Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Mkutano wa kimataifa kuhusu suala la usalama wa Iraq wafanya juhudi kuboresha usalama nchini Iraq
  •  2007/05/03
    Mkutano wa kimataifa kuhusu suala la usalama wa Iraq ambao pia ni mkutano wa wajumbe wa makubaliano ya kimataifa kuhusu Iraq, unafanyika mjini Sham el-Sheikh tarehe 3 na tarehe 4
  • Rais George Bush akataa mswada wa sheria ya kutenga fedha kwa ajili ya vita
  •  2007/05/02
    Rais George W. Bush wa Marekani tarehe mosi mwezi Mei alikataa mswada wa sheria ya kutenga fedha kwa ajili ya vita uliowasilishwa na bunge, jambo hilo limeongeza mvutano kati ya Ikulu na bunge la Marekani kuhusu suala la kutenga fedha kwa ajili ya vita.
  • Amani na usalama bado haujatimizwa mjini Baghdad miaka minne baada ya kumalizika kwa vita vya Iraq
  •  2007/05/01
    Tarehe mosi mwezi Mei mwaka 2003 Rais George W. Bush alitangaza kumalizika kwa vita vya Iraq. Lakini miaka minne tangu Marekani itoe ahadi ya Marekani kuhusu kutimiza amani na usalama nchini Iraq haijatimizwa. Bw. Jamal ni mkazi wa mji wa Baghdad aliyeshuhudia vita vya Iraq
  • Msimamo wa serikali ya China kuhusu suala la Darfur ya Sudan
  •  2007/04/30
    Siku zote kwenye mgogoro wa Darfur wa Sudan, serikali ya China inatetea kulinda mamlaka ya Sudan na ukamilifu wa ardhi yake, na kutatua suala hilo kwa amani kwa njia ya mazungumzo
  • Ziara ya waziri mkuu wa Japan Mashariki ya Kati inalenga kuhakikisha usalama wa nishati wa Japan
  •  2007/04/29
    Waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe tarehe 28 alifika Riyadh na kuanza ziara nchini Saudi Arabia. Na baadaye pia atazizuru Misri, Kuwait, Qatar na umoja wa falme za kiarabu. Wachambuzi wanasema ziara hiyo ya Bw. Abe katika nchi za Mashariki ya Kati inalenga kuimarisha uhusiano kati ya Japan na nchi zinazozalisha mafuta
  • Pande husika za mgogoro wa Palestina na Israel zajizuia kutokana na hali ya wasiwasi ya hivi sasa
  •  2007/04/27
    Kundi lenye silaha la Palestina tarehe 26 liliishambulia Israel kwa makombora mawili kutoka sehemu ya Gaza, hii ni siku ya tatu mfululizo kwa kundi lenye silaha la Palestina kurusha makombora kwa Israel baada ya tarehe 24. Wakati huo huo kundi la Jihad lilisema, halitatekeleza ahadi za kundi la Hamas kuhusu kurudi katika makubaliano ya kusimamisha vita usiku wa tarehe 25, na itaendelea kuishambulia Israel, lakini pande nyingine husika bado zimejizuia
  • Umoja wa Ulaya wajaribu kuangalia uwezekano wa kuendelea na mazungumzo kuhusu suala la nyuklia la Iran
  •  2007/04/26
    Tarehe 25 mjumbe wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya nje na sera za usalama Bw. Javier Solana na mjumbe wa kwanza wa mazungumzo wa Iran Bw. Ali Larijani kwa mara ya kwanza walifanya mazungumzo tokea mwezi Februari. Kutokana na hali ya hivi karibuni, pande zote mbili hazikuwa na matumaini yoyote kama mazungumzo hayo yangeweza kuondoa vikwazo vya mazungumzo kuhusu suala la nyuklia la Iran.
  • Kujiuzulu kwa waziri wa mambo ya ndani wa Palestina kumeonesha mgongano kwenye eneo la usalama
  •  2007/04/25
    Waziri wa mambo ya ndani wa Palestina Bw. Hani Kawasmeh tarehe 23 mwezi Aprili alimkabidha waziri mkuu Ismail Haniyeh ombi la kujiuzulu. Ingawa ombi hilo lilikataliwa, na Bw. Hani Kawasmeh aliamua kubaki na wadhifa huo, lakini wachambuzi wanaona kuwa kwa kiwango fulani, kujiuzulu kwa waziri wa mambo ya ndani wa Palestina, kunaonesha mgongano katika eneo la usalama ndani ya serikali ya nchi hiyo. 
  • Ushirikiano kati ya China na Afrika wapaswa kuzisaidia nchi za Afrika zipate maendeleo ya pamoja
  •  2007/04/25
    Mkutano wa Baraza la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Kenya ulifunguliwa tarehe 24 Aprili huko Nairobi Kenya, Mkutano huo unalenga kuimarisha ushirikiano kati ya China na Kenya na bara la Afrika katika sekta za uchumi na biashara.
  • Jeshi la Marekani lapingwa kujenga ukuta wa utenganishaji nchini Iraq
  •  2007/04/24
    Baada ya waziri mkuu wa Iraq Bw. Nuri al-Maliki kuonesha upinzani dhidi ya jeshi la Marekani kujenga ukuta nchini Iraq, balozi wa Marekani nchini Iraq Bw. Ryan Crocker tarehe 23 alisema ataheshimu maoni ya serikali ya Iraq, lakini hakusema wazi kusimamisha ujenzi wa ukuta huo.
  • Bw. Maliki yuko ziarani nchini Misri kufanya maandalizi ya kufanyika kwa mkutano wa kimataifa kuhusu usalama wa Iraq
  •  2007/04/23
    Waziri mkuu wa Iraq Bwana Nuri al-Maliki tarehe 22 aliwasili Cairo kufanya ziara yake ya kwanza nchini Misri tangu ashike madaraka. Lengo la ziara ya Bw. Maliki nchini Misri ni kufanya maandalizi ya kufanyika kwa mkutano wa kimataifa kuhusu usalama wa Iraq mwanzoni mwa mwezi ujao huko Sharm el-Sheikh nchini Misri.
  • Kufuata njia ya maendeleo ya utandawazi wa miji kwa kufuata hali halisi ya nchi
  •  2007/04/20
    Mkutano wa 21 wa Baraza la Shirika la mipango ya makazi ya binadamu la Umoja wa Mataifa unaendelea kufanyika huko Nairobi Kenya, kiongozi wa ujumbe wa China ambaye pia ni naibu waziri wa ujenzi wa China Bibi Fu Wenjuan alipotoa hotuba kwenye Mkutano huo alisema, ili kusukuma mbele maendeleo endelevu ya utandawazi wa miji, ni lazima kushikilia njia ya kufuata hali halisi ya nchi.
  • Hali ya usalama nchini Iraq inazidi kuwa mbaya
  •  2007/04/19
    Waziri mkuu wa Iraq Bw. Nuri al-Maliki tarehe 18 alisema jeshi la usalama la Iraq litapokea madaraka ya kusimamia usalama wa taifa, lakini masaa machache tu baada ya kutoa kauli hiyo kulitokea milipuko minne mjini Baghdad, watu karibu 200 walikufa na 250 kujeruhiwa. Hili ni tukio kubwa kabisa tokea jeshi la Marekani nchini Iraq na jeshi la usalama la Iraq kuanza kutekeleza mpango mpya wa usalama mwezi Februari.
  • Iran yaonesha tena msimamo mkali kuhusu suala la nyuklia
  •  2007/04/18
    Mwenyekiti wa shirika la nishati ya atomiki la Iran Bw. Gholam Reza Aghazadeh tarehe 17 katika mji wa Natanz alisema, kazi ya kufunga mashinepewa katika mji huo haijawahi kusimama, na Iran itajitahidi kadiri iwezavyo kukamilisha mpango wake wa kufunga mashinepewa elfu 50.
  • China imeonesha juhudi zake za kiujenzi katika suala la Darfur
  •  2007/04/17
    Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bwana Zhai Jun hivi karibuni akiwa mjumbe maalum wa serikali ya China alifanya ziara nchini Sudan.
  • Ni kwa nini mazungumzo kati ya viongozi wa Palestina na Israel hayakuhusisha masuala nyeti?
  •  2007/04/16
    Waziri mkuu wa Israel Bw. Ehud Olmert na mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas tarehe 15 walifanya mazungumzo huko Jerusalem. Hayo ni mazungumzo ya kwanza kati yao tangu utaratibu wa viongozi hao wawili kukutana kila baada ya kipindi fulani uanzishwe.
  • Je, Korea ya Kaskazini inaweza kufunga miundo mbinu ya nyuklia ya Yongbyon kwa wakati?
  •  2007/04/13
    Tarehe 14 Aprili ni siku ya mwisho kwa Korea ya Kaskazini kufunga miundo mbinu ya nyuklia ya Yongbyon. Hii ni siku iliyowekwa katika makubaliano ya duru la tano la mazungumzo ya pande sita, kuweza au kutoweza kwa Korea ya Kaskazini kufunga miundo mbinu hiyo kwa wakati uliopangwa ni suala linalofuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa.
  • Kutangaza mafanikio ya nyuklia kwa Iran kunazingatia zaidi mtizamo wa kisiasa kuliko wa kiteknolojia
  •  2007/04/12
    Rais Mohmoud Ahmadinejad wa Iran hivi karibuni alitangaza "mafanikio mapya ya nyuklia", yaani Iran hivi sasa imeanza kuzalisha kwa wingi nishati ya nyuklia, mwakilishi wa kwanza wa Iran kwenye mazungumzo ya nyuklia Bw Ali Larijani alihakikisha kuwa, wahandisi wa nchi hiyo wameweka hewa ya UF6 katika kinu cha kuzalisha uranium nzito.
  • Kwa ajili ya kuimarisha urafiki na ushirikiano
  •  2007/04/12
    Tarehe 12 Aprili, waziri mkuu wa China Bw Wen Jiabao ambaye yuko ziarani Japan alitoa hotuba kuhusu "urafiki na ushirikiano" kwa wabunge zaidi ya 400 kwenye ukumbi wa baraza la chini la bunge la Japan. Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa China kutoa hotuba kwenye bunge la Japan katika miaka 22 iliyopita.
  • Umoja wa Mataifa wasema kuongezeka kwa joto duniani kutaleta maafa makubwa kwa binadamu
  •  2007/04/11
    Shirika husika la Umoja wa Mataifa tarehe 10 mwezi Aprili lilitoa taarifa ikieleza athari zitakazoletwa moja kwa moja kwa maisha ya binadamu katika siku za baadaye kutokana na hali ya hewa duniani kubadilika kuwa joto. Taarifa inasema kama hali ya hewa duniani itaendelea kuongezeka kuwa joto zaidi, basi katika miongo kadhaa ijayo binadamu watakabiliwa na maafa makubwa.
  • Ufunguzi wa Mwaka wa maingiliano kati ya China na Korea ya kusini wafanyika huko Seoul
  •  2007/04/11
    Ufunguzi wa Mwaka 2007 wa maingiliano kati ya China na Korea ya kusini ulifanyika usiku wa tarehe 10 Aprili kwenye Jumba la michezo ya sanaa la taifa huko Seoul, mji mkuu wa Korea ya kusini. Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao ambaye yuko ziarani nchini Korea ya kusini na waziri mkuu wa Korea ya Kusini Bwana Han Duck Soo walihudhuria ufunguzi huo.
  • Shughuli za "Mwaka wa maingiliano kati ya China na Japan kwenye sekta za utamaduni na michezo" zaendelea vizuri
  •  2007/04/10
    Huu ni mwaka wa 35 tangu uhusiano wa kibalozi kati ya China na Japan uwe wa kawaida, na mwaka huu pia umeamuliwa na viongozi wa nchi hizo mbili kuwa "Mwaka wa maingiliano kati ya China na Japan kwenye sekta za utamaduni na michezo", ambapo nchi hizo mbili zitafanya shughuli za aina mbalimbali za utamaduni na michezo, ili kuongeza zaidi maingiliano kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.
  • Kwa nini Iran imejitangaza kuwa nchi ya "klabu ya nyuklia"?
  •  2007/04/10
    Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran tarehe 9 alikagua miundombinu ya nyuklia iliyoko katika Natanz, kisha kwenye mkutano wa kusherehekea mafanikio ya shughuli za nyuklia alisema, Iran imekuwa na uwezo wa kuzalisha nishati ya nyuklia, na kusema kwamba tokea hapo Iran "imejiunga na klabu ya nyuklia". Kauli hiyo mara ilisababisha mshituko mkubwa kwa jumuiya ya kimataifa.
  • Hali ya Cote d'Ivoire yaelekea kuwa tulivu hatua kwa hatua
  •  2007/04/09
    Vyombo vya habari vya Cote d'Ivoire tarehe 8 viliikariri tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo ikisema, jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa na jeshi la Ufaransa yataondoka Cote d'Ivoire kuanzia tarehe 16 mwezi huu. Siku moja kabla ya hapo, serikali ya mpito ya Cote d'Ivoire iliyoongozwa na waziri mkuu mpya Bw. Guillaume Soro iliundwa.
  • Askari wanamaji wa Uingereza waliokamatwa na Iran waachiwa huru na kurudi nyumbani
  •  2007/04/06
    Tarehe 23 Machi askari 15 wanamaji wa Uingereza walikamatwa na Iran kwa sababu ya kuingia eneo la bahari ya Iran bila idhini. Baada ya juhudi nyingi za vuta nikuvute, mwishowe tarehe 5 Aprili askari hao wanamaji waliachiliwa huru na kurudi nyumbani.
  • Kwa nini tukio la "askari wa jeshi la maji" limeweza kutatuliwa kwa njia ya amani?
  •  2007/04/05
    Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran tarehe 4 alitangaza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika huko Tehran kuwa, Iran imeamua kuwasamehe na kuwaachia huru askari 15 wa jeshi la maji la Uingereza waliozuiliwa nchini humo kuanzia tarehe 23 Machi. Vyombo vya habari vinaona kuwa, tukio hilo limeweza kutatuliwa kwa njia ya amani ni kutokana na sababu mbalimbali.
  • Mkutano wa wakuu wa Umoja wa ushirikiano wa kanda ya Asia Kusini wafunguliwa
  •  2007/04/04
    Mkutano wa 14 wa wakuu wa Umoja wa ushirikiano wa kanda ya Asia Kusini ulifunguliwa tarehe 3 huko New Delhi, mji mkuu wa India. Pamoja na viongozi wa nchi wanachama wa umoja huo, wajumbe wa nchi tano wachunguzi za China, Korea ya Kusini, Japan, Marekani na Umoja wa Ulaya, pia walihudhuria ufunguzi wa mkutano huo. Huu ni mkutano wa kwanza wa wakuu kufanyika baada ya umoja huo kupokea nchi mpya mwanachama na wachunguzi.
  • Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu usalama wa afya duniani wafanyika nchini Singapore
  •  2007/04/03
    Tarehe 7 Aprili ni "siku ya afya duniani", kauli mbiu ya siku hiyo mwaka huu ni "usalama wa afya duniani". Ili kueneza kauli mbiu hiyo, Shirika la Afya Duniani WHO pamoja na serikali ya Singapore tarehe mbili zilifanya mkutano wa ngazi ya juu kuhusu usalama wa afya duniani huko Singapore.
  • Kituo cha kimataifa cha kupunguza athari ya maafa ya ukame chaanzishwa Beijing
  •  2007/04/03
    Kituo cha kimataifa cha kupunguza athari ya maafa ya ukame kilianzishwa tarehe 2 Aprili mjini Beijing, kituo hicho kilianzishwa chini ya ushirikiano kati ya Kamati ya upunguzaji wa atahari ya maafa ya China na Shirika la mikakati ya upunguzaji wa athari ya maafa duniani la Umoja wa Mataifa.
  • Ziara ya Chansela Merkel wa Ujerumani kwenye sehemu ya Mashariki ya Kati yabainisha msimamo wa Umoja wa Ulaya
  •  2007/04/02
    Chansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye yuko ziarani huko Mashariki ya Kati, tarehe mosi Aprili alisema Umoja wa Ulaya unapenda kuzisaidia pande mbili za Palestina na Israel katika juhudi za kuleta amani.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44