• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Wizara ya biashara ya China yasema hatua ya Marekani ya kuzuia baadhi ya bidhaa kuuzwa kwa China itajidhuru
   06-28 16:17

  Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, Marekani inatumai kuuza bidhaa nyingi zaidi kwa China, ili kupunguza urari mbaya wa biashara, lakini wakati huo huo inazuia baadhi ya bidhaa zake kuuzwa kwa China. Bw. Gao amesema kwa kufanya hivyo Marekani inajidhuru yenyewe.

  • Rais wa China akutana na waziri wa ulinzi wa Marekani 06-27 21:01

  Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. James Mattis. Rais Xi amesema, uhusiano kati ya China na Marekani ni moja ya uhusiano muhimu zaidi kati ya nchi mbili duniani, nchi hizo mbili zina maslahi makubwa ya pamoja katika sekta mbalimbali. Wakati huo huo si rahisi kuepuka kuzungumzia maoni tofauti kati ya nchi hizo mbili, na kusema China ina msimamo thabiti na dhahiri katika suala la mamlaka na ukamilifu wa ardhi.

  • Idara za uendeshaji wa mashtaka za China zakabiliana na uhalifu wa dawa za kulevya kwa juhudi kubwa
   06-26 19:20

  Leo ni siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya. Idara kuu ya uendeshaji wa mashtaka ya China imetoa ripoti ikisema, kuanzia mwezi Januari hadi April mwaka huu, idara za uendeshaji wa mashtaka katika ngazi mbalimbali nchini China zimeidhinisha kuwakamata watu 31,679, na kuwashtaki watu 35,193 waliotuhumiwa kuhusika na uhalifu wa dawa za kulevya, ili kudumisha shinikizo kubwa dhidi ya uhalifu huo.

  • Watu laki 2.4 walazimishwa kuacha kutumia dawa za kulevya nchini China
   06-25 18:45

  Tarehe 26 Juni ni siku ya kimataifa ya kupiga marufuku dawa za kulevya. Naibu waziri wa sheria wa China Bw. Liu Zhiqiang leo hapa Beijing amesema, hivi sasa nchini China kuna watu laki 2.4 wanaolazimishwa kuacha kutumia dawa za kulevya.

  • Rais Xi Jinping asisitiza umuhimu wa sera ya kufungua mlango 06-22 16:45

  Rais Xi Jinping wa China jana hapa Beijing alipokutana na wakuu wa mashirika makubwa ya kimataifa walioko China kuhudhuria mkutano wa kilele wa kamati ya watendaji wakuu duniani, amesema China imetekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango kwa miaka 40, na inaamini kuwa sera hiyo ni njia muhimu ya kuhimiza maendeleo ya taifa.

  • China yaweka "Siku ya mavuno ya wakulima" ili kuhimiza ustawi vijijini 06-21 20:11

  Waziri wa kilimo na vijiji wa China Bw. Han Changfu leo hapa Beijing ametangaza kuwa, kuanzia mwaka huu China itaweka siku ya nusu ya majira ya mpukutiko (Autumnal Equinox) kwa kalenda ya kilimo ya China kuwa "Sikukuu ya mavuno ya wakulima ya China", ambayo ni siku ya kwanza inayowekwa na serikali ya China kwa ajili ya wakulima.

  • Gazeti la China lasema rais wa Marekani anacheza kamari kwa kutumia maslahi ya wamarekani 06-19 18:56

  Gazeti la Global Times la China limetoa makala likisema rais Donald Trump wa Marekani anacheza kamari na China kwa kutumia maslahi ya wamarekani. Hii ni kufuatia taarifa aliyoitoa jana kupitia Ikulu ya Marekani akiiagiza Ofisi ya wajumbe wa biashara ya Marekani, kuangalia uwezekano wa kuongeza ushuru wa forodha kwa asilimia 10 kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200.

  • Wachina wa sehemu mbalimbali washerehekea Sikukuu ya Duan Wu 06-18 18:53

  Leo tarehe 5 ya mwezi wa tano kwa Kalenda ya kilimo ya China ni sikukuu ya Duan Wu nchini China, ambapo watu wa sehemu mbalimbali wanasherehekea sikukuu hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kufanya mashindano ya mbio za mashua ya Dragoni, kutengeneza chakula cha Zongzi, kutalii kwa magari ya n.k.

  • China yatarajia kuwa na wachangiaji damu 15 kwa kila watu elfu moja ifikapo mwaka 2020 06-18 08:19
  Kamati ya afya ya taifa ya China imesema China itaendelea na juhudi za kuhamasisha umma kuchangia damu na kutarajia kuwa na wachangia damu 15 kati ya kila watu elfu moja ifikapo mwaka 2020.
  • China ina imani ya kupata ushindi kwenye mapambano dhidi ya kujilinda kibiashara kwa Marekani 06-16 19:24

         Tarehe 15 mwezi Juni serikali ya Marekani ilitangaza orodha ya bidhaa za China zitakazoongezwa asilimia 25 ya ushuru wa forodha, ambazo inahusisha bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50 zinazoagizwa kutoka China kwa mwaka. Hatua hii imekiuka na kuharibu sana maslahi halali ya China na wananchi wake. Halafu serikali ya China ilitoa taarifa ikitangaza kuongeza asilimia 25 ya ushuru wa forodha kwa bidhaa za aina 659 za Marekani zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50.

  • China yaharakisha kujenga mfumo wa muamana
   06-15 17:32

  China inaharakisha kujenga mfumo wa muamana. Ofisa wa idara kuu ya maendeleo na mageuzi ya China leo hapa Beijing amesema, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei, mahakama zimetangaza orodha ya watu milioni 10.89 waliofanya makosa ya muamana, na kati yao milioni 2.54 walitekeleza wajibu wao ili kuepuka kuadhibiwa. Baadaye China itaendelea kusukuma mbele ujenzi wa mfumo wa jumla wa muamana, kwa kuharakisha kujenga mfumo mpya wa usimamizi, kuimarisha ujenzi wa mfumo wa muamana katika sekta muhimu, na kukamilisha utaratibu wa kutuza na kutoa adhabu.
  • Uwekezaji wa China katika nchi za nje waongezeka kwa kasi katika miezi mitano iliyopita
   06-14 17:15

  Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng leo kwenye mkutano na waandishi wa habari ametoa takwimu mbalimbali za uchumi na biashara, akisema katika miezi mitano iliyopita uwekezaji wa China katika nchi za nje umefikia dola za kimarekani bilioni 47.89, ambalo ni ongezeko la karibu asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, wakati huo huo China imevutia uwekezaji wa nchi za nje wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 52.66, ambalo ni ongezeko la asilimia 1.3.

  • China kujenga utaratibu wa kurekebisha bima ya malipo ya uzeeni kati ya mikoa mbalimbali
   06-13 17:50

  China itajenga utaratibu wa kurekebisha bima ya malipo ya uzeeni kati ya mikoa mbalimbali, ili kuhakikisha wazee wa sehemu tofauti wanapata bima wanayostahili kwa wakati.

  • Shughuli za hakimiliki za ujuzi nchini China zaendelea kwa utulivu
   06-12 16:58

  Kituo cha utafiti wa maendeleo ya shughuli za hakimiliki za ujuzi cha China, leo kimetoa ripoti ikisema mwaka jana China ilipata maendeleo yenye utulivu katika shughuli za hakimiliki za ujuzi, na kusonga mbele duniani.

  • China yaanza wiki ya kueneza kubana matumizi ya nishati
   06-11 18:19

  Wiki ya 28 ya kueneza kubana matumizi ya nishati imeanza rasmi leo, na kauli mbiu ya mwaka huu ni "kubana matumizi ya nishati na kuhifadhi anga ya kibuluu". Maofisa wa kamati kuu ya maendeleo na mageuzi ya China na wizara ya uhifadhi wa mazingira ya China wameeleza kuwa, katika miaka mitano iliyopita, kiwango cha matumizi ya nishati katika uzalishaji mali kimepungua kwa asilimia 20, na kasi ya ongezeko la utoaji wa Carbon Dioxide imepungua.

  • Mkutano wa 18 wa kamati ya viongozi wa SCO wafanyika mjini Qingdao, China
   06-10 17:22

  Mkutano wa 18 wa kamati ya viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai SCO umefanyika leo mjini Qingdao, China. Baada ya kumaliza ajenda zote, viongozi waliohudhuria mkutano huo walikutana na waandishi wa habari, huku rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba ya kujulisha matokeo ya mkutano huo.

  • Eneo la kujiendeleza kiuchumi la Kashgar latoa mchango kwa mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za jumuiya ya SCO 06-08 17:11

  Kutokana na kuungwa mkono na sera nafuu za taifa, eneo la kujiendeleza kiuchumi la Kashgar mkoani Xinjiang limekuwa moja ya maeneo muhimu ya maendeleo ya uchumi na biashara yanalovutia uwekezaji, teknolojia na watu wenye ujuzi wa ndani na nje ya nchi. Eneo hilo limeonesha umuhimu mkubwa katika kuhimiza ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, na mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai SCO.

  • Rais Putin wa Russia azungumzia uhusiano kati ya Russia na China 06-06 06:48
  Kabla ya kufunga safari ya kuja China kuhudhuria Mkutano wa kilele wa Baraza la viongozi wa nchi wanachama wa Shirika la ushirikiano wa Shanghai SCO na kufanya ziara ya kitaifa nchini China, rais Vladimir Putin wa Russia amefanyiwa mahojiano na mkuu wa Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha Taifa cha China Bw. Shen Haixiong, na kuzungumzia uhusiano kati ya Russia na China, na mustakabali wa SCO baada ya kupanuliwa kwake.
  • China yapongeza taarifa ya pamoja ya Russia na Korea Kaskazini kuhusu kutokuwepo kwa silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea 06-01 19:20

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema China inapongeza taarifa iliyotolewa na Russia na Korea Kaskazini kuhusu kutokuwepo kwa silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea, na kuitaka Russia kuendelea na mchakato mzuri wa kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea kwa njia ya kisiasa.

  • China kujenga mfumo wa kuwasaidia watoto walemavu kupona
   06-01 17:06

  Kuanzia tarehe mosi, Oktoba mwaka huu, China itajenga mfumo wa kuwasaidia watoto walemavu kupona, na kutoa msaada wa gharama za upasuaji, vifaa na huduma za mazoezi kwa watoto walemavu wenye umri wa chini ya miaka 6 kutoka familia maskini.

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako