Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
v Serikali ya mji wa Wulumuqi yawasaidia watu wa makabila madogo madogo kupata ajira 2008/01/23
Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang uko kwenye mpaka wa kaskazini magharibi nchini China. Kwenye mkoa huo kuna watu wa makabila 46 madogo madogo.
v Vipindi vya uhifadhi wa mazingira shuleni kwenye uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet 2008/01/16
Sehemu ya kusini magharibi ya mkoa wa Qinghai, inajulikana kama Chanzo cha Mito Mitatu kutokana na kuwa na vyanzo vya mito mitatu mikubwa ya China ya Changjiang, Huanghe na Lancangjiang. Sehemu hiyo iliyoko katikati ya Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet ina mito na maziwa mengi, ni chanzo muhimu cha maji nchini China.
v Hatua za serikali ya Qinghai zawahimiza wafugaji wa makabila madogo madogo kuongeza mapato kupitia kushiriki kwenye shughuli za utamaduni 2008/01/09
Kikundi cha Aisaimai kilianzishwa mwaka 2004, waimbaji na wachezaji wa kikundi hicho wengi ni wa makabila ya Watibet na Wamongolia. Katika miaka mitatu iliyopita, kikundi hicho kilifanya maonesho kwenye sehemu mbalimbali nchini China
v Juhudi za kuhifadhi mazingira mkoani Tibet 2008/01/02
Mkoa unaojiendesha wa Tibet ulioko kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet unajulikana kama paa la dunia na ncha ya tatu duniani. Kwenye mkoa huo, kuna wakazi wa makabila mbalimbail yakiwemo ya Watibet, Wahan, Wahui, Wamenba, Waluoba, Wanaxi, Wanu na Wadulong, na miongoni mwao watu wa kabila la Watibet ni wengi zaidi.
v Maisha mapya ya wafugaji wa kabila la Watibet wanaoishi mkoani Qinghai 2007/12/26
Sehemu ya kusini magharibi ya mkoa wa Qinghai, inajulikana kama Chanzo cha Mito Mitatu kutokana na kuwa na vyanzo vya mito mitatu mikubwa ya China ya Changjiang, Huanghe na Lancangjiang.
v Mchango wa baiskeli katika kupunguza msongamano barabarani 2007/12/20
Ukweli wa mambo unaonesha kuwa baiskeli ni njia rahisi ya mawasiliano katika hali ya msongamano wa barabarani. Kwa mfano mjini Beijing, kwenye kipindi pilikapilika nyingi za matumizi ya magari barabarani, magari yanakwenda kwa kasi ya wastani wa kilomita 8 hadi 12 kwa saa, wakati baiskeli zinaweza kwenda kwa kilomita 15 kwa saa.
v Ngoma ya Sarhe ya kabila la Wa-tu 2007/12/19
Kwenye vijiji vya kabila hilo wakati wazee wanapofariki dunia, wanavijiji husanyika kucheza ngoma ya Sarhe usiku kucha, na hata kwa siku kadhaa. Inasemekana kuwa chanzo cha ngoma hiyo ni ngoma ya vita na ya sadaka ya wahenga wa kabila la Wa-tu.
v Kabila la Washui mkoani Guizhou, China 2007/12/05
Miongoni mwa makabila mbalimbali nchini China, watu wa kabila la Washui wanaoishi kwenye mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China wana lugha yao na maandishi ya lugha, makabila kama hilo ni machache nchini China.
v Familia kubwa ya kabila la Warussia 2007/11/28
Wapendwa wasikilizaji, karibuni katika kipindi hiki cha makabila madogo madogo nchini China. Kwenye mji wa Yining wa mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang, kuna familia moja ya kabila la Warussia yenye watu wengi, wakiwemo bibi Nina, Bw. Nicola ambaye ni mkuu wa shule ya kabila la Warussia, na Bw. Alexander ambaye anaendesha kituo cha kutengeneza kodiani, Bibi Dina mwenye duka la mikate, na watu wengine wengi. Leo tutawaletea maelezo kuhusu familia hiyo.
v Familia ya kabila la Watibet kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet 2007/11/21
Bw. Kharsicer mwenye umri wa miaka 57 ni mfugaji mmoja wa kawaida anayeishi kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet. Nyumba yake iko kwenye mbuga ya heri kando ya ziwa Qinghai, na ina vyumba tisa. Kutokana na kuwa kwenye uwanda wa juu, vyumba hivyo vilifungwa vizuri kwa vioo ili kuzuia baridi.
v Mjumbe wa kabila la Watibet kwenye mikutano mikuu ya Chama cha Kikomunisti cha China  Bw. Gesangdunzhu 2007/11/14
Mkurugenzi wa kamati ya mambo ya makabila madogo madogo ya mkoa wa Yunnan Bw. GeSangdunzhu, ambaye alichaguliwa kuwa mjumbe wa kabila la Watibet kwenye mikutano mitatu mikuu mfululizo ya Chama cha Kikomunisti cha China.
v Watu wa kabila la Wasala wanaoishi kando ya Mto Huanghe 2007/11/07
Kwenye sehemu ya juu ya Mto Huanghe, kuna kabila dogo la Wasala linaloamini dini la Kiislamu na lenye historia ya zaidi ya miaka 800. Watu wa kabila hilo hasa wanaishi kwenye wilaya inayojiendesha ya kabila la Wasala la Xunhua mkoani Qinghai. Leo tutawaletea maelezo kuhusu watu wa kabila hilo.
v Madarasa ya wanafunzi wa mkoa wa Xijiang ya shule za sekondari zilizoko katika miji mikubwa iliyoendelea nchini China 2007/10/31
Karibuni katika kipindi hiki cha makabila madogo madogo nchini China. Zamani kwa wanafunzi wa shule za sekondari wanaoishi kwenye sehemu za mbali za mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang magharibi mwa China, kusoma kwenye shule za miji mikubwa iliyoendelea kulikuwa ni ndoto tu, lakini tangu mwaka 2000 serikali ya China ianzishe madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa mkoa wa Xinjiang kwenye shule za miji mikubwa, ndoto ya wanafunzi wengi wa mkoa huo imetimia.
v Utamaduni wa makabila madogo madogo huko Shangri-la 2007/10/24
Katika kipindi cha wiki iliyopita tuliwaletea maelezo kuhusu maisha mazuri ya watu wanaoishi kwenye sehemu ya Shangri-la mkoani Yunnan, na leo tutawaelezea utamaduni wa makabila madogo madogo ya sehemu ya Shangri-la ya wilaya ya Diqing.
v Maisha mazuri ya watu wa Diqing 2007/10/17
Wilaya ya Diqing iko kaskazini magharibi mwa mkoa wa Yunnan, na iko jirani na mkoa unaojiendesha wa Tibet. Maana ya Diqing kwenye lugha ya Kitibet ni sehemu yenye baraka na heri, watu wa makabila 26 likiwemo kabila la Watibet, la Walisu, la Wanaxi na la Wahan wanaishi kwenye wilaya hiyo, na miongoni mwao, watu wa kabila la Watibet wanachukua theluthi moja ya idadi ya watu wa huko.
v Kijiji cha Najiaying cha watu wa kabila la Wahui mkoani Yunnan 2007/10/10
Kijiji cha Najiaying cha tarafa ya Nagu kiko kusini magharibi mwa mkoa wa Yunnan, kijiji hicho kina historia ndefu na kumewahi kuwa na watu maarufu wengi kizazi baada ya kizazi, wakiwemo profesa Nazhong wa Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing, ambaye pia ni mtaalamu maarufu wa historia ya lugha ya kiarabu aliyepewa tuzo ya kimataifa ya Sharjah la utamaduni wa kiarabu na Shirika la Elimu, Sayansi, na Utamaduni la Umoja wa Mataifa
v Watu wa kabila la Watajik wanaoishi kwenye uwanda wa juu wa Pamirs 2007/10/03
Uwanda wa juu wa Pamirs uliopo kusini magharibi mwa sehemu inayojiendesha ya kabila la wauyghur ya Xinjiang, unajulikana sana nchini na nje kutokana na kuwa na milima 14 yenye urefu wa mita zaidi ya 8,000. Wachina wa makabila madogo madogo yakiwemo makabila ya Watajik, la Wauyghur, la Wakeerkezi na Wahui wanaishi kwenye uwanda huo wa juu, miongoni mwao, watu wa kabila la Watajik wanachukua asilimia 90 ya idadi ya watu wa huko
v Mabadiliko kwenye sehemu ya Linzhi mkoani Tibet 2007/09/26
Mkoa unaojiendesha wa Tibet uko kwenye uwanda wa juu, na inajulikana kama paa la dunia. Linzhi iliyoko mashariki mwa Tibet ni sehemu ya ajabu sana. Kuna dawa ya miti shamba ya Xuelianhua ambayo hukua kwenye sehemu yenye baridi ya mzizimo, pia kuna ndizi ambazo hukua kwenye sehemu ya joto.
v Wauguzi wa makabila madogo madogo mkoani Xinjiang 2007/09/13
Hospitali ya kwanza iliyo chini ya Chuo kikuu cha udaktari cha Xinjiang ni hospitali kubwa zaidi katika sehemu inayojiendesha ya kabila la wauygur ya Xinjiang. Hivi karibuni hospitali hiyo imekuwa na wauguzi wengi wanaofanya kazi vizuri, ambao ni wa makabila madogomadogo.
v Kuhifadhi nyimbo za kabila la washe waishio kusini mashariki nchini China 2007/09/05
Kabila la washe ni moja ya makabila madogo madogo nchini China, wengi wao wanaishi katika sehemu ya pwani ya mkoa wa Fujian na mkoa wa Zhejiang. Mababu wa kabila la washe walikuwa wanapenda kuishi maisha ya kuhamahama, na waliwahi kuishi katika sehemu nyingi za kusini mwa China.
v Mabadiliko ya "shule za msingi zilizojengwa kwenye migongo ya farasi" 2007/08/30
Miaka 30 iliyopita, kwenye mbuga kubwa ya Xilinguole ya mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, matakwa makubwa kabisa ya Siqinbilige aliyekuwa na umri wa miaka 12 yalikuwa kukutana na mwalimu wake aliyefika mara moja kwa wiki kwa kupanda farasi kuwafundisha yeye na wenzake kusoma na kuandika na kuwasimulia hadithi.
v Mtaa wa kabila la Wahui mjini Xian, China 2007/08/29
Xian ni mji mkuu wa mkoa wa Shanxi, uliopo kaskazini magharibi mwa China, ambao ni mji mkongwe maarufu, pia ni sehemu ya kwanza walipoishi Waislamu wa China. Mjini Xian, kuna mtaa wenye historia ndefu sana wa watu wa kabila la Wahui, ambao ni Waislamu.
v Wachangjiao ambao ni tawi moja la kabila la wamiao waishio mkoani Guizhou nchini China 2007/08/22
Katika kitongoji cha Suoga cha mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, wanaishi wachangjiao, ambao ni tawi moja ya kabila la wamiao. Tawi hilo lina idadi ya watu zaidi ya 4000, ambao wanaishi kwenye milima mirefu na yenye hali ya hewa ya baridi. Watu hao wanasemekana bado wanaishi maisha ya kiasili.
v Karquga--kijiji cha waluobu kilichoko kwenye jangwa la Takelamagan, kaskazini magharibi mwa China 2007/08/15
Katika mkoa unaojiendesha wa kabila la wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, kuna jangwa kubwa la Takelamagan. Kwenye jangwa hilo kuna Mto Talimu, na kwenye mtiririko wake kuna maziwa madogo madogo na maeneo yenye majani.
v Ngoma za makabila madogo zawajumuisha vijana kutoka sehemu mbalimbali 2007/08/02
Katika Chuo Kikuu cha Makabila Madogo madogo cha China, kuna kikundi cha ngoma za makabila madogo cha wanafunzi. Japokuwa vijana hao wanatoka kwenye makabila mbalimbali na wanasomea kozi tofauti, lakini wamekusanyika pamoja kutokana na kupenda kucheza ngoma za makabila madogo madogo.
v Ufundi wa watu wa kabila la wamiao mkoani Guizhou wa kuweka michoro kwenye vitambaa kwa kutumia nta 2007/07/26
Kuweka michoro kwenye vitambaa kwa kutumia nta, ni moja ya ufundi wa jadi wa kutengeneza vitu vya sanaa ya mikono nchini China, yaani kuweka michoro kwenye vitambaa kwa kutumia nta kwenye vitambaa vilivyofumwa kwa nyuzi asilia zilizotengenezwa kwa katani, hariri, pamba na sufu, halafu kuwekwa rangi. Sehemu zilizowekwa nta haziwezi kupata rangi, hivyo baada ya nta kuondolewa kutoka kwenye sehemu zilizowekwa kwenye kitambaa, sehemu iliyokuwa na nta inaonekana kama ni maua meupe yanayopendeza.
v Kilimo na ufugaji maalum wa sehemu ya Linzhi mkoani Tibet 2007/07/19
Sehemu ya Linzhi iko kusini mashariki mwa mkoa unaojiendesha wa Tibet, ina mandhari nzuri, na wanaishi watu wa makabila madogo madogo kama vile kabila la Wamenba na kabila la Waluoba. Katika miaka ya hivi karibuni, sehemu ya Linzhi inapojitahidi kulinda na kuongeza uwezo wa uzalishaji wa nafaka mbalimbali, pia imechukua hatua mwafaka kuhimiza kilimo na ufugaji wenye umaalum wa kipekee, na maisha ya wakulima na wafugaji wa huko yanaboreshwa mwaka hadi mwaka.
v "Mfugaji Xibao Ligao na mpango wake wa kujiendeleza kwa familia kwenye ardhi ya mchanga 2007/07/04
Xibao Ligao ni mkulima anayeishi katika wilaya ya Naiman ya mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani. Maskani yake yako kwenye sehemu yenye mchanga ya Kerqin, ambayo ni sehemu yenye ardhi kubwa kabisa ya mchanga nchini China.
v Ngoma ya "Huadeng" ya kabila la Wa-Tu waishio mkoani Guizhou 2007/06/27
Wakazi wa kabila la Tu wa mji wa Xujiabei wa wilaya ya Sinan, mkoani Guizhou wakisikia muziki wa ngoma wanajua kuwa, ngoma ya "Huadeng" itachezwa. Kwenye ua mmoja wa familia ya mkulima, watazamaji walijaa, wakiwaangalia wachezaji waliovaa mavazi ya rangi mbalimbali wakichezea vipepeo na vitambaa walivyoshika mikononi huku wakiimba nyimbo kwa furaha
v Hekalu la Jokhang--Fahari ya kabila la Wa-tibet 2007/06/20
Katika sehemu ya kati kati ya Lahsa, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa Tibet kuna Hekalu kubwa la Jokhang linalojulikana sana. Hekalu la Jokhang lilijengwa mwanzoni mwa karne ya 7, ni jengo lilojejengwa kwa mbao lenye nakshi za mtindo wa makabila ya Wa-han na Wa-tibet yenye historia ndefu kabisa mkoani Tibet.
1 2 3 4 5