• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Mkutano wa APEC wa Lima wafungwa, na azimio lililofikiwa limesukuma mbele ujenzi wa eneo la biashara huria la kanda hiyo 2016-11-21
  Mkutano usio rasmi wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki APEC umemalizika huko Lima, mji mkuu wa Peru, na "Azimio la Lima" lililopitishwa kwenye mkutano huo linaonesha kuwa pendekezo la China la kuanzisha eneo la biashara huria la Asia na Pasifiki limepiga hatua moja muhimu.
  • Xi na Obama wakubaliana kudumisha ongezeko zuri na tulivu la uhusiano kati ya China na Marekani 2016-11-20
  Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Marekani Barack Obama wamekutana leo na kukubaliana kudumisha maendeleo mazuri na tulivu ya uhusiano wa pande hizo mbili.
  • Rais wa China awasili Peru kwa ajili ya mkutano wa APEC 2016-11-19
  Rais wa China Xi Jinping amewasili nchini Peru kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ushikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pacific (APEC) na kufanya ziara yake ya kwanza ya kiserikali nchini humo.
  • Chombo cha anga za juu cha Shenzhou-11 charejea duniani 2016-11-18
  Chombo cha anga za juu cha Shenzhou-11 kimerudi duniani saa moja na dakika 59 mchana kwa saa za Beijing. Wanaanga wawili waliokuwa ndani ya chombo hicho wameripotiwa kuwa na hali nzuri, ikiwa ni ishara kuwa safari hiyo ya kupeleka watu kwenda anga za juu imepata mafanikio.
  • "Uchumi wa Mikutano" wahimiza maendeleo ya uchumi 2016-11-18

  Mkutano wa tatu wa Mtandao wa Internet duniani umefanyika leo mjini Wuzhen, mkoani Zhejiang. Huu ni moja kati ya mikutano mikubwa ya kimataifa iliyofanyika nchini China mwaka huu. Waraka wa Mkutano wa China uliochapishwa mwaka 2015 umeeleza kuwa, China inaandaa mikutano zaidi ya milioni 10 kila mwaka na kuleta faida ya kiuchumi zaidi ya yuan trilioni 1. Je, mikutano hiyo inaleta faida hizo kwa njia gani?

  • Uchumi wa China wahimizwa na matumizi ya Mtandao wa Internet 2016-11-18

  Kwa sasa sikukuu nyingi nchini China zinachukuliwa na wafanyabiashara kama fursa ya biashara, hasa wafanyabiashara wenye maduka kwenye mtandao wa Internet maarufu kama Online shopping.

  • Wanaanga wa China kurejea duniani baada ya kumaliza majukumu yao kwenye anga ya juu 2016-11-17
  Chombo cha anga za juu cha Shenzhou-11 kimejitenga na maabara ya anga za juu ya Tiangong-2, na kuanza safari ya kurejea duniani.
  • Internet yawa moja ya maeneo ambayo ni fursa ya maendeleo kwa watumiaji 2016-11-16
  Mkutano kuhusu maendeleo ya internet duniani umefunguliwa leo katika mji wa Wuzhen, Mkoani Zhejiang kusini mwa China. Mkutano huu wa kila mwaka unafanyika wakati China inapata maendeleo ya kasi kwenye teknolojia ya mawasiliano na habari, na inashirikiana na nchi mbalimbali za Afrika kupiga hatua kwenye eneo hilo.
  • China yatazamiwa kutimiza lengo la ongezeko la uchumi la zaidi ya asilimia 6.5 2016-11-14
  Idara ya takwimu ya China imetangaza takwimu mpya kuhusu faida za viwanda, uwekezaji wa mali za kudumu, uendelezaji, uwekezaji, na mauzo ya mali zisizohamishika. Ofisa wa idara hiyo amekadiria kuwa uchumi wa China unatazamiwa kutimiza lengo la ongezeko la uchumi la zaidi ya asilimia 6.5.
  • China yataka madaraka wanayopewa polisi wa kulinda amani yawe ya uwazi na kutekelezeka 2016-11-11
  Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, madaraka wanayopewa polisi wa kulinda amani yanatakiwa kufuata mahitaji na hali halisi ya nchi wanazopelekwa na ya nchi zinazowapeleka, pia yanapaswa kurekebishwa kuendana na mabadiliko ya mazingira ili kutimiza malengo ya operesheni za kulinda amani.
  • Zaidi yuan bilioni 10 zatumika ndani ya dakika 7 tu baada ya kuanza kwa tamasha la kibiashara la Novemba 11 2016-11-11
  Thamani ya biashara ya biadhaa zilizouzwa kwenye mtandao wa internet wakati wa siku ya punguzo kubwa imezidi dola bilioni 1.47 za kimarekani, dakika 7 tu baada ya siku hiyo kuanza.
  • Rais wa China apongeza kufanyika kwa kongamano la kimataifa la majumba ya makumbusho 2016-11-10
  Rais Xi Jinping wa China amepongeza kufunguliwa kwa kongamano la kimataifa kuhusu majumba ya makumbusho lililoanza leo mjini Shenzhen, China.
  • Rais wa China azungumza na wanaanga kwenye maabara ya anga za juu 2016-11-09
  Rais Xi Jinping wa China leo amezungumza na wanaanga wawili waliomo kwenye maabara ya anga za juu ya Tiangong-2 katika Kituo cha Kudhibiti Usafiri wa Anga za Juu cha Beijing.
  • China kuwa na kilowati milioni 58 za umeme wa nyuklia ifikapo mwaka 2020 2016-11-07
  China inatarajiwa kuwa na kilowati milioni 58 za umeme unaotokana na nguvu ya nyuklia itakapofika mwaka 2020, ikiwa ni jitihada za nchi hiyo kupanua mtandao wa nishati safi na ukuaji wa uchumi usiochafua mazingira.
  • China na Afrika zinashirikiana kwenye ulinzi wa ziwa la maji baridi 2016-11-06
  Ziwa Poyang na Ziwa Victoria, maziwa makubwa zaidi ya maji baridi katika nchi ya China na bara la Afrika mtawalia yanalenga kushirikiana zaidi kwenye ulinzi wa mazingira na maendeleo.
  • China yarusha roketi ya Changzheng No.5 2016-11-04
  China imerusha roketi ya Changzheng No 5 yenye uwezo mkubwa zaidi wa kubeba mizigo jana usiku.
  • Maonesho ya 11 ya kimataifa ya safari za anga na anga ya juu yafunguliwa China 2016-11-02
  Maonesho ya 11 ya kimataifa ya safari za anga na anga ya juu yanafanyika mjini Zhuhai mkoani Guangdong kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 6 mwezi Novemba. Maonesho hayo yanafanyika wakati China inaadhimisha miaka 60 ya tangu China ianzishe shughuli zake za safari za anga ya juu.
  • China kutoa mchango mkubwa zaidi katika masuala ya haki za binadamu duniani 2016-10-31
  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema, China itatumia fursa ya kuendelea kuwa mwanachama wa Baraza la Haki za Binadamu, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika masuala ya haki za binadamu duniani.
  • China yaadhimisha miaka 45 tangu irudishiwe kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa 2016-10-26
  Wizara ya mambo ya nje ya China imefanya tafrija ya kuadhimisha miaka 45 tangu irudishiwe kiti chake halali kwenye Umoja wa Mataifa. Mjumbe wa taifa Bw. Yang Jiechi akihutubia maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Beijing amesema katika kipindi cha miaka 45, China imekuwa ni mjenzi wa amani na mchangiaji wa maendeleo ya dunia.
  • Maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa safari ya masafa marefu yafanyika 2016-10-21
  Maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa safari ya masafa marefu ya jeshi la chama cha kikomunisti cha China CPC yamefanyika leo asubuhi hapa Beijing.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako