Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Maendeleo yapatikana katika ushirikiano kati ya tume ya uchunguzi ya kimataifa wa tukio la kuuawa kwa Bw Hariri na Syria
  •  2005/09/13
    Mkuu wa tume ya uchunguzi wa kimataifa wa kesi kuhusu kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Al-Hariri Bw. Detlev Mehlis alifanya mazungumzo na mshauri wa sheria wa wizara ya mambo ya nje ya Lebanon Bw. Riad Daoudi tarehe 12 mjini Damascus Syria
  • Jeshi la Israel laanza kuondoka kutoka sehemu ya Gaza
  •  2005/09/12
    Jeshi la ulinzi la Israel tarehe 11 alasiri lilifanya shughuli ya kuaga na kushusha bendera ya taifa katika makao makuu yake yaliyoko karibu na makazi ya zamani ya Wayahudi katika sehemu ya Gaza.
  • Uchaguzi mkuu wa Japan wakaribia
  •  2005/09/09
    Uchaguzi wa baraza la chini la bunge la Japan utafanyika tarehe 11. Ingawa kimbunga nambari 14 cha Nabi kiliikumba Japan na kuleta athari, na kuwafanya viongozi na wagombea wa vyama mbalimbali wapunguze idadi ya hotuba wanazotoa hadharani na wagombea wanajitahidi kupata kura nyingi zaidi katika uchaguzi huo
  • Pendekezo la Uingereza la kuchunguza mawasiliano ya simu dhidi ya ugaidi lazusha migongano katika Umoja wa Ulaya
  •  2005/09/09
  • Pande husika za mazungumzo ya pande sita zafanya maandalizi ya kurejeshwa kwa mazungumzo hayo
  •  2005/09/08
    Waziri wa mambo ya nje na biashara wa Korea ya Kusini Bwana Ban Ki-Moon tarehe 7 huko Seoul alisema kuwa, serikali ya nchi yake itashiriki kwenye mkutano wa kipindi cha pili wa mazungumzo ya duru la nne ya pande sita, kwa msingi wa matokeo ya majadiliano kati yake na pande husika nyingine. Vyombo vya habari vinaona kuwa, ingawa tarehe halisi ya kufanya mkutano wa kipindi cha pili bado haijathibitishwa, lakini pande mbalimbali zote zimefanya maandalizi ya kurejeshwa kwa mazungumzo hayo wiki ijayo.
  • Misri yafanya uchaguzi wa urais wa moja kwa moja kwa mara ya kwanza
  •  2005/09/08
    Tarehe 7 Misri ilifanya uchaguzi wa rais wa moja kwa moja kwa mara ya kwanza unaowashirikisha wagombea kumi akiwemo Hosni Mubarak, ambaye ni rais wa sasa , Ayman Nour ambaye ni mgombea wa chama cha Al-Ghad
  • Jumuiya ya kimataifa yaweza kukabiliana na mfumko wa bei ya mafuta
  •  2005/09/07
    Tangu shirika la nishati duniani liamue kutuliza bei ya soko la mafuta kwa kutumia mafuta ya akiba ya kimkakati, bei ya mafuta sokoni ilipungua kwa siku tatu mfululizo.
  • Sharon ajibu mashambulizi kutoka Netanyahu na kupata mafanikio
  •  2005/09/07
    Mabadiliko yametokea hivi karibuni katika kugombea nafasi ya mwenyekiti wa chama cha Likud kati ya waziri mkuu wa Israel Bw. Ariel Sharon na waziri wa fedha wa zamani Bw. Benjamin Netanyahu.
  • Kitendo cha upande mmoja wa Israel kitakuwa na ufanisi mkubwa kiasi gani katika nchi za kiislam?
  •  2005/09/06
    Hivi karibuni serikali ya Israeli ikitumia fursa ya kutekeleza mpango wa vitendo wa upande mmoja ilifanya shughuli nyingi za kidiplomasia ili kuboresha uhusiano na nchi jirani za kiarabu, na ilipata maendeleo fulani.
  • Marekani yaanza kutoa misaada kwa pande zote na hali ya mji wa New Orleans inaelekea kutulia
  •  2005/09/05
    Kutokana na athari kubwa ya kimbunga kiitwacho "Katrina", mji wa New Orleans ulikumbwa na fujo, watu elfu kumi kadhaa walipoteza makazi.
  • Palestina yatumai kuanzisha mchakato wa amani haraka iwezekanavyo
  •  2005/09/05
    Mwenyekiti wa mamlaka ya Palestina Bw. Mahmoud Abbas hivi karibuni alieleza kuwa Palestina inatumai kurejesha mara moja mazungumzo kati yake na Israel baada ya kukamilisha mpango wa upande mmoja kwa Israel, kuhusu masuala mengi ambayo bado hayajatatuliwa, ili kuanzisha nchi ya Palestina mwaka kesho
  • Russia yaadhimisha mwaka mmoja wa tukio la utekaji nyara la Beslan
  •  2005/09/02
    Tarehe mosi mwezi Septemba ni siku ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu tukio la utekaji nyara litokee mjini Beslan, Jamhuri ya Osetia ya Kaskazini ya Russia.
  • Mji wa New Orleans wa Marekani Wapata Maafa Makubwa
  •  2005/09/01
    Kimbunga kinachojulikana kwa jina la Katrina kimeikumba sehemu ya kusini ya Marekani, nguvu yake na uharibifu wake ulizidi makadirio ya watu.
  • Mandelson ataka Umoja wa Ulaya upitishe bidhaa za nguo za China
  •  2005/08/31
    Mjumbe wa kamati ya Umoja wa Nchi za Ulaya Bw. Peter Mandelson tarehe 30 alipotoa hotuba kwenye kamati ya biashara ya bunge la Ulaya alitoa wito kuzitaka nchi za Umoja wa Ulaya ziruhusu bidhaa za nguo za China zilizozuiliwa kwenye bandari mbalimbali za Umoja wa Ulaya, ziingie kwenye soko la umoja huo.
  • Mkutano wa Kupunguza Silaha Haukupiga Hatua kwa Muda Mrefu
  •  2005/08/30
    Mkutano wa kupunguza silaha mwaka 2005 hivi sasa unafanyika mjini Geneva. Ukiwa mkutano pekee wa kupunguza silaha duniani umekwama bila mafanikio yoyote katika muda wa miaka sita iliyopita.
  • Iran Yataka Kuvunja Muundo wa Mazungumzo
  •  2005/08/29
    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bw. Hamid Reza Asefi tarehe 28 alisema kuwa Iran haioni Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ni nchi pekee za kushiriki katika mazungumzo na Iran kuhusu suala la nyuklia, na pengine nchi hizo tatu zitasukumwa pembeni katika mazungumzo ya baadaye
  • Hali ya usalama ni hatari kabla ya uchaguzi wa bunge la Afghanistan
  •  2005/08/29
    Polisi wa Afghanistan tarehe 28 walithibitisha kuwa mgombea mbunge mwingine wa Afghanistan tarehe 27 aliuawa katika mashambulizi yaliyotokea kusini mwa Afghanistan.
  • Iran yapenda nchi zinazoshiriki kwenye mazungumzo ya suala la nyuklia ziongezeke
  •  2005/08/26
    mwakilishi wa kwanza katika mazungumzo ya suala la nyuklia la Iran Bw. Ali Larijani tarehe 25 alieleza kupitia kituo cha televisheni cha Iran kuwa, Iran inatumai nchi tatu za Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani zinazoshiriki kwenye mazungumzo ya suala la nyuklia zitaongezeka na kuwa nchi wanachama wote wa baraza la Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani
  • Kwanini Umoja wa Ulaya umejitumbukiza katika hali ngumu ya kutoa uamuzi mwafaka
  •  2005/08/25
    Chini ya shinikizo za nchi za Ufaransa na Italia ambazo ni nchi zinazozalisha bidhaa nyingi za nguo na mashirika ya nguo ya Umoja wa Ulaya, kamati ya Umoja wa Ulaya na idara za serikali ya China mwezi Juni zilifikia kumbukumbu ya maelewano kuhusu suala la bidhaa za nguo za China
  • Marekani yalegeza kwa kiasi fulani msimamo wake kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea
  •  2005/08/25
    Duru la 4 la mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea linatazamiwa kuendelea ndani ya wiki moja itakayoanzia tarehe 29 mwezi huu.
  • Hali ya Palestina na Israel bado inakabiliwa na mabadiliko
  •  2005/08/25
    Tarehe 23 usiku, mpango wa upande mmoja wa Israel wa kuwaondoa walowezi wayahudi kutoka kwenye ukanda wa Gaza na kaskazini ya sehemu ya magharibi wa mto Jordan ulimalizika kimsingi.
  • Mswada wa katiba mpya ya Iraq wakabiliwa na hatari ya kutofanikiwa
  •  2005/08/24
    Usiku wa manane wa tarehe 22 kwa saa za Iraq, Bunge la mpito la Iraq lilipokea mswada wa katiba mpya ulioungwa mkono na madhehebu ya Shia na Wakurd. Kutokana na mswada huo kutokubaliwa na madhehebu ya Sunni, bunge la mpito halikuupigia kura mswada huo, bali kuamua kutoa siku tatu nyingine za kufanya majadiliano zaidi, ili katiba hiyo mpya ikubaliwe na makundi mbalimbali.
  • Mkutano wa Shirika la afya duniani wafuatilia suala la afya Barani Afrika
  •  2005/08/23
    Mkutano wa 55 wa kamati ya sehemu ya Afrika ya Shirika la afya duniani WHO, ulifunguliwa tarehe 22 huko Maputo, mji mkuu wa Msumbiji. Mawaziri wa afya na wawakilishi wao kutoka nchi wanachama wa WHO, wajumbe wa mashirika ya pande nyingi na pande mbili na jumuiya zisizo za kiserikali wapatao mia kadhaa wamehudhuria mkutano huo.
  • Hali ya kugombea madaraka ya mamlaka ya ukanda ya Gaza
  •  2005/08/23
    Baada ya wakazi wa Israel kuondoka kutoka kwenye ukanda wa Gaza, udhibiti wa mamlaka ya taifa ya Palestina kwenye ukanda wa Gaza unakabiliwa changamoto kali ya chama cha upinzani cha kiislamu cha Palestina (Hamas) ambacho ni kundi la kijeshi lenye nguvu kubwa kabisa katika sehemu hiyo.
  • Kwa nini shughuli za Israel kuondoa makazi ya Wayahudi zimeendelezwa bila vikwazo
  •  2005/08/22
    Shughuli za Israel kuondoa makazi ya Wayahudi yaliyoko kwenye sehemu ya Gaza, tarehe 21 zilikaribia kukamilika. Hadi siku hiyo, makazi 20 kati ya makazi yote 21 yalikuwa tayari yameondolewa. Shughuli za kuondoa makazi hayo zilifanyika bila vikwazo na bila matarajio ya watu.
  • Polisi ya London yajitetea kuhusu kifo cha kijana wa Brazil
  •  2005/08/22
    Jamaa za Menezes na wakili walisema kuwa ni vigumu kuamini kuwa Ian Blair alitangaza hivyo katika hali ya kutofahamu ukweli wa mambo, kwa upande mmoja waliwalaani polisi kuwa hawakusahihisha makosa yao. Kwa upande mwingine walisema kuwa Ian Blair anapaswa kuwajibika kuhusu kifo cha Menezes na kumtaka ajiuzulu.
  • Nchi mbalimbali za Jumuiya ya SADC zahimiza utandawazi wa kikanda
  •  2005/08/19
    Mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC ulifungwa tarehe 18 huko Gaborone, mji mkuu wa Botswana.
  • Chama cha Polisalio chawaachia huru mateka wote wa Morocco
  •  2005/08/19
    Kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ilitoa taarifa tarehe 18 mjini Geneva ilisema kuwa, chama cha Polisalio siku hiyo iliwaachia huru mateka 404 wa mwisho wa Morocco.
  • Israeli yatumia nguvu kutekeleza mpango wa vitendo
  •  2005/08/18
     Askari polisi wa Israel walipotekeleza amri ya kuondoa wakazi walipingwa vikali na baadhi ya wakazi wa huko ambao waliwatupia chupa za maji, mayai na vitu vingine, na askari mmoja mwanamke alijeruhiwa kwa kuchomwa kisu. Mbele ya upinzani wa wakazi, askari hao walichukua msimamo thabiti na kujizuia.
  • Wabunge wa Burundi kumteua rais
  •  2005/08/18
    Tarehe 19, wabunge wa Burundi watamteua rais wa nchi hiyo katika harakati za kumaliza mapigano ambayo yameangamiza watu wapatao 300,000.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44