Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • China na India zaanzisha mazungumzo ya kimkakati
  •  2005/01/26

    Mazungumzo ya raundi ya kwanza ya kimkakati kati ya China na India yalimalizika tarehe 25 mjini New Dehli. Mazungumzo hayo yalihusu hasa masuala makubwa ya kimataifa na kikanda yanayohusiana na nchi hizo mbili na madhumuni yake ni kupanua eneo la ushirikiano na kuleta nafasi ya kuimarisha uhusiano kati yao.

  • India na Pakistan zapuuza kwa makusudi tukio la kukiuka mkataba wa kusimamisha vita
  •  2005/01/25
    Baada ya India kulaani mara mbili Pakistan kukiuka mkataba wa kusimamisha vita katika sehemu ya Kashmir wiki iliyopita, tarehe 24 Pakistan pia iliilaani India kwa kukiuka mkataba katika siku ya tarehe 21. Lakini wasemaji wa wizara za mambo ya nje za nchi mbili wote walikanusha kuwahi kulaaniana. Wachunguzi wanaona kuwa ingawa mkwaruzano kweli ulitokea katika sehemu ya Kashmir hivi karibuni, lakini mkwaruzo mkwruzano huo hautaathiri mazungumzo ya amani ya pande mbili.
  • Serikali ya muda ya Iraq yaandaa uchaguzi mkuu katika hali ya ugaidi
  •  2005/01/25
    Wiki moja kasoro imebaki kabla kufikia tarehe 30 mwezi huu siku uchaguzi mkuu utakapofanyika nchini Iraq. Ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika bila vikwazo, serikali ya muda ya Iraq imechukua hatua kali mfululizo za usalama, ili kuzuia shughuli mbalimbali za ugaidi wakati ikiandaa kwa juhudi uchaguzi mkuu.
  • Umoja wa Mataifa kukumbuka miaka 60 tangu kukombolewa kwa kambi ya Auscgwitz.
  •  2005/01/25
    Baraza kuu la 59 la Umoja wa Mataifa jana lilifanya mkutano maalum kukumbuka miaka 60 tangu kukombolewa kwa kambi ya Auscgwitz. Hii ni mara ya kwanza kwa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kufanya mkutano maalum kuhusu tukio hilo, mkutano ambao umeanzisha shughuli za kuadhimisha miaka 60 tangu upate ushindi katika vita vya kupambana na ufashisti duniani.
  • Mpango wa miaka 10 ya kupunguza maafa ya kimaumbile waandaliwa katika mkutano wa Kobe, Japan
  •  2005/01/24
        Mkutano wa kupunguza maafa ya kimambile uliofanyika huko Kobe, Japan ulimalizika tarehe 22. Mkutano huo umeandaa mpango wa jinsi ya kupunguza maafa ya kimaumbile duniani katika muda wa miaka 10 ijayo.
  • Mahmoud Abbas aonesha uwezo wake wa kutatua mgogoro
  •  2005/01/24
    Hali wasiwasi kati ya Palestina na Israel iliyosababishwa na mashambulizi dhidi ya kituo cha ukaguzi cha jeshi la Israel imetulia dhahiri hivi karibuni. Maoni ya watu yanaonesha kuwa, kupunguzwa kwa hatua ya mwanzo kwa mgogoro huo kunatokana na mkakati wa kisiasa na hatua imara zenye unyumbufu zilizochukuliwa na mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Mahmoud Abbas.
  • Mgogoro wa uchaguzi wa rais wa Ukraine watulia
  •  2005/01/21
    Bunge la Ukraine jana lilipitisha azimio likitangaza kuwa sherehe ya kuapishwa kwa Rais Viktor Yushchenko itafanyika tarehe 23 mwezi Januari. Mgogoro wa uchaguzi wa rais wa Ukraine hatimaye umetulia.
  • Sherehe ya Kumwapisha Rais Bush Yafanyika Washington
  •  2005/01/21
    Tarehe 20 saa za mchana kwa saa za sehemu ya mashariki ya Marekani rais George Bush aliyeshinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika Novemba mwaka jana aliapishwa na kuwa rais kwa kipindi cha pili mfululizo nchini Marekani, na kuwa rais wa 55 wa Marekani.
  • Israel yarejesha mawasiliano na mamlaka ya utawala wa Palestina
  •  2005/01/20
        Baraza la usalama la Israel jana liliamua kurejesha mawasiliano na mamlaka ya utawala wa Palestina. Wakati huo, waziri wa mambo ya nje wa Palestina Bw. Shaath siku hiyo alisema kuwa, mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas anatarajiwa kufikia makubaliano na makundi ya wanamgambo wa Palestina kuhusu suala la kusimamisha vita katika muda mfupi ujao.
  • Uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani Utakuwaje baada ya Bushi Kushika Utawala wa Marekani katika Kipindi cha Pili ?
  •  2005/01/20
    Tarehe 20 mwezi huu rais George Bushi wa Marekani ataanza kipindi chake cha pili cha utawala wa Marekani. Serikali ya Bush haitaacha sera yake ya kutenda mambo kwa upande mmoja tu ili kuimarisha nafasi yake ya "ubabe"duniani, na nchi nyingi za Ulaya zinatetea "dunia iwe ya pande nyingi zinazoshirikiana na kuzuiana".
  • Yushchenko ataapishwa kuwa Rais wa Ukraine
  •  2005/01/19
    Mahakama kuu ya Ukraine jana ilitoa amri kufuta hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo tarehe 11 kuhusu kupiga marufuku kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa Ukraine. Hukumu hiyo imetandika njia kwa rais mteule Bw.Viktor Yushchenko kushika madaraka rasmi.
  • Raia wa China watekwa nyara nchini Iraq
  •  2005/01/19
        Ubalozi wa China nchini Iraq tarehe 18 ulithibitisha kuwa raia wanane wachina wametekwa nyara nchini Iraq na wanadiplomasia wa China wanafanya juhudi kadiri kwa wawezavyo kuwaokoa mateka hao.
  • China yatoa msimamo kwenye mkutano wa kupunguza maafa duniani
  •  2005/01/19
    Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu kupunguza maafa duniani ulifunguliwa jana mjini Kobe, Japan. Mkutano huo utajadili jinsi ya kupunguza hasara zinazosababishwa na maafa ya kimaumbile. Ujumbe wa China ulioongozwa na waziri wa mambo ya raia wa China Bwana Li Xueju umehudhuria mkutano huo, na kutoa pendekezo la kuanzisha mfumo wa usimamizi, kinga na utoaji tathmini wa kukabiliana na maafa makubwa ya kimaumbile
  • Mapambano makali kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini Iraq
  •  2005/01/18
    Japokuwa zimebaki wiki mbili tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Iraq, lakini hali ya usalama ya nchi hiyo bado haina dalili yoyote ya kuboreshwa. Mapambano makali kati ya Marekani na serikali ya muda ya Iraq na vikundi vya wanamgambo vya Iraq yanaendelea kupamba moto
  • Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu kupunguza maafa duniani wafanyika mjini Kobe, Japan
  •  2005/01/18
    Mkutano wa wa Umoja wa Mataifa kuhusu kupunguza maafa duniani umefunguliwa leo mjini Kobe, Japan. Hii ni mara ya pili kwa mkutano wa aina hiyo kufanyika katika miaka kumi iliyopita.
  • Abbas achukua hatua za kuwazuia watu wenye siasa kali kuishambulia Israel
  •  2005/01/18
    Ili hali kati ya Palestina na Israel isiendelee kuwa mbaya, mamlaka ya utawala wa Palestina hivi karibuni imechukua hatua nyingi mfululizo ili kuwazuia watu wenye silaha wa Palestina kuendelea kuishambulia Israel.
  • Hali ya Banda aceh yaelekea kuwa ya kawaida
  •  2005/01/17
    Zaidi ya siku 20 zimepita tangu yatokee maafa ya mawimbi makubwa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi (tsunami) baharini Hindi. Kutokana na msaada wa jumuiya ya kimataifa na juhudi za serikali na wananchi wa Indonesia, watu wa Banda aceh, mji ulioathirika vibaya na maafa ya tsunami, sasa wameanza kuishi kama kawaida.
  • Tume ya uchaguzi mkuu wa Jamhuri Huru ya Abukhaziya ya Georgia yatangaza matokeo
  •  2005/01/14
    Tume ya uchaguzi mkuu wa Jamhuri huru ya Abkhaziya jana ilitangaza kuwa Bw. Sergei Bagapsch ameshinda kabisa katika uchaguzi uliofanyika juzi. Vyombo vya habari vinaona kuwa matokeo hayo yataathiri hali ya siasa ya kanda hiyo.
  • Mchakato wa amani ya Cote D'ivoire wakabiliwa tena na changamoto
  •  2005/01/13
    Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya kusini tarehe 12 alimaliza usuluhishi wa kidiplomasia nchini Cote D'ivoire. Kutokana na kuwa wawakilishi wa jeshi la upinzani la zamani la chama cha New Forces kukataa kushiriki kwenye mkutano maalum wa serikali ya maafikiano ya kitaifa ya Cote D'ivoire uliopendekezwa na rais Mbeki, hivyo juhudi za usuluhishi wa Mbeki hazikupata maendeleo halisi na mchakato wa amani ya Cote D'ivoire.
  • Mashambulizi ya kimabavu yasumbua uchaguzi mkuu wa Iraq
  •  2005/01/13
        Leo zikiwa zimebaki siku 17 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Iraq kufanyika tarehe 30 mwezi huu, mashambulizi ya kimabavu, mauaji ya kisiri na matukio ya utekaji nyara nchini humo bado yanaongezeka.
  • Ujumbe wa uchunguzi wa China wamaliza kazi kwa mafanikio kwenye uchaguzi mkuu wa Palestina
  •  2005/01/12
    Kutokana na mwaliko wa mamlaka ya utawala wa Palestina, Ujumbe wa uchunguzi wa China uliongozwa na balozi Yao Kuangyi tarehe 9 ulishuhudia uchaguzi wa mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina, na kumaliza kazi hiyo kwa mafanikio.
  • Mkutano wa Kimataifa kuhusu Maafa Yaliyosababishwa na Tetemeko la Ardhi Baharini Hindi Wazaa Matunda
  •  2005/01/12
    Mkutano wa kimataifa kuhusu maafa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi katika bahari ya Hindi ulifanyika jana huko Geneva. Kwenye mkutano huo nchi mbalimbali zilijadiliana na kuafikiana wazo la namna moja kuhusu kutimiza ahadi ya kutoa misaada ya fedha, Mkutano huo umeonesha moyo wa ushirikiano mkubwa wa binadamu katika dhiki na faraja.
  • Nchi za Afrika zajitahidi kutafuta njia ya kuondoa migogoro ya kisehemu
  •  2005/01/11
    Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika jana liliitisha mkutano wa wakuu huko Libreville, mji mkuu wa Gabon. Hii ni mara ya kwanza kwa baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika kuitisha mkutano wa wakuu tangu kuanzishwa kwake mwaka jana, hadhi muhimu ya Umoja wa Afrika inainuka siku hadi siku
  • Pande mbili za kusini mwa Sudan zasaini makubaliano ya amani kwa pande zote
  •  2005/01/10
    Makamu wa rais wa Sudan Osman Ali Taha na kiongozi wa jeshi la upinzani la chama cha ukombozi wa umma cha Sudan Bw John Garang tarehe 9 walisaini makubaliano ya amani huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya, hii imeonesha kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 21 kusini mwa Sudan vimemalizika
  • Mnara wa historia wa bara la Afrika
  •  2005/01/10
    Serikali ya Sudan na chama cha upinzani kinachojulikana kwa jina la chama cha ukombozi cha watu wa Sudan wamesaini mkataba wa amani tarehe 9 huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Mkataba huo unahusu masuala mengi muhimu yakiwa ni pamoja na usimamishaji wa mapambano, kugawana madaraka na mali.
  • Ukarabati baada ya maafa ya mawimbi makubwa yaliyotokea kutokana na tetemeko la ardhi katika bahari ya Hindi ni mgumu na wa muda mrefu
  •  2005/01/10
    Nchi zilizoathirika na maafa makubwa ya dhoruba lililosababishwa na tetemeko la ardhi kwenye bahari ya Hindi zimeingia katika kipindi cha ukarabati. Kutokana na makadirio, ukarabati huo pengine unahitaji muda wa miaka mitano hadi miaka 10 kabla kukamilika, na gharama za ukarabati zitazidi dola za Kimarekani bilioni 10.
  • Mwenyekiti wa kamati ya utendaji wa Chama cha Ukombozi cha Palestina Bw. Mahmoud Abbas
  •  2005/01/10
    Katibu mkuu wa Ikulu ya Palestina Bw. al-Taib Abdel Rahim tarehe 9 kuwa kutokana na matokeo ya mwanzo, mgombea wa Fatah, kundi kubwa la chama cha ukombozi cha Palestina Bw. Mahmoud Abbas ameshinda katika uchaguzi mkuu wa Palestina, na kuwa mwenyekiti mpya wa mamlaka ya utawala wa Palestina.
  • Kutoa ni moyo na sio utajiri
  •  2005/01/07
    Baada ya tetemeko la ardhi na mawimbi makubwa yaliyosababishwa na tetemeko hilo kutokea tarehe 26 mwezi Desemba mwaka jana katika bahari ya Hindi, jumuiya ya kimataifa ikiwa na moyo wa kibinadamu ilifululiza kuzisaidia sehemu zilizokumbwa na maafa kwa njia mbalimbali katika kupambana na maafa na kufanya ukarabati.
  • Mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine watulia
  •  2005/01/06
    Idara ya habari ya rais ya Ukraine imetangaza kuwa, rais Kuchma tarehe 5 alisaini amri ya kuvunja serikali, na kuitaka serikali ya sasa iendelee kutekeleza wajibu wake kabla ya serikali mpya kuanzishwa.
  • Iran yalegeza tena masharti utatuzi wa suala la nyuklia wapiga hatua
  •  2005/01/06
    Katibu mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Bw. Mohammed el Baradei tarehe 5 huko Vienna alisema kuwa kutokana na kukubaliwa na Iran, wataalamu wa shirika lake watafanya ukaguzi wa zana za kijeshi katika sehemu ya Parchin nchini Iran ndani ya muda wa siku au wiki kadhaa zijazo. Vyombo vya habari vinaona kuwa hii ni hatua mpya katika utatuzi wa suala la nyuklia, kwa kuwa mwaka jana wakaguzi wa shirika hilo hawakuruhusiwa kuingia kwenye sehemu hiyo
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44