Umoja wa Ulaya wafanya mageuzi juu ya sera za kilimo 2008/11/21 Mawaziri wa kilimo wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya baada ya kufanya majadiliano makubwa kwa saa 18, walifikia makubaliano tarehe 20 huko Brussels kuhusu kufanya mageuzi juu ya sera za umoja huo za utoaji ruzuku ya kilimo, ambapo utoaji huo wa ruzuku ya kilimo utapunguzwa na kuongezwa mgao wa uzalishaji wa maziwa, hayo ni mafanikio muhimu tangu Umoja wa Ulaya unuie kufanya mageuzi kwa mara ya 5 kuhusu sera za kilimo mwaka 2003.
|
Rais wa China atoa hotuba kuhusu kujenga ushirikiano wa kiwenzi kwa pande zote kati ya China na Latin Amerika 2008/11/21 Rais Hu Jintao wa China ambaye yuko ziarani nchini Peru tarehe 20 alitoa hotuba muhimu kwenye bunge la Peru, ambapo alisifu sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Latin Amerika, akisema China inapenda kufanya juhudi pamoja na nchi za Latin Amerika katika kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili.
|
Mazungumzo kuhusu suala la Georgia yapata maendeleo 2008/11/20 Mkutano wa pili kuhusu suala la Georgia, ambao uliandaliwa na Umoja wa Mataifa, jumuiya ya usalama ya Ulaya na Umoja wa Ulaya ulifanyika tarehe 19 katika Jumba la Palais Des Nations kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ya Ulaya mjini Geneva. Wawakilishi kutoka nchi za Russia na Georgia walikuwa na mazungumzo ya ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa mapigano kati ya pande mbili mwezi Agosti mwaka huu, wakati mikutano ya vikundi viwili vya kazi kuhusu masuala ya wakimbizi na usalama ilipata baadhi ya maendeleo.
|
Ziara ya rais Hu Jintao wa China katika nchi za Latin Amerika itasukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili 2008/11/18 Rais Hu Jintao wa China alifanya ziara nchini Costa Rica kuanzia tarehe 16 hadi 17 mwezi huu. Baadaye rais Hu atatembelea Cuba na Peru, na pia atahudhuria mkutano wa 16 usio rasmi wa wakuu wa Shirika la ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasikifiki utakaofanyika nchini Peru.
|
Mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 20 waongeza imani za nchi za kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani 2008/11/17 Mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 20 kuhusu soko la fedha na uchumi wa dunia ulifungwa jumamosi iliyopita nchini Marekani. Watalaamu wa China wamesema, ingawa mkutano huo haukutoa mpango mzuri wa kukabiliana na msukosuko wa fedha, lakini taarifa iliyotolewa na pande mbalimbali zilizohudhuria mkutano huo imeongeza imani za nchi mbalimbali za kukabiliana na msukosuko.
|
Mafanikio aliyoyapata spika Wu Bangguo katika ziara ya barani Afrika 2008/11/17 Baada ya kumalizika kwa ziara ya spika wa bunge la umma la China Bw. Wu Bangguo, katika nchi 5 za Afrika, naibu spika Bw. Cao Weizhou, ambaye aliandamana naye katika ziara hiyo, alisema, ziara hiyo ya Bw. Wu Bangguo imeimarisha mawasiliano ya viongozi wa China na wa nchi za Afrika, kuhimiza utekelezaji wa hatua za matokeo ya mkutano wa Beijing wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika , na kuongeza mambo mapya ya uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa China na Afrika.
|
Jumuiya ya kimataifa yatakiwa kuukabili msukosuko wa fedha kwa ushirikiano 2008/11/16 Mkutano wa wakuu wa nchi wa kundi la nchi 20 kuhusu soko la fedha na uchumi wa dunia ulifanyika tarehe 15 huko Washington, mji mkuu wa Marekani. Rais Hu Jintao wa China alihudhuria mkutano na kutoa hotuba isemayo "Tuondoe matatizo kwa kuimarisha ushirikiano, ambayo ilifafanua chanzo cha msukosuko wa fedha, na kueleza msimamo wa China kuhusu baadhi ya masuala nyeti ya duniani yakiwemo namna ya kuukabili msukosuko wa fedha na kufanya mageuzi juu ya utaratibu wa mambo ya fedha wa dunia.
|
Balozi wa China atoa hotuba kupinga kuhusisha ugaidi na nchi, kabila na dini 2008/11/14 Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Yesui tarehe 13 alipotoa hotuba kwenye mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa alisema kuwa, China inapinga kuhusisha ugaidi na nchi fulani, kabila na dini, na pia inafuatilia ufufuzi wa fikra yenye msimamo mkali ya kupinga uislamu, pamoja na ufashisti mpya.
|
Kundi la wasanii la Mkoa wa Qinghai latembelea Kenya 2008/11/12 Hivi karibuni kundi la wasanii la mkoa wa Qinghai China lilishiriki Tamasha la "Wiki ya Utamaduni" katika Chuo Kikuu cha Kenyata jijini Nairobi. Katika tamasha la wiki hiyo wasanii wa kundi hilo walifanya maonesho ya nyimbo na ngoma yenye mitindo pekee ya makabila madogomadogo ya mkoa wa Qinghai wakiwaletea watazamaji wa Kenya uhondo mkubwa wa utamaduni wa China
|
Spika Wu Bangguo ahudhuria sherehe ya kuanza kwa ujenzi wa jengo la mkutano la Umoja wa Afrika 2008/11/11 Spika wa bunge la umma la China Bw. Wu Bangguo ambaye yuko ziarani nchini Ethiopia, tarehe 10 asubuhi amehudhuria sherehe ya kuzindua ujenzi wa jengo la mkutano la Umoja wa Afrika ambalo linajengwa kwa msaada wa serikali ya China.
|
Obama kujenga upya mfumo wa sera 2008/11/11 Rais mteule wa Marekani, Bw. Barack Obama tarehe 10 alasiri alikuwa na mazungumzo na rais Bush katika Ikulu, hii ni mara ya kwanza kwa rais mteule kuitembelea Ikulu. Vyombo vya habari vinasema, matembezi yaliyofanyika mara tu baada ya Bw. Obama kuchaguliwa kuwa rais yana maana ya kuonesha haraka ya kufanya makabidhiano ya madaraka ya urais.
|
Kundi la nchi 20 limefikia kwenye mwafaka kuhusu msukosuko wa fedha 2008/11/10 Mkutano mkuu wa mawaziri wa fedha na wakuu wa benki kuu za kundi la nchi 20 wa mwaka 2008, ambao ulifanyika kwa siku mbili huko Sao Paulo, Brazil, ulifungwa tarehe 9 mwezi Novemba. Mkutano huo umefikia kwenye mwafaka kuhusu kufanya ushirikiano ili kukabiliana na msukosuko wa fedha.
|
Medvedev atoa taarifa kuhusu mambo ya taifa 2008/11/06 Rais Dimitri Medvedev wa Russia tarehe 5 alitoa taarifa kuhusu mambo ya taifa kwa mabaraza mawili ya bunge la shirikisho la Russia. Hii ni mara ya kwanza kwa rais huyo kutoa taarifa kuhusu mambo ya taifa kwa bunge la taifa tangu achaguliwe kuwa rais, ambayo pia ni taarifa ya 15 kuhusu mambo ya taifa iliyotolewa na rais wa nchi hiyo.
|
"Kiu ya kutaka mageuzi" yamsaidia Obama kushinda uchaguzi mkuu kirahisi 2008/11/05 Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa na vyombo vya habari nchini Marekani, mgombea wa Chama cha Demokratic ambaye ni seneta wa jimbo la Ilinois Bw. Obama tarehe 4 ameshinda uchaguzi mkuu, na atakuwa rais wa 56 wa Marekani. Wachambuzi wanaona kuwa kushinda uchaguzi huo kirahisi kwa Bw. Obama kumeonesha kwa mara nyingine kwamba kutaka mageuzi ni nia ya Marekani.
|
Wu Bangguo kutembelea nchi 5 za Afrika 2008/11/03 Kutokana na mwaliko wa viongozi wa mabunge ya nchi 5 za Algeria, Gabon, Ethiopia, Madagasca na Seychelles, spika wa bunge la China, Bw. Wu Bangguo atafanya ziara rasmi ya kirafiki katika nchi hizo kuanzia tarehe 3 mwezi huu, tena ataitembelea kamati ya Umoja wa Nchi za Afrika, ambao makao makuu yake yako Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.
|
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa laitisha mkutano maalumu kunasua msukosuko wa fedha 2008/10/31 Baraza kuu la 63 la Umoja wa Mataifa liliitisha mkutano maalumu tarehe 30 mwezi Oktoba katika makao makuu yake mjini New York, washiriki wa nchi mbalimbali pamoja na wataalamu wa uchumi wanajadili mbinu za kunasua msukosuko wa fedha uliopo hivi sasa duniani, na namna ya kutathimini mfumo wa mambo ya fedha wa dunia. Washiriki wanasema, dunia inapaswa kufanya mageuzi kuhusu mfumo wa mambo ya fedha uliopo hivi sasa.
|
Tetemeko la ardhi latokea Pakistan 2008/10/30 Tetemeko kubwa la ardhi la nguvu ya 6.5 kwenye kipimo cha Richter lilitokea tarehe 29 katika mkoa wa Baluchistan, sehemu ya kusini magharibi nchini Pakistan, na limesababisha vifo vya watu wengi na hasara kubwa ya mali. Hivi sasa, serikali ya Pakistan inajitahidi kadiri iwezavyo kupunguza hasara inayosababishwa na maafa hayo.
|
Mkutano wa mawaziri wakuu wa China na Russia wafanyika 2008/10/29 Waziri mkuu wa China, Bw. Wen Jiabao na waziri mkuu wa Russia, Bw. Vladimir Putin tarehe 28 mwezi Oktoba huko Moscow walihudhuria mkutano wa 13 wa mawaziri wakuu wa China na Russia unaofanyika kila baada ya muda fulani. Pande mbili zilibadilishana maoni kuhusu kuhimiza ushirikiano kati ya China na Russia kwenye maeneo mbalimbali pamoja na masuala muhimu ya kimataifa na kikanda zinayoyafuatilia, na zilikuwa na maoni ya namna moja.
|
Mazungumzo ya uundaji wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Zimbabwe yashindwa tena 2008/10/28 Mazungumzo ya Harare yaliyoitishwa na umoja wa maendeleo wa kusini mwa Afrika, (SADC) kuhusu suala la Zimbabwe yalishindwa alfajiri ya tarehe 28 kwa saa ya huko. Chama tawala na chama cha upinzani nchini Zimbabwe vilikuwa na mazungumzo marefu ya saa 13, lakini havikuafikiana kuhusu nani atachukua wadhifa wa waziri wa mambo ya ndani ya serikali ya umoja ya nchi hiyo
|
Waziri mkuu wa Kazakhstan ahojiwa na waandishi wa habari wa China 2008/10/27 Kabla ya kufunga safari kwa waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao kuelekea Kazakhstankwa ziara rasmi na kuhudhuria mkutano wa 7 wa mawaziri wakuu wa nchi wanachama wa Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai, waziri mkuu wa KazakhstanBw. Karim Masimov alihojiwa na waandishi wa habari wa China akiwemo wa Radio China Kiamtaifa, ambapo akizungumzia uhusiano kati ya China na Kazakhstanalisema, hivi sasa uhusiano kati ya nchi hizo mbili uko katika kiwango cha juu sana cha maendeleo
|
Ushirikiano kati ya Asia na Ulaya utatoa mchango kwa maendeleo ya dunia 2008/10/22 Mkutano wa 7 wa Baraza la wakuu wa Asia na Ulaya utafanyika Beijing kuanzia tarehe 24 hadi 25 mwezi huu. Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Liu Jieyi alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, ushirikiano kati ya Asia na Ulaya katika kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani utakuwa suala kubwa litakalojadiliwa zaidi kwenye mkutano huo, na ushirikiano huo utatoa mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya dunia nzima.
|
Lengo la kutimiza utandawazi wa uchumi wa Afrika 2008/10/21 Wakuu wa nchi 26 wa jumuiya 3 kubwa za Afrika zikiwemo Jumuiya ya Afrika mashariki(EAC), Soko la umoja la Afrika mashariki na kusini(COMESA) pamoja na Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika(SADC) wamekutana Kampala, mji mkuu wa Uganda wakihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya hizo tatu na kujadili namna ya kuharakisha utandawazi wa uchumi wa Afrika na kutimiza lengo la kuunda umoja wa uchumi wa Afrika.
|
Uchaguzi mkuu wa Marekani umeingia kipindi cha mwisho kabla ya kufanyika 2008/10/17 Kufuatia kongamano la mwisho la kugombea uchaguzi mkuu kumalizika tarehe 15 jioni, shughuli za uchaguzi mkuu nchini Marekani zimeingia katika kipindi cha mwisho kabla ya kufanyika. Katika siku zaidi ya kumi zilizosalia, mgombea urais wa Chama cha Rupublican Bw. John McCain na mgombea urais wa Chama cha Democratic Bw. Barack Obama hawatakuwa na fursa nyingine ya kutangaza ilani zao.
|
Usalama wa chakula duniani wakabiliwa na changamoto mpya 2008/10/16 Tarehe 16 mwezi Okatoba mwaka huu ni "siku ya nafaka duniani" ya mwaka wa 28. Shirika la nafaka na kilimo duniani, FAO, limebuni kauli-mbiu ya siku ya nafaka ya dunia ya mwaka huu kuwa ni "usalama wa nafaka duniani: changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na nishati ya mimea", likitarajia watu wazingatie zaidi changamoto zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa na nishati ya mimea.
|
Syria yatangaza kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Lebanon 2008/10/15 Tarehe 14 Rais wa Syria Bw. Bashar al-Assad alitangaza amri ya kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Lebanon. Hii inadhihirisha kuwa Syria imeitambua Lebanon kuwa ni nchi huru, lakini kuufanya uhusiano wa pande mbili uwe wa kawaida kunahitaji muda.
|
Umoja wa Ulaya watoa mpango wa kuokoa masoko ya fedha 2008/10/14 Baada ya mkutano wa wakuu wa nchi zinazotumia fedha ya Euro kupitisha mpango wa vitendo wa kusaidia benki kukusanya mitaji, nchi zinazotumia Euro zilitoa sera kamili tarehe 13 ili kuokoa masoko, Euro trilioni 1 zitaongeza imani ya watu juu ya masoko ya fedha ya Ulaya na ya dunia. Mpango huo kabambe wa kuokoa masoko ya fedha hatimaye utaweza kukomesha duru hilo la msukosuko wa fedha.
|
Suala la nyuklia la Peninsula ya Korea lapata maendeleo muhimu 2008/10/13 Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Korea ya Kaskazini tarehe 12 Oktoba alikaribisha Marekani kutangaza kuiondoa Korea ya Kaskazini kutoka kwenye orodha yake ya nchi zinazounga mkono ugaidi, ambapo Korea ya Kusini na Japan zimetoa misimamo tofauti juu ya hatua hiyo Marekani, na vyombo vya habari vinaona kuwa, hali hiyo inaonesha kuwa suala la nyuklia la Peninsula ya Korea lililokwama limepata maendeleo muhimu.
|
Jumuiya ya uchumi ya duniani yatoa wito kuimarisha imani juu ya masoko 2008/10/10 Hivi karibuni Shirika la mfuko wa fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia zitaitisha mkutano wa mwaka huko Washinton kujadili sera kuhusu misukosuko ya mambo ya fedha inayozikabili baadhi ya nchi za viwanda hivi sasa.
|
Benki kuu za Ulaya zapunguza faida ya fedha zilizowekwa benkini 2008/10/09 Ili kukabiliana na msukosuko wa fedha kwa pamoja, na kuhimiza ongezeko la uchumi, benki kuu ya Ulaya pamoja na benki kuu za nchi nyingine za Ulaya na Marekani tarehe 8 zilipunguza faida ya akiba zilizowekwa benkini kwa basic point 50, hatua hiyo imeshangiliwa mara moja na sekta mbalimbali.
|
Umoja wa Ulaya watoa mwito wa kuongeza uratibu katika kutoa msaada wa kuokoa soko la fedha 2008/10/08 Hivi karibuni msukosuko wa fedha wa Marekani umeathiri soko la fedha la Ulaya, ambapo mabenki kadha wa kadha makubwa ya Umoja wa Ulaya yamekumbwa na matatizo, na serikali za nchi mbalimbali zililazimishwa kutia mitaji mikubwa kwa mabenki au kuyataifisha ili kuepusha mabenki hayo yasifilisike.
|