Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Serikali mpya ya Iraq yakabiliwa na changamoto kubwa ya hali mbaya ya usalama
  •  2006/05/22
    Tarehe 21 waziri mkuu mpya wa Iraq Nuri al-Maliky kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, serikali mpya ya Iraq itachukua hatua kali kutuliza ghasia nchini Iraq. Lakini katika siku hiyo hiyo milipuko isiyopungua mitatu ilitokea na kusababisha watu zaidi ya 70 kufariki na kujeruhiwa. Hali mbaya ya usalama imekuwa changamoto kubwa kwa serikali iliyoanzishwa siku chache zilizopita.
  • Spika wa bunge la umma la China atarajia uhusiano kati ya China na Ulaya utaendelea siku hadi siku
  •  2006/05/19
    Spika wa Bunge la umma la China Bwana Wu Bangguo akisema, China inaiunga mkono Romania kujiunga na Umoja wa Ulaya na kuamini kuwa mchakato wa Romania kujiunga na Umoja wa Ulaya utatia uhai mpya kwa maendeleo ya Umoja wa Ulaya, pia utaleta fursa mpya kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ulaya.
  • Waziri wa mambo ya nje wa Iran afanya ziara ya ghafla nchini Syria
  •  2006/05/19
    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Manouchehr Mottaki tarehe 18 alifanya ziara ya ghafla nchini Syria bila taarifa, na kufanya mazungumzo na rais wa Syria Bashar al-Assad. Kwenye mazungumzo walibadilishana maoni na kusawazisha misimamo kuhusu hali ya hivi sasa ya Iraq, Marekani na nchi nyingine za Magharibi kuendelea kuzishinikiza Iran na Syria katika suala la Iran na uhusiano kati ya Syria na Lebanon.
  • Rais wa Iran akataa mapendekezo mapya ya Umoja wa Ulaya
  •  2006/05/18
    Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran tarehe 17 alikataa hadharani mapendekezo mapya ya Umoja wa Ulaya ambayo bado yanajadiliwa. Msimamo huo mgumu umeyafanya mapendekezo hayo yanayosifiwa na Umoja wa Ulaya kuwa ni mapendekezo yenye "ushawishi mkubwa" yazame katika hali mbaya kabla hayajatangazwa rasmi.
  • Umoja wa Mataifa kutuma askari wake kwenye sehemu ya Darfur
  •  2006/05/17
    Tarehe 16 Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio la kutuma jeshi lake kwenye sehemu ya Darfur. Azimio hilo limesema, katika muda wiki moja Umoja wa Mataifa utatuma kikundi cha uchunguzi katika sehemu ya Darfur ili kuweka msingi wa kupeleka jeshi lake la kulinda amani katika sehemu hiyo.
  • Umoja wa Ulaya kutoa mapendekezo mapya ya kutatua suala la nyuklia la Iran
  •  2006/05/16
    Tarehe 15 mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Umoja wa Ulaya walifanya mkutano huko Brussels na kujadili mapendekezo mapya ya nchi tatu Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuhusu utatuzi wa suala la nyuklia la Iran.
  • Kikundi cha upinzani chakataa kutia saini mkataba wa amani nchini Sudan
  •  2006/05/15
    Tarehe 14 kiongozi wa kikundi cha kundi kubwa la upinzani "the Sudan Liberation Army", SLA, Bw. Mohammed al-Nur kwa mara nyingine tena alikataa ombi la Umoja wa Afrika la kukitaka kikundi hicho kisaini mkataba wa amani na kuufanya mchakato wa amani nchinin Sudan umekwe.
  • Suala la nyuklia la Iran laingia katika kipindi kipya cha mazungumzo
  •  2006/05/12
    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi.Condoleezza Rice hivi karibuni amesema, Umoja wa Ulaya utaanza tena juhudi za mazungumzo ya kidiplomasia kuhusu utatuzi wa suala hilo na utatoa mlolongo wa mapendekezo ndani ya wiki moja au mbili
  • Jeshi la Uingereza lakumbwa na matatizo nchini Iraq
  •  2006/05/11
    Waziri mkuu wa Uingereza Bw. Tony Blair tarehe 8 kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, iwapo baraza la mawaziri la waziri mkuu mpya Bw. Nouri al-Maliki litakuwa tayari kuchaguliwa, nchi zilizopeleka majeshi nchini Iraq zitajadiliana jukumu la kila nchi
  • Hali ya kukwama kuundwa kwa serikali ya Iraq inatazamiwa kutatuliwa
  •  2006/05/10
    Waziri mkuu mpya wa Iraq Bw. Nouri al-Maliki tarehe 9 alitangaza kuwa, ingawa mawaziri wa wizara za biashara na mawasiliano ambazo ni idara nyeti katika ukarabati wa uchumi hawajachaguliwa
  • Kwa nini rais Mahmoud Ahmadinejad amwandikie barua rais Bush
  •  2006/05/09
    Msemaji wa serikali ya Iran, Bw. Gholamhossein Elham, tarehe 8 huko Tehran alisema, rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran alimwandikia barua rais Bushi wa Marekani na kutoa "mapendekezo mapya" kuhusu utatuzi wa masuala ya kimataifa na kupunguza hali ya wasiwasi duniani.
  • Milipuko inaongezeka kabla ya serikali mpya ya Iraq kuundwa
  •  2006/05/08
    Wakati waziri mkuu mpya wa Iraq Bw. Jawad al-Maliki anaposhughulika kufanya mazungumzo ya mwisho na viongozi wa makundi mbalimbali kuhusu mgawanyiko wa madaraka ya serikali, milipuko inazidi kuongezeka nchini Iraq.
  • Mazungumzo ya amani ya suala la Darfur ya Sudan yakwama tena
  •  2006/05/05
    Makundi makuu mawili ya jeshi la upinzani la Sudan yanayoshiriki mazungumzo ya amani ya suala la Darfur ya Sudan tarehe 5 alafajiri yalitangaza huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria kuwa, yanakataa kutia saini kwenye mswada wa mapatano ya amani uliotolewa na Umoja wa Afrika kuhusu mgogoro wa Darfur.
  • Jitihada za kupambana na madawa ya kulevya zahitaji ushirikiano wa kimataifa
  •  2006/05/04
    Kuanzia miaka ya 60 ya karne iliyopita, madawa ya kulevya yalikuwa yameenea duniani kama ugonjwa wa tauni, ambapo idadi ya watu wanaotumia madawa ya kulevya inaongezeka siku hadi siku, na athari zilizoletwa na madawa hayo yamezidi kuwa mbaya siku hadi siku.
  • Suala la nyuklia la Iran bado liko kwenye njia ya utatuzi wa kidiplomasia
  •  2006/05/03
    Mkutano wa Paris uliomalizika tarehe 2 usiku haukuweza kufikia makubaliano kuhusu suala la nyuklia la Iran. Mawaziri wa nchi hizo sita wataendelea kufanya mazungumzo kuhusu suala hilo tarehe 9 huko New York.
  • Wahamiaji milioni moja nchini Marekani wafanya mgomo mkubwa
  •  2006/05/02
    Wahamiaji kutoka nchi za nje wanaoishi katika sehemu mbalimbali nchini Marekani tarehe 1 Mei walifanya maandamano na mgomo wa kazi, wakidai serikali ya Marekani ibadilishe sera ya wahamiaji na kulinda haki na maslahi halali ya wahamiaji.
  • Marekani na Iran yaanzisha mvutano mpya
  •  2006/05/01
    Baada ya Bw. Baradei kuwasilisha ripoti kuhusu suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la IAEA na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa,  Iran ilionya kuwa, kama baraza la usalama litachukua hatua kali dhidi ya Iran, Iran itachukua hatua zinazolingana. 
  • Rais Hu Jintao wa China alihutubia Bunge la Nigeria
  •  2006/04/28
    Rais Hu Jintao wa China tarehe 27 alilihutubia bunge la Nigeria, ambapo alifafanua kikamilifu sera na mapendekezo ya China kuhusu kuendeleza uhusiano kati ya China na Afrika.
  • Hali ya usalama nchini Iraq bado duni
  •  2006/04/28
    Tarehe 27 mwezi huu dada wa makamu mpya wa rais wa Iraq Bw. Tarek al-Hashimi aliuawa kwa kupigwa risasi mbele ya nyumba yake mjini Baghdad, na askari wawili wa Italia pamoja na askari mmoja wa Romania waliuawa katika mlipuko uliotokea kusini mwa Iraq
  • Kitivo cha Confucius cha chuo kikuu cha Nairobi
  •  2006/04/27
    Rais Hu Jintao wa China anatazamiwa kufanya ziara ya kiserikali nchini Kenye kuanzia tarehe 27 hadi 29 mwezi Aprili. Katika ziara yake hiyo, rais Hu Jintao atakuwa na mazungumzo na wanafunzi wa kitivo cha Confuxius cha chuo kikuu cha Bairobi.
  • Suala la nyuklia la Iran limekwama vibaya
  •  2006/04/27
    Kwa mujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa Baraza la Usalama iliyopitishwa tarehe 29 Machi, tarehe 28 mwezi huu ni siku ya mwisho kwa Iran kusimamisha shughuli zote za kusafisha uranium. Katika muda wa mwezi mmoja, Iran kwa mara nyingi ilikataa taarifa hiyo, na nchi za magharibi, hasa Marekani, zilishughulika sana kidiplomasia kwa ajili ya kuiadhibu Iran
  • Kwa nini Iran inatishia kwa kueneza teknolojia ya nyuklia?
  •  2006/04/26
    Kiongozi wa kiroho wa Iran Ali Khamenei tarehe 25 mwezi huu alipokutana na rais wa Sudan Omar Al-Bashir alisema, "Iran itaeneza uzoefu, elimu na teknolojia ya wanasayansi wa Iran kwa nchi nyingine".
  • Milipuko ya kigaidi yaishtua tena Misri
  •  2006/04/25
    Milipuko mitatu ilitokea tarehe 24 usiku kwenye sehemu maarufu ya utalii iliyoko katika penisula ya Sinai nchini Misri, Dahab milipuko hiyo iliua watu zaidi ya 30 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 150. Milipuko hiyo imeleta pigo kubwa kwa hali ya usalama na sekta ya utalii nchini Misri, ambayo imekumbusha mfululizo wa milipuko iliyotokea katika eneo la Sharm el-Sheikh.
  • Rais Hu Jintao atoa mapendekezo 6 juu ya kusukuma mbele ushirikiano wa kiujenzi kati ya China na Marekani
  •  2006/04/21
    Rais Hu Jintao wa China ambaye yuko Marekani kwa ziara ya kiserikali tarehe 20 usiku huko Washington alitoa hotuba kwa makundi ya kirafiki ya Marekani, ambapo alitoa mapendekezo 6 juu ya kusukuma mbele ushirikiano wa kiujenzi kati ya China na Marekani.
  • Tofauti kati ya Russia na Marekani kuhusu suala la nyuklia la Iran imekuwa ya wazi zaidi
  •  2006/04/21
    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Bw. Mikhail Kamynin tarehe 20 huko Moscow alitangaza kuwa Marekani haina msingi wowote wa kisheria kuitaka Russia isimamishe ushirikiano na Iran katika kituo cha umeme cha nyuklia kilichopo Bushenr nchini Iran
  • Kutatua suala la nyuklia la Iran kwa njia ya kidiplomasia kunanufaisha pande zote mbili, Marekani na Iran
  •  2006/04/20
    Baada ya mkutano wa nchi tano wanachama za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi ya Ujerumani kufanyika tarehe 18 huko Moscow kuhusu suala la nyuklia la Iran, siku ya pili wajumbe wa "kundi la nchi nane" pia walijadili suala hilo kwa kutumia wakati walipopumzika katika siku za mkutano wao wa kuandaa mkutano wa viongozi wa kundi hilo utakaofanyika Julai huko Saint Petersburg, lakini haukupata matokeo yoyote.
  • Rais Hu Jintao atoa hotuba juu ya uhusiano kati ya China na Marekani katika sekta za uchumi na biashara
  •  2006/04/20
    Rais Hu Jintao wa China tarehe 19 huko Seattle, Marekani aliandaliwa tafrija ya adhuhuri na watu wa sekta za viwanda na biashara na marafiki wa jimbo la Washington na mji wa Seattle
  • Viongozi wapya wa Palestina na Israel wajaribiwa na shambulio la bomu la kujitolea muhanga
  •  2006/04/18
    Watu 9 wameuawa na zaidi ya 40 kujeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga lililolipuka katika mji mkuu wa Israel, Tel Aviv tarehe 17 alasiri.
  • Utatuzi wa suala la nyuklia la Iran uko kwenye njia panda
  •  2006/04/17
    Wajumbe kutoka nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na Ujerumani wanatarajiwa kukutana tarehe 18 huko Moscow, kujadilia njia za kutatua mgogoro wa nyuklia wa Iran. Mkutano huo umechukuliwa kuwa ni jitihada nyingine kubwa ya kidiplomasia kabla ya tarehe 29 mwezi huu ambapo mkurugenzi mkuu wa Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA atawasilisha taarifa mpya ya suala la nyuklia la Iran kwa Baraza la usalama.
  • Mji mkuu wa Chad washambuliwa na vikosi vya uasi
  •  2006/04/14
    Vikosi vya upinzani vilivyoongozwa na chama cha upinzani, United Force for Change, tarehe 13 alfajiri vilishambulia N'djamena, mji mkuu wa Chad, vikijaribu kuuteka mji huo na kuipindua serikali. Baada ya mapambano makali ya muda wa saa kadhaa, rais Idriss Deby alitangaza kupitia redio akisema "Jeshi la serikali limeshinda vikosi vya upinzani", mji mkuu N'djamena na hali ya taifa zima iko chini ya udhibiti wa serikali, na uchaguzi mkuu utafanyika katika tarehe 3 Mei kama ulivyopangwa.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44