Barghouti afuatiliwa baada ya kutangaza kushiriki kwenye uchaguzi mkuu 2004/12/03 Kiongozi wa Fatah Bw. Marwan Barghouti, ambaye hivi sasa amefungwa na Israel, juzi alitangaza ghafla kuwa atashiriki kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Januari mwaka kesho kugombea nafasi ya mwenyekiti wa mamalaka ya utawala wa Palestina.
|
Kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya amani na maendeleo 2004/12/03 Mkutano wa 5 wa mwaka wa Shirikisho la amani la mabunge ya Asia ulifungwa jana huko Islamabad, mji mkuu wa Pakistan.
|
Kwa nini baadhi ya Wamarekani wanataka Bw. Kofi Annan ajiuzuru? 2004/12/03 Baada ya kashfa ya ufisadi wa mpango wa mafuta-kwa-chakula kuanza kujulikana na watu, baadhi ya watu nchini Marekani wamemtaka Bw. Annan ajiuzuru kwa mara nyingi
|
Serikali ya mpito ya Somalia yaundwa 2004/12/02 Waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia Bw. Ali mohamed ghedi jana huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya alitangaza orodha ya mawazi wa serikali ya mpito ya Somalia. Baada ya Bw. ghedi kutangaza orodha hiyo, mawaziri 27 waliapisha mara moja. Kuundwa kwa serikali ya mpito ya Somalia kunamaanisha kuwa Somalia imepiga hatua muhimu katika kumaliza hali ya kutokuwa na serikali kwa muda wa miaka 13.
|
Kuanzishwa kwa eneo la biashara huru kati ya China na Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini Mashariki kutaharakisha utandawazi wa uchumi wa Asia 2004/12/02 Mkutano wa nane wa viongozi wa China na umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki umemalizika huko Vientian, mji mkuu wa Laos.
|
Nani anaweza kuchukua nafasi ya Alan Greenspan ? 2004/12/02 Pamoja na kuharakishwa kwa uundaji wa kundi la maofisa wanaoshughulikia mambo ya uchumi katika awamu ya pili ya rais Bush wa Marekani, maofisa wa idara mbalimbali za kiuchumi za serikali ya Marekani wameanza kufahamika siku hadi siku
|
Hali ya kwenye mpaka kati ya Jamhuri ya demokrasia ya Kongo na Rwanda yawa ya wasiwasi tena 2004/12/02 Ofisa mwandamizi wa ujumbe maalumu ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya demokrasia ya Kongo Bw. M'hand Ladjouzi tarehe 1 alithibitisha kuwa kuwa, jeshi la serikali ya Rwanda limevuka mpaka na kuingia sehemu ya Goma mashariki ya Jamhuri ya demokrasia ya Kongo.
|
Serikali ya Bw. Sharon inakabiliana na hatari ya kuangushwa 2004/12/02 Tarehe 1 mwezi Desemba bunge la Israel lilizuia mswada wa bajeti uliotolewa na serikali ya Bw. Sharon. Kutokana na sababu hiyo, baadaye Bw. Sharon aliwaondoa madarakani mawaziri 4 wa serikali ya shirikisho la chama tawala-chama cha mageuzi kilichopiga kura ya hapana, na kuuacha shirikisho la chama tawala kukabiliwa na hatari ya kuangushwa.
|
Mikutano ya wakuu wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki yafungwa 2004/12/01 Mikutano ya siku mbili ya wakuu wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki ilifungwa jana huko Vientiane, mji mkuu wa Laos. Mikutano hiyo imepiga tena hatua kubwa kwa kusukuma mbele maendeleo ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki katika nyanja za siasa, uchumi, na utandawazi wa utamaduni
|
Kitu Iran inachopata na wasiwasi wake kutokana na azimio jipya 2004/12/01 Baada ya Iran kuelewana na Umoja wa Ulaya, Shirika la Nishati ya Atomiki duniani IAEA juzi lilipitisha azimio jipya kuhusu suala la nyuklia la Iran.
|
Kikundi cha Maofisa waandamizi cha suala la mageuzi ya Umoja wa Mataifa chatoa dhana mpya ya usalama wa pamoja 2004/12/01 Ripoti iliyowasilishwa kwa Umoja wa Mataifa inasema kuwa, dunia ya hivi sasa imebadilika sana ikilinganishwa na ile wakati Umoja wa Mataifa ulipoanzishwa, matishio makubwa yanayohatarisha amani na usalama wa kimataifa yamekuwa na aina nyingi zaidi, kwa hivyo inapaswa kuwepo kwa dhana mpya ya usalama kwa pamoja.
|
Kuwafuatilia kina mama na kupambana na ugonjwa wa ukimwi 2004/11/30 Mwaka 1988 Shirika la afya duniani WHO liliamua kuwa tarehe mosi Desemba ya kila mwaka ni siku ya dunia nzima kutoa elimu kuhusu kinga na tiba ya ukimwi, ili kuwahamasisha watu wa dunia nzima washirikiane katika kupambana na ugonjwa wa ukimwi.
|
AAPP yaendelea kukua 2004/11/30 Mkutano wa 5 wa Shirikisho la mabunge ya nchi za Asia kwa ajili ya amani (AAPP) utafanyika huko Islamabad, mji mkuu wa Pakistan kuanzia leo hadi tarehe 2, Desemba.
|
Upepo wa Suala la Nyuklia la Iran Umetulia Tena 2004/11/30 Tarehe 29 huko Vienna Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki lilipitisha azimio bila kupigiwa kura, likionesha "kuridhika" na Iran kusimamisha shughuli za kusafisha uranim, na likitaka Iran itekeleze kikamilifu makubaliano na nchi tatu za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza. Azimio hilo linasema halitawasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kufikia hapo upepo wa suala la nyuklia la Iran umetulia kwa mara nyingine tena.
|
|