• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • China yahimiza ushirikiano wa kimataifa kukabiliana na COVID-19 04-08 19:53
  Tangu kutokea kwa maambukizi ya virusi vya Corona, kwa kufuata mawazo ya jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na msimamo wa kuwajibika, China imetoa taarifa wazi na kwa wakati kuhusu maambukizi ya virusi hivyo, wakati huo huo imeshirikiana na jamii ya kimataifa, na kutoa misaada kwa nchi zinazohitaji.
  • Kipindi maalum cha kujadili changamoto ya virusi vya Corona katika Siku ya Qingming 04-04 07:43

  Tarehe 4, Aprili kwa mwaka huu ni Siku ya Qingming hapa China. Hii ni siku maalum ambayo inatengwa na China kila mwaka kuwakumbuka marehemu. Katika siku hii wachina wote wanapewa mapumziko ya siku moja ili kufanya shughuli za kuwakumbuka marehemu wao wapendwa, mashujaa na watu wengine.

  • Biashara kati ya China na nchi za nje yaanza kufufuka 04-03 10:45
  Wakati biashara ya kimataifa inaathiriwa vibaya na maambukizi ya virusi vya corona, uchukuzi wa mizigo wa reli kati ya Wuhan na miji ya Ulaya umerejeshwa katika hali ya kawaida, huku matunda kutoka nchi za Kusini Mashariki mwa Asia yanasafirishwa kuja kwenye soko la China kwa njia ya reli.
  • Ukarabati wa reli waendelea baada ya treni kuacha njia yake katikati ya China 03-31 09:31
  Ukarabati wa reli unaendelea baada ya treni moja kuacha njia yake kwenye mji wa Chenzhou, mkoani Hunan, katikati ya China, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 127 kujeruhiwa.
  • China yatuliza uchumi wa dunia kwa hatua halisi
   03-30 19:53

  Rais Xi Jinping wa China jana alikagua bandari ya Zhoushan mkoani Zhejiang, ambayo inashika nafasi ya kwanza duniani kwa kupokea na kusafirisha mizigo, na wakati dunia ikikabiliwa na maambukizi ya virusi vya COrona, China imetoa ishara ya kujitahidi kulinda utulivu wa mnyororo wa ugavi duniani.

  • Nia ya rais wa Marekani kutenganisha Marekani na China yaleta matokeo mabaya
   03-30 19:49

  Jarida la the Atlantic la Marekani limechapisha makala iliyoandikwa na Profesa Peter Beinart wa Chuo Kikuu cha Mji wa New York, ikisema kitendo cha rais Donald Trump wa Marekani kutenganisha nchi yake na China kimeleta matokeo mabaya.

  • China yaimarisha kwa pande zote hatua za kutuliza ajira zinazokabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona 03-25 18:29

  Baraza la Serikali la China limesema, ili kukabiliana na athari ya maambukizi ya virusi vya Corona, China imetekeleza hatua za kinga na udhibiti kwa usahihi, kuharakisha makampuni kuanza tena uzalishaji, kuwaongoza wafanyakazi vibarua kupata ajira kwa usalama na utaratibu, pia kuongeza nafasi za ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu, ili kuhakikisha utulivu wa jumla wa ajira.

  • China kuadhibu vikali vitendo vinavyokiuka sheria za ukaguzi wa afya katika forodha 03-24 20:06

  Kutokana na hali mbaya ya kuenea kwa virusi vya Corona duniani, China imetoa kipaumbele katika kukinga maambukizi ya nje katika kukabiliana na ugonjwa huo. Hivi karibuni mahakama kuu, idara kuu ya uendeshaji wa mashtaka, wizara ya usalama wa umma, wizara ya sheria na idara kuu ya forodha nchini China zimetoa kwa pamoja mapendekezo kuhusu uhalifu dhidi ya ukaguzi wa afya katika vituo vya forodha.

  • Nusu ya wagonjwa wa COVID-19 watoka hospitali ya Leishenshan ya Wuhan baada ya kupona 03-18 09:26

  Naibu mkurugenzi wa hospitali ya Leishenshan ya Wuhan Bw. Yuan Yufeng jana kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, karibu nusu ya wagonjwa wa COVID-19 waliopewa matibabu kwenye hospitali hiyo wameruhusiwa kutoka baada ya kupona.

  • Kiwango cha kurejea kwa uzalishaji nchini China chafikia asilimia 90 isipokuwa mikoa michache
   03-17 17:47

  Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China imesema kiwango cha kurejea kwa uzalishaji nchini humo kimefikia zaidi ya asilimia 90 isipokuwa mikoa michache ukiwemo Hubei, na shughuli za uzalishaji za kampuni za nje pia zinarudi katika hali ya kawaida.

  • Rais Xi Jinping asema China itatuma wataalamu zaidi wa matibabu nchini Italia 03-17 09:29

  Rais Xi Jinping wa China amesema, China itatuma wataalamu zaidi wa matibabu nchini Italia, pia itafanya juhudi kadiri iwezekanavyo kutoa vifaa vya matibabu na misaada mingine kwa Italia.

  • Ripoti ya ukiukwaji wa haki za binamu wa Marekani kwa mwaka 2019 03-13 17:01

  Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la Jamhuri ya Watu wa China

  Machi, 2020

  • China yasisitiza ari ya kuondoa umaskini kwa wakati uliopangwa licha ya athari ya COVID-19 03-12 17:34

  Mkurugenzi wa ofisi ya kupambana na umasikini iliyo chini ya Baraza la Serikali la China Bw. Liu Yongfu leo amesema, baada ya juhudi za zaidi ya miaka minne, wilaya zenye umaskini uliokithiri nchini China imepungua na kufikia 52 kutoka 832 mwishoni mwa mwaka 2012. Amesisitiza kuwa, maambukizi ya COVID-19 hayataathiri vigezo, muda na kazi ya kuondoa umaskini, pia hayatabadilisha imani na nia ya China ya kutimiza lengo hilo kwa wakati uliopangwa.

  • China kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuondoa umaskini kwa sifa ya juu 03-10 18:55

  China imepanga kukamilisha kazi ya kuondoa umasikini katika maeneo ya vijijini mwaka huu wa 2020, na hiyo ni ahadi iliyotolewa na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ambayo ni lazima itimizwe kwa wakati uliopangwa. Katika semina ya kuondoa umaskini, rais Xi Jinping wa China ametoa amri mpya ya kupata ushindi katika mapambano dhidi ya umaskini.

  • Vijana wa Wuhan wachangia kazi ya kukabiliana na maambukizi 03-05 17:57

  Leo tarehe 5 Machi ni siku ya vijana wanaojitolea nchini China. Katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona, mbali na madaktari na wauguzi, vijana wa Wuhan, mji ulioathiriwa vibaya na maambukizi hayo, pia wamejitolea kuchangia katika mapambano hayo.

  • Maelfu ya watu wanaojitolea wafanya kazi katika mapambano dhidi ya virusi vya Korona 03-04 18:25

  Wakati madaktari wanajitahidi kuokoa wagonjwa wanaoambukizwa COVID-19, watu wa sekta mbalimbali pia wanasaidia katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo mjini Wuhan. Kuanzia misaada ya matibabu, chakula na bidhaa, na msaada wa kisaikolojia, usafirishaji na huduma za kijamii, maelfu ya watu wanaojitolea wanajibu kwa haraka na kwa makini baada ya Wuhan kufungwa ili kupunguza kuenea kwa virusi hiyo.

  • Wataalamu wa WHO wasema hatua za China za kupambana na COVID-19 zimepata mafanikio 02-25 09:07
  Baada ya kufanya ukaguzi nchini China kwa siku 9, jopo la wataalamu wa China na shirika la afya duniani WHO, jana lilifanya mkutano na waandishi wa habari hapa Beijing. Kiongozi wa watalaamu wa nchi za nje Bw. Bruce Aylward amesema baada ya kufanya ukaguzi kwa makini na kwa pande mbalimbali, watalaamu wanaona hatua zilizochukuliwa na China kupambana na virusi hiyo, zimezuia kwa ufanisi hali ya kuenea kwa virusi hivyo kwa kasi.
  • Maambukizi ya virusi vya korona hayatabadili maendeleo ya muda mrefu ya biashara ya China na nje
   02-24 17:18

  Wizara ya Biashara ya China imesema maambukizi ya virusi vya korona COVIC-19 hayatabadili mwelekeo wa maendeleo ya muda mrefu ya biashara ya China na nchi za nje na nguvu ya ushindani ya China katika kuvutia fedha za kigeni, na China itaendelea kuwa sehemu inayowekezwa zaidi na kampuni za kimataifa.

  • Mradi wa kujitolea kupambana na virusi vya korona mjini Wuhan wavutia zaidi ya watu elfu 10 02-24 10:01

  Mradi wa kujitolea umewavutia watu zaidi ya elfu 10 katika mji wa Wuhan, ambao ni kiini cha maambukizi ya virusi vipya ya korona vinavyosababisha nimonia (COVID-19), mkoani Hubei, China, muda mfupi tu baada kuanzishwa.

  • Afrika haipaswi kuchukuliwa na Marekani kuwa uwanja wa vita dhidi ya China
   02-23 19:55

  Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo hivi karibuni alimaliza ziara nchini Senegal, Angola na Ethiopia na katika Umoja wa Afrika. Hii ni mara yake ya kwanza kufanya ziara katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa Sahara, katika karibu miaka miwili iliyopita, tangu ateuliwe kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako