Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
v Watu wanaotunza Kasri la Potala 2007/06/13
Kwenye mlima mwekundu wa Lahsa, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa Tibet, kusini magharibi mwa China kuna Kasri la Potala linalojulikana sana duniani. Ili kuhifadhi kasri hilo takatifu la kabila la Watibet, na kuwawezesha watu dunia kujionea utakatifu na uzuri wa kasri hilo, wafanyakazi na watawa wa idara ya usimamizi wa Kasri la Potala wamefanya juhudi kubwa katika kulitunza kasri hilo.
v Mtunzi wa muziki wa kabila la Wa-mongolia Bwana Yong Rubu 2007/05/23
Bwana Yong Rubu alizaliwa kwenye mbuga mzuri wa Kerqin wa mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani, ambako ni maskani maarufu ya nyimbo na ngoma ya kabila la wamongolia. Kutokana na kuathiriwa na muziki wa huko, Bwana Yong Rubu alikuwa anapenda sana muziki tangu utotoni mwake, alipokuwa na umri wa miaka 14 alijiunga na jeshi na kuwa askari wa michezo ya sanaa
v Vitu vya sanaa za mikono vya makabila madogo madogo mkoani Qinghai  2007/05/09
Katika mkoa wa Qinghai, kaskazini magharibi mwa China, wanaishi watu wa makabila mengi yakiwemo Wa-han, Wa-tibet, Wa-hui, Wa-tu, Wa-sala na Wa-mongolia. Watu wa makabila hayo wanapojitahidi kujiendeleza kiuchumi, pia wamevumbua utamaduni wenye umaalum wa kikabila. Hadi baadhi ya ustadi wa kutengeneza vitu vya sanaa kwa mkono bado unaenea.
v Kabila la wamiao la China 2007/05/02
Miao ni moja kati ya makabila madogomadogo ya China. Nchini China kuna wamiao milioni saba na laki nne, ambao wanakaa huko Guizhou, Yunan, Guangxi, Hainan na mikoa mingine zaidi ya 10. Hapo zamani, wamiao walikuwa wanahamahama kukimbilia vita na maisha magumu. Kwa hivyo, wamiao wanaishi katika sehemu mbalimbali nchini kote, na hata wamevuka bahari na kuelekea katika nchi za ng'ambo.
v Maisha ya watawa wa mahekalu ya dini ya kibudha ya Kitibet 2007/04/19
Hekalu la Mingzhulin lililoko katika wilaya ya Zhalang, kusini mwa mkoa unaojiendesha wa Tibet ni la kundi la Ningma la dini ya kibudha ya Kitibet, hekalu hilo watawa 54 na limekuwa na historia ya miaka zaidi ya 300.
v Watu wa kabila la Wa-elunchun waishio milimani 2007/04/11
Mliyosikia ni sauti iliyoko kwenye filamu iliyopigwa katika miaka ya 60 ya karne iliyopita iitwayo "Watu wa kabila la Wa-elunchun". Filamu hiyo ilionesha watu wa kabila la Wa-elunchun wenye idadi ya watu wasiozidi elfu 10 walivyoishi sehemu ya milimani kwa kuwinda wanyama pori.
v Maisha ya wafugaji wa kabila la Wamongolia yaboreshwa 2007/04/04
Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani ulioko kaskazini mwa China unajulikana kwa kuwa na mbuga pana za kimaumbile, wafugaji wa kabila la Wamongolia waliwahi kuishi maisha ya kuhamahama, walitafuta maji na malisho huku wakiweka makambi kila mahali walikoenda. Hivi sasa maisha ya wafugaji kwenye mbuga za Mongolia ya ndani yamepata mabadiliko makubwa.
v Mtaa wa Beijing wanakoishi wakazi wengi wa makabila madogo madogo 2007/03/28
Katika mtaa wa Hepingli Jiaotong ulioko kwenye sehemu ya mashariki ya Beijing, wanaishi wakazi wa makabila madogo madogo 29 wakiwemo kabila la Wa-mongolia, Wa-tibet, Wa-hui, Wa-zhuang na Wa-yi.
v Kabila la Wa-Tu wanavyosherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi ya China 2007/03/14
Kijiji cha Wushi kiko katika wilaya inayojiendesha ya kabila la Wa-Tu ya mkoa wa Qinghai, kaskazini magharibi mwa China, kijiji hicho kina familia zaidi ya 160 ambazo ni za makabila matatu ya Wa-Tu, Wa-Han na Wa-Tibet, idadi kubwa ya watu wa kijiji hicho ni Wa-Tu.
v China yavumbua simu ya mkononi inayotumia maandishi ya lugha za makabila madogo 2007/03/07
China ina idadi ya watu zaidi ya bilioni 1.3, licha ya kabila la Wa-Han ambalo linachukua asilimia zaidi ya 90 ya idadi ya jumla ya watu wa China, bado kuna makabila 55 madogo, na makabila mengi madogo yana maandishi ya lugha zake.
v Bw. Essa Han na kampuni yake ya kutengeneza mavazi na vifaa vya kiislamu 2007/02/22
Huko Xining, mkoani Qinghai kaskazini magharibi mwa China, kuna kampuni inayoitwa Yijia inayoshughulikia utengenezaji na biashara ya mavazi na vifaa vya kiislamu. Katika karakana za kisasa za kiwanda hicho, wafanyakazi walikuwa wanatumia mitambo kwa ustadi wakitengeneza mavazi mbalimbali ya kiislamu
v Mafundi wa kabila la Wahezhe waendeleza ufundi wa jadi 2007/02/15
Mliosikia ni wimbo unaojulikana miongoni mwa watu wa kabila la Wahezhe, uitwao kaka aliyekwenda kuwinda amerudi nyumbani. Hapo awali Wahezhe walikuwa wanajishughulisha na uvuvi na uwindaji, walikuwa hodari katika mambo ya uvuvi na uwindaji, kama vile kutengeneza mashua kwa magamba ya miti na kutengeneza nguo kwa kutumia ngozi ya samaki. Hivi sasa baadhi ya Wahezhe wameanza kujishughulisha na kilimo au viwanda. Je, ufundi wa jadi wa kabila hilo unaendelea vipi?
v Mlinzi wa mpaka wa kabila la Wakyrgiz 2007/02/08
China na Kyrgizistan ni nchi jirani. Zaidi ya kilomita 100 za mpaka kati ya nchi hizo mbili zipo katika wilaya ya Tugumaiti ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Wauygur, kaskazini magharibi mwa China. Katika wilaya hiyo, mbali na wanajeshi wa China, watu wa kabila la Wakyrgiz pia wanashiriki kwenye shughuli za kulinda mpaka.
v Kuwatembelea Wamaonan nyumbani kwao 2007/01/25
Kabila la Wamaonan lina watu wapatao elfu 80 tu, ni moja kati ya makabila madogomadogo 22 yenye watu wachache nchini China. Wamaonan wanaishi kwenye mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China.
v Dada Gulpiye, mrembo wa kabila la Wauygur 2007/01/18
Fainali ya mashindano ya tatu ya kumtafuta mwanamitindo mrembo wa China ilimalizika hivi karibuni huko Sanya, mkoani Hainan, kusini mwa China. Wasichana wapatao 48 kutoka kila kona ya China walishiriki kwenye kinyang'anyiro hicho. Msichana Gulpiye mwenye umri wa miaka 14 tu kutoka kabila la Wauygur ni mmoja kati ya wasichana hao. Yeye ni msichana mdogo kuliko wenzake wengine walioshiriki.
v Watu wa kabila la Wajing wanaoishi visiwani karibu na mpaka wa Vietnam 2007/01/11
Miongoni mwa makabila yote 56 hapa nchini China, kabila la Wajing ni kabila lenye watu wachache sana, ambao wanaishi kwenye visiwa vitatu vilivyopo kusini mwa China, kwenye mpaka kati ya China na Vietnam. Hivi karibuni mwandishi wetu wa habari aliwatembelea watu hao kwenye kijiji kiitwacho Wanwei.
v Lugha ya Kitatar yasaidia kupokezana kwa utamaduni wa kabila la Watatar 2007/01/04
Miongoni mwa waislamu wanaoishi katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauygur wa Xinjiang, China, Watatar ni kabila lenye watu wachache zaidi kuliko makabila mengine. Kabila hilo sasa lina watu elfu 6 hivi, ni kabila dogo kati ya makabila madogomadogo yapatayo 55 ya China
v Wakhazak wapata uwezo kwa kuendeleza utalii wa aina ya kabila hilo 2006/12/28
Wakhazak ni miongoni mwa watu wa makabila 55 madogomadogo ya China. Kabila hilo ni kabila la wafugaji wanaohamahama, kwa hiyo Wakhazak wanatupa taswira ya watu wanaoambatana na farasi.
v Utalii waleta maisha mapya kwa wakazi wa mkoani Xinjiang 2006/12/14
Mkoa unaojiendesha wa Uigur wa Xinjiang ulioko kaskazini magharibi mwa China una maliasili nyingi za utalii, sehemu za kiutamaduni, mandhari ya kimaumbile na mila na desturi za makabila madogo madogo zina umaalum wa kipekee.
v Vijana kutoka makabila madogomadogo ya China kuhitimu masomo ya chuo kikuu mwaka huu 2006/11/30
Nchini China mamilioni ya vijana wanahitimu masomo ya vyuo vikuu kila mwaka. Miongoni mwao kuna vijana wa makabila madogomadogo ambao maskani yao yako mbali na miji. Hivi karibuni mwandishi wetu wa habari alizungumza na wanafunzi kadhaa wa vyuo vikuu wanaotoka kwenye makabila madogomadogo ambao wanatarajiwa kuhitimu mwakani.
v Maisha mapya ya wafugaji wa kabila la Wamongolia wa China 2006/11/16
Mji wa Erdos upo katika sehemu ya magharibi ya mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani wa China, ambako wanaishi watu wengi wa kabila la Wamongolia. zamani sehemu hiyo ilikuwa na hali mbaya na mazingira asili na hali duni ya kimaendeleo
v Kijiji cha kabila la Wadulong kilichopo milimani 2006/10/26
Wadulong wanaishi Katika eneo la mtiririko wa mto wa Dulong kusini magharibi mwa China. Kabila hilo sasa lina watu 5,800 tu, ni miongoni mwa makabila yenye watu wachache sana hapa nchini China.
v Mafanikio yaliyopatikana mkoani Guangxi, China katika kuondoa umaskini yawavutia maofisa wa nchi za Afrika 2006/10/12
Mwezi Julai mwaka huu wageni kutoka Afrika walitembelea vijiji vya mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, China.
v Mwalimu wa kabila la Wapumi aliyeanzisha tovuti ya utamaduni wa Kipumi  2006/09/21
Bw. Xiong Guihua anafanya kazi kwenye kompyuta, akiwa na pilika pilika za kuboresha tovuti moja kwenye mtandao wa Internet iitwayo pumi.
v Watu wa kabila la Wanu wapata maendeleo kwa kujishugulisha na utalii 2006/09/14
Kabila la Wanu ni kabila lenye watu wachache nchini China. Wanu wengi wanaishi kando ya bonde la mto wa Nujiang, mkoani Yunnan, kusini magharibi mwa China. Eneo hilo la milima lina hali duni ya mawasiliano, hali ambayo imefanya kabila hilo liwe nyuma kimaendeleo 
v Sikukuu ya mwenge ya kabila la Wayi 2006/09/07
Mliosikia ni wimbo maarufu wa kabila la Wayi uitwao "Nyimbo za kienyeji zinazotoka mto wa Yuni". Kati ya makabila madogo mbalimbali ya China, kabila la Wayi linajulikana kwa kuwa na utamaduni maalumu na sikukuu za jadi.
v Wasichana wa milimani wanaopenda kuimba nyimbo  2006/08/31
Mwezi Juni mwaka huu, kutokana na mwaliko wa Radio China Kimataifa watoto 10 kutoka sehemu ya milimani wanakoishi watu maskini mkoani Guizhou, kusini magharibi mwa China walitembelea ofisi za Radio China Kimataifa.
v Wanafunzi wa vyuo vikuu wa China waanzisha biashara kwenye mtandao wa Internet 2006/08/24
Je, unataka kuanzisha duka lako kwenye mtandao wa Internet? Hivi sasa hapa nchini China wanafunzi wengi wa vyuo vikuu wanavutiwa na mpango huo na baadhi yao wameanza kuutekeleza.
v Wageni wafurahia uzinduzi wa reli ya Qinghai-Tibet 2006/08/10
Reli ya Qinghai-Tibet iliyoko kwenye uwanda wa juu wenye mwinuko mkubwa kabisa duniani ilizinduliwa tarehe mosi Julai mwaka huu, jambo hilo lilimaliza historia ya mkoa unaojiendesha wa Tibet, kutokuwa na reli inayoiunganisha na mikoa mingine ya China.
v Kampeni ya kuwafuatilia watoto wa kike: China yachukua hatua kuzuia hali ya kutokuwepo kwa uwiano wa kijinsia 2006/07/27
Kutokana na Sensa iliyofanywa na serikali ya China mwaka 2000, miongoni mwa watoto waliozaliwa nchini China, uwiano wa idadi ya watoto wa kiume na wa kike ni 119 kwa 100, lakini wastani wa kiasi cha kawaida ni kati ya watoto wa kiume 103 na 107 kwa watoto wa kike 100.
1 2 3 4 5