• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Rais Xi Jinping asisitiza kukumbuka ushindi mkubwa na kusonga mbele kwa hatua madhubuti 10-23 18:03
    Rais Xi amewasisitiza wachina kukumbuka mioyoni ushindi mkubwa wa jeshi la China kwenye mapambano dhidi ya uvamizi wa Marekani nchini Korea Kaskazini, wawe na ushupavu na busara kwenye mapambano na kuendelea kusukuma mbele kwa hatua madhubuti jukumu kuu la kuendeleza ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya.
    • Uchumi wa China wadumisha mwelekeo mzuri wa kufufuka 10-21 18:01
    Takwimu zilizotolewa jumatatu na serikali ya China zinaonesha kuwa, katika robo tatu za mwanzo za mwaka huu, Pato la Ndani la China (GDP) liliongezeka kwa asilimia 0.7 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki. Katika robo ya pili na ya tatu ya mwaka huu, uchumi wa China ulikua kwa asilimia 3.2 na asilimia 4.9 mtawalia. Takwimu hizo zimefuatiliwa sana na vyombo vya habari vya kimataifa.
    • Uchunguzi waonesha mkoa wa Xinjiang unatilia maanani suala la ajira kwa watu wa makabila madogomadogo 10-20 17:16
    Kituo cha Utafiti wa Maendeleo ya Xinjiang leo kimetoa ripoti ya uchunguzi kuhusu kazi na ajira kwa watu wa makabila madogomadogo mkoani Xinjiang. Uchunguzi unaonesha kuwa mkoa wa Xinjiang unatilia maanani suala hilo, na kuheshimu nia na hiari yao ya kufanya kazi na kutafuta ajira.
    • Wasomi na vyombo vya habari vya Afrika wakanusha shutuma za udukuzi wa China barani Afrika 10-19 18:40
    Mwezi Mei mwaka huu, jopo la washauri bingwa la Marekani Heritage Foundation lilitoa ripoti ya kuishutumu China kufanya udukuzi katika majengo ya serikali za nchi za Afrika yaliyojengwa au kukarabatiwa na kampuni za China. Hivi karibuni katika kipindi cha kuadhimisha miaka 20 ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, ripoti hiyo ya uongo imeanza kuenezwa tena na baadhi ya vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii, ili kuharibu uhusiano na ushirikiano mzuri kati ya China na Afrika.
    • Takwimu za matumizi katika wiki ya mapumziko ya Siku ya Taifa zaonesha kuwa uchumi wa China unafufuka kwa kasi 10-09 17:10
    Takwimu za matumizi katika wiki ya mapumziko ya Siku ya Taifa na Sikukuu ya Mbalamwezi iliyoanzia Oktoba 1 hadi Oktoba 8, zinaonesha kuwa uchumi wa China unafufuka kwa kasi, haswa kwenye sekta za utalii, usafiri wa umma, migahawa, manunuzi na burudani.
    • Muujiza wa China wachangia kazi ya uondokanaji umaskni duniani 10-06 17:15
    Takwimu zilizotolewa na Benki ya Dunia (WB) zinaonyesha kuwa, mafanikio yaliyopatikana nchini China yamechangia asilimia 70 ya juhudi za dunia katika kuondokana na umaskini. Ni katika miaka minane tu kuanzia mwaka 2012 hadi 2019, idadi ya watu maskini nchini China imepungua kwa milioni 90.
    • Rais wa China ahutubia mjadala wa kawaida wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa 09-23 09:31

    Rais Xi Jinping wa China jana amehutubia mjadala wa kawaida wa mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Rais Xi amesisitiza kuwa, China itaendelea kubadilishana uzoefu wake katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona na teknolojia ya matibabu, kuunga mkono na kutoa msaada kwa nchi zinazohitaji, kuhakikisha utulivu wa mnyororo wa ugavi wa vifaa vya mapambano dhidi ya virusi vya Corona duniani, na kushiriki kwenye utafiti wa kutafuta chanzo na njia za kuenea kwa virusi hivyo.

    • China yatarajiwa kuchangia zaidi uchumi wa dunia 09-21 17:01
    Mwaka huu China imeweka mpango wa kujenga muundo mpya wa maendeleo unaozingatia mizunguzo miwili ya ndani na ya kimataifa. Mpango huo ni uamuzi wa kimkakati wa kuelekeza maendeleo ya kiuchumi ya China katika siku zijazo.
    • Waraka wa China wa miaka 75 ya UM wathibitisha dhamira ya China ya kulinda utaratibu wa pande nyingi
     09-11 18:41

    Wizara ya mambo ya nje ya China jana Alhamisi ilitoa Waraka wa Msimamo wa China kuhusu Miaka 75 ya Umoja wa Mataifa, unaofafanua msimamo na maoni ya China juu ya hadhi ya Umoja wa Mataifa, hali ya kimataifa, maendeleo endelevu, ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona na masuala mengineyo.

    • Hafla ya kukamilisha na kuzinduliwa kwa mfumo wa uongozaji wa satelite wa Beidou No. 3 kufanyika kesho 07-30 09:58

    Taarifa iliyotolewa jana na mamlaka ya mfumo wa uongozaji wa satelite ya China imetangaza kuwa, satelite ya 55 ambayo ni ya mwisho kwenye mfumo wa satelite ya Beidou imeanza kufanya kazi katika mtandao wa satelite baada ya kukamilisha majaribio kwenye mzunguko na tathmini ya kuingia kwenye mtandao.

    • Huawei yasema hatua ya Uingereza kuipiga marufuku kampuni hiyo itarudisha nyuma maendeleo ya kidigitali 07-15 09:28

    Kampuni ya Huawei ya China imesema uamuzi wa serikali ya Uingereza kuipiga marufuku kampuni hiyo kushiriki kwenye utengenezaji wa mtandao wa 5G 'ni wa kukatisha tamaa' na unatishia 'kupunguza kasi ya maendeleo ya kidigitali ya Uingereza, kufanya gharama za huduma ziwe juu na kuongeza pengo la kidigitali.'

    • Watu 21 wafariki baada ya basi kutumbukia ziwani mjini Anshun 07-07 19:51
    Watu 21 wamefariki dunia na wengine 15 wamejeruhiwa baada ya basi kutumbukia ziwani katika mji wa Anshun, uliopo katika mkoa wa Guizhou kusini magharibi mwa China.
    • China yashuhudia wagonjwa wengi zaidi wa COVID-19 wakipona
     07-03 18:42

    Jumla ya wagonjwa 60 wa COVID-19 wametibiwa hospitali na kuruhusiwa kurudi nyumbani katika wiki moja iliyopita hapa nchini China, ikiwa ni ongezeko la asilimia 46 kuliko katika wiki zilizopita.

    • Chama cha Kikomunisti cha China chajitolea kwa ajili ya China na dunia
     07-01 19:24

    Leo tarehe mosi Julai ni mwaka wa 99 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China CPC ambacho ni chama kikubwa zaidi cha kisiasa duniani. Chama hicho ambacho wanachama wake wameongezeka kutoka zaidi ya 50 hadi zaidi ya milioni 90 kimetawala China kwa miaka 71.
    • Maonesho ya 127 ya biashara ya China kwa kupitia mtandao wa Internet ni ishara chanya ya China katika kupanua ufunguaji mlango 06-25 19:29

    Maonesho ya 127 ya biashara ya kimataifa ya China yaliyofanyika kwa siku 10 mjini Guangzhou yamemalizika jana.

    • Kupaka matope kwa makusudi mabaya hakuwezi kukwamisha urafiki kati ya China na Afrika 06-16 10:35
    Hivi sasa, janga la virusi vya Corona linaenea kwa kasi barani Afrika. Kwa mujibu wa takwimu kutoka Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa cha Afrika, hadi kufikia tarehe 14 Juni, nchi 54 barani Afrika zimeripoti watu laki 2.3 waliothibitika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo, na idadi ya vifo imezidi elfu 6.2.
    • Kupaka matope kwa makusudi mabaya hakuwezi kukwamisha urafiki kati ya China na Afrika 06-16 10:02
    • China yatoa waraka kuhusu mapambano dhidi ya virusi vya Corona 06-07 17:21

    Ofisi ya habari ya baraza la mawaziri la China leo asubuhi (June 7) imetoa waraka kuhusu mapambano dhidi ya virusi vya Corona wenye jina "Mapambano dhidi ya COVID-19: Juhudi za China".

    • Balozi wa China nchini Marekani aeleza sababu na kujibu wasiwasi wa watu juu ya utungaji sheria ya usalama wa taifa kwa Hong Kong 05-31 18:45
    Balozi wa China nchini Marekani Cui Tiankai amesema sheria ya kulinda usalama wa taifa kwa Hong Kong itahakikisha kuwa sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" sio tu itatekelezwa ipasavyo, bali pia kwa muda mrefu, kwani Hong Kong haitakuwa na maendeleo na ustawi wa kudumu kama usalama wa taifa haukuwepo.
    • Jumuiya ya kimataifa yasema mikutano miwili ya kisiasa ya China itaimarisha imani ya dunia
     05-25 09:29

    Mikutano mikuu miwili ya kisiasa nchini China ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China na Mkutano wa Bunge la Umma la China inayoendelea kufanyika, inafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa, ambayo inasema mikutano hiyo itaimarisha imani ya dunia.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako