• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Xi kutumia hadhi yake mpya kushawishi maendeleo Afrika 2017-10-26

    Rais Xi Jinping sasa anasema atatumia hadha aliyotunukiwa katika jamii ya Kichina kuboresha maisha ya wengi katika nchi zinazoendelea. Xi anasema mawazo yake sasa zinatoa mbinu mbadala kupambana na changamoto zinazokabili nchi nyingi.

    • Xi atangaza mwamko mpya katika awamu ya pili ya utawala wake. 2017-10-26

    BAADA ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa Chama tawala cha kikomunisti,Rais wa China Xi Jinping ametangaza safu mpya ya uongozi wa kamati kuu ya chama hicho kwa muhula mpya wa miaka mitano,yenye lengo la kuimarisha ustawi na kupanua ushawishi wa taifa hilo kimataifa.

    • Balozi wa Jamhuri ya Kongo nchini China asema China imetoa mfano wa kuigwa katika kuondoa umaskini 2017-10-25

    Balozi wa Jamhuri ya Kongo nchini China Bw. Daniel Owassa amesema, tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha kikomunisti cha China ufanyike miaka mitano iliyopita, China imepata mafanikio makubwa katika kuondoa umaskini na kutoa mfano wa kuigwa kwa nchi mbalimbali duniani. Pili Mwinyi ana maelezo zaidi.

    • Kujenga mfumo wa uchumi wa kisasa kutaongoza uchumi wa China uendelezwe vizuri kwa utulivu na kupata maendeleo endelevu 2017-10-24

    Ripoti ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China imetangaza kuwa Ujamaa wenye umaalumu wa China umeingia kwenye Zama mpya. Ripoti hiyo pia imesisitiza kujenga mfumo wa uchumi wa kisasa kwa kuimarisha mageuzi ya muundo wa utoaji wa bidhaa na huduma, kuharakisha kujenga nchi yenye uvumbuzi, kutekeleza mkakati wa kusitawishavijiji na maendeleo ya uwiano wa kikanda, kuharakisha kukamilisha utaratibu wa uchumi wa soko huria wa kijamaa na kusukuma mbele hali mpya ya kufungua mlango. Wajumbe wa mkutano huo wanaona, kujenga mfumo wa uchumi wa kisasa utasaidia maendeleo endelevu ya uchumi wa China.

    • Enzi mpya China na kuongezeka kwa ushawishi wake ulimwenguni 2017-10-23

    Kote duniani, wengi wamekuwa makini na kuelekeza macho Beijing siku za hivi karibuni kutokana na mkutano wa kitaifa wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China. Bila shaka, viongozi wa dunia na watu kutoka kila ngazi ya maisha wanakodolea jicho tukio hilo linalofanyika mara moja kila baada ya miaka mitano linalofanyika kwenye mji mkuu wa China, ikiwa taarifa ni za kuaminika. Lakini, matokeo ya mkutano huo yatakayowekwa hadharani mwishoni yanasubiriwa kwa hamu na gamu zaidi na wote.

    • CPC waandaa maonyesho ya mafanikio ya awamu ya kwanza ya Rais Xi ikiwemo kuimarika ushirikiano na nchi za Afrika. 2017-10-23

    WAKATI mkutano wa taifa ya 19 wa Chama cha Kikomunisti (CPC) ukiendelea mjini hapa ,Chama hicho kimefungua maonyesho katika ukumbi mkubwa wa vyumba 10 na kuonyesha mafanikio ya awamu ya kwanza ya utawala wa Rais wa nchi hiyo Xi Jinping ikiwemo mahusiano yaliyopo baadhi ya nchi mbalimbali duniani.

    • China ya zama hizi yaweza kutoa mchango kwenye maendeleo ya dunia 2017-10-23
    Ripoti iliyotolewa na rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China imesema, Ujamaa wenye umaalumu wa China umeingia katika kipindi kipya, na China imeingia kwenye kipindi cha kihistoria na kuwa na ushawishi zaidi duniani. Lakini je China ya zama tulizonazo itakuwa na ushawishi gani kwenye hali ya dunia?
    • Wachina katika nchi za nje wasifu ripoti ya mkutano mkuu wa 19 wa CPC 2017-10-22

    Kwenye ripoti ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, rais Xi Jinping wa China ameeleza mkakati wa kuharakisha mageuzi ya utaratibu wa ustaarabu wa kiikolojia, kuhimiza maendeleo bila uchafuzi na kujenga China yenye mazingira mazuri. Wachina wengi katika nchi za nje wamesema, mazingira mazuri bila uchafuzi ni utajiri, kujenga ustaarabu wa kiikolojia ni majukumu makubwa ya wachina.

    • Kuimarisha mawasiliano ya utamaduni ni njia muhimu ya kuhimiza maelewano kati ya wananchi wa China na nchi nyingine 2017-10-21

    Wajumbe kutoka sekta za utamaduni na sanaa wanaohudhuria mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China jana wamefanya mawasiliano ya moja kwa moja na waandishi wa habari wa nchini na nje.

    • Rais Xi kuupa kipaumbele mfumo wa Ukanda mmoja Njia moja katika awamu yake ya pili madarakani 2017-10-21

    WIKI hii macho na masikio duniani yalielekezwa nchini China kunakofanyika Mkutano Mkuu wa 19 wa chama cha kikomunisti cha CPC,kinachotawala nchini hapa. Katika mkutano huo unaohudhuriwa na wajumbe 2,307 huku ukifuatiliwa kwa karibu za vyombo vya habari zaidi ya 3000,umekuwa gunzo kubwa hususan baada ya msemaji wa Chama hicho kuweka wazi Agenda za Mkutano huo.

    • China yaahidi mahusiano dhabiti na nchi marafiki baada ya mafanikio yake ya kiuchumi 2017-10-21

    Rais wa China Xi Jinping sasa anasema uchumi wa nchi yake ilistahimili dhoruba kali na kuinuka tena baada ya kipindi ambapo ilisajili utendaji usio wa kuridhisha. Kiongozi huyo wa Kichina alisema hayo huku akisisitiza kuwa Beijing itabaki mwamba wa kiuchumi duniani. Rais huyo alifichua kwamba pato la nchi yake limeongezeka kwa trilioni 4 Dola za Marekani katika miaka mitano iliyopita.

    • Maofisa wa Afrika wajadili ripoti iliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa 19 wa CPC
     2017-10-20

    Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC unafanyika hapa Beijing. Ripoti iliyotolewa na katibu mkuu wa Kamati kuu ya chama hicho Bw. Xi Jinping ambaye pia ni rais wa China kwenye mkutano huo inafuatiliwa sana na dunia nzima zikiwemo nchi za Afrika.

    • Wajumbe waona ripoti ya kamati kuu ya CPC imedhihirisha mwelekeo wa kazi katika muda mrefu za baadaye
     2017-10-19

    Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC ulifunguliwa jana hapa Bejing. Kwa niaba ya Kamati kuu ya 18 ya CPC, Bw. Xi Jinping alitoa ripoti ya Kukamilisha Kujenga Jamii yenye Maisha Bora kwa Pande zote, na Kupata Mafanikio Makubwa ya Ujamaa wenye Umaalumu wa China katika Kipindi Kipya. Wajumbe wanaohudhuria mkutano huo wanajadili ripoti hiyo, na kuona imedhihirisha mwelekeo wa kazi katika muda mrefu wa baadaye.

    • Xi Jinping atangaza Ujamaa wenye umaalumu wa China kuingia kipindi kipya
     2017-10-18

    Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China umefunguliwa leo hapa Beijing. Kwa niaba ya kamati kuu ya 18 ya chama hicho, Bw. Xi Jinping amehutubia mkutano huo akitangaza kuwa, kwa kufuata itikadi ya Ujamaa wenye umaalumu wa China katika kipindi kipya, Chama cha Kikomunisti cha China kitaongoza wananchi wa China kukamilisha kazi ya kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

    • Mwandishi wa habari wa Jamhuri ya Watu wa Congo atarajia maendeleo mazuri zaidi ya China
     2017-10-17

    Mwandishi wa habari mwandamizi wa Gazeti la Le Potentiel la Jamhuri ya Watu wa Congo Bw. Cyprien Kapuku ambaye yupo China kuripoti Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China jana alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari amesema, mafanikio ya maendeleo ya China yamepatikana kutokana na juhudi za wachina chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, na anatarajia China itapata maendeleo mazuri zaidi baada ya mkutano huo.

    • Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China kutunga mpango wa maendeleo ya China
     2017-10-16

    Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China utafunguliwa tarehe 18 hapa Beijing. Profesha Yan Shuhan kutoka Chuo cha Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China amesema, mkutano huo utafanya majumuisho ya uzoefu wa miaka iliyopita, na kutunga mipango ya siku zijazo, na utafanya kazi muhimu katika mchakato wa kuendeleza shughuli za ujamaa wenye umaalumu wa China .

    • Chama cha CCM Zanzibar chaeleza matumaini yake kwa mkutano mkuu wa 19 wa CPC cha China 2017-10-16
    • Mkurugenzi wa kituo cha kuwaokoa wanyama pori nchini Zimbabwe amsifu rais Xi Jinping wa China kwa nia yake ya kuwahifadhi wanyama 2017-10-13

    Mwishoni mwa mwaka 2015 rais Xi Jinping wa China na mke wake walipofanya ziara nchini Zimbabwe walitembelea kituo cha kuwaokoa wanyama pori nchini humo. Hii ni mara ya kwanza kwa kituo hicho chenye historia ya miaka 20 hivi kutembelewa na kiongozi wa nchi ya nje. Mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Roxy Danckwerts alipokumbuka kukutana na rais Xi Jinping, alisema rais Xi ni mtu mwenye nia halisi ya kuhifadhi wanyama.

    • Kumbukumbu ya mwalimu wa chuo kikuu nchini Jamhuri ya Congo kuhusu rais Xi Jinping wa China 2017-10-12

    Tarehe 30 mwezi Machi mwaka 2013, rais Xi Jinping wa China aliyefanya ziara nchini Jamhuri ya Congo, yeye pamoja na mwenyeji wake rais Denis Sassou-Nguesso walishiriki kwenye sherehe ya kuzinduliwa kwa maktaba ya Chuo Kikuu cha Marien Ngouabi iliyojengwa kwa msaada wa China. Rasi Xi pia alifanya mazungumzo na mwalimu wa chuo cha Confucius Bi. Ai Jia. Hivi sasa ni miaka 4 imepita tangu rais Xi afanye ziara hiyo, lakini Bi. Ai Jia bado anakumbuka hali ya wakati ule.

    • Kuboreshwa kwa mazingira ya biashara nchini China kunazinufaisha kampuni za nchi za nje 2017-10-11

    Wakurugenzi wa kampuni nyingi za nchi za nje nchini China hivi karibuni walipohojiwa na waandishi wa habari wa Redio China Kimataifa walisema, katika miaka mitano iliyopita kampuni zao zimeona mabadiliko mazuri ya soko la China, pia zimenufaika na sera husika za China. Kutokana na utekelezaji wa pendekeo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na mpango wa "Made in China 2025", kampuni hizo zina imani kubwa na mustakabali wa soko na uchumi wa China.

    • Uzoefu wa China kwenye kupunguza umaskini waigwa na dunia 2017-10-10

    Mkutano wa ngazi ya juu wa kupunguza umaskini na kupata maendeleo umefanyika jana hapa Beijing. Ikiwa nchi iliyotoa mwito wa kupunguza umaskini na nguvu kubwa ya kuhimiza shughuli za kupunguza umaskini duniani, China imepata mafanikio makubwa, na uzoefu wa China kwenye kupunguza umaskini unaigwa na nchi nyingine duniani.

    • Xi Jinping ahimiza kuunda jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu wote
     2017-09-26

    Mkutano mkuu wa Shirika la Polisi la Kimataifa Interpol umefunguliwa leo hapa Beijing. Rais Xi Jinping wa China amehudhuria na kuhutubia mkutano huo, akihimiza pande mbalimbali kuunda jumuiya yenye mustakabali wa pamoja inayoweza kuhakikisha usalama wa binadamu wote, na kutoa mapendekezo kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano wa usalama wa utekelezaji wa sheria duniani.

    • Maonesho ya 24 ya kimataifa ya vitabu yafanyika Beijing 2017-08-23
    Maonesho ya 24 ya kimataifa ya vitabu yamefunguliwa leo hapa Beijing. Mashirika zaidi ya 2,500 kutoka nchini mbalimbali duniani yameonesha aina zaidi ya laki tatu za vitabu vilivyochapishwa hivi karibuni, na kati ya mashirika hayo, asilimia 58 yanatoka nchi za nje.
    • Kituo cha ujuzi wa maendeleo ya dunia cha China chazinduliwa 2017-08-22

    Kituo cha ujuzi wa maendeleo ya kimataifa cha China kimezinduliwa rasmi hapa Beijing, sambamba na ripoti kuhusu hatua inayopigwa na China katika kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030. Hizi ni hatua mbili zilizochukuliwa na China ili ya kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 iliyowekwa na Umoja wa Mataifa. Rais Xi Jinping wa China na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa walitoa salamu za pongezi.

    • Muujiza wa kubadilisha jangwa kuwa msitu huko Saihanba 2017-08-07

    Msitu wa Saihanba wenye ukubwa wa hekta elfu 74.7 ulioko kilomita 200 kaskazini mwa mji wa Beijing nchini China, ni msitu mkubwa zaidi duniani uliopandwa na watu. Wafanyakazi wa shamba la msitu huo wametimiza muujiza wa kubadilisha jangwa kuwa msitu katika zaidi ya nusu karne iliyopita.

    • Wakulima wa mkoa wa Xizang wanufaika na utalii wa vijiji 2017-08-04

    Kijiji cha Zhangba mkoani Xizang kiliunda shirikisho la utalii wenye umaalumu wa huko mwezi Oktoba mwaka 2010. Kuanzia wakati ule, kijiji hicho kimeshughulikia utalii unaoshirikisha chakula cha Xizang, nyimbo na ngoma, desturi ya maisha ya huko, michezo na kukaa kwenye nyumba za wakulima. Utalii umeleta faida halisi kwa kijiji hicho, na kutoa mchango mkubwa kwa juhudi za kijiji hicho kuondoa umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako