Shirika la chakula duniani laadhimisha siku ya chakula duniani 2007/10/17 Tarehe 16 mwezi Oktoba ni siku ya chakula duniani. Siku hiyo shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, lilifanya shughuli katika makao makuu yako yake mjini Rome kuadhimisha siku ya 27 ya chakula duniani. Mkuu wa shirika hilo Bw. Jacques Diouf, rais Horst Koehler wa Ujerumani na rais Jakaya Kikwete wa Tanzania walishiriki kwenye shughuli za maadhimisho na kutoa hotuba wakisisitiza kuwa "haki ya kupata chakula" ni haki ya kimsingi ya binadamu
|
Kwa nini bei ya mafuta inaendelea kupanda kwenye soko la New York 2007/10/16 Tarehe 15 bei ya mafuta kwenye soko ya kimataifa ilipanda tena baada ya tarehe 12 kupanda na kuwa dola za Kimarekani 83,69 kwa pipa. Siku hiyo kwenye soko la New York bei ya mafuta ya mwezi Novemba ilipanda kwa dola za Kimarekani 2.44 na kuwa 86.13 kwa pipa, na katika soko la London bei ya mafuta ya mwezi Novemba ilipanda kwa dola za Kimarekani 2.20 na kuwa 82.75.
|
Itakuwa ni vigumu kwa ziara ya Bi Rice kwenye sehemu ya mashariki ya kati kupata mafanikio 2007/10/15 Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Condoleezza Rice tarehe 14 Oktoba aliwasili nchini Israel kwa ziara nyingine katika sehemu hiyo, na kuendelea kufanya maandalizi kwa ajili ya mkutano wa kimataifa kuhusu suala la mashariki ya kati unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba nchini Marekani.
|
Mazungumzo kati ya Russia na Marekani yafuatiliwa 2007/10/12 Mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya nje na mawaziri wa ulinzi kati ya Russia na Marekani yanafanyika tarehe 12 huko Moscow, mada ya mazungumzo hayo ni suala ya usalama wa kimkakati ambalo linahusisha mfumo wa kukinga makombora unaopangwa kuwekwa na Marekani barani Ulaya, "makubaliano kuhusu nguvu za kawaida za kijeshi barani Ulaya" na masuala ya Iran na Kosovo. Kwa hiyo mazungumzo hayo yanafuatiliwa sana.
|
Kwa nini waziri mkuu wa Japan anapinga "haki ya kujihami kwa pamoja" 2007/10/11 Habari zilizochapishwa kwenye gazeti moja kubwa la mjini Tokyo, toleo la tarehe 10 mwezi Oktoba zinasema, waziri mkuu wa Japan Bw. Yasuo Fukuda katika mkutano wa majadiliano wa kamati ya bajeti ya baraza la chini na bunge la Japan, alieleza msimamo wake wa kupinga kutumia "haki ya kujihami kwa pamoja", msimamo huo wa Bw Yasuo Fukuda ni tofauti na ule wa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Bw. Shinzo Abe, ambaye alitaka kufikia lengo la kutumia "haki ya kujihami kwa pamoja" kwa kuhimiza marekebisho ya katiba ya nchi.
|
Ulinzi wa hakimiliki ya ubunifu, sekta mpya ya maendeleo ya nchi zinazoendelea 2007/10/10 Hivi karibuni katika biashara ya kimataifa, hali inayovutia ni kwamba nchi zilizoendelea mara kwa mara zinazilaumu nchi zinazoendelea kwa kudai kukiuka hakimiliki ya ubunifu, hakimiliki ya ubunifu imekuwa ngome ya teknolojia mpya. Kutokana na hali hiyo, je nchi zinazoendelea zifanyeje ili kupambana na hali hiyo?
|
Mazungumzo kati ya Palestina na Israel yaanza katika hali ngumu 2007/10/09 Kikundi cha maandalizi ya mazungumzo kati ya Palestina na Israel kilifanya mkutano tarehe 8 huko Jerusalem kuhusu mswada wa taarifa ya pamoja ya mkutano wa kimataifa wa suala la Mashariki ya Kati. Kikundi hicho kimeundwa kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi wa Palestina na Israel tarehe 10 Septemba.
|
Nani anapaswa kuwajibika na tukio la mauaji ya "Black Water"? 2007/10/08 Ukitembea barabarani huko Baghdad, mji mkuu wa Iraq, ukiambiwa chukua tahadhari juu ya mabomu yaliyotegwa kando ya barabara pamoja na kampuni binafsi za usalama za Marekani, si mzaha wala jambo la kuchekesha, bali hii ni hali ilivyo sasa inayowatia watu wasiwasi mkubwa.
|
Rais Pervez Musharraf wa Pakistan atazamiwa kushinda katika uchaguzi wa rais wa awamu nyingine 2007/10/05 Wakati uchaguzi mkuu wa Pakistani unapokaribia kufanyika hapo tarehe 6 Oktoba, rais Pervez Musharraf amechukua hatua mbalimbali ili achaguliwe tena kuwa rais wa nchi hiyo. Vyombo vya habari vya Pakistan vimechambua kuwa, rais Pervez Musharraf anatazamiwa kupata ushindi kwenye uchaguzi huo
|
Kwa nini jeshi la Marekani limeshindwa kupata mahala pa kujenga ofisi za kituo chake barani Afrika? 2007/10/04 Jeshi la Marekani tarehe 2, Oktoba lilitangaza kuwa, kituo chake kinachoshughulikia kuratibu shughuli za kiusalama na mapambano dhidi ya ugaidi barani Afrika kilianza kufanya kazi tarehe mosi Oktoba. Hivi sasa makao makuu ya kituo hicho yako mjini Stuttgart, nchini Ujerumani.
|
Uingereza yatoa mpango mpya wa kuondoa wanajeshi wake kutoka Iraq 2007/10/03 Katika hali isiyotarajiwa, waziri mkuu wa Uingereza Bw. Gordon Brown tarehe 2 Oktoba alifanya ziara ya ghafla nchini Iraq. Baada ya kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Iraq Bw. Nouri Maliki, Brown aliwaambia waandishi wa habari kuwa, wanajeshi elfu moja wa Uingereza kati ya wale walioko huko Basra, mji wa kusini mwa Iraq wataondolewa kabla ya mwishoni mwa mwaka huu
|
Vladimir Putin amepanga kugombea nafasi ya ubunge kwenye baraza la chini la bunge la Russia 2007/10/02 Rais Vladimir Putin wa Russia amesema atagombea nafasi ya ubunge kwenye baraza la chini la bunge la Russia kwa tiketi ya chama cha Allied United Russia katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 2, mwezi Desemba. Rais Putin alitoa kauli hiyo tarehe 1 Oktoba kwenye mkutano mkuu wa chama hicho
|
Maonesho ya picha kuhusu maisha ya Wachina yawavutia Wamisri 2007/10/01 Maonesho ya picha kuhusu maisha ya watu wa China yaliyoanza kufanyika tarehe 29, Septemba huko Cairo yanawavutia watu wengi wa Misri. Maonesho hayo ni kama madirisha yaliyofunguliwa kwa watazamaji, ambayo yanaweza kuwaletea ufahamu kuhusu historia ya China, utamaduni wake na maisha ya watu wa kawaida wa nchi hiyo.
|
Mkutano wa pande sita kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea wafunguliwa 2007/09/28 Mkutano wa kipindi cha pili cha mazungumzo ya pande sita ya duru la sita kuhusu suala la nyuklia ya peninsula ya Korea ulifunguliwa tarehe 27 Beijing, wajumbe kutoka nchi sita husika China, Korea ya Kaskazini, Korea ya Kusini, Marekani, Japan na Russia wanahudhuria mkutano huo.
|
Mkutano mkuu wa 62 wa Umoja wa Mataifa wafanya kongamano la kawaida 2007/09/26 Tarehe 25 mkutano mkuu wa 62 wa Umoja wa Mataifa ulifanya mkutano wa kawaida. Siku hiyo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon, mwenyekiti wa mkutano huo Bw. Srdjan Kerim pamoja na viongozi wa nchi 27 kutoka Brazil, Marekani, Ufaransa, Iran na nchi nyingine walitoa hotuba na kueleza misimamo yao kuhusu mageuzi ya Umoja wa Mataifa, mabadiliko ya hali ya hewa,maendeleo na haki za binadamu.
|
Viongozi wa nchi mbalimbali wakusanyika kwenye Umoja wa Mataifa kujadili suala la mabadiliko ya hali ya hewa duniani 2007/09/25 Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala la mabadiliko ya hali ya hewa duniani ulifunguliwa tarehe 24 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa yaliyopo mjini New York. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo katibu mkuu wa Umoja huo Bw. Ban Ki-moon alizitaka nchi zilizoendelea ziwe mfano katika juhudi za kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani.
|
Suala la amani ya Mashariki ya Kati lajadiliwa 2007/09/24 Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Russia na Marekani tarehe 23 Septemba zilikuwa na mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi kamili wa mgogoro kati ya Palestina na Israel. Kwenye mazungumzo hayo, wawakilishi wa pande hizo nne ambazo zinasimamia utaratibu wa amani ya Mashariki ya Kati walisikiliza ripoti ya kwanza kuhusu hali ya Mashariki ya Kati iliyowasilishwa na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Bw. Tony Blair.
|
Ziara ya pili ya Condoleezza Rice nchini Palestina na Israel haikupata matokeo yaliyotarajiwa 2007/09/21 Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice tarehe 20 amemaliza ziara yake nchini Palestina na Israel. Hii ni ziara yake ya sita mwaka huu kwenye nchi hizo. Shughuli za ziara ya Condoleezza Rice zilikuwa nyingi, tarehe 19 mchana alifika Jerusalem na tarehe 20 alasiri aliondoka.
|
Israel kuichukulia Gaza kuwa kundi la kiadui kutaleta tatizo jipya 2007/09/20 Baraza la usalama la Israel lilipiga kura tarehe 19 mwezi Septemba kuamua kuichukulia Hamas inayodhibiti ukanda wa Gaza hivi sasa kuwa adui yao, na kuweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya ukanda wa Gaza. Hayo ni matokeo ya watu wenye silaha wa ukanda wa Gaza kushambulia Israel kwa makombora mara kwa mara.
|
Mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa wafunguliwa mjini New York 2007/09/19 Mkutano wa baraza kuu la awamu ya 62 la Umoja wa Mataifa ulifunguliwa mjini New York alasiri ya tarehe 18 mwezi Septemba, wajumbe wa nchi mbalimbali wanashiriki kwenye mkutano mkuu wa baraza hilo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na kujadili masuala wanayofuatilia.
|
Nchi za EU zina maoni tofauti kuhusu kuiwekea vikwazo Iran 2007/09/18 Waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi Bw. Maxime Verhagen tarehe 17 Septemba alisema, Uholanzi na Ufaransa zitajitahidi kuzishawishi nchi nyingi zikubali kuiwekea vikwazo Iran vinavyolenga kuilazimisha nchi hiyo iache mpango wake wa nyuklia ukiwemo wa kusafisha uranium nzito.
|
Mtindo dhahiri wa kiutamaduni waonekana kwenye Mkutano wa 9 wa wafanyabiashara wachina wa sehemu mbalimbali duniani 2007/09/17 Mkutano wa 9 wa wafanyabiashara wachina wa sehemu mbalimbali duniani unaoendelea huko Japan umeonesha dhahiri mtindo wake pekee wa sanaa na utamaduni wa China, ambapo maonesho ya michoro ya kichina, maandiko ya Kichina yanafanyika pia wakati wa mkutano huo
|
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lapitisha "Taarifa ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wananchi wa asili" 2007/09/14 Mkutano wa 61 wa wajumbe wote wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 13 ulipitisha "Taarifa ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wananchi wa asili" kwa kura 143 za ndio, kura 4 za hapana, na kura 11 hazikupigwa.
|
Mwaka wa sita baada ya tukio la "Septemba 11", Mapambano dhidi ya ugaidi yanahitaji ushirikiano wa pande zote 2007/09/12 Tarehe 11 ilikuwa ni siku ya kuadhimisha mwaka wa sita baada ya tukio la "Septemba 11". Watu wengi wamegundua kwamba mwaka huu Marekani haikufanya shughuli nyingi kukumbuka siku hiyo kama ilivyokuwa zamani
|
Je Marekani imekuwa salama zaidi miaka sita baada ya tukio la "Septemba 11"? 2007/09/11 Tarehe 11 Septemba mwaka 2001 kundi la Al-Qaeda liliishambulia Marekani kwa shambulizi kubwa la kigaidi ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Marekani, na kusababisha vifo vya watu karibu 3,000, baadaye Marekani ilianzisha vita dhidi ya Afghanistan na Iraq na huku nchini ikiwa imeimarisha vitendo vya kusikiliza kisirisiri mawasiliano ya watu, na kuchukua hatua kali za usalama
|
Mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya APEC wajadili kwanza suala la mabadiliko ya hali ya hewa, halafu kuzungumza mambo ya uchumi 2007/09/07 Mkutano wa 15 usio rasmi wa viongozi wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki APEC unatazamiwa kufanyika huko Sydney, Australia kuanzia tarehe 8 hadi 9 Septemba, ambapo viongozi au wajumbe wa nchi wanachama wa Jumuiya ya APEC akiwemo rais Hu Jintao wa China watajadili masuala makubwa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa
|
Tishio la ugaidi lakaribia nchini Ujerumani 2007/09/06 Mkurugenzi mkuu wa Idara ya uendeshaji wa mashitaka ya Ujerumani Bibi Monika Harms tarehe 5 alitangaza kuwa, idara ya usalama ya Ujerumani tarehe 4 ilivunja njama ya magaidi ya kujaribu kushambulia vikali kwa mabomu kituo cha Marekani nchini Ujerumani.
|
Rais Hu Jintao atoa hotuba kwenye Mkutano wa kilele wa mambo ya biashara wa APEC 2007/09/06 Mkutano wa kilele wa mambo ya biashara wa jumuiya ya ushirikiano wa uchumi wa Asia na sehemu ya Pasifiki, APEC, ambao utafanyika kwa siku 2, umefunguliwa tarehe 6 mwezi Septemba kwenye jumba la michezo ya opera la Sydney, Australia.
|
Je "ramani ya amani ya Iraq" inaweza kuiletea Iraq amani? 2007/09/05 Wajumbe wa madhehebu ya Shia na Suni hivi karibuni walifanya mazungumzo ya faragha kwa siku nne nchini Finland na wametunga "ramani ya amani ya Iraq", pande mbili ziliahidi kuwa zitafanya juhudi bila kusita ili kuleta utatuzi wa kudumu wa migogoro nchini Iraq.
|
Ban Ki-moon afanya ziara kwenye nchi tatu za Afrika ili kusukuma mchakato wa kisiasa wa Darfur 2007/09/04 Kuanzia tarehe 3 katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon ameanza kufanya ziara rasmi ya siku sita nchini Sudan na nchi jirani Chad na Libya. Tangu Bw. Ban Ki-moon awe katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa siku zote ana matumaini ya mafanikio fulani kwa juhudi zake katika utatuzi wa suala la Darfur.
|