![]() Mwaka 2019 ni mwaka wa 6 tangu pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" litolewe. Katika miaka 6 iliyopita, China imesaini nyaraka 197 za ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na nchi 137 na mashirika 30 ya kimataifa. |
![]() 12-27 17:06 Rais Xi Jining wa China amehudhuria mikutano minne ya kimataifa iliyofanyika nchini China, na shughuli zaidi ya mia moja za pande mbili au pande nyingi, na kufanya ziara saba katika nchi za nje katika mwaka huu. |
Siasa ya kifedha chanzo muhimu cha pengo la kisiasa na kijamii nchini Marekani 12-26 18:09 Taasisi ya utafiti wa haki za binadamu ya China leo imetoa makala yenye kichwa cha "siasa ya kifedha yaonesha ukosefu wa demokrasia nchini Marekani", na kudhihirisha kuwa siasa ya kifedha ni sababu muhimu ya pengo la kisiasa na kijamii nchini humo. |
China yasisitiza umuhimu wa misaada ya kijamii katika vita dhidi ya umaskini 12-25 16:39 Baraza la Serikali la China leo limekabidhi ripoti kwa mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, ili kujulisha maendeleo ya utoaji wa misaada ya kijamii, na vita dhidi ya umaskini. |
Habari za kupotosha ukweli huwa na madhumuni maovu 12-25 09:38 Hivi karibuni aliyekuwa mwanahabari wa Uingereza aliyewahi kutumikia kifungo hapa nchini China Peter Humphrey alitoa makala kwenye gazeti la Sunday Times, akisema msichana wa London mwenye miaka sita kwenye kadi ya Krismasi aliyonunua kutoka kwenye supamaketi ya Tesco, aligundua maandishi ya kiingereza yanayosema "Sisi ni wafungwa wa kigeni kwenye gereza la Qingpu mjini Shanghai, tumelazimika kufanya kazi za sulubu. Tafadhali tusaidie na kuripoti kwa mashirika ya haki za binadamu." Baadaye, habari hiyo ya ajabu iliripotiwa na vyombo vingi vya habari vya Magharibi ikiwemo BBC na Sky News, vikishambulia na kuipaka matope China. |
![]() 12-24 20:50 Mwenyekiti wa kampuni ya Uchapishaji ya Zhejiang Yunguang Bw. Lu Yunbiao amekana tuhuma za kulazimisha wafanyakazi kuchapisha kadi za Krismas ambazo husambazwa katika maduka makubwa ya manunuzi ya Tesco ya Uingereza, na kusema madai hayo ni ya uongo. |
China, Japan na Korea ya Kusini zahimizwa kushirikiana kuzidisha ustawi na utulivu wa kikanda 12-24 19:08 Mkutano wa nane wa viongozi wa China, Japan na Korea ya Kusini umefanyika leo mjini Chengdu, China, na kuhudhuriwa na waziri mkuu wa China Li Keqiang, rais Moon Jae-in wa Korea ya Kusini na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe. Kwenye mkutano huo Bw. Li amehimiza nchi hizo kushirikiana ili kuzidisha ustawi na utulivu wa kanda ya Asia ya mashariki. |
![]() 12-24 19:07 Mwenyekiti wa kampuni ya Uchapishaji ya Zhejiang Yunguang Bw. Lu Yunbiao amekana tuhuma za kulazimisha wafanyakazi kuchapisha kadi za Krismas ambazo husambazwa katika maduka makubwa ya manunuzi ya Tesco ya Uingereza, na kusema madai hayo ni ya uongo. |
![]() 12-23 18:13 Meli ya "Safina ya Amani" ni meli ya kwanza ya hospitali ya jeshi la majini la China. Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita tangu ijiunge na jeshi la China, meli hiyo imetembelea nchi 43 na kutoa huduma za matibabu kwa watu laki 2.3 wa nchi hizo. |
![]() 12-10 17:59 Huu ni mwaka wa 20 tangu Macao kurudi China. Katika miaka hiyo, kikosi cha ulinzi cha China kwenye mkoa huo wenye utawala maalumu kimefuata kithabiti sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" na sheria husika, na kutekeleza majukumu ya kulinda mamlaka ya taifa, utulivu na ustawi wa Macao. |
Wakazi wa Xinjiang wailaani Marekani kwa kupitisha mswada kuhusu mkoa huo 12-09 19:38 Hivi karibuni, Baraza la wawakilishi la bunge la Marekani lilipitisha "mswada wa mwaka 2019 wa sera ya haki za binadamu za Wauyghur". Kitendo hiki kimelaumiwa na wakazi wa mkoani Xinjiang, ambao wamesema hakuna nguvu yoyote inayoweza kuzuia maendeleo ya mkoa huo, na usumbufu na hila yoyote vitazidi kuongeza mshikamano wa watu milioni 25 wa mkoa huo. |
![]() 11-27 18:16 China leo imetoa ripoti ya mwaka 2019 kuhusu sera na hatua zake za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Naibu waziri wa mazingira ya China Bw. Zhao Yingmin amesema, tangu mwaka jana, China imepunguza utoaji wa hewa yenye Carbon kwa mfululizo, na itaendelea kudhibiti utoaji wa hewa zinazoweza kuongeza joto duniani, na kuhimiza maendeleo yasiyoleta uchafuzi. |
China yatoa waraka unaoweka wazi ukosefu wa usawa wa kijinsia nchini Marekani 11-26 16:59 Kituo cha Elimu ya Haki za Binadamu cha China kimetoa waraka uliopewa jina la "Suala la ukosefu wa usawa wa jinsia nchini Marekani ni kikwazo kikubwa cha kutimiza haki za wanawake nchini humo" hii leo. Waraka huo umesema, Marekani bado haijafanyia marekebisho Mkataba wa Kuondoa Aina Zote za Kutengwa kwa Wanawake, ambao ni moja ya mikataba mikuu ya haki za binadamu nchini humo, na wala haijasuluihisha tatizo kubwa la nchi hiyo la ukosefu wa usawa wa kijinsia, na kuongeza kuwa, jambo hili limezuia kwa kiasi kikubwa kutimia kwa haki za wanawake nchini Marekani. |
![]() 11-25 19:42 China imetoa waraka wa "mapendekezo ya kuimarisha ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu" ili kupanga kazi ya kulinda haki hizo katika zama mpya. Mamlaka ya ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu ya China imesema, China inaheshimu na kulinda hakimiliki za kiubunifu za nchi za nje, pia inataka nchi za nje zilinde haki hizo za China. |
![]() China imerusha satellite mbili za mambo ya habari na kuingia kwenye njia yake kwa mafanikio. Satellite hizo mbili kwa ajili ya mawasiliano duniani, zikiwa ni za miradi ya ushirikiano wa kibiashara wa kimataifa. |
![]() 11-13 16:58 Mkutano wa 11 wa viongozi wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zinazounda kundi la BRICS utafanyika kwa siku mbili kuanzia leo nchini Brazil, ukiwa na kauli mbiu ya "Ukuaji wa uchumi: Kuanzisha mustakabali wenye uvumbuzi". Wakuu wa makampuni ya nchi za kundi hilo walioshiriki kwenye Maonesho ya pili ya Kimataifa ya Uingizaji wa Bidhaa za nje ya China wanatumai kuwa, ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya nchi hizo utaimarika siku hadi siku. |
![]() Wageni zaidi ya 1,000 kutoka nchi 79 wamekutana hapa Beijing kwenye Mkutano wa Mtandao wa Nishati Duniani Mwaka 2019 na Mkutano wa Nishati na Umeme kati ya China na Afrika, wakijadili ushirikiano kuhusu maendeleo endelevu kwenye sekta ya nishati. |
![]() 11-01 18:13 Mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC umefungwa. Kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika leo hapa Beijing, maofisa wandamizi wa serikali ya China wamesema, mkutano huo una maana kubwa, kwani umejibu swali muhimu kwamba, China inapaswa kushikilia, kuimarisha, kukamilisha na kuendeleza nini katika mfumo na utawala wa kitaifa. |
![]() 10-31 18:22 Wizara ya maendeleo ya viwanda na teknolojia ya habari ya China na Kampuni tatu za upashanaji habari za China leo kwenye maonesho ya kimataifa ya teknolojia za upashanaji habari zimezindua rasmi matumizi ya kibiashara ya teknolojia ya 5G, ikimaanisha kuwa zama ya 5G imeanza nchini China. |
![]() Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo hapa Beijing amekutana na makamu wa rais wa Afrika Kusini David Mabuza ambaye yuko ziarani nchini China na kuhudhuria mkutano wa 7 wa wajumbe wote wa kamati ya pande mbili za China na Afrika Kusini. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |