![]() 02-24 17:18 Wizara ya Biashara ya China imesema maambukizi ya virusi vya korona COVIC-19 hayatabadili mwelekeo wa maendeleo ya muda mrefu ya biashara ya China na nchi za nje na nguvu ya ushindani ya China katika kuvutia fedha za kigeni, na China itaendelea kuwa sehemu inayowekezwa zaidi na kampuni za kimataifa. |
![]() Mradi wa kujitolea umewavutia watu zaidi ya elfu 10 katika mji wa Wuhan, ambao ni kiini cha maambukizi ya virusi vipya ya korona vinavyosababisha nimonia (COVID-19), mkoani Hubei, China, muda mfupi tu baada kuanzishwa. |
Afrika haipaswi kuchukuliwa na Marekani kuwa uwanja wa vita dhidi ya China 02-23 19:55 Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo hivi karibuni alimaliza ziara nchini Senegal, Angola na Ethiopia na katika Umoja wa Afrika. Hii ni mara yake ya kwanza kufanya ziara katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa Sahara, katika karibu miaka miwili iliyopita, tangu ateuliwe kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani. |
![]() China inafanya juhudi zote kuwatibu wagonjwa wa nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vya korona katika mji wa Wuhan ambao ndio kiini cha mlipuko wa virusi hivyo, wakati idadi ya vitanda vya hospitali kwa ajili ya wagonjwa wa COVID-19 imeongezeka na kuzidi elfu 40, huku idadi ya wafanyakazi wa afya waliojitolea kutoka nje ya mkoa, ikizidi elfu 30. |
![]() Chombo cha anga ya juu cha China kinachoitwa Chang'e kimeanza tena kazi yake ya uchunguzi kwa siku ya 15 ya mwandamo baada ya kulala wakati wa usiku wa baridi kali. |
Kushinda COVID-19 kwa niaba ya jumuiya yenye hatma ya pamoja 02-19 17:26 Tangu kutokea kwa maambukizi ya virusi vipya ya korona vinavyosababisha nimonia (COVID-19), watu wa nchi mbalimbali duniani wameeleza kuiunga mkono China. |
![]() Mtaalamu wa magonjwa kwenye mfumo wa kupumua Bw. Zhong Nanshan amesisitiza utafiti wa dawa ya jadi ya kichina TCM kwenye mapambano dhidi ya nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vya korona. |
![]() Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inahimiza Marekani kushughulikia kwa haki kampuni za China na ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili na kuacha vitendo vya uchochezi. |
Adui mkubwa zaidi sio virusi vya korona, bali ni habari za kupotosha zinazoweza kuwatenga watu 02-18 18:36 China bado inajitahidi kupambana na maambukizi ya virusi vipya vya korona vinavyosababisha nimonia (COVID-19). Wakati huohuo, badala ya kutoa misaada, baadhi ya nchi za magharibi zinapaka matope China kutokana na ugonjwa huo. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri inayouliza, "Adui mkubwa zaidi kuliko virusi ni nini". |
![]() Wataalamu wa China wamethibitisha kuwa dawa ya malaria aina ya Chloroquine Phosphate ina ufanisi wa kutibu ugonjwa wa nimonia unaosababishwa na virusi vya korona COVID-19. |
![]() Mjumbe wa Baraza la Taifa la China ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi amesema virusi havina mipaka, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya kazi kwa pamoja kupigana na virusi vipya vya korona (COVID-19). |
![]() Rais Xi Jinping wa China ameagiza madaktari wengine 2,600 wa kijeshi kupelekwa wametumwa mjini Wuhan, ambao umeathirika zaidi na maambukizi ya virusi vipya ya korona COVID-19. |
![]() Idara ya nguvukazi na huduma za jamii ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur, nchini China imesema, mwaka jana imezindua sera kadhaa na kuwasaidia watu 75,000 kuanza biashara zao wenyewe. |
China inaendelea kutoa msaada kwa Afrika ili kuitayarisha kukabili virusi vya korona ikiwa vitatokea barani humo. |
![]() Rais Xi Jinping wa China amemwambia mwenzake wa Marekani Donald Trump kuwa China ina imani na uwezo wa kushinda vita dhidi ya maambukizi ya virusi vipya vya korona. Rais Xi amesema hayo alipoongea na rais Trump leo kwa njia ya simu, na pia amesema China imechukua hatua kamili na kujibu kwa haraka maambukizi hayo. Rais Xi pia amemwahakikishia mwenzake wa Marekani kuwa mustakbali wa ukuaji wa uchumi wa muda mrefu haujabadilika. |
![]() Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi Hua Chunying amesema, hadi kufikia jana mchana, China imepokea msaada wa vitu vya kupambana na maambukizi ya virusi vya korona kutoka kwa serikali za nchi 21 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, na China inapongeza na kushukuru jamii ya kimataifa kwa uelewa, uungaji mkono na msaada wake. Hua amesisitiza kuwa ushindi wa China ndio ni ushindi wa dunia, na China ina uwezo na imani ya kushinda vita hivyo. |
![]() Hadi kufikia saa mbili usiku wa tarehe 2, zaidi ya wahudumu 8000 wa afya kutoka sehemu mbalimbali za China na jeshi la China wamekusanyika mkoani Hubei, China wakisaidia mkoa huo ulioko mstari wa kwanza katika mapambano dhidi ya maambikizi ya virusi vipya vya korana. Jana usiku, hospitali ya Huoshenshan iliyojengwa hivi karibuni ilianza kuwapokea wagonjwa walioambukizwa virusi vya korona. |
![]() China imeikosoa Marekani kwa kuchukua hatua kupita kiasi ambazo ni kinyume cha ushauri wa Shirika la Afya Duniani WHO kuhusiana na maambukizi ya virusi vipya vya korona. |
![]() Kundi la wasomi nchini China limelitaka Bunge la Umma la China kufanyia marekebisho Sheria ya Ulinzi wa Wanyamapori ili kujumuisha usalama wa afya ya jamii katika matumizi ya bidhaa za wanyamapori. Wataalam hao wanataka kutungwa kwa sheria na kanuni mpya kuhusu wanyamapori. Wanasayansi na wasomi wanataka kuona mwisho wa biashara haramu na ulaji wa wanyamapori, na kusema yanahatarisha afya ya umma. |
![]() Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, China inastahili kupongezwa na kuheshimiwa na jamii ya kimataifa kwa kuchukua hatua kali sana katika kudhibiti mlipuko wa virusi vipya vya korona na kuzuia visienee nje ya China. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |