![]() Idara ya nguvukazi na huduma za jamii ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur, nchini China imesema, mwaka jana imezindua sera kadhaa na kuwasaidia watu 75,000 kuanza biashara zao wenyewe. |
China inaendelea kutoa msaada kwa Afrika ili kuitayarisha kukabili virusi vya korona ikiwa vitatokea barani humo. |
![]() Rais Xi Jinping wa China amemwambia mwenzake wa Marekani Donald Trump kuwa China ina imani na uwezo wa kushinda vita dhidi ya maambukizi ya virusi vipya vya korona. Rais Xi amesema hayo alipoongea na rais Trump leo kwa njia ya simu, na pia amesema China imechukua hatua kamili na kujibu kwa haraka maambukizi hayo. Rais Xi pia amemwahakikishia mwenzake wa Marekani kuwa mustakbali wa ukuaji wa uchumi wa muda mrefu haujabadilika. |
![]() Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi Hua Chunying amesema, hadi kufikia jana mchana, China imepokea msaada wa vitu vya kupambana na maambukizi ya virusi vya korona kutoka kwa serikali za nchi 21 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, na China inapongeza na kushukuru jamii ya kimataifa kwa uelewa, uungaji mkono na msaada wake. Hua amesisitiza kuwa ushindi wa China ndio ni ushindi wa dunia, na China ina uwezo na imani ya kushinda vita hivyo. |
![]() Hadi kufikia saa mbili usiku wa tarehe 2, zaidi ya wahudumu 8000 wa afya kutoka sehemu mbalimbali za China na jeshi la China wamekusanyika mkoani Hubei, China wakisaidia mkoa huo ulioko mstari wa kwanza katika mapambano dhidi ya maambikizi ya virusi vipya vya korana. Jana usiku, hospitali ya Huoshenshan iliyojengwa hivi karibuni ilianza kuwapokea wagonjwa walioambukizwa virusi vya korona. |
![]() China imeikosoa Marekani kwa kuchukua hatua kupita kiasi ambazo ni kinyume cha ushauri wa Shirika la Afya Duniani WHO kuhusiana na maambukizi ya virusi vipya vya korona. |
![]() Kundi la wasomi nchini China limelitaka Bunge la Umma la China kufanyia marekebisho Sheria ya Ulinzi wa Wanyamapori ili kujumuisha usalama wa afya ya jamii katika matumizi ya bidhaa za wanyamapori. Wataalam hao wanataka kutungwa kwa sheria na kanuni mpya kuhusu wanyamapori. Wanasayansi na wasomi wanataka kuona mwisho wa biashara haramu na ulaji wa wanyamapori, na kusema yanahatarisha afya ya umma. |
![]() Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, China inastahili kupongezwa na kuheshimiwa na jamii ya kimataifa kwa kuchukua hatua kali sana katika kudhibiti mlipuko wa virusi vipya vya korona na kuzuia visienee nje ya China. |
![]() Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema WHO haiungi mkono baadhi ya nchi kuwaondoa wananchi wao nchini China ili kuepuka maambukizi ya virusi vipya vya korona mjini Wuhan, China na kwamba WHO ina imani na uwezo wa China katika kuzuia na kudhibiti maambukizi hayo. |
![]() 01-22 18:45 Mamlaka ya afya ya China imetangaza kuwa, hadi kufikia Jumanne, watu 440 wamethibitishwa kuambukizwa na virusi vipya vya korona (2019-nCoV) vinavyoweza kusababisha ugonjwa wa nimonia katika mikoa 13 nchini humo. |
![]() Shirika la Afya Duniani WHO limesema litafanya mkutano wa dharura kesho mjini Geneva ili kutathmini kama maambukizi ya virusi vya korona vya aina mpya yanayotokea hivi karibuni nchini China ni"tukio la dharura la afya ya umma duniani" au la, na litatoa ushauri juu ya jinsi ya kudhibiti maambukizi hayo. |
![]() 01-20 17:04 Miji zaidi ya nchini China imeongeza usimamizi, udhibiti, na kinga ya magonjwa yanayotokana na mfumo wa hewa baada ya kuongezeka kwa kesi zaidi zinazohusishwa na ugonjwa wa nimonia. |
![]() Rais Xi Jinping wa China yuko ziarani mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China katika ziara ya ukaguzi kabla ya mwaka mpya wa jadi wa kichina. Rais Xi huyo ameenda kijiji cha kabila la Wa kilichoko kwenye wilaya ya Qingshui mjini Tengchong, ili kufahamu kuhusu kazi ya kuondokana na umaskini, huku akitoa salamu za mwaka mpya wa jadi kwa wanakijiji. |
Waziri wa mambo ya nje wa China apongeza mwanzo mzuri wa mambo ya diplomasia ya China mwaka 2020 01-19 16:45 Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ameipongeza ziara ya rais Xi Jinping wa China nchini Myanmar kuwa ni mwanzo mzuri wa shughuli za kidiplomasia za China kwa mwaka 2020. Bw. Wang amewaambia wanahabari hayo baada ya kumalizika kwa ziara ya siku mbili ya rais Xi nchini Myanmar, akieleza kuwa rais Xi ameshiriki kwenye shughuli 12 na kushuhudia kusainiwa kwa nyaraka 29 za ushirikiano katika nyanja mbalimbali katika mji mkuu wa nchi hiyo Nay Pyi Taw. |
![]() China na Myanmar zimekubaliana kutumia fursa ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati yao na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya nchi hizo pamoja na kuhimiza uhusiano wao uingie kwenye zama mpya. |
![]() Idara Kuu ya Takwimu ya China leo imetangaza kuwa Pato la Taifa GDP la China limefikia dola za kimarekani trilioni 14.38, likiwa ni ongezeko la asilimia 6.1 kuliko mwaka jana wakati kama huo, na limepita lengo lililowekwa kati ya asilimia 6 na asilimia 6.5. |
![]() Habari kutoka mkutano wa tatu wa bunge la 13 la umma la mkoa wa Xinjiang, China, zimesema mkoa huo umepokea watalii zaidi ya milioni 200 mwaka 2019, na pato lililotokana na utalii mkoani humo lilifikia dola zaidi ya bilioni 50 za kimarekani. |
![]() Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Misri Sameh Shoukry mjini Cairo, Wang amesisitiza kuwa suala la Xinjiang ni mambo ya ndani ya China, na kinachotokea Xinjiang ni suala la kupambana na mfarakano na ugaidi, sio suala la haki za binadamu au dini. |
Waziri wa mambo ya nje wa China afafanua msimamo wa China kuhusu suala la Mashariki ya Kati 01-09 17:10 Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yupo ziarani barani Afrika jana huko Cairo alipokutana na wanahabari pamoja na mwenzake wa Misri Sameh Shoukry, alifafanua msimamo wa China kuhusu masuala ya Mashariki ya Kati. |
![]() Tarehe 1 Januari mwaka 2020, mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG Bw. Shen Haixiong alitoa hotuba ya mwaka mpya kwa wasikilizaji walioko ndani na nje ya nchi kupitia Radio China Kimataifa CRI na mtandao wa Internet. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |