• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Umoja wa Mataifa wasisitiza Korea Kaskazini itekeleze kikamilifu azimio la Baraza la Usalama 2017-03-21
  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameisisitiza Korea Kaskazini itekeleze azimio la Baraza la Usalama la Umoja huo kwa pande zote na kuepuka vitendo zaidi vya uchokozi.
  • Martin Schulz kutoa changamoto kwa Merkel kwenye uchaguzi Ujerumani 2017-03-20

  Chama cha Social Democratic cha Ujerumani SPD kimethibitisha kwenye mkutano wa chama uliofanyika Jumapili kuwa kiongozi wake Bw. Martin Schulz atatoa changamoto kwa chansela Bibi Angela Merkel kwenye uchaguzi mkuu wa Ujerumani unaotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu.

  • Waziri mkuu wa Uholanzi adai ushindi katika uchaguzi wa wabunge 2017-03-16

  Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte amesema, nchi hiyo imeamua kusimamisha aina mbaya ya mfumo wa serikali unaofuata maoni ya umma.

  • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani kufanya ziara nchini China 2017-03-15

  Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson, anatarajiwa kufanya ziara nchini China mwishoni mwa wiki hii.

  • Russia kuteketeza silaha zote za kemikali nchini humo mwaka huu 2017-03-14

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kupunguza Silaha za Kemikali ya Russia Mikhail Babich amesema nchi hiyo inaweza kuteketeza silaha zake zote za aina hiyo mwaka huu.

  • Uturuki watangaza hatua madhubuti dhidi ya Uholanzi 2017-03-14
  Naibu waziri mkuu wa Uturuki Bw Numan Kurtulmus ametangaza kuwa Uturuki itachukua hatua za mfululizo dhidi ya Uholanzi, ili kujibu vitendo vyake vya kuwazuia maofisa wa Uturuki kuingia Uholanzi na kuwatawanya waandamanaji wa Uturuki nchini humo.
  • Jeshi la Iraq lakaribia kuingia katikati ya mji wa Mosul 2017-03-13

  Serikali ya Iraq imedhibiti zaidi ya theluthi moja ya eneo la magharibi mwa mji wa Mosul baada ya mapambano ya wiki nne ambayo yaliliwezesha jeshi la nchi hiyo kukaribia eneo kongwe la mji huo na kuzuia njia zote za kutoroka kwa wapiganaji wa kundi la IS mjini humo.

  • Mvutano baina ya Uholanzi na Uturuki kuongezeka endapo Waziri wa Uturuki kusimamishwa mjini Rotterdam 2017-03-12

  Mvutano wa kidiplomasia kati ya Uholanzi na Uturuki uliibuka Jumamosi usiku baada ya msafara wa Waziri wa familia na Sera za kijamii wa Uturuki Betul Sayan Kaya kusimamishwa kwa masaa karibu na Ubalozi wa Uturuki mjini Rotterdam.

  • China yatoa msaada wa dola za kimarekani milioni moja kwa wakimbizi wa Afghanistan 2017-03-10
  Serikali ya China imelikabidhi Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR dola za kimarekani milioni moja ambazo zitatumika kutoa msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi nchini Afghanistan.
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani shambulizi la kigaidi lililotokea huko Kabul 2017-03-09
  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani shambulizi la kigaidi lililotokea kwenye hospitali ya jeshi huko Kabul nchini Afghanistan, likisisitiza kupambana na ugaidi kwa nguvu zote.
  • Umoja wa Nchi za Kiarabu wasema ni mapema sana kujadili suala la kuirudisha Syria kwenye Umoja huo 2017-03-08

  Katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu Bw. Ahmed Abul-Gheit amesema ni mapema sana kujadili suala la kuirudisha Syria kwenye Umoja huo.

  • Umoja wa Mataifa waitaka Korea Kaskazini isimamishe majaribio ya makombora 2017-03-07
  Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Fahan Haq amesema katibu mkuu Bw. António Guterres ameilaani Korea Kaskazini kwa kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu kinyume cha maazimio ya Baraza la usalama la umoja huo, na kuitaka nchi hiyo isimamishe majaribio hayo na kutekeleza wajibu wake wa kimataifa.
  • Rais wa Marekani alitaka bunge kuchunguza kama serikali ya Obama ilitumia ovyo haki ya uchunguzi 2017-03-06
  Ikulu ya Marekani jana imetoa taarifa ikisema rais Donald Trump amelitaka bunge la nchi hiyo kuchunguza kama serikali ya Obama ilitumia ovyo haki ya uchunguzi kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka jana.
  • Baraza la Seneti la Marekani laidhinisha uteuzi wa Rick Perry kuwa waziri wa nishati 2017-03-03

  Baraza la Seneti nchini Marekani limeidhinisha uteuzi wa Rick Perry aliyependekezwa na rais Donald Trump kuwa waziri wa nishati kwa kura za ndio 62 dhidi ya 37 za hapana.

  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani vikali mashambulizi ya mabomu nchini Afghanistan 2017-03-02

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mashambulizi ya mabomu yaliyotokea tarehe 1 mjini Kabul, Afghanistan.

  • Trump alitaka bunge kupitisha mpango wa uwekezaji wa miundombinu 2017-03-01

  Rais Donald Trump wa Marekani amesema atalitaka bunge kupitisha mpango wa kuwekeza dola za kimarekani trilioni 1 kwenye miundombinu nchini Marekani ili kutoa mamilioni ya nafasi za ajira.

  • Mjumbe wa taifa wa China akutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani 2017-03-01
  Mjumbe wa taifa wa China Bw. Yang Jiechi ambaye yuko ziarani nchini Marekani jana alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw Rex Tillerson mjini Washington. Kwenye mazungumzo yao Bw. Yang amesema China inapenda kuimarisha ushirikiano na Marekani kwenye msingi wa kutogongana, kuheshimiana na kunufaishana.
  • Wizara ya ulinzi wa Marekani yatoa mpango wa kupambana na kundi la IS 2017-02-28

  Waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis amewasilisha mpango wa mwanzo wa kupambana na kundi la IS kwenye Ikulu uliotungwa na jeshi la Marekani.

  • ZTE yazindua simu ya smartphone inayotumia mtandao wa 5G 2017-02-27

  Kampuni ya mawasiliano ya China ZTE imezindua simu mpya iitwayo Sunday Gigabit Phone ambayo ni simu ya kwanza ya smartphone inayotumia mtandao wa 5G duniani kwenye maonyesho ya simu ya MWC yanayofanyika huko Barcelona, Hispania.

  • Polisi nchini Indonesia wamkamata mpiganaji baada ya shambulizi la bomu mkoa wa Java 2017-02-27

  Polisi wa kitengo cha kupambana na ugaidi nchini Indonesia wamemkamata mtu anayetuhumiwa kuwa gaidi baada ya mtu huyo kulipua bomu na kuchoma jengo la ofisi katika mji mkuu wa mkoa wa Java Magharibi.

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako