• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • China kusukuma mbele mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa kazi za kukabiliana na hali ya dharura
   01-22 18:23

  Maofisa wa wizara ya usimamizi wa kazi ya kukabiliana na hali ya dharura wamesema, wizara hiyo iliyoanzishwa mwaka jana imerekebisha idara husika, na imejenga mfumo wa kimsingi wa usimamizi wa kazi za kukabiliana na hali ya dharura wenye umaalumu wa kichina na kuweza kikidhi mahitaji ya zama mpya, na mwaka huu wataendelea kusukuma mbele mageuzi ya mfumo huo, na kupunguza hasara kutokana na maafa kadiri iwezavyo.

  • Wizara ya mambo ya nje ya China yakanusha ripoti za CNN kuhusu yaliyotokea wanawake wa kabila la Wauygur 01-22 08:56
  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, baada ya uchunguzi wa makini, China imethibitisha kuwa ripoti zilizotolewa na Shirika la habari la Marekani CNN kuhusu mwanamke mmoja wa kabila la wauygur aliyefungwa katika gereza la Urumqi kushuhudia vifo vya wanawake wengine tisa wauygur na kifo cha mtoto wake katika hospitali ya watoto ya Urumqi, ni "uongo mtupu wa makusudi".
  • GDP ya China ya mwaka jana yaongezeka kwa asilimia 6.6
   01-21 17:37

  Mkuu wa Idara Kuu ya Takwimu ya China Bw. Ning Jizhe amesema, takwimu za awali zinaonesha kuwa, mwaka jana pato la taifa GDP la China liliongezeka kwa asilimia 6.6 ikilinganishwa na mwaka 2017. Amesema mwaka huu China ina msingi, mazingira, imani na uwezo wa kudumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uchumi.

  • Kampuni ndogondogo nchini China zina fursa ya kupunguza kodi zao 01-18 17:11

  Mwanzoni mwa mwaka huu, serikali ya China ilitangaza sera mpya mfululizo ili kutia nguvu ya uhai sokoni, na kukabiliana na shinikizo la kupungua kwa ongezeko la uchumi. Sera iliyotangazwa kwanza ni kupunguza kodi za kampuni ndogondogo ili kuzinufaisha, ambayo itatekelezwa kwa miaka mitatu. Sera hiyo imechukuliwa kuwa mwanzo wa sera mfululizo zitakazotekelezwa na serikali ya China mwaka huu katika kupunguza kodi, na itahimiza maendeleo ya uchumi wa China.

  • China ni mwenzi asiyekosekana wa Afrika katika kutimiza "Ajenda ya Mwaka 2063"
   01-18 10:39

  Mkutano wa 32 wa kilele wa Umoja wa Afrika utafanyika mwezi ujao mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mjumbe wa kudumu wa umoja huo nchini China Bw. Rahmat Mohamed Osman jana alipohojiwa na waandishi wetu wa habari alisema, China inatekeleza kihalisi ahadi yake ya kuiunga mkono Afrika kutimiza amani na maendeleo, na ni mwenzi asiyekosekana wa Afrika katika kutimiza "Ajenda ya Mwaka 2063".

  • China yajaribu kuondoa mzizi wa ugaidi kwa mafunzo ya ajira mkoani Xinjiang
   01-17 12:23

  Waandishi wa habari waliohudhuria awamu ya 7 ya "Safari ya Watu Mashuhuri wa Nchi za Njia ya Hariri nchini China" hivi karibuni walitembelea kituo cha mafunzo ya ajira cha mji wa Kashi kusini mwa mkoa unaojiendesha wa kabila la wauyghur wa Xinjiang. Wageni hao kutoka Uturuki, Misiri, Afghanistan, Pakistan, Bangladesh na Sri Lanka walibadilishana maoni kwa kina na wanafunzi na walimu wa huko.

  • China kufungua mlango zaidi katika sekta ya uzalishaji 01-11 17:18

  Waziri wa viwanda na teknolojia ya habari wa China Bw. Miao Wei, amesema China itaboresha mazingira kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya uzalishaji, kwa kuendelea kupunguza ushuru na gharama, na kufungua mlango zaidi, ili kuharakisha maendeleo yenye ubora wa juu ya sekta hiyo.

  • Matokeo mazuri ya mwisho kupatikana kutokana na juhudi za pamoja za China na Marekani
   01-10 17:00

  Mazungumzo ya ngazi ya naibu mawaziri kati ya China na Marekani kuhusu suala la uchumi na biashara yalifungwa jana mjini Beijing. Haya ni mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya pande hizo mbili kwa ajili ya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili nchini Argentina.

  • Viongozi wa kisiasa na kibiashara wa China na Marekani wataka nchi hizo mbili ziendelee kukuza ushirikiano
   01-09 17:02

  Tafrija ya mwaka 2019 ya shirikisho kuu la wafanyabiashara wa China nchini Marekani ilifanyika tarehe 7 usiku nchini Marekani. Viongozi wa kisiasa na kibiashara wa China na Marekani kwa kauli moja wameona kuendelea kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali, ni jambo muhimu kwa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi zao na hata kwa amani na usalama wa duniani.

  • China yatoa tuzo kwa wanasayansi waliotoa mchango muhimu
   01-08 19:35

  Mkutano wa kutoa tuzo za sayansi na teknolojia ulioandaliwa na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Serikali la China umefanyika leo hapa Beijing. Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa chama na serikali akiwemo rais Xi Jinping, pamoja na wanasayansi waliotoa mchango muhimu kwa ajili ya maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini China.

  • China kuongeza nguvu katika kulinda haki miliki za kiubunifu
   01-07 18:24

  Mkuu wa Idara Kuu ya Haki Miliki za Kiubunifu ya China Bw. Shen Changyu amesema mwaka jana idadi ya hataza zilizoandikishwa nchini China ilizidi milioni 1.6, likiwa ni ongezeko la karibu asilimia 20 ikilinganishwa na mwaka 2017. Amesema mwaka huu China itaongeza nguvu katika kulinda haki miliki za kiubunifu, na kuzidisha ushirikiano wa kimataifa.
  • Fanya kazi kwa bidii, kimbia kwa kasi ya kichina
   01-01 10:39

  Rais Xi Jinping wa China jana alitoa hotuba ya kukaribisha mwaka mpya, akifanya majumuisho ya mafanikio ya China katika mwaka 2018, na kuwahamasisha wachina wote kuendelea kuchapa kazi ili kutimiza ndoto, na pia kueleza udhati na wema wa China katika kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja duniani.

  • Mfumo wa utambuzi wa mahali wa Beidou No. 3 wa China waanza kutoa huduma kwa dunia nzima
   12-28 16:29

  Msemaji wa mfumo wa utambuzi wa mahali kupitia satalaiti wa Beidou No. 3 wa China Bw. Ran Chengqi ametangaza kuwa, mfumo huo umekamilika kimsingi, na kuanza kutoa huduma kwa dunia nzima.

  • Maeneo ya sekta ya teknolojia mpya na za hali ya juu yahimiza maendeleo yenye ubora zaidi nchini China
   12-27 17:10

  Huu ni mwaka wa 30 tangu China ianze kujenga maeneo ya sekta ya teknolojia mpya na za hali ya juu. Katika miaka 30 iliyopita, maeneo hayo yameendelea kwa kasi, na kutoa matokeo mengi ya teknolojia na bidhaa mpya.

  • China yapongezwa kwa kulinda usalama wa ghuba ya Aden
   12-26 17:20

  Katika miaka 10 iliyopita, manowari za China zimetoa ulinzi kwa ajili ya meli za nchi mbalimbali zilizopita ghuba ya Aden, na kusifiwa na jumuiya ya kimataifa. Ghuba ya Aden ni njia pekee ya kuunganisha bahari ya Hindi na Bahari Nyekundu, na inapitiwa na meli zaidi ya elfu kumi kwa mwaka. Kutokana na mashambulizi ya maharamia, ghuba hiyo ni moja kati ya sehemu yenye hatari zaidi duniani.

  • China kuchangia zaidi bajeti ya Umoja wa Mataifa
   12-25 17:02

  Baraza kuu la Umoja wa Mataifa hivi karibuni lilipitisha azimio la kuongeza mchango wa China kwa bajeti ya kawaida ya umoja huokutoka asilimia 7.9 na kuwa asilimia 12.01, na bajeti ya kulinda amani ya umoja huo kutoka asilimia 10.2 kuwa asilimia 15.2, na China itakuwa mchangiaji mkubwa wa pili kwa bajeti ya Umoja wa Mataifa.

  • Mradi wa Kaskazini Tatu wa hifadhi za misitu wa China wainua kiwango cha ardhi kufunikwa na misitu hadi asilimia 13.57 12-24 18:55
  Mwaka huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza mradi wa Kaskazini Tatu wa kujenga hifadhi za misitu katika sehemu za kaskazini, kaskazini mashariki na kaskazini magharibi. Ripoti ya tathimini ya jumla ya mwaka 40 ya mradi huo imetolewa leo, na kuoneysha kuwa, hadi sasa mradi huo umejenga misitu yenye ukubwa wa hekta milioni 30.143, kiwango cha ardhi kufunikwa na misitu imefikia asilimia 13.57 kutoka asilimia 5.05.
  • Uchumi wa China kukua kwa utulivu
   12-24 16:53

  Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ilifanya mkutano kuhusu kazi ya uchumi wiki iliyopita, ili kufanya majumuisho ya kazi ya uchumi kwa mwaka huu, na kupanga kazi ya mwakani.

  • China yafanya maadhimisho makubwa ya miaka 40 tangu ya sera ya mageuzi na kufungua mlango 12-18 12:26
  Mkutano wa maadhimisho ya miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango umefanyika leo mjini Beijing. Rais Xi Jinping ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na mwenyekiti wa Baraza la kijeshi la kamati hiyo amehudhuria na kuhutubia mkutano huo.
  • Kuielewa China kutoka pande tatu, Mwaka huu ni madhimisho ya miaka 40 ya utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango wazi ya China, jumuiya ya magharibi imetoa maswali mengi kuhusu "China itaelekea wapi katika siku za baadaye?" 12-18 10:37

  Mwaka huu ni madhimisho ya miaka 40 ya utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango wazi ya China, jumuiya ya magharibi imetoa maswali mengi kuhusu "China itaelekea wapi katika siku za baadaye?", "China ni mwenzi au mshindani?","China ni fursa au changamoto?" Kwa kukabiliana na hali hiyo, mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu "Kuielewa China" umefanyika hapa Beijing.

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako