![]() Mamlaka ya usafiri wa anga nchini Kazakhastan imesema, idadi ya watu waliofariki katika ajali ya kuanguka kwa ndege imefikia 15. |
![]() Gazeti la New York Tims jana liliripoti kuwa, waziri wa ulinzi wa taifa wa Marekani Bw. Mark Esper anafikiria mpango wa kuondoa askari wa nchi hiyo kutoka nchi za Afrika magharibi, ambao ni sehemu moja ya mpango wa kupunguza tena askari 200,000 waliopo nchi za nje. |
![]() Kiongozi wa Chama cha Kihafidhina cha Uingereza Bw. Boris Johnson jana aliapishwa rasmi kuwa waziri mkuu wa Uingereza baada ya kushinda kwenye uchaguzi wa Baraza la chini la bunge la Uingereza. |
Umoja wa Afrika watoa mwito wa kukabiliana na mzigo unaosababishwa na ugonjwa wa UKIMWI kwa makundi dhaifu 2019-12-02 Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat ametoa wito wa kuwepo kwa juhudi za makusudi kupunguza mzigo wa ugonjwa wa UKIMWI kwa watu wazima walioko kwenye makundi yaliyo hatarini, hasa wakimbizi, watu wanaorudi makwao na wakimbizi wa ndani. |
![]() 2019-11-28 Wanadhimu Wakuu wa Majeshi ya Korea Kusini wamesema, Korea Kaskazini imerusha makombora mawili yasiyotambulika katika Bahari ya Mashariki. |
![]() 2019-11-15 Mkutano wa 11 wa viongozi wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zinazounda kundi la BRICS umefanyika mjini Brasilia, Brazil, na kuhudhuriwa na marais Jair Bolsonaro wa Brazil, Xi Jinping wa China, Vladmir Putin wa Russia, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na waziri mkuu wa India Narendra Modi. Rais Xi amehutubia ufunguzi wa mkutano huo akizihimiza nchi hizo kubeba majukumu ya kutetea na kutekeleza utaratibu wa pande nyingi. |
![]() Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na Shirika la Utangazaji la Brazil EBC EBC zimesaini makubaliano ya ushirikiano. Kutokana na makubaliano hayo, pande mbili zitafanya ushirikiano wa pande zote katika kubadilishana maudhui, kutengeneza na kusambaza vipindi kwa pamoja, maingiliano ya watu, na teknolojia za radio, televisheni na vyombo vipya vya habari vya 5G. |
![]() Wizara ya usalama wa umma ya Vietnam imethibitisha kuwa wahanga wote 39 waliokutwa wamekufa ndani ya lori katika kaunti ya Essex nchini Uingereza wamethibitishwa kuwa ni raia wa Vietnam. Wizara hiyo imesema watu hao wanatoka katika maeneo sita ya Vietnam. |
![]() Serikali ya Yemen na kamati ya mpito ya kusini STC zimesaini makubaliano ya kugawana madaraka huko Riyadh, Saudi Arabia. |
![]() Nchi 54 zimetangaza kwa pamoja kuunga mkono hatua za China cha kukabiliana na ugaidi na msimamo mkali katika Mkoa Unaojiendesha wa Xinjiang Uygur. |
![]() Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limetangaza orodha ya washindi wa tuzo ya kimataifa ya utafiti wa sayansi ya maisha, kwa ajili ya mashirika au watu waliotoa mchango muhimu katika kuboresha ubora wa maisha ya watu. Orodha ya mwaka huu ina watu watatu akiwemo Tu Youyou wa China aliyegundua dawa ya Artemisinin, na kuokoa maisha ya mamilioni ya watu. |
![]() Viongozi wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya isipokuwa Uingereza jana wamefikia makubaliano na kupitisha azimio la kuunga mkono makubaliano mapya yaliyofikiwa kati ya kamati ya umoja huo na serikali ya Uingereza. |
![]() Shirika la fedha duniani IMF limetoa Ripoti ya Makadirio kuhusu Uchumi wa Dunia, likipunguza makadirio ya ongezeko la uchumi wa dunia kwa mwaka 2019 hadi asilimia 3, ambayo imepunguzwa kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na makadirio yaliyotolewa mwezi Julai. Hiki pia ni kiwango cha chini zaidi tangu msukosuko wa fedha ulipuke mwaka 2008. |
![]() Naibu waziri mkuu wa China ambaye pia ni kiongozi wa China kwenye mazungumzo ya kiuchumi kati ya China na Marekani Liu He, mjumbe wa biashara wa Marekani Robert Lighthizer, na waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin walifanya mazungumzo ya raundi mpya kuhusu uchumi na biashara kuanzia tarehe 10 hadi 11 mwezi huu huko Washington. |
![]() Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ametoa pongezi kwa miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China na kutarajia uhusiano kati ya nchi hizo mbili uwe na mustakabali mzuri zaidi. |
![]() Rais wa zamani wa Ufaransa Bw. Jacques Chirac amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86. Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kulia na kati alikuwa anajulikana zaidi kwa kuamua kupinga operesheni ya kijeshi dhidi ya Iraq ya mwaka 2003 iliyoongozwa na Merekani. Uamuzi huo ulimletea heshima nchini mwake, lakini ulidhuru uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Marekani. |
![]() Bodi ya utendaji ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF imeidhinisha uteuzi wa Kristalina Georgieva raia wa Bulgaria aliyekuwa ofisa mtendaji wa Benki ya Dunia, kuwa mkurugenzi wa shirika hilo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Oktoba Mosi. |
![]() Mwenyekiti wa Kamati ya Ulaya Bw. Jean Claude Juncker amesema Umoja wa Ulaya hauwajibiki na matokeo ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja huo, na kwamba Umoja huo haupaswi kulaumiwa kwa uamuzi wa Uingereza. |
![]() Kiongozi wa Iran Ali Khamenei jana alisisitiza kuwa, Iran haitafanya mazungumzo ya ngazi yoyote na Marekani. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la habari la kiserikali la nchi hiyo, Khamenei amesisitiza kuwa Marekani imekuwa na matumaini ya kufanya mazungumzo na Iran ili kuilazimisha Iran ipokee nia yake |
![]() Uturuki, Russia na Iran zinafuatilia suala la usalama nchini Syria wakati wa mazungumzo kati ya pande hizo tatu, na kusisitiza mahitaji ya makubaliano ya muda mrefu ya kusimamisha vita katika eneo la Idlib, kaskazini magharibi nchini humo. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |