Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu waingia kipindi cha utekelezaji
  •  2007/08/21
    Tarehe 27 mwezi Julai, "Baraza la pili la ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu" lilifungwa huko Nanning, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, China.
  • Ulinzi wa alama za kijiografia wasaidia kuhimiza maendeleo ya kilimo cha China
  •  2007/08/07
    Alama za kijiografia ni alama zinazotumika katika bidhaa zenye vyanzo maalum vya kijiografia na sifa zinazohusika na sehemu zinazotengeneza bidhaa hizo. Kwa ufupi, alama za kijiografia zinatengenezwa kwa jina la sehemu zinazotengeneza bidhaa hizo.
  • Sekta ya uchapishaji wa kitarakimu yapata maendeleo ya kasi nchini China
  •  2007/07/31
    Katika miaka ya hivi karibuni, sekta ya uchapishaji wa kitarakimu imepata maendeleo ya kasi nchini China. Kwa mujibu wa takwimu zisizokamilika, katika mwaka 2006 mapato ya sekta ya uchapishaji wa kitarakimu yalikuwa yuan bilioni 20.
  • Kuendeleza kilimo kinachobana matumizi ya maji kuna manufaa mengi
  •  2007/07/17
    Kilimo ni sekta inayotumia maji mengi zaidi nchini China. Matumizi ya maji kwenye sekta hiyo yanachukua asilimia 64 ya matumizi yote ya maji nchini kote, lakini kwenye uzalishaji wa kilimo nusu ya maji yanapotea. Kutokana na kuwa na upungufu mkubwa wa maji, sehemu nyingi za China zimeanza kuendeleza kilimo kinachobana matumizi ya maji.
  • Hong Kong yaendelea kuwa sehemu yenye uchumi wa soko huria kabisa duniani
  •  2007/07/03
    Hongkong ni bandari huria maarufu duniani, pia ni moja ya sehemu zinazopata mafanikio duniani katika kutekeleza uchumi wa soko huria. Kwa mujibu wa Sheria ya Kimsingi, baada ya kurudi China, Hongkong inaendelea kutekeleza mfumo wa uchumi wa soko huria wa kibepari. Katika miaka 10 iliyopita, kutokana na msingi wa sera ya "nchi moja mifumo miwili", Hongkong imeendelea kuwa sehemu yenye uchumi wa soko huria kabisa duniani.
  • Utawala wa moja kwa moja wa serikali kuu ya China wasukuma mbele maendeleo ya haraka ya mji wa Chongqing
  •  2007/06/19
    Mwezi Machi mwaka 1997, ili kutatua masuala kadhaa yaliyotokana na ujenzi wa mradi wa maji wa magenge matatu ya Mto Changjiang yakiwemo uhamiaji wa wakazi milioni moja katika sehemu ya magenge matatu na hifadhi ya mazingira ya viumbe, mji wa Chongqing uliamuliwa kuwa mji unaotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu ya China
  • Shirikisho la ushirikiano vijijini mjini Ruian nchini China
  •  2007/06/12
    Kubaki nyuma kwa maendeleo ya mambo ya fedha siku zote kumekuwa tatizo kubwa linalokwamisha maendeleo ya uchumi wa vijiji nchini China, lakini mjini Ruian mkoani Zhejiang, mashariki mwa China, ukusanyaji wa mitaji sio tatizo tena kwa wakulima wa huko, kwani wanaweza kupata mikopo midogo yenye riba ndogo kutoka kwa shirikisho la ushirikiano vijijini ili kufanya shughuli za uzalishaji."Ni hao"-Hujambo", "Ni lai ma?"-Utakuja? "Ni shi wo de lao shi"-Wewe ni mwalimu wangu. Mke wa rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe anarudia mara kwa mara maneno hayo ya Kichina. Ingawa bado ana shida ya kutamka vizuri maneno hayo, lakini anajifunza kwa makini sana, na humwuliza mwalimu wake kama anatamka sahihi.
  • Sehemu ya katikati ya China kuwa sehemu mpya inayofuatiliwa na wafanyabiashara wa nchi za nje
  •  2007/05/29
    Maonesho ya pili ya uwekezaji na biashara ya sehemu ya katikati ya China yalifanyika mwezi uliopita mjini Zhengzhou mkoani Henan, China, ambapo makampuni zaidi ya 300 yaliyoingia kwenye safu ya makampuni 500 yenye nguvu kubwa duniani, yakiwemo Microsoft, Metro na Carrefour yalishiriki kwenye maonesho hayo.
  • Baraza la Asia la Boao latoa mwito kuwa nchi za Asia ya mashariki kuimarisha ushirikiano wa nishati
  •  2007/05/15
    Kwenye mkutano wa mwaka wa baraza la Asia la Boao uliofungwa hivi karibuni, usalama wa nishati kwa Asia ya mashariki ulikuwa ni suala lililofuatiliwa na watu waliohudhuria mkutano huo. Maofisa na wanaviwanda wa nchi nyingi za Asia ya mashariki waliona kuwa, hivi sasa malimbikizo ya nishati kwa Asia ya mashariki siyo mengi yasiyo na kikomo, lakini mahitaji ni makubwa.
  • Maonesho ya viwanda ya kimataifa ya Hanover yavutia
  •  2007/05/01
    Maonesho ya viwanda ya kimataifa katika mji wa Hanover Ujerumani yalifunguliwa tarehe 16, mashirika zaidi ya 500 ya China yalishiriki kwenye maonesho hayo. Maonesho ya China yanachukua mita za mraba 5,500 ambayo ni makubwa kuliko nchi nyingine isipokuwa tu Italia.
  • Kampuni za China na za nchi za nje zapokea kwa utulivu "kuweka kigezo cha namna moja kodi mbili"
  •  2007/04/17
    Kwenye mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China uliofungwa hivi karibuni, sheria mpya ya kodi ya mapato ya viwanda na makampuni ilipitishwa kwa kura nyingi. Sheria hiyo imeweka kigezo cha namna moja kodi za mapato ya makampuni na viwanda vya mitaji ya kigeni na ya China, na kuweka kiwango kipya cha kodi kuwa asilimia 25.
  • China kudhibiti matumizi ya ardhi
  •  2007/04/03
    Katika miaka ya karibuni, uwekezaji wa mali zisizohamishika umekuwa ukiongezeka kwa kasi. Ongezeko hilo linaposukuma mbele maendeleo ya uchumi wa China, pia linaleta changamoto kwa utulivu wa uendeshaji wa uchumi kwa jumla
  • China inafanya juhudi kupunguza tofauti ya mapato na kujenga jamii yenye masikilizano
  •  2007/03/20
    Kutokana na maendeleo ya uchumi wa China, mapato ya Wachina yamekuwa yakiongezeka haraka. Lakini wakati huohuo, tofauti ya mapato pia imekuwa ikiongezeka. Katika miaka ya hivi karibuni, suala hilo limekuwa linafuatiliwa na watu mbalimbali wa China, na limekuwa suala muhimu la kijamii ambalo linashughulikiwa na serikali ya China kwa makini
  • Mkoa wa Qinghai wajaribu kuwa na mtizamo mpya wa kuwasaidia watu maskini kuanzisha shughuli iil kuondokana na umaskini
  •  2007/03/13
    Mkoa wa Qinghai uko kwenye uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, kaskazini magharibi mwa China. Ingawa mkoani humo kuna maliasili nyingi, lakini kutokana na kuwa na idadi ndogo ya watu, na kutokuwa na hali nzuri ya mawasiliano, ukilinganishwa na sehemu zilizoendelea za mashariki mwa China, mkoa huo ni sehemu ambayo bado haijaendelea kiuchumi, na idadi ya watu maskini mkoani humo bado ni kubwa
  • Weifang-maskani yangu ya pili
  •  2007/03/06
    Bw. Xu Zhongche ni mfanyabiashara kutoka Taiwan, ambaye hapo awali alifanya biashara ya vito nchini Thailand, na miaka zaidi ya 10 iliyopita alipanua shughuli zake za biashara hadi China bara. Kwenye mji wa Weifang wa mkoani Shandong ulioko sehemu ya mashariki mwa China
  • China ya jitahidi kuongeza ajira
  •  2007/02/20
    China ni nchi yenye watu bilioni 1.3, ni nchi yenye idadi kubwa kabisa ya watu duniani, hivyo utatuzi wa suala la ajira ni kazi kubwa. Katika miaka ya karibuni, serikali ya China imekuwa ikizingatia kuongeza ajira, na kulichukulia suala hilo kuwa ni kazi muhimu ya kutatua matatizo ya maisha ya watu
  • Bima ya maisha yarudi kwenye soko la hisa nchini China
  •  2007/02/13
    Shirika la bima ya maisha la China, ambalo linachukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa miongoni mwa mashirika ya bima ya maisha nchini China, tarehe 9 mwezi Januari lilianza kuuza hisa zake kwenye soko la bima nchini China. Hii ni mara ya kwanza kwa shirika hilo kuuza hisa zake nchini China baada ya kuuza hisa zake kwenye masoko ya hisa ya Hong Kong na Marekani.
  • China yaongeza masharti kwa magari yanayosafirishwa kwa nje
  •  2007/02/06
    Kuanzia tarehe 1 mwezi Machi mwaka huu, China itaanza kutekeleza utaratibu wa kuomba kibali kwa magari yanayosafirishwa kwa nchi za nje, ukiagiza kuwa ni kampuni bora na za kutoa huduma kamili kwa magari yanayouzwa tu, ndizo zinazoweza kupewa leseni ya kusafirisha magari kwa nchi za nje.
  • Udhibiti wa mpango mkuu wa uchumi wa taifa kwa mwaka 2006 ulipata ufanisi
  •  2007/01/30
    Mwaka 2006 ulikuwa ni mwaka wa kwanza wa kutekeleza mpango wa 11 wa maendeleo wa miaka mitano ya uchumi na jamii ya China. Katika mambo ya uchumi kwa mwaka huo, vitu viwili vilikuwa muhimu sana, ambayo ni "ongezeko la kasi" na "udhibiti wa mpango mkuu wa uchumi wa taifa".
  • China yaendelea kujiunga na dunia kwa haraka
  •  2007/01/23
    China ilijiunga na shirika la biashara duniani, WTO tarehe 11 mwezi Desemba miaka 5 iliyopita, na kuingia kipindi cha ongezeko la kasi la uchumi, ambacho watu mbalimbali duniani wanalishangaa.
  • Benki ya Ujenzi ya China yanunua tawi la Asia la Benki ya Marekani
  •  2007/01/16
    Bodi ya Benki ya Ujenzi ya China tarehe 29 mwezi Desemba mwaka 2006 ilitangaza kuwa imenunua hisa zote za tawi la Asia la Benki ya Marekani. Baada ya hapo tawi la Asia la Benki ya Marekani lilibadilishwa jina na kuitwa "tawi la Asia la Benki ya Ujenzi ya China", ambapo alama za mikataba na nyaraka za benki pamoja na majina ya vitengo vya benki hiyo pia yalibadilika. 
  • Mazingira ya kuanzisha shughuli kwa kampuni ndogo na za wastani za Beijing yaboreshwa kwa udhahiri
  •  2007/01/09
    Eneo la ustawishaji wa sayansi na teknolojia la Zhongguancun la Beijing linachukua nafasi ya kwanza kwa umuhimu katika maeneo ya sayansi na teknolojia ya nchini China, karibu kampuni zote kiasi cha elfu 16 zilizoko kwenye eneo hilo, ziko katika kipindi cha mwanzo au kipindi cha kukua.
  • Mikwaruzano ya biashara ya kimataifa yapima uwezo wa China
  •  2007/01/02
    Wakati sekta za nguo na viatu za China zinapokumbwa na mikwaruzano ya biashara duniani na kutafuta ufumbuzi, sekta za chuma, chuma cha pua, mitambo na elektroniki pia zinakabiliwa vizuizi na kufanyiwa uchunguzi kuhusu kuuza bidhaa kwa bei ya chini, mikwaruzano ya kibiashara inayotokea mara kwa mara inapima uwezo wa serikali na kampuni za China.
  • Kilimo mkoani Hainan kimekuwa sekta inayowekezwa sana na wafanyabiashara kutoka Taiwan
  •  2006/12/26
    Mwaka 1999 mkoa wa Hainan ulioko kusini mwa China ulithibitishwa na serikali kuwa ni mkoa pekee wa majaribio ya ushirikiano katika sekta ya kilimo kati ya pande mbili za mlango bahari wa Taiwan.
  • Naibu mkuu wa benki ya maendeleo ya Asia apongeza maendeleo iliyoyapata China
  •  2006/12/19
    Naibu mkuu wa benki ya maendeleo ya Asia, Bw. Roluns Greenwood tarehe 11 alipohojiwa na mwandishi wa habari wa shirika la habari la Xinhua aliipongeza China kwa maendeleo iliyoyapata katika miaka mitano iliyopita tangu ijiunge na shirika la biashara duniani, WTO.
  • Mji wa Guizhou wawasaidia watu wenye kipato kidogo kwa mikopo kutoka benki
  •  2006/12/12
    Benki kutoa mikopo midogo ni njia yenye ufanisi ya kuwasaidia watu wenye kipato kidogo, ambayo ilianzishwa miaka zaidi ya 20 iliyopita na mwana-benki wa Bangladesh Bw. Muhammad Yunus aliyepata tuzo ya Nobel. China ilijaribu kuwasaidia watu wenye kipato kidogo kwa mikopo midogo ya benki kwenye baadhi ya sehemu tokea mwaka 1993
  • Serikali ya China yasaidia viwanda vidogo kupata mitaji
  •  2006/12/05
    Tokea miaka miwili iliyopita, kutokana na uungaji mkono wa idara husika ya serikali, viwanda vidogo vilivyoko kwenye baadhi ya sehemu za hapa China, sasa vinaweza kupewa mikopo midogo bila kuweka rehani, isipokuwa unaangaliwa uwezo wake wa kurudisha fedha za mikopo
  • Akiba ya fedha za kigeni ya China yazidi dola za kimarekani trilioni 1
  •  2006/11/28
    Ilipofika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu, akiba ya fedha za kigeni ya China ilifikia zaidi ya dola za kimarekani trilioni moja. Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Benki ya Wananchi wa China zinaonesha kuwa, akiba ya fedha za kigeni ya China hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Septemba ilifikia dola za kimarekani bilioni 987.9
  • Kuimarisha uvumbuzi kwahitaji kuhimiza uwekezaji unaoweza kukabiliana na hatari na ujenzi wa soko la mitaji
  •  2006/11/21
    Waziri wa sayansi na teknolojia ambaye ni mjumbe wa taasisi ya sayansi ya China, Bw. Xu Guanhua amesema, kuimarisha uwezo wa uvumbuzi kunatakiwa kuhimiza uwekezaji wenye uwezo wa kukabiliana na hali ya hatari na ujenzi wa soko la mitaji ili kuimarisha uwezo wa uvumbuzi wa kampuni na viwanda vya wastani na vidogo.
  • Ni kwanini pato linalotokana na uuzaji wa bidhaa nje la China linaongezeka kwa mfululizo?
  •  2006/11/14
    Takwimu zilizotolewa na forodha ya China zinaonesha kuwa, thamani ya biashara ya nje ya China iliweka rekodi mpya katika mwezi Agosti mwaka huu, ambapo thamani ya usafirishaji bidhaa kwa nchi za nje kwa mara ya kwanza ilizidi dola za kimarekani bilioni 90 na kufikia bilioni 90.77
    1 2 3 4 5 6 7