• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Jack Ma astaafu kama mwenyekiti wa Alibaba 09-11 09:10

  Jack Ma amestaafu rasmi kama mwenyekiti wa kampuni ya Alibaba na kukabidhi nafasi hiyo kwa Mkurugenzi mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Daniel Zhang. Katika barua yake aliyotoa kwa umma Septemba, 10, mwaka jana, bilionea huyo ambaye pia ni mwanzilishi wa kampuni hiyo kubwa ya biashara ya mtandaoni alisema Alibaba kamwe haimilikiwi naye peke yake, lakini atakuwa nayo daima.

  • China Mobile yajenga vituo elfu 20 vya 5G 09-06 09:43
  Kampuni kubwa zaidi ya simu nchini China, China Mobile imetangaza kujenga vituo zaidi ya elfu 20 vya 5G katika miji 52 muhimu nchini humo. Na inapanga kutoa huduma za kibiashara za 5G katika miji zaidi ya 50 kabla ya mwishoni mwa mwaka 2019.
  • China yakana kuwa chanzo kikuu cha Fentanyl nchini Marekani
   09-03 18:11

  Ofisi kuu inayopambana na dawa za kulevya ya China leo imetangaza kuwa, tangu China ianze kuweka dawa ya Fentanyl chini ya usimamizi wa serikali tarehe mosi Mei, haijagundua uhalifu wa magendo ya dawa hiyo. Naibu mkurugenzi wa tume ya kitaifa ya kupambana na dawa za kulevya ya China Bw. Liu Yuejin amesisitiza kuwa, China si chanzo kikuu cha dawa ya Fentanyl nchini Marekani.

  • China yatoa waraka wa kwanza wa usalama wa nyukilia 09-03 18:10

  Ofisi ya habari ya baraza la serikali la China leo imetoa waraka wa kwanza wa "Usalama wa Nyukilia nchini China". Waraka huo unasema China imepitisha nyaraka zote za kimataifa kuhusu usalama wa nyukilia, na kuunga mkono juhudi za pande nyingi za kuimarisha usalama huo. Pia itaendelea kuhimiza ushirikiano wa kimataifa, na ujenzi wa mfumo wa kimataifa wa usalama wa nyukilia.

  • Chombo cha China Chang'e-4 chaendelea na kazi kwa siku ya 9 katika Mwezi 08-26 09:00
  Chombo cha uchunguzi cha China Chang'e-4 kimeendelea na kazi kwa siku ya tisa katika sehemu ya nyuma ya Mwezi baada ya "kulala" katika usiku wa baridi kali.
  • Kenya yatarajia kuiuzia China maparachichi mabichi
   08-23 18:22

  Balozi wa Kenya nchini China Bi. Sarah Serem amesema, Kenya inafanya mazungumzo na China kuhusu kuiuzia maparachichi mabichi, baada ya kutambua makubaliano ya zamani hayawezi kuwanufaisha wakulima wadogo wa Kenya.

  • Balozi wa Kenya nchini China atarajia injini mpya ya ushirikiano kati ya nchi hizo
   08-23 18:21

  Balozi wa Kenya nchini China Sarah Serem amesema, Kenya inatumai kujifunza na kuiga kwa makini uzoefu wa maendeleo ya China, na kuleta injini mpya kwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

  • China kujenga mji wa Shenzhen kuwa eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China
   08-22 17:02

  Serikali ya China imetoa waraka wa kuunga mkono kuujenga mji wa Shenzhen kuwa eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China, na kuutaka mji huo kuhimiza ujenzi wa eneo kubwa la ghuba ya Guangdong, Hong Kong na Macao.

  • Jinsi tetemeko kubwa la ardhi la 2008 lilivyowapelekea Wachina kufanya juhudi za pamoja kwa kujijenga upya 08-22 10:24

  Mei 12, mwaka 2008, tetemeko kubwa la ardhi lilitokea kwenye Wilaya ya Wenchuan mkoani Sichuan, kusini magharibi mwa China, na kusababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi, pamoja na uharibifu mkubwa wa mali, miundombinu, viwanda, kilimo na huduma za kijamii, katika mikoa ya Sichuan, Gansu na Shaanxi.

  • Maonesho ya kimataifa ya vitabu ya Beijing yalenga Maadhimisho ya miaka 70 tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya watu wa China 08-22 09:15
  Maonesho ya 26 ya kimataifa ya vitabu ya Beijing yamefunguliwa jana na yanalenga Maadhimisho ya Miaka 70 tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Kampuni zaidi ya 2,600 zinashiriki kwenye maonesho hayo, zikionesha vitabu zaidi ya laki 3.
  • Shanghai yavumbua njia ya kuvutia watu wenye uwezo ili kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu
   08-21 16:51

  Mji wa Shanghai ni mtangulizi wa utekelezaji wa sera ya mageuzi na kufungua mlango na maendeleo yenye sifa ya juu. Wakati mji huo unahimiza maendeleo yenye sifa ya juu, pia unafanya majaribio na uvumbuzi katika nyanja mbalimbali, haswa namna ya kuvutia watu wenye uwezo.

  • Juhudi za China katika kutokomeza umaskini uliokithiri zaonyesha mafanikio 08-21 13:30

  Tangu sera ya mageuzi na kufungua mlango ilipoanza kutekelezwa mwishoni mwa mwaka 1978, China imepata mafanikio makubwa katika kupunguza umaskini. Kwa mujibu wa vigezo vya kimataifa vya kupunguza umaskini, idadi ya watu wa China wanaokumbwa na umaskini imepungua kwa kiasi kikubwa.

  • China kujenga mji wa Shenzhen kuwa eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China
   08-19 18:14

  Serikali ya China imetangaza kuunga mkono kuujenga mji wa Shenzhen kuwa eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China, ili kusukuma mbele sera ya mageuzi na kufungua mlango, na kutekeleza vizuri zaidi mkakati wa eneo kubwa la ghuba ya Guangdong, Hong Kong na Macao.

  • Uchumi wa China kwa mwezi wa Julai waendelea kukua kwa utulivu
   08-14 17:12

  Takwimu zilizotolewa leo na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, mwezi Julai uchumi wa China umeendelea kukua kwa kasi inayofaa. Katika kipindi kijacho, China itaimarisha uhamasishaji wa uvumbuzi kwa uchumi, na kuongeza uhai wa soko, ili kuhimiza uchumi wa China kuendelea vizuri kwa utulivu na mfululizo.

  • Gazeti la The Wall Street Journal la Marekani laonya sera isiyo sahihi ya kibiashara itasababisha kushuka kwa uchumi wa nchi hiyo 08-09 17:25

  Gazeti la The Wall Street Journal la Marekani limetoa tahariri inayoonya juu ya sera isiyo sahihi ya kibiashara iliyotolewa na serikali ya rais Donald Trump wa Marekani, na kusema itasababisha kushuka kwa uchumi wa nchi hiyo.

  • China kupanua masoko ya vijijini 08-05 16:59
  Mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuhusu kazi za uchumi kwa nusu ya pili ya mwaka huu uliofanyika wiki iliyopita umetaka kupanua soko katika sehemu za vijijini. Wasomi nchini China wanasema, wakati China inapopanua mahitaji ya ndani ya nchi, hadhi ya masoko ya vijijini imeanza kuzingatiwa zaidi.
  • Jumuiya ya kimataifa yasifu waraka uliotolewa na China kuhusu mambo ya kihistoria ya Xinjiang
   07-23 17:11

  Ofisi ya habari ya baraza la serikali ya China imetoa waraka wa "masuala ya kihistoria ya mkoa wa Xinjiang", na kukosoa makundi yenye uhasama ya ndani na nje ya China kwa kupotosha historia na ukweli wa mambo ya mkoa huo. Watu wa hali mbalimbali wa jumuiya ya kimataifa wamepongeza waraka huo, wakisema mkoa wa Xinjiang ni sehemu isiyotengeka ya China, na kutokana na sera nzuri ya makabila, mkoa huo umepata ustawi na maendeleo ya mfululizo.
  • Rais wa China azungumza na mrithi wa ufalme wa Abu Dhabi wa Falme za Kiarabu
   07-22 16:45

  Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amefanya mazungumzo na mrithi wa ufalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan ambaye yupo ziarani nchini China. Rais Xi amesema, uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni mfano wa kuigwa wa ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi zenye utamaduni na mtindo tofauti na kutoka kwenye kanda tofauti, na China inapenda kushirikiana na Falme za Kiarabu kuhimiza uhusiano huo kupata mafanikio mapya, ili kuwanufaisha wananchi wao.

  • Wawakilishi wa Afrika wasifu umuhimu wa kiujenzi wa China katika sekta ya amani na usalama 07-17 19:56
  Mkutano wa kwanza wa amani na usalama kati ya China na Afrika umefunguliwa tarehe 15 mjini Beijing, na kuhudhuriwa na mawaziri wa ulinzi na wanadhimu wakuu 15 wa majeshi kutoka nchi za Afrika zikiwemo Cameroon na Ghana, wajumbe waandamizi wa nchi 50 za Afrika na idara za ulinzi za Umoja wa Afrika, pamoja na wawakilishi wa jeshi la China. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, wajumbe kutoka Afrika wamesifu mchango wa kiujenzi uliotolewa na China katika sekta ya amani na usalama.
  • Nchi za Afrika zatarajia kuimarisha ushirikiano wa kiusalama na China 07-17 10:37

  Kongamano la Amani na Usalama kati ya China na Afrika linaendelea hapa Beijing, ambapo maofisa waandamizi karibu 100 kutoka nchi 50 za Afrika na idara ya ulinzi ya Umoja wa Afrika pamoja na wajumbe wa jeshi la China wanajadili jinsi ya kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika mambo ya amani na usalama.

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako