• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Xi Jinping asisitiza kujenga uhusiano wa wenzi wa kimaendeleo duniani ili kuhimiza ustawi wa pamoja 2017-08-21
  Kwenye mkutano wa tano wa viongozi wa nchi za BRICS uliofanyika mwaka 2013 mjini Durban, Afrika Kusini, Rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba kuhusu "Kushirikiana ili Kupata Maendeleo ya pamoja", na kusisitiza umuhimu wa kujenga uhusiano wa wenzi wa kimaendeleo duniani, ili kuhimiza ustawi wa pamoja. Ni miaka minne sasa imepita tangu rais Xi Jinping atoe hotuba hiyo. Hotuba ya rais Xi imekuwa na maana gani kwa shughuli za kimataifa za hivi sasa?
  • Rais wa China apongeza uzinduzi wa kituo cha ujuzi wa maendeleo ya kimataifa 2017-08-21

  Hafla ya uzinduzi wa kituo cha ujuzi wa maendeleo ya kimataifa cha China na utoaji wa ripoti ya utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030 nchini China imefanyika hapa Beijing.

  • Semina ya uongozi ya nchi za BRICS yafungwa 2017-08-18

  Semina ya siku mbili kuhusu uongozi ya nchi za BRICS imefanyika kuanzia jana huko Quanzhou, mkoani Fujian, na kuhudhuriwa na watu zaidi 160 kutoka nchi za BRICS na nchi nyingine zinazoendelea.

  • Fan Changlong akutana na mwenyekiti mnadhimu wa jeshi la Marekani 2017-08-17

  Naibu mwenyekiti wa kamati ya kijeshi ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Fan Changlong, leo hapa Beijing amekutana na mwenyekiti mnadhimu wa jeshi la Marekani Jenerali Joseph F. Dunford.

  • China yaendelea na kazi ya uokoaji baada ya tetemeko la ardhi mkoani Sichuan 2017-08-11

  Hadi kufikia jana tarehe 10, tetemeko la ardhi lililotokea katika wilaya ya Jiuzhaigou mkoani Sichuan limesababisha vifo vya watu 20, na wengine 431 kujeruhiwa. Watu zaidi ya elfu 70 waliokwama kwenye eneo hilo, wamehamishwa katika sehemu salama. Hivi sasa kazi za uokoaji bado zinaendelea.

  • Serikali kuu ya China yatoa dola za Marekani milioni 27.1 kwa kazi za uokoaji za tetemeko la ardhi 2017-08-11

  Wizara ya fedha ya China imesema serikali kuu ya China imetoa dola za kimarekani milioni 27.1 kwa kazi za uokoaji mkoani Sichuan na Xinjiang, baada ya kuathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi.

  • Macho ya kulinda msitu 2017-08-09

  Kuzuia ajali ya moto ni muhimu zaidi kati ya kazi za kulinda misitu. Katika msitu wa Saihanba ulioko mkoani Hebei, China, ingawa mitambo ya kisasa kama vile rada ya kugundua moto na kamera za uchunguzi zimewekwa, lakini uchunguzi wa binadamu bado ni muhimu zaidi, na watu wa kuchunguza ajali ya moto wanajulikana kama macho ya kulinda misitu.

  • Watu saba wamefariki dunia baada ya tetemeko lenye nguvu ya 7 kwenye kipimo cha Ritchter kutokea kusini magharibi mwa China 2017-08-09

  Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7 kwenye kipimo cha Richter limeikumba sehemu ya ndani ya mkoa wa Sichuan, ulioko magharibi mwa China, na kusababisha vifo vya watu tisa na wengine 164 kujeruhiwa.

  • Muujiza wa kubadilisha jangwa kuwa msitu huko Saihanba 2017-08-07

  Msitu wa Saihanba wenye ukubwa wa hekta elfu 74.7 ulioko kilomita 200 kaskazini mwa mji wa Beijing nchini China, ni msitu mkubwa zaidi duniani uliopandwa na watu. Wafanyakazi wa shamba la msitu huo wametimiza muujiza wa kubadilisha jangwa kuwa msitu katika zaidi ya nusu karne iliyopita.

  • Wakulima wa mkoa wa Xizang wanufaika na utalii wa vijiji 2017-08-04

  Kijiji cha Zhangba mkoani Xizang kiliunda shirikisho la utalii wenye umaalumu wa huko mwezi Oktoba mwaka 2010. Kuanzia wakati ule, kijiji hicho kimeshughulikia utalii unaoshirikisha chakula cha Xizang, nyimbo na ngoma, desturi ya maisha ya huko, michezo na kukaa kwenye nyumba za wakulima. Utalii umeleta faida halisi kwa kijiji hicho, na kutoa mchango mkubwa kwa juhudi za kijiji hicho kuondoa umaskini.

  • Wizara ya mambo ya nje ya China yatoa maoni kuhusu jeshi la India kuingia ardhi ya China 2017-08-03

  China imetoa waraka wa "ukweli kuhusu kikosi cha ulinzi wa mpakani cha India kuingia ardhi ya China katika eneo la Sikkim la mpaka kati ya China na India na msimamo wa China". Akizungumzia suala hilo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Geng Shuang amesema ingawa sasa India inazungumzia amani, ni vema vitendo vikafuatiliwa zaidi kuliko maneno.

  • Uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika nchini China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu waongezeka kwa asilimia 46 2017-08-03

  Takwimu zilizotolewa leo na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, biashara kati ya China na Afrika inaongezeka, na thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili katika nusu ya kwanza ya mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 19. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, uchumi wa Afrika umeonesha hali ya kufufuka. Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa imekadiria kuwa, ongezeko la uchumi wa Afrika kwa mwaka huu litafikia asilimia 3.2, na kuongezeka kwa asilimia 1.7 kuliko mwaka jana wakati kama huu.

  • Makubaliano manane ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara yasainiwa kwenye mkutano wa mawaziri wa nchi za BRICS 2017-08-02

  Waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan leo ametangaza kuwa, Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zimefikia maoni ya pamoja kwenye pande nane zikiwemo kupitisha mpango wa ushirikiano wa biashara ya huduma kati yao, mpango wa ushirikiano wa kurahisisha uwekezaji na mfumo wa ushirikiano wa kiuchumi.

  • Rais Xi Jinping wa China asisistiza kushikilia njia ya kujenga jeshi lenye nguvu kubwa iliyo na umaalumu wa China 2017-08-01

  Mkutano wa kuadhimisha miaka 90 tangu kuanzishwa kwa jeshi la ukombozi la umma la China PLA umefanyika leo hapa Beijing, rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano huo na kusisitiza kuwa, ili kutimiza ustawi wa China na maisha mazuri zaidi kwa wachina, ni lazima kulijenga jeshi la China kuwa na nguvu kubwa duniani. Pia amesema China itashikilia njia ya kuimarisha uwezo wa jeshi kwa umaalumu wa China.

  • China yaandaa tafrija ya kuadhimisha miaka 90 ya jeshi lake 2017-08-01

  Wizara ya ulinzi ya China jana hapa Beijing iliandaa tafrija ya kuadhimisha miaka 90 tangu kuanzishwa kwa jeshi la ukombozi la umma la China PLA, ambayo ilihudhuriwa na rais Xi Jinping, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na viongozi wengine wa China.

  • Mfumo wa matumizi ya uwekezaji wa nje nchini China uliendelea kuboreshwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu 2017-07-31
  Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo hapa Beijing, ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China imeeleza hali ya biashara na nje nchini China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu. Thamani ya biashara kati ya China na nchi nyingine katika nusu ya kwanza ya mwaka huu imefikia yuan trilioni 13.14, na kuongezeka kwa asilimia 19.6, biashara kati ya China na nchi zilizoko kwenye "Ukanda mmoja na Njia moja" zimeongezeka kwa kasi.
  • Rais Xi Jinping wa China atoa agizo la kujenga jeshi lenye kiwango cha juu duniani 2017-07-31

  Rais Xi Jinping wa China jana alikagua gwaride la jeshi la ukombozi wa Umma la China na kutoa agizo la kujenga jeshi hilo kuwa la kiwango cha juu duniani.

  • Gwaride la kijeshi lafanyika kuadhimisha miaka 90 ya kuanzishwa kwa jeshi la China 2017-07-30
  Katika maadhimisho ya miaka 90 ya kuanzishwa kwa jeshi la ukombozi la umma la China, gwaride la kijeshi limefanyika leo asubuhi katika kituo cha kijeshi cha Zhurihe, mkoani Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China.
  • Mkutano wa mawaziri wa kazi na ajira wa BRICS wafungwa 2017-07-28

  Mkutano wa mawaziri wa kazi na ajira wa nchi za BRICS wa mwaka 2017 umefungwa tarehe 27 mjini Chongqing, China, ambapo mawaziri wa kazi na ajira wa nchi za BRICS, wajumbe wa wenzi wa kijamii, pamoja na maofisa waandamizi wa Shirika la Kazi Duniani ILO na Shirikisho la Kimataifa la Utoaji wa Huduma za Kijamii, wamehudhuria mkutano huo na kufikia makubaliano mengi kuhusu masuala yanayofuatiliwa.

  • Sehemu ya kwanza ya Luteka ya pamoja ya majeshi ya majini ya China na Russia yamalizika 2017-07-28
  Kundi la manowari la Jeshi la majini la China lilifunga safari mkoani Hainan, kusini mwa China tarehe 18 mwezi Juni na kuwasili bandari ya Baltiysk ya Russia tarehe 21 mwezi huu, na kushiriki kwenye luteka hiyo tarehe 25.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako