• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Rais wa Marekani asema makubaliano ya amani kati ya Palestina na Israel yaweza kufikiwa 2017-05-04
  Rais Donald Trump wa Marekani amesema nchi yake itafanya juhudi katika kuzihimiza Israel na Palestina zifikie makubaliano ya amani, na lengo hilo linaweza kutimia.
  • China yaitaka jumuiya ya kimataifa ilinde mamlaka ya kanuni ya kutoeneza silaha za nyuklia 2017-05-03

  Balozi wa China anayeshughulikia maswala ya silaha kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Fu Cong amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kulinda na kuhimiza mamlaka, ushawishi na ufanisi wa kanuni ya kutoeneza silaha za nyuklia.

  • Polisi wanne wajeruhiwa kwenye maandamano ya siku ya wafanyakazi Ufaransa 2017-05-02

  Wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa imesema vuguru zilizotokea jana katika maandamano ya siku ya wafanyakazi mjini Paris, zimesababisha polisi wanne kujeruhiwa, wawili wao wamejeruhiwa vibaya.

  • Umoja wa Ulaya wafikia mwongozo wa kuzungumza na Uingereza kuhusu BREXIT 2017-05-01
  Umoja wa Ulaya jana umefanya mkutano wa viongozi wa nchi wanachama 27 isipokuwa Uingereza, na kujadili mazungumzo na Uingereza kuhusu Brexit.
  • Mkutano wa ngazi ya mawaziri wa Baraza la Usalama leo kujadili suala la nyuklia la Peninsula ya Korea 2017-04-28

  Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi atahudhuria mkutano wa wazi wa ngazi ya mawaziri kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea utakaofanywa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo huko New York.

  • Mlipuko mkubwa watokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa mjini Damascus, Syria 2017-04-27

  Mlipuko mkubwa umetokea katika eneo linalozunguka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus nchini Syria mapema leo.

  • China kuimarisha ushirikiano na Ujerumani kwenye kundi la G20 2017-04-27
  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China itaiunga mkono Ujerumani kwa pande zote kuandaa mkutano wa kilele wa kundi la G20 utakaofanyika mjini Hamburg, na pia inapenda kuimarisha ushirikiano na Ujerumani kwenye kundi hilo.
  • Chansela wa Ujerumani akutana na waziri wa mambo ya nje wa China 2017-04-26
  Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel amekutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini humo kuhudhuria mazungumzo ya duru ya tatu kuhusu mikakati ya diplomasia na usalama kati ya China na Ujerumani.
  • China na Marekani zahimizwa kushirikiana kuleta uwiano katika biashara yao 2017-04-25

  Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai ametoa wito kwa nchi hizo kufanya juhudi kwa pamoja ili kutimiza uwiano katika biashara yao.

  • Bw Macron na Bibi Le Pen waingia katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa 2017-04-24

  Kwa mujibu wa makadirio ya upigaji kura na matokeo ya mwanzo ya kiserikali, mgombea wa chama cha mrengo wa kati Bw. Emmanuel Macron aliyekuwa waziri wa uchumi, na mgombea wa chama cha mrengo wa kulia Bibi Marine Le Pen wameongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa.

  • Polisi mmoja auawa katika tukio la ufyatuaji risasi Ufaransa 2017-04-21
  Polisi mmoja ameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa katika tukio la ufyatuaji risasi lililotokea jana jioni katika mtaa wa Champs Elysees mjini Paris, Ufaransa.
  • Bw. Achim Steiner kuongoza shirika la mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa 2017-04-20
  Katibu mkuu wa Umoja huo Bw. António Guterres amemteua Bw. Achim Steiner kuwa mkuu wa Shirika la mipango ya Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP.
  • Watu 6 wauawa katika mlipuko uliotokea mkoani Aleppo nchini Syria 2017-04-19

  Televisheni ya taifa ya Syria imesema watu 6 wameuawa na wengine 32 kujeruhiwa mapema leo katika mlipuko uliotokea Salahuddien, kaskazini mwa mji wa Aleppo nchini Syria.

  • Marekani kuzingatia machaguo yote kwa kuihimiza Korea Kaskazini iache silaha za nyuklia 2017-04-18

  Makamu wa rais wa Marekani Bw. Mike Pense aliyeko ziarani nchini Korea Kusini amesema, Marekani inataka kuihimiza Korea Kaskazini kuacha kutumia silaha za nyuklia kwa njia ya amani lakini pia itazingatiamachaguo yote.

  • Umoja wa Mataifa waitaka Korea Kaskazini ichukue hatua kutuliza hali ya kikanda 2017-04-18
  Umoja wa Mataifa umeitaka Korea Kaskazini ichukue hatua zote kupunguza hali ya wasiwasi kwenye peninsula ya Korea na kurudi kwenye mazungumzo ya amani na kuondoa silaha za nyuklia.
  • Russia yamtia mbaroni mwanamume anayeshukiwa kupanga shambulizi la St. Petersburg 2017-04-18
  • Watu 126 wauawa katika shambulizi la mabomu dhidi ya washia Syria 2017-04-17

  Shirika la haki za binadamu nchini Syria limesema shambulizi la mabomu dhidi ya msafara wa mabasi yanayobeba washia elfu tano waliokuwa wanaondoka eneo la Rashideen, pembezoni mwa jimbo la Aleppo, limesababisha vifo vya watu 126, wakiwemo wanawake na watoto 80.

  • Wapiganaji 36 wa kundi la IS wauawa katika shambulizi la bomu lililofanywa na Marekani nchini Afghanistan 2017-04-14

  Wapiganaji 36 wa kundi la IS wameuawa mashariki mwa mkoa wa Nangarhar nchini Afghanistan baada ya vikosi vya Marekani kushambulia maeneo yao kwa bomu kubwa.

  • Abiria aliyeburuzwa nje ya ndege ya United Airlines kufungua mashtaka 2017-04-14
  Wakili wake Bw. Tom Demetrio amesema, abiria huyo David Dao mwenye umri wa miaka 69 alipata majeraha makubwa na madhara ya kisaikolojia kutokana na kutendewa kikatili na maofisa usalama wa uwanja wa ndege.
  • Wapiganaji 35 wa IS wauawa nchini Iraq 2017-04-13

  Wapiganaji 35 wa kundi la IS wameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la serikali ya Iraq katika maeneo yaliyo karibu na mji wa Mosul, kaskazini mwa nchi hiyo.

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako