![]() Zaidi ya watu 1,500 wakiwa ni wanawake na watoto kutoka familia za wapiganaji wa kundi la Islamic State wanashikiliwa na mamlaka za nchini Iraq, na serikali ya Iraq inajadiliana na nchi wanazotoka ili kuamua hatma yao. |
![]() Tume ya uchaguzi ya Russia imetoa taarifa kuwa, baada ya ukaguzi wa kikamilifu, tume hiyo imeamua kupitisha na kusajili wagombea wanane kwa ajili ya kumpata rais mpya wa Russia, akiwemo, rais wa sasa Vladimir Putin. |
![]() Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, WHO itaunda kikosi cha kukabiliana na matukio ya dharura ya uhitaji wa huduma za afya duniani ambacho kinajumuisha maelfu ya wafanyakazi wa afya kutoka nchi 50. |
![]() Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres amelaani matumizi ya silaha za kikemikali nchini Syria na kutoa wito kwa baraza la Usalama kuhahikisha wahusika wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. |
![]() Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema ni muhimu kuanzisha utaratibu mpya wa kuchunguza matumizi ya silaha za kikemikali nchini Syria, ili kujua ukweli wa tukio hilo na kuepusha tukio kama hilo lisitokee tena, na kwamba pande zote za baraza la usalama zinapaswa kufanya jitihada za pamoja. |
![]() Naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergey Ryabkov amesema Russia na Marekani zinapaswa kurudia mazungumzo kuhusu ulinzi dhidi ya makombora. |
![]() Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani shambulizi la mabomu liliotokea jana mjini Benghazi, Libya na kueleza kushtushwa na uvumi wa kutokea kwa mauaji ya kulipiza kisasi baada ya shambulizi hilo. |
![]() Rais Vladmir Putin wa Russia na mwenzake Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki wamejadiliana kwa njia ya simu kuhusu hali ya Syria, na kusema wataendelea kushirikiana kusaidia kutatua mgogoro unaoendelea nchini humo. |
![]() Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov amesema Marekani haitafanikiwa kuilazimisha Russia ibadilishe sera ya diplomasia kwa kuiwekea vikwazo. |
![]() Korea Kusini na Korea Kaskazini zimekubaliana kuunda ujumbe wa pamoja chini ya bendera ya pamoja ya peninsula ya Korea kwenye gwaride la ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi , itakayofanyika mwezi ujao mjini PyeongChang nchini Korea Kusini. Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya mazungumzo ya manaibu mawaziri kwenye eneo la usalama lililoko kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili. |
![]() Chama cha ukombozi cha Palestina PLO Jumapili kimeitisha mkutano kujadili mkakati mpya wa kukabiliana na hatua ya Marekani kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, licha ya kususiwa na makundi makubwa ya Palestina Hamas na Jihad. |
![]() 2018-01-12 Waziri Mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May amezindua mkakati mkubwa wa mazingira ambao haijawahi kutokea nchini humo, akiahidi kufuta taka zote za plastiki zinazoweza kuepukika ifikapo mwaka 2042. |
![]() Mkutano wa pili wa viongozi wa ushirikiano wa Lancang-Mekong wenye kauli mbiu "Mto wa amani na maendeleo endelevu" umefanyika leo huko Phnom Penh, Cambodia. |
![]() Korea Kaskazini imekubali kutuma ujumbe wa ngazi ya juu wa wachezaji na ujumbe wa kamati ya Olimpiki ya nchi hiyo kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya PyeongChang. |
![]() Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA imeonya kuwa, shambulizi la hivi karibuni la kujitoa mhanga mjini Kabul, linaweza kutambuliwa kama tukio la uhalifu wa kivita. |
![]() Watu wasiopungua 40 wameuawa wakiwemo washambuliaji wawili na wengine wengi kujeruhiwa kwenye milipuko miwili ya kujitoa mhanga dhidi ya jengo moja magharibi mwa Kabul, mji mkuu wa Afghanistan. |
![]() Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov jana ameongea na mwenzake wa Marekani Bw. Rex Tillerson kwa njia ya simu na kusema, Marekani hairuhusiwi kuongeza hali ya hatari kwenye peninsula ya Korea kwa kauli za uchochezi na kuongeza jeshi lake kwenye peninsula hiyo. |
![]() Serikali ya Philippines imesema, watu 164 wamefariki na wengine 171 hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha kusini mwa nchi hiyo wiki iliyopita. |
![]() Baraza la umoja wa mataifa limepitisha azimio kuhusu hadhi ya Jerusalem, litakalofanya uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani kutambua mji huo kuwa mji mkuu wa Israel usiwe na nguvu ya kisheria. |
![]() Nchi 6 zinazojishughulikisha na suala la nyuklia la Iran na Iran zimefanya mkutano wa 10 wa tume ya ushirikiano ya makubaliano ya pande zote kuhusu suala la nyuklia la Iran huko Vienna. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |