Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
v Watoto wa kabila la Wapumi waliokosa elimu warudi shuleni 2006/07/13
Kabila la Wapumi lina watu wasiozidi elfu 30, ni miongoni mwa makabila madogomadogo yenye watu wachache hapa nchini China. Wapumi wengi wanaishi katika wilaya ya Lanping, mkoani Yunnan, kusini magharibi ya China, ambapo kutokana na umaskini sehemu hiyo haikuwa na shule, na watoto wengi wa kabila la Wapumi walikuwa wanashindwa kupata elimu
v Wabuyi wapata maendeleo ya kiuchumi na kuboresha mazingira  2006/07/06
Kabila la Wabuyi lina watu milioni 3 hivi, ni moja kati ya makabila madogomadogo hapa nchini China. Wabuyi wengi wanaishi katika mikoa ya Guizhou, Yunnan na Sichuan, kusini magharibi mwa China. Hapo awali Wabuyi walikuwa wanajishughulisha na kilimo tu, kama vile kilimo cha mipunga.
v Serikali ya China yasaidia makabila madogo yenye watu wachache 2006/06/29
China ni nchi yenye makabila mengi. Mbali na kabila la Wahan, kuna makabila mengine 55 madogomadogo, na miongoni mwa makabila hayo, 22 yana idadi ya watu isiyozidi laki moja kwa kila moja, kwa hiyo yanaitwa makabila madogo yenye watu wachache.
v Maisha ya mhamiaji wa kwanza katika mradi wa maji wa magenge matatu yalivyo sasa 2006/06/15
Mradi wa magenge matatu katika mto Changjiang nchini China, ni mradi mkubwa kabisa wa maji duniani wenye malengo ya kudhibiti mafuriko, kuzalisha umeme na kuhimiza usafiri wa meli. Ujenzi wa mradi huo ulioanzishwa mwaka 1992 unatarajiwa kukamilika kabisa mwaka 2009
v Harakati ya kuokoa lugha ya Kiman yatekelezwa nchini China 2006/06/01
Kabila la Waman ni kabila kubwa la tatu nchini China, ambalo lina watu milioni 10. Lakini hivi sasa watu wanaofahamu kuongea lugha ya Kiman hawazidi 100. Kwa mujibu wa makadirio ya wataalamu, uzungumzaji sanifu wa Kiman utatoweka kabisa ndani ya miaka mitano au kumi ijayo kama hatua za haraka hazijachukuliwa.
v Msomi wa Tibet Bw. Puqiong na wanafunzi wake wa kigeni 2006/05/11
Mwezi Machi mwaka jana, watu 6 kutoka Japan, Italia, Marekani na Korea ya Kusini waliwasili katika Chuo kikuu cha Tibet, huko Lhasa, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa Tibet, na kuanza masomo ya fasihi ya lugha ya Kitibet yatakayochukua muda wa miaka miwili
v Washabiki wa Wushu wa Kabila la Wahui  2006/05/04
Kati ya makabila madogomadogo hapa nchini China, kabila la Wahui ni kabila linalopenda Wushu. Tangu enzi na dahari, kulikuwa na desturi za kufanya mazoezi ya Wushu katika makazi wanayoishi Wahui wengi. Hapa mjini Beijing ambao ni mji mkuu wa China, hivi sasa pia kuna Wahui wengi wanaocheza Wushu.
v Kabila la Wazhuang na utamaduni wa matamasha ya nyimbo za kienyeji 2006/04/27
Tamasha la nyimbo za kienyeji la kabila la Wazhuang linajulikana nchini China. Tamasha hilo ni utamaduni maalumu wa Wazhuang wanaoishi katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini magharibi mwa China.
v Waliotegemea misaada ya chakula sasa wabadilika kuwa watu wenye uwezo  2006/04/20
Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang upo kwenye sehemu ya mpaka wa kaskazini na magharibi mwa China. Kijiji cha Daxi mkoani humo kinapakana na jangwa la Taklimakan.
v Hifadhi ya utamaduni wa makabila madogomadogo nchini China 2006/04/13
China ni nchi yenye makabila madogomadogo yapatayo 55, kila kabila lina utamaduni maalumu. Utamaduni wa jadi ni kielelezo cha kabila, lakini sambamba na maendeleo ya uchumi na jamii, utamaduni huo ni rahisi kupotea kama ukikosa hifadhi mwafaka.
v Mkulima Mzee Zheng na shughuli zake za kuonesha filamu 2006/04/06
Siku moja wakati wa mchana katika majira ya Mchipuko, mkulima mzee Zheng na mke wake walichukua mashine kongwe ya kuoneshea filamu na sanduku moja la chuma lenye rangi ya kijani kutoka kwenye nyumba yao. Halafu wakulima hao wa kijiji cha Shuiqiao, mkoani Sichuan, China walimbebesha farasi mmoja mwekundu vitu hivyo.
v Bw. Yang Fuxi na pinde za jadi za kabila la Waman 2006/03/16
Kabila la Waman ni miongoni mwa makabila madogomadogo nchini China. Waman wengi wanaishi katika eneo la kaskazini la China, hasa mkoa wa Liaoning uliopo kaskazini mashariki ya China.
v Maisha ya ajabu ya mwanamke aliyekuwa mtumwa huko Tibet ya zamani  2006/03/09
Mama Tshering Ihamo ana umri wa miaka 79, anaishi kwenye makazi yake yaliyopo katika wilaya ya Nedong, kanda ya Lhoka mkoani Tibet.
v Wakulima na wafugaji mkoani Tibet wafurahia filamu zinazotafsiriwa kwa lugha ya Kitibet  2006/03/02
Kuonesha filamu zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kitibet ni jambo linalowafurahisha watu wa Tibet. Bibi Zholma kutoka kabila hilo alieleza kuwa anafurahia filamu hizo kwa kuwa, anapata sura ya dunia iliyo nje ya maskani yake na ujuzi unaomsaidia katika shughuli za kilimo. 
v Waandishi hodari wa Kabila la Wamulao 2006/02/23
Watu wa kabila la Wamulao wanaishi katika mkoa wa Guangxi, kusini mwa China. Kabila hilo lina watu wapatao laki moja na elfu 50 kwa hivi sasa, lakini miongoni mwao wamejitokeza waandishi hodari zaidi ya 50 ambao wanatunga fasihi kuhusu maisha ya watu wa kabila la Wamulao.
v Msanifu wa mavazi ya kabila la Wahui Bi. Ma Shumin 2006/02/09
Kabila la Wahui ni moja ya makabila madogo madogo yenye idadi kubwa ya watu nchini China, walienea katika sehemu mbalimbali nchini China. Kutokana na kuishi pamoja na makabila mengine kwa muda mrefu, umaalum wa mavazi yao umekuwa ukififia siku hadi siku
v Sehemu ya hifadhi ya kimaumbile ya Qiangtang ya China 2006/01/26
Sehemu ya hifadhi ya kimaumbile ya Qiangtang iliyoko kwenye sehemu ya mpaka kati ya mkoa unaojiendesha wa Tibet, mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur na mkoa wa Qinghai ni moja ya sehemu ambazo mazingira ya viumbe yamehifadhiwa vizuri duniani, na yenye aina nyingi za wanyama na mimea pori.
v Idara za dini za China zaimarisha maingiliano na mawasiliano ya kimataifa 2006/01/19
Shirikisho la maingilaino ya utamaduni wa kidini la taifa la China ambalo ni jumuiya ya kiraia inayoundwa na makundi ya dini mbalimbali ya China, lilianzishwa tarehe 30 Desemba mwaka 2005 hapa Beijing.
v Waislamu wa China wapate urahisi kwenda kuhiji huko Makka 2006/01/12
Mwezi wa Desemba mwaka 2005 ulikuwa mwezi wa waislamu waishio katika sehemu mbalimbali duniani kwenda Makka, kufanya hija, na kati ya mahujaji milioni moja hivi, walikuwepo waislamu 7000 hivi kutoka China.
v Profesa wa muziki wa chuo kikuu cha sanaa cha Xinjiang Bw. Sulaman Imin 2006/01/05
Muda si mrefu uliopita muziki wa jadi wa kabila la Wauygur uitwao "Mukham 12" ulithibitishwa kuwa urithi wa utamaduni simulizi na shirika la elimu, sayansi ya utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO. Muziki wa "Mukham 12" ulitungwa na kukamilika baada ya miaka mia kadhaa, ni mchanganyiko wa nyimbo, ngoma na muziki, umesifiwa kuwa mama wa muziki wa kabila la Wauygur.
v Sketi zenye malinda zaelezea maisha kamili ya wanawake wa kabila la Wayi 2005/12/29
Ukienda kwenye sehemu ya kusini magharibi mwa China wanakoishi watu wa kabila la Wayi, utawaona wanawake wa kabila hilo waliovaa sketi zenye malinda hapa na pale. Wimbo mliosikia ulieleza uzuri wa wanawake waliovaa sketi zenye malinda.   
v Panchen Lama wa 11 amekuwa kiongozi anayeheshimiwa sana na waumini wa dini ya kibudha ya kitibet 2005/12/22
Zaidi ya miaka 10 iliyopita, mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 5 wa kabila la watibet alirithi rasmi kuwa Panchen Lama wa 11 kutokana na utaratibu wa dini ya kibudha ya kitibet. Tarehe 8 mwezi huu sherehe ya kuadhimisha miaka 10 tangu Panchen Lama wa 11 arithi nafasi hiyo
v Maisha ya watawa wa madhehebu ya kibudha ya Kitibet 2005/12/08
Hekalu la Mingzhulin lililoko katika wilaya ya Zhalang, kusini mwa mkoa unaojiendesha wa Tibet linamilikiwa na kikundi cha Ningma cha madhehebu ya kibudha ya Kitibet, lina watawa 54 na limekuwa na historia ya miaka zaidi ya 300.
v Bi. Bahargul aliyestaafu kuanzisha shule ya kazi za kiufundi 2005/12/01
Bi. Bahargul alikuwa mwalimu kwenye mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, kaskazini magharibi mwa China. Baada ya kustaafu, tofauti na watu wengine wa rika lake waliopumzika nyumbani na kujiburudisha kwa kutalii hapa na pale, yeye alianzisha shule ya kazi za kiufundi kwa kukusanya fedha. 
v Watu wa kabila la Wamongolia waabudu rangi nyeupe 2005/11/17
Kwenye mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani, kaskazini ya China, wanaishi watu wa kabila la Wamongolia ambao wanaoishi maisha ya kuhamahama.  
v Sanaa za utamaduni wa jadi wa kitibet zawavutia wateja 2005/11/10
Watu wa kabila la watibet waishio kwenye uwanda wa juu kabisa duniani, wamevumbua utamaduni mzuri wa jadi uliokuwepo katika maelfu ya miaka iliyopita, ambao ni pamoja na unajimu, kalenda ya jadi, ustadi wa kisanaa, matibabu, fasihi, mavazi, mapambo na michoro yenye umaalum wa kikabila 
v China yaboresha maisha ya makabila yenye idadi ndogo ya watu 2005/10/27
Kabila la Wamaonan ni moja ya makabila yenye idadi ndogo sana ya watu nchini China, wanaishi katika wilaya inayojiendesha ya kabila la Wamaonan ya mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China.
v Wakulima wa Xinjiang wanaopata maendeleo ya kiuchumi haraka  2005/10/20
Eneo la mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur linachukua moja kati ya sita ya eneo lote la ardhi ya China, ni mkoa wenye eneo kubwa kabisa nchini China, una mashamba ya kilimo zaidi ya hekta milioni tatu.
v Mradi wa kupunguza maafa ya tetemeko la ardhi waletea maisha mazuri kwa watu wa makabila mbalimbali wa Xinjiang  2005/10/13
Mkoa unaojiendelesha wa Xinjiang Uyghur uko Kaskazini-Magharibi mwa China ambako tetemeko la ardhi hutokea mara kwa mara. Mwaka 2003 matetemeko ya ardhi yenye nguvu ya 4 kwenye kipimo cha Richter yalitokea mara 61
v Utalii waleta maisha mapya kwa wakazi wa mkoani Xinjiang 2005/10/06
Mkoa unaojiendesha wa Uigur wa Xinjiang ulioko kaskazini magharibi mwa China una maliasili nyingi za utalii, sehemu za kiutamaduni, mandhari ya kimaumbile na mila na desturi za makabila madogo madogo zina umaalum wa kipekee. Baada ya maendeleo ya miaka kumi kadhaa, utalii umetoa mchango mkubwa kwa uchumi wa mkoa huo 
1 2 3 4 5