pendekezo hilo litasaidia kuhimiza uchumi wao katika miaka 5 ijayo, na nchi nyingi ziliunga mkono mashirika ya pande mbalimbali yaliyoongozwa na China.

  • Saudi Arabia yashauriana na Marekani kuhusu kutuma jeshi nchini Syria 2018-04-18

  Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir amesema, nchi hiyo inashauriana na Marekani kuhusu kutuma jeshi nchini Syria.

  • Mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria wazuia makombora mengi yaliyolenga viwanja viwili vya jeshi la anga 2018-04-17
  Vyombo vya habari vya Syria vimeripoti kuwa, mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria umefanikiwa kuzuia makombora mengi yaliyolenga viwanja viwili vya jeshi la anga nchini Syria leo alfajiri.
  • Mazungumzo ya 4 ya ngazi ya juu ya uchumi kati ya China na Japan yafanyika 2018-04-16

  Mjumbe wa taifa ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na mwenzake wa Japan Bw. Kouno Tarou leo huko Tokyo wameendesha mazungumzo ya nne ya ngazi ya juu ya uchumi kati ya China na Japan.

  • Marekani yaanza kushambulia maeneo ya Syria, milipuko yasikika 2018-04-14
  Marekani imeanza mashambulizi dhidi ya Syria katika mji mkuu wa Damascus kabla siku ya jumamosi ambapo milio mikali yenye miale miekundu ya mabomu ilionekana katika anga.

  Milio ya sauti za milipuko ilisikika katika mji mkuu huo katika maeneo yote, huku majeshi ya anga yaSyria nayo yakionekana kurusha makombora yake kutokea mlima Qasion, ambao unatazamamana na mji mkuu wa Damascus.

  • Marekani hakika itashindwa kwenye vita ya kibiashara inayotaka kufanya na China kutokana na makosa yake matatu 2018-04-08

  Historia huwa haijirudii, lakini huweza kueleza. Wakati serikali ya Trump inapotishia China kwa fimbo la mgogoro wa kibiashara, watu wanaweza kukumbuka kauli maarufu aliyoitoa Jenerali Omar Bradley tarehe 15, Mei mwaka 1951 bungeni akiwa mwenyekiti wa wanadhimu wakuu kwa wazo la kutaka kupanua Vita ya Korea hadi China. Kauli hiyo ni kuwa "itakuwa ni vita isiyofaa, katika sehemu isiyofaa, katika wakati usiofaa na dhidi ya adui asiyefaa" Hivi sasa, serikali ya Trump inataka kuanzisha vita ya biashara na China, jambo ambalo pia amefanya makosa matatu na hakika Marekani itashindwa katika vita hiyo.

  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aunga mkono utandawazi duniani na mfumo wa biashara wa pande mbalimbali 2018-04-06

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana alifafanua kuwa vitendo vya kujilinda kibiashara si njia sahihi ya kutatua mivutano ya biashara, na pia alieleza kuunga mkono utandawazi duniani na mfumo wa biashara wa pande mbalimbali.

  • Mkutano wa usalama wa kimataifa wafuatilia mfumo wa usalama wa kimataifa na mapambano dhidi ya ugaidi 2018-04-05

  Mkutano wa 7 wa usalama wa kimataifa umefanyika jana mjini Moscow, Russia, ambapo wajumbe waliohudhuria mkutano huo walijadili mwelekeo wa kufanya juhudi katika kupambana na ugaidi katika siku zijazo na kusisitiza kulinda mfumo wa usalama wa kimataifa na maelewano, haki na usawa.

  • China yatarajia jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa mchango kuboresha hali ya Haiti 2018-04-04

  Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuendelea kutoa mchango kuboresha hali ya Haiti na kuhimiza pande zote za nchi hiyo kuongeza nguvu kuendeleza uchumi wao na kuboresha maisha ya watu.

  • Raia elfu 40 warejea Ghouta Mashariki nchini Syria
   2018-04-03

  Jumla ya raia elfu 40 wamerejea kwenye makazi yao katika eneo la Ghouta Mashariki, pembezoni mwa mji mkuu wa Syria, Damascus, ambapo jeshi la serikali linakaribia kuukomboa mji huo.

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako