Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
 • Hadithi ya mfanyabiashara wa Taiwan aliyeanzisha kampuni yake katika China bara
 •  2008/11/21
  Mkoa wa Fujian ulioko kusini mashariki mwa China unapakana na kisiwa cha Taiwan. Mazingira ya kijiografia, hali ya hewa na desturi za sehemu hiyo mbili zinafanana. Meneja wa kampuni ya viatu ya Yuesheng ya Fuzhou Bw. Wang Jiankun ni mfanyabiashara wa Taiwan mwenye asili ya mkoa wa Fujian. Kuanzisha shughuli zake katika China bara ni matumaini yake tangu zamani.
 • Eneo la viwanda la Suzhou lajenga eneo jipya la kisasa
 •  2008/11/07
  Eneo la viwanda la Suzhou lililoko mashariki mwa mkoa wa Jiangsu ni eneo la aina mpya la vielelezo vya ustawishaji wa viwanda. Ukienda eneo hilo utagundua kuwa katika eneo hilo si kama tu kuna vituo vya viwanda vya teknolojia mpya za hali ya juu, bali pia kuna jumba la opera na majengo ya nyumba za wakazi.
 • Mahojiano na meneja mkuu wa kampuni ya bidhaa za Kiislamu ya Abudunla ya Ningxia Bw. Yue Wenhai
 •  2008/10/26
  Kampuni ya bidhaa za Kiislamu ya Abudunla ya Ningxia ni kampuni inayoshughulikia uvumbuzi, utengenezaji na uuzaji wa bidhaa za kikabila ambazo nyingi zinauzwa katika nchi za nje. Thamani ya uuzaji kwa mwaka ni zaidi ya yuan milioni 2. Lakini katika miaka kadhaa iliyopita, kampuni hiyo bado ilipata hasara.
 • Kampuni ya Taishan yapata mafanikio kwa kutumia fursa ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing
 •  2008/10/07
  Bidhaa zinazotengenezwa na China zinatambuliwa na dunia nzima, lakini inua sifa na umaarufu wa bidhaa zinazotengenezwa na China bado ni kazi kubwa ya makampuni mengi ya China.
 • Mustakabali wa maendeleo ya ushirikiano wa kiuchumi wa eneo kubwa la Ghuba ya Beibu ni mzuri
 •  2008/09/23
  Mmkutano wa baraza la ushirikiano wa kiuchumi wa eneo kubwa la Ghuba ya Beibu ulifunguliwa tarehe 31 mwezi Julai huko Beihai, mkoani Guangxi. Maofisa wa serikali, wataalamu na wanaviwanda karibu mia 6 kutoka nchi mbalimbali zikiwemo China, Singapore, Philippines na Vietnam walihudhuria mkutano huo.
 • Makampuni ya China yajitahidi kujipatia "medali ya dhahabu" kwenye michezo ya Olimpiki ya Beijing
 •  2008/09/16
  Wanamichezo wa China walikuwa na matumaini ya kujipatia ushindi na kunyakua medali za dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki ya Beijing. Katika miaka ya karibuni wakati uchumi uliohusiana na michezo ya Olimpiki ulipata maendeleo siku hadi siku, wanaviwanda wa China walifanya juhudi kujipatia "medali ya dhahabu", yaani umaarufu duniani.
 • Makampuni ya teknolojia za hali ya juu za mji wa Beijing yapata maendeleo makubwa katika kufanya uvumbuzi kwa kujitegemea
 •  2008/07/29
  Eneo la sayansi na teknolojia la Zhongguancun liko kaskazini magharibi mwa mji wa Beijing. Kwenye eneo hilo kuna makampuni karibu elfu 20 ya teknolojia za hali ya juu. Katika miaka ya hivi karibuni, makampuni hayo yakisaidiwa na serikali, yamevumbua bidhaa na teknolojia nyingi mpya, ambazo baadhi yake zimefikia kiwango cha kisasa duniani, na makampuni hayo yamepata masoko ya nchini na nchi za nje.
 • Maendeleo makubwa ya shughuli za utengenezaji wa soksi mjini Datang
 •  2008/07/15
  Mji mdogo wa Datang haujulikani kwa watu wengi, lakini unajulikana kwa wanaviwanda kutokana na shughuli zake za soksi. Shughuli kamili za kutengeneza malighafi mbalimbali na soksi na kuuza soksi zimeanzishwa huko. Baada ya kusitawisha shughuli hizo kwa miaka 20 iliyopita, watu wengi zaidi wa mji huo wametambua kuwa, mji huo hauwezi kuwa kituo muhimu cha soksi duniani kwa kuongeza utengenezaji wa soksi tu, bali ni lazima wafanye uvumbuzi ili bidhaa zao ziingie kwenye masoko ya kimataifa.
 • Mkoa wa Hainan wapata mafanikio makubwa katika kazi ya kuhifadhi mazingira.
 •  2008/07/01
  Mkoa wa Hainan umesifiwa kuwa bustani wa mwaka mzima nchini China. Mwaka 2007 eneo linalofunikwa na miti mkoani humo lilikuwa zaidi ya asilimia 57, ambayo ni mara tatu ya wastani wa kiasi hicho nchini China. Mkoani humo kuna bustani 8 za misitu za ngazi ya kitaifa na hifadhi 69 za maumbile. Robo ya eneo la mkoa huo ni hifadhi ya mazingira ya viumbe ya kitaifa. Wakati uchumi wake unapopata maendeleo ya haraka, mkoa huo unahakikisha mazingira mazuri zaidi ya viumbe.
 • Mfanyabiashara wa Taiwan aliyeanzisha kampuni yake mjini Xiamen mkoani Fujian
 •  2008/06/17
  Mji wa Xiamen mkoani Fujian ulioko kusini mashariki mwa China ni mji ulio karibu zaidi na Taiwan kwenye China bara. Kutokana na maendeleo ya mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya kando mbili za mlangobahari wa Taiwan, wafanyabiashara wengi wa Taiwan wamekwenda Xiamen kuwekeza kuanzisha makampuni yao mjini humo. Kutokana na juhudi zao za miaka mingi na maendeleo makubwa ya uchumi wa China bara, shughuli zao zimepata maendeleo hatua kwa hatua
 • Mji wa Shouguang unaosifiwa kuwa kijiji cha uzalishaji wa mboga nchini China
 •  2008/06/03
  Mboga ni chakula kinachohitajika katika maisha ya kila siku. Tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, uzalishaji wa mboga umekuwa unapata maendeleo makubwa nchini China. Mwaka jana uzalishaji wa mboga ulizidi tani milioni 580, na uuzaji wa mboga katika nchi za nje ulichukua nafasi ya kwanza duniani.
 • Kilimo cha mazao ya kitropiki mkoani Hainan
 •  2008/05/13
  Kutokana na uzalishaji mkubwa wa mboga na matunda, mkoa wa Hainan umasifiwa kuwa ni mkoa unaozalisha mboga na matunda kwa wingi nchini China. Mazao yanayozalishwa mkoani humo si kama tu yanauzwa katika miji zaidi ya 100 nchini China, bali pia yanauzwa katika nchi na sehemu zaidi ya 20 duniani ikiwemo Marekani, Ulaya, Russia, Japan na nchi za Asia ya Kusini Mashariki
 • Bw. Michel Perrin kutoka Ufaransa na magurudumu ya chapa ya Michellin
 •  2008/04/29
  Kampuni ya Michellin ni moja ya makampuni maarufu inayotengeneza magurudumu duniani. Wakati michezo ya Olimpiki ya Beijing inapokaribia, watu watakaokuja Beijing kutazama michezo hiyo kutoka sehemu mbalimbali duniani wataweza kupanda mabasi yanayotumia magurudumu ya chapa ya Michellin. Magurudumu hayo yanatengenezwa na kampuni ya magurudumu ya Michellin mjini Shenyang.
 • Bw. Brain A. Hodge kutoka Canada anayeishi mjini Fuzhou
 •  2008/04/15
  Bw. Brain A. Hodge kutoka Canada anaishi katika mji wa Fuzhou ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Fujian ulioko kusini mashariki mwa China. Katika kipindi hiki cha nchi yetu mbioni, tutawaelezea habari kuhusu anavyoishi na kufanya kazi mjini humo.
 • Naibu meneja mkuu wa kampuni ya dawa ya Astellas Bw. Hideaki Mochizuki
 •  2008/03/25
  Bw. Hideaki Mochizuki ni naibu meneja mkuu wa kampuni ya dawa ya Astellas ya Japan nchini China, anafanya kazi mjini Shenyang, China. Bw. Mochizuki alianza kufanya kazi zinazohusu dawa baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, mpaka sasa amefanya kazi hizo kwa miaka 23
 • Bw. Mugodo Joseph kutoka Zimbabwe na duka lake la zawadi
 •  2008/03/11
  Mjini Taiyuan mkoani Shanxi kuna duka moja la zawadi lililoanzishwa na mgeni, duka hilo linaitwa nyumba dogo la Qiaoqiao. Zawadi zinazouzwa kwenye duka hilo ni pamoja na vitu vilivyochongwa kwa mizizi, mbao na jade kutoka Ulaya, Asia na Afrika.
 • Mfuko wa kusaidiana wa ngazi ya kijiji kwa ajili ya maendeleo, unavyobadilisha maisha ya wanakijiji wa kijiji cha Matouchuan
 •  2008/02/26
  Zamani kijiji cha Matouchuan cha wilaya ya Longxi mkoani Gansu, China kilikuwa ni kijiji kilicho nyuma kiuchumi. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na mfuko wa kusaidiana wa ngazi ya kijiji kwa ajili ya maendeleo, maisha ya wanakijiji wa kijiji hicho yanaboreshwa siku hadi siku, na sura ya kijiji imebadilika kuwa nzuri.
 • Mke na mume kutoka Ujerumani walioamua kuishi nchini China
 •  2008/02/12
  Kabla ya miaka kadhaa iliyopita Bw. Bauwer Braun toka Ujerumani alikuja China na kujifunza kichina mjini Xi'an. Alipokuwa mjini Xi'an alisikia kuwa mkoa wa Qinghai ulioko kwenye uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet ni sehemu yenye maajabu mengi, ambao una maliasili nyingi, mazingira ya kipekee
 • Mahojiano na meneja mkuu wa tawi la kampuni ya zana za umeme nyumbani ya Bosch na Siemens nchini China
 •  2008/01/29
  Kampuni ya zana za umeme za nyumbani ya Bosch na Siemens ni kampuni maarufu inayotengeneza zana hizo duniani. Thamani ya uuzaji wa bidhaa ya kampuni hiyo inachukua nafasi ya kwanza barani Ulaya na inachukua nafasi ya tatu duniani. Mwaka 1994 kampuni hiyo ilifungua tawi lake nchini China, na baadaye ikaanza kupata maendeleo yenye utulivu.
 • Bw. Kamal Sanusi anayefanya biashara mjini Guiyang
 •  2008/01/15
  "Nilipokuja kufanya kazi hapa mkoani Guizhou, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuja China. Kabla ya kuja China, marafiki zangu wengi walinielezea habari kuhusu China, na nilitafuta habari nyingi kuhusu China na mkoa wa Guizhou kwenye mtandao wa Internet na vitabu.
 • Maendeleo ya uchumi wa China yasifiwa na dunia
 •  2008/01/01
  Katika mwaka 2007 uchumi wa China umepata mafanikio ya kufurahisha. Kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Septemba mwaka 2007 uchumi wa China ulipata maendeleo ya haraka na yenye utulivu, mapato ya wakazi wa mijini na vijijini yaliongezeka kwa kiasi kikubwa, kazi ya kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji na maji taka na hewa chafu ilipata maendeleo mapya.
 • Meneja wa kampuni ya Japan anayetilia maanani uhifadhi wa mazingira
 •  2007/12/18
  Katika miaka ya hivi karibuni, familia nyingi zaidi za China zimenunua magari. Watu wengi wanajua kampuni ya Toyota ya Japan ambayo ni kampuni maarufu ya utengenzaji wa magari, lakini ni watu wachache wanaojua kuwa kampuni ya Aisin ina uhusiano wa karibu na kampuni ya Toyota. Kampuni ya Aisin ya Japan ni moja ya kampuni 500 yenye nguvu kubwa zaidi duniani. Katika miaka miwili iliyopita, kampuni hiyo ilifungua tawi lake mjini Tangshan, China.
 • Biashara yenye nguvu kubwa ya uhai kati ya China na Russia huko Manzhouli
 •  2007/12/11
  Tukizungumzia biashara ya mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani, kaskazini mwa China na nje, hatuna budi kutaja mji wa Manzhouli. Mji huo uko kaskazini mwa mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani, unapakana na Russia na Mongolia, ambao ni forodha kubwa kabisa ya nchi kavu kati ya China na Russia.
 • Sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia ya Xining
 •  2007/11/27
  Mkoa wa Qinghai uko kaskazini magharibi mwa China, na pia kaskazini mashariki ya uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, ambako ni chanzo cha mito mikubwa nchini China ikiwa ni pamoja na Mto Changjiang na Mto Manjano, pia ni mmoja kati ya mikoa inayotekeleza mkakati wa uendelezaji wa sehemu ya magharibi ya China
 • Kundi la Xugong, Kampuni ya kutengeneza mashine ya Xuzhou nchini China inayoelekea kwenye soko la kimataifa
 •  2007/11/13
  "Xugong Xugong, itakusaidia kuelekea kwenye mafanikio". Hili ni tangazo linalofahamika kote nchini China. "Kundi la Xugong" ni ufupi wa jina la Kichina la kundi la viwanda vya kutengeneza mashine la Xuzhou, hivi sasa kundi hilo limekuwa linaongoza katika sekta ya uzalishaji wa mashine nchini China.
 • Ushirikiano wa kikanda wa Asia ya kaskazini mashariki waendelezwa kwa kina
 •  2007/10/30
  Maonesho ya 3 ya uwekezaji na biashara ya Asia ya kaskazini mashariki yalifungwa mwanzoni mwa mwezi Septemba huko Changchun, mji mkuu wa mkoa wa Jilin, China. Katika maonesho hayo ya siku nne, wajumbe waliohudhuria mkutano huo walifanya majadiliano kuhusu "kuhimiza ushirikiano wa kikanda wa sehemu ya Asia ya kaskazini mashariki" na "kustawisha kituo kikongwe cha viwanda vya kaskazini mashariki ya China".
 • Sifa na usalama wa mazao ya majini ya China vimehakikishwa
 •  2007/10/16
  Sifa na usalama wa mazao ya majini ni suala linalofuatiliwa sana na nchi za nje. Mwandishi wetu wa habari alipotembelea katika mikoa ya Guangdong na Jiangxi ambayo inazalisha mazao ya majini kwa wingi, alifahamishwa kuwa sifa na usalama wa mazao ya kilimo ya China vinainuliwa hatua kwa hatua na una uhakikisho, hasa sifa za mazao yanayouzwa katika nchi za nje.
 • Viwanda vya serikali vya China vyaharakisha kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu
 •  2007/10/02
  Katika miaka ya hivi karibuni, uchumi wa China umekuwa unaendelezwa kwa kasi, lakini migongano kati ya maendeleo ya uchumi na mazingira pia imekuwa inaonekana siku hadi siku. Ili kutatua migongano hiyo, China imeweka lengo la kipindi cha kati la kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu, ili kutimiza maendeleo endelevu ya uchumi na jamii.
 • Kisiwa cha Changxing chaongoza kwenye wimbi la uwekezaji
 •  2007/09/18
  Kisiwa cha Changxing kiko mkoani Liaoning, kaskazini mashariki mwa China. Katika miaka ya hivi karibuni, kisiwa hicho kimekuwa kinawavutia wawekezaji wengi wa nchini na wa nje siku hadi siku.
 • Hali ya kiwanda cha kwanza cha kuzalisha umeme kwa nishati ya viumbe nchini China
 •  2007/09/04
  Wilaya ya Shan mkoani Shandong mashariki mwa China, ni sehemu inayozalisha pamba kwa wingi nchini China. Mwishoni mwa mwaka jana, kiwanda cha kwanza cha kuzalisha umeme kwa nishati ya viumbe nchini China-Kampuni ya kuzalisha umeme kwa nishati ya viumbe ya wilaya ya Shan ya Guoneng ilianzishwa huko
  1 2 3 4 5 6 7