• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Nyaraka muhimu zatangazwa baada ya kufungwa kwa Mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing 2018-09-05
    Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofungwa jana hapa Beijing ulitangaza nyaraka mbili muhimu zikiwemo Azimio la Beijing, na Mipango ya utekelezaji, ambazo zimeonesha kwa pande zote maafikiano kati ya China na Afrika kuhusu masuala muhimu duniani kwa hivi sasa. Rais Xi Jinping wa China ameeleza kuwa mkutano wa kilele wa FOCAC wa mwaka huu umefungua ukurasa mpya wa kihistoria wa uhusiano kati ya pande hizo mbili, na kuweka mnara mpya katika ushirikiano kati ya kusini na kusini katika zama mpya.
    • Mashaka ya nchi za magharibi hayatazuia ushirikiano wenye ufanisi mkubwa kati ya China na Afrika 2018-09-04
    Mkutano wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaendelea hapa mjini Beijing. Katika miaka 18 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Baraza hilo, kumekuwa na mashaka na kupaka matope ushirikiano kati ya pande hizo mbili, lakini hata hivyo, ushirikiano kati ya China na Afrika umepiga hatua thabiti na kupata matunda mazuri. Wakati huo huo baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za magharibi na washauri bingwa ambao walitilia shaka juu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili wametoa ripoti inayoonesha ukweli wa mambo.
    • Rais Xi Jinping wa China ahutubia ufunguzi wa Mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC 2018-09-04
    Tarehe 3 Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika umefunguliwa kwa shangwe kwenye Jumba la mikutano ya umma la Beijing. Rais Xi Jinping wa China alihudhuria ufunguzi wa mkutano na kutoa hotuba isemayo "Tushirikiane kwa kuelekea mustababali wetu wa pamoja na kuhimiza maendeleo kwa moyo mmoja",
    • Sekta mbalimbali zapongeza hotuba ya rais Xi kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya wakuu wa China na Afrika na wajumbe wa biashara 2018-09-04

    Rais Xi Jinping wa China jana hapa Beijing alitoa hotuba ya "Kuelekea kwa Pamoja Kwenye Ustawi" kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya viongozi wa China na Afrika na wajumbe wa sekta za viwanda na biashara na mkutano wa sita wa wajasiriamali wa China na Afrika uliofanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Beijing wa mwaka 2018 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, na kusisitiza kuwa China inaziunga mkono nchi za Afrika zishiriki kwenye ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, kupenda kufanya kazi na Afrika katika kuunganisha mikakati yao, na kujenga njia ya kujiendeleza ya kiwango cha juu inayoendana na hali halisi ya nchi, inayowashirikisha na kuwanufaisha watu wote, kusaidiana na kunufaishana, ili kuboresha maisha ya watu. Sekta mbalimbali barani Afrika zimepongeza hotuba hiyo ya rais Xi Jinping, na kuona hotuba hiyo imezielekeza nchi za Afrika kushiriki kwa kina kwenye ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kushirikiana na China kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja.

    • Mkutano wa mwaka 2018 wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wafunguliwa Beijing 2018-09-03

    Mkutano wa mwaka 2018 wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika umefunguliwa leo hapa Beijing, ambapo rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwenye mkutano huo. Amesisitiza kuwa, China inapenda kushirikiana na Afrika kujenga jumuiya yenye mutakabali wa pamoja inayobeba majukumu kwa pamoja, kufanya ushirikiano wa kunufaishana, kusitawisha pamoja tamaduni, kujenga mazingira ya usalama kwa pamoja na kuishi pamoja katika hali ya masikilizano. China itashirikiana na nchi za Afrika kuweka mkazo katika kutekeleza vitendo vinane katika miaka mitatu ijayo, kuimarisha ushirikiano katika kuhimiza maendeleo ya viwanda, kufangamanisha miundombinu, kurahisisha biashara, kujiendeleza bila ya kuchafua mazingira, kujenga uwezo, afya na matibabu, mawasiliano ya utamaduni, na Amani na usalama.

    • China yafanya juhudi kujenga Jumuiya yenye hatma ya pamoja iliyo karibu zaidi kati yake na Afrika 2018-09-03

    Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika ulioanza leo hapa Beijing.

    Katika hotuba hiyo, rais Xi amesema katika miaka mitatu ijayo na kipindi kifuatacho, China itajenga Jumuiya yenye hatma ya pamoja kati yake na Afrika iliyo ya karibu zaidi kwa njia ya kutekeleza mipango katika sekta nane zikiwemo kuhimiza maendeleo ya viwanda, ujenzi wa njia za mawasiliano, kurahisisha njia za kufanya biashara, na maendeleo yasiyo na uchafuzi wa mazingira. Hili ni wazo jipya na hatua mpya zinazotolewa na China inayotupia macho siku za mbele, ambalo limeweka mipango wa maendeleo kuhusu uhusiano kati ya China na Afrika.

    • China inaunga mkono nchi za Afrika kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kunufaika kwa pamoja na matunda yake 2018-09-03

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amehudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa viongozi na wadau wa viwanda na biashara kati ya China na Afrika na ufunguzi wa mkutano wa 6 wa wajasiriamali kati ya China na Afrika. Katika hotuba yake yenye kichwa cha "kuelekea kwa pamoja njia ya kujitajirisha", rais Xi amesisitiza kuwa China inaunga mkono nchi za Afrika kushiriki kwenye ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kupenda kufanya kazi na Afrika katika kuunganisha mikakati yao, na kujenga njia ya kujiendeleza ya kiwango cha juu inayoendana na hali halisi ya nchi, inayowashirikisha na kuwanufaisha watu wote, kusaidiana na kunufaishana, ili kuboresha maisha ya watu.

    • Mradi wa televisheni ya digitali wanufaisha wanavijiji wa Kenya 2018-09-01

    Mwezi Desemba mwaka 2015, kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na Afrika kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, na kutoa mipango 10 mikubwa ya ushirikiano katika sekta za viwanda, kilimo, miundombinu, fedha, maendeleo yasiyoleta uchafuzi wa mazingira, kurahisisha biashara na uwekezaji, kuondoa umaskini na kuwanufaisha watu, afya, utamaduni, amani na usalama.

    • Msemaji wa serikali ya Tanzania: "uzoefu wa China" utasaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania 2018-09-01

    Msemaji wa serikali ya Tanzania Bw. Hassan Abbas amesema Tanzania inafaa kuiga "uzoefu wa China", na pendekezo lililotolewa na China la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" litasaidia ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

    • Ujenzi wa reli tatu barani Afrika washuhudia mchakato wa China na Afrika katika kukabiliana kwa pamoja matatizo na kutafuta maendeleo ya pamoja 2018-08-31
    China inatajwa kama nchi inayofanya ujenzi kwa wingi zaidi wa miundo mbinu, na miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundo mbinu ikiwemo reli ya TAZARA iliyojengwa katika miaka ya 1960 pia imeshuhudia urafiki kati ya China na Afrika katika miaka mingi iliyopita. Wakati China ilipotoa msaada katika ujenzi wa reli ya TAZARA katika miaka 40 iliyopita, haikuwa na vifaa na teknolojia za kisasa, ilichokuwa nacho ni moyo wa dhati kwa watu wa Afrika. Ujenzi wa reli hiyo ulikamilika mwezi Julai mwaka 1976 baada ya wafanyakazi 60 kujitoa muhanga, na umekuwa ukichangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi pamoja na mapambano ya ukombozi wa taifa katika sehemu ya katikati na kusini mwa Afrika, na kuwa alama muhimu ya China katika kuziunga mkono kazi ya kujipatia ukombozi na uhuru ya nchi za Afrika.
    • Mpango wa China wa kupambana na malaria wawanufaisha watu wa Afrika 2018-08-31
    Mwezi Desemba mwaka 2015, kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na Afrika kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, na kutoa mipango 10 mikubwa ya ushirikiano katika sekta za viwanda, kilimo, miundombinu, fedha, maendeleo yasiyoleta uchafuzi wa mazingira, kurahisisha biashara na uwekezaji, kuondoa umaskini na kuwanufaisha watu, afya, utamaduni, amani na usalama. Leo tutakuletea sehemu ya nane iitwayo "Mpango wa China wa kupambana na malaria unawanufaisha watu wa Afrika".
    • Mbegu za maisha bora zaota mizizi Afrika 2018-08-30

    Mwezi Desemba mwaka 2015, Rais Xi Jinping wa China alitoa taarifa katika mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Johannesburg, kuwa China itazidisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote na nchi za Afrika. Rais Xi alisema Mipango kumi ya Ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya viwanda, kilimo cha kisasa, miundo mbinu, uchumi, maendeleo yasiyosababisha uchafuzi, uwekezaji na biashara, kupunguza umaskini, afya, utamaduni, amani na usalama imefungua mlango mpya wa uhusiano kati ya China na Afrika. Wakati mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika unakaribia kufanyika mjini Beijing, tunafuatilia Mipango kumi ya Ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuona jinsi uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika unavyozidi kukua. Tunaanza kuhusu Mbegu za maisha bora zaota mizizi Afrika.

    • Jukwaa la biashara la kielektroniki la Amanbo larahisisha biashara kati ya China na Afrika 2018-08-29

    Mwezi Desemba mwaka 2015, kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na Afrika kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote, na kutoa mipango 10 mikubwa ya ushirikiano katika sekta za viwanda, kilimo, miundombinu, fedha, maendeleo yasiyochafua mazingira, kurahisisha biashara na uwekezaji, kuondoa umaskini na kuwanufaisha watu, afya, utamaduni, amani na usalama. Katika kipindi cha leo, utasikiliza ripoti ya sita "Jukwaa la biashara la kielektroniki la Amanbo linavyohimiza na kurahisisha biashara kati ya China na Afrika".

    • Ushirikiano wa ulinzi wa mazingira kati ya China na Afrika wachangia mazingira ya Afrika 2018-08-28
    Mwezi Desemba mwaka 2015, kwenye Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na Afrika kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote. Pia alitoa mipango 10 mikubwa ya ushirikiano katika sekta za viwanda, kilimo, miundombinu, fedha, maendeleo yasiyoleta uchafuzi wa mazingira, kurahisisha biashara na uwekezaji, kuondoa umaskini na kuwanufaisha watu, afya, utamaduni, amani na usalama.
    • Ushirikiano wa mambo ya fedha wachangia maendeleo ya kasi ya ushirikiano kati ya China na Afrika 2018-08-27
    Mwezi Desemba mwaka 2015, kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na Afrika kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote. Pia alitoa mipango 10 mikubwa ya ushirikiano katika sekta za viwanda, kilimo, miundombinu, fedha, maendeleo yasiyoleta uchafuzi wa mazingira, kurahisisha biashara na uwekezaji, kuondoa umaskini na kuboresha maisha ya watu, afya, utamaduni, amani na usalama. Katika kipindi cha leo, tunakuletea maelezo kuhusu ushirikiano wa mambo ya fedha kati ya pande hizo mbili.
    • Kituo cha kuzalisha umeme cha Karuma kinawawezesha watu wa Uganda waone mwanga wa maendeleo 2018-08-26
    • Balozi wa Uganda nchini China aeleza ushirikiano kati ya China na Uganda 2018-08-25
    • Rais wa China asimulia hadithi kuhusu wanandoa wa China kwenda Tanzania kwa ajili ya fungate 2018-08-24
    • Kujenga taswira ya maisha bora kwa kutumia chuma na saruji 2018-08-24
    Mwezi Desemba mwaka 2015, kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na Afrika, kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote. Pia alitoa mipango 10 mikubwa ya ushirikiano katika sekta za viwanda, kilimo, miundombinu, fedha, maendeleo yasiyochafua mazingira, kurahisisha biashara na uwekezaji, kuondoa umaskini na kuboresha maisha ya watu, afya, utamaduni, amani na usalama. Katika kipindi cha leo, unasikiliza sehemu ya kwanza ya mfululizo wa ripoti zetu, kuhusu "Kujenga taswira ya maisha bora kwa kutumia chuma na saruji".
    • FOCAC kuhusianisha Ukanda Mmoja, Njia Moja na agenda za AU, UN 2018-08-23

    Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, FOCAC, utakaofanyika kati ya Septemba 3 na 4 unategemewa kuhusianisha malengo ya Ukanda Mmoja, Njia Moja, Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Maendeo Endelevu na Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika.

    • Balozi wa Rwanda nchini China aeleza ushirikiano kati ya China na Rwanda 2018-08-23
    "Katika makumi ya miaka iliyopita, China na Afrika zimeshirikiana na kushikamana kwa dhati. Zinadumisha hali ya kuwa jumuiya yenye hatma na maslahi ya pamoja." hayo yamesemwa na rais Xi Jinping wa China wakati alipotembelea Afrika mwezi Juni, mwaka huu. Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. FOCAC utakaofanyika hivi karibuni, unafuatiliwa sana duniani. Kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo, waandishi wa habari wa CRI wamefanya mahojiano na mabalozi wa Tanzania, Zimbabwe, Rwanda, Uganda, Burundi na Afrika Kusini nchini China, kuhusu mafanikio na maendeleo yaliyopatikana chini ya mfumo wa FOCAC, kuhimiza ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ili kupata maslahi ya pamoja ya China na Afrika. Hivi karibuni tumemhoji balozi wa Rwanda nchini China Bw. Charles Kayonga akieleza ushirikiano kati ya China na Rwanda.
    • Beijing iko tayari kwa mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika
     2018-08-22

    Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika hapa Beijing kuanzia tarehe 3 hadi 4, mwezi Septemba. Mjumbe wa taifa ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, huu ni mkusanyiko mwingine wa familia kubwa ya China na Afrika, na pia ni mkutano mkubwa zaidi wa mwaka huu nchini China. Sasa mji wa Beijing uko tayari, na utawapokea marafiki wa China kutoka nchi mbalimbali za Afrika kwa ukarimu.

    • Uhusiano wa Burundi na China watajwa kuingia kwenye kipindi kizuri zaidi katika historia 2018-08-22

    Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Bw Alain Aime Nyamitwe amesema Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano wa China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi Septemba mjini Beijing utasaidia kuimarisha uhusiano kati ya Burundi na China, na kuhimiza maendeleo ya Burundi.

    • Ethiopia yatarajia mkutano ujao wa FOCAC wa Beijing uimarishe mafanikio ya ushirikiano kati ya China na Afrika 2018-08-22

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Bw Meles Alem amesema serikali ya Ethiopia inatarajia Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano wa China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi ujao mjini Beijing utazidi kuimarisha mafanikio ya ushirikiano kati ya China na Afrika. Bw Meles ameisifu China kwa kuzipatia nchi za Afrika msaada kwa miaka mingi. Amesema,

    • Balozi wa Zimbabwe nchini China aeleza ushirikiano kati ya China na Zimbabwe 2018-08-21

    "Katika makumi ya miaka iliyopita, China na Afrika zimeshirikiana na kushikamana kwa dhati. Zinadumisha hali ya kuwa jumuiya yenye hatma na maslahi ya pamoja." Hayo yamesemwa na rais Xi Jinping wa China wakati alipotembelea Afrika mwezi Juni, mwaka huu. Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. FOCAC utakaofanyika hivi karibuni, unafuatiliwa sana duniani. Kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo, waandishi wa habari wa CRI wamefanya mahojiano na mabalozi wa Tanzania, Zimbabwe, Rwanda, Uganda, Burundi na Afrika Kusini nchini China, kuhusu mafanikio na maendeleo yaliyopatikana chini ya mfumo wa FOCAC, kuhimiza ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ili kupata maslahi ya pamoja ya China na Afrika. Hivi karibuni tumemhoji balozi wa Zimbabwe nchini China Bw. Paul Chikawa akieleza ushirikiano kati ya China na Zimbabwe.

    • Katibu mkuu wa UNCTAD asema mfumo wa FOCAC unahimiza biashara kati ya China na Afrika 2018-08-20

    Katibu mkuu wa Mkutano wa biashara na maendeleo wa Umoja wa Mataifa UNCATD Bw. Mukhisa Kituyi amesema chini ya msukumo wa mfumo wa baraza la ushirikiano wa China na Afrika FOCAC, biashara kati ya China na Afrika inaendelea kuboreshwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako