Matukio ya utekaji nyara yanayotokea mara kwa mara nchini Afghanistan yanafuatiliwa na jumuiya ya kimataifa 2007/07/23 Msemaji wa kundi la Taleban la Afghanistan Bw. Yousuf Ahmadi tarehe 22 Julai usiku alisema, kutokana na kuwa serikali ya Korea ya Kusini inawasiliana na kundi hilo, kundi hilo limeamua kuahirisha kuwaua mateka 23 wa Korea ya Kusini kwa saa 24. Matukio ya utekaji nyara yanayotokea mara kwa mara nchini Afghanistan yanafuatiliwa na jumuiya ya kimataifa.
|
Mkutano wa viongozi wa ujumbe utakaohudhuria duru la 6 la mazungumzo ya pande 6 wafanyika kihalisi 2007/07/20 Idara husika imedokeza kuwa Mkutano wa viongozi wa ujumbe utakaohudhuria duru la 6 la mazungumzo ya pande 6 unaotazamiwa kumalizika tarehe 19 umerefushwa, wakati huo huo hatua ya Korea ya kaskazini ya kufunga majengo ya nyuklia pia imekaribishwa na pande mbalimbali.
|
Mazungumzo ya pande nne kuhusu suala la Mashariki ya Kati yafanyika mjini Lisbon 2007/07/20 Mazungumzo ya pande nne kuhusu suala la Mashariki ya Kati yalifnyika tarehe 19 mjini Lisbon, mji mkuu wa Ureno, na kujadili pendekezo la Marekani la "kuitisha mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati". Huu ni mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu kufanyika baada ya kundi la Hamas kuudhibiti ukanda wa Gaza na baada ya waziri wa zamani wa Uingereza Bw. Blair kuteuliwa kuwa mjumbe maalumu wa pande nne anayeshughulikia suala la Mashariki ya Kati. Kwa hiyo mkutano huo unafuatiliwa sana.
|
Jeshi la Marekani lamkamata kiongozi mwandamizi wa tawi la Al-Qaida nchini Iraq 2007/07/19 Tarehe 18 jeshi la Marekani lilitangaza kuwa kiongozi mwandamizi wa tawi la Al-Qaida nchini Iraq Khalid al-Mashhadani alikamatwa tarehe 4 na jeshi la Marekani katika mji wa Mosul kaskazini mwa Iraq.
|
Libya yatoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa wauguzi watano na daktari mmoja wa Bulgaria waliohusika na kueneza virusi vya Ukimwi 2007/07/18 Kamati kuu ya sheria ya Libya tarehe 17 usiku huko Tripoli ilitoa taarifa ikitangaza kutoa kifungo cha maisha badala ya hukumu ya kifo kwa wauguzi watano na daktari mmoja wa Bulgaria walioshitakiwa kwa kuhusika na tukio la kueneza virusi vya ukimwi ya Benghazi.
|
Mkutano wa kimataifa kuhusu suala la Darfur waonesha wazi mwelekeo wa utatuzi wa mgogoro wa Darfur 2007/07/17 Mkutano wa kimataifa kuhusu suala la Darfur ulimalizika tarehe 16 huko Tripoli, mji mkuu wa Libya. Mkutano huo umeonesha wazi mwelekeo wa utatuzi wa mgogoro wa Darfur.
|
Mkutano wa kimataifa wa kujadili suala la Darfur wafunguliwa 2007/07/16 Mkutano wa kimataifa wa kujadili suala la Darfur ulifunguliwa tarehe 15 huko Tripoli, Libya, ukilenga kuweka ratiba kwa ajili ya kuanza tena kwa mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudan na makundi yote ya waasi katika jimbo la Darfur, nchini Sudan.
|
Ikulu ya Marekani yatoa ripoti kuhusu hali ya Iraq 2007/07/13 Tarehe 12 serikali ya Marekani imetoa ripoti kuhusu hali ya Iraq ikijaribu kupunguza malalamiko kutoka bungeni na kwa raia wa Marekani, ya kutaka kuondoa jeshi la Marekani kutoka Iraq, lakini baraza la chini la bunge la Marekani halikudanganywa na ripoti hiyo, bali katika siku ya ripoti hiyo ilipotangazwa bunge lilipitisha sheria moja ikitaka serikali ya George Bush iondoe kabisa jeshi la Marekani kutoka Iraq kabla ya tarehe mosi Aprili mwaka kesho.
|
Mahakama kuu ya Libya inaunga mkono hukumu ya awali ya kesi ya kueneza UKIMWI mjini Benghazi 2007/07/12 Tarehe 11 mahakama kuu ya Libya ilitangaza kuunga mkono hukumu ya awali ya kifo kuhusu kesi ya wauguzi watano na daktari mmoja wa Palestina ambaye sasa ni raia wa Bulgaria, kueneza virusi vya UKIMWI miaka minane iliyopita katika mji wa Benghazi nchini Libya.
|
Tukio lililotokea kwenye Msikiti Mwekundu nchini Pakistan lakaribia kumalizika 2007/07/11 Msemaji wa jeshi la Pakistan Bw. Waheed Arshad tarehe 10 alisema, katika siku hiyo jeshi la Pakistan lilichukua hatua na limedhibiti sehemu nyingi za Msikiti Mwekundu, kiongozi wa pili wa msikiti huo Bw. Abdul Rasheed Ghazi aliuawa kwa kupigwa risasi. Wachambuzi wanaona kuwa tukio ambalo lilianza tokea tarehe 3 katika Msikiti Mwekundu, limekaribia kumalizika.
|
Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki litatuma tena wakaguzi wa zana za nyukilia nchini Korea ya Kaskazini 2007/07/10 Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki tarehe 9 ilifanya mkutano na kuidhinisha pendekezo lililotolewa tarehe 3 na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw. Mohamed el-Baradei. Kwa mujibu wa pendekezo hilo shirika hilo litatuma tena kundi la wakaguzi wa nyukilia kwenda nchini Korea ya Kaskazini ili kuhakikisha zana za nyukilia zilizopo Yongbyon zinafungwa.
|
Wimbi la kujifunza Kichina lapamba moto nchini Ujerumani 2007/07/09 Tarehe 7 Julai shughuli za siku ya China zilifanyika kwenye Chuo cha Confucius Nurnberg-Erlangen nchini Ujerumani, ambapo maonesho ya utamaduni wa China kama vile sanaa ya dansi, maandishi ya Kichina na uchoraji picha kwa mtindo wa Kichina
|
Umoja wa Mataifa wafanya mkutano mkubwa kuhusu makubaliano ya dunia kwa makampuni 2007/07/06 Ili makampuni yalete maendeleo endelevu ya uchumi na yawajibike kwa jamii, miaka saba iliyopita Umoja wa Mataifa ulianzisha harakati za "makubaliano ya dunia kwa makampuni" (Global Compact). Tarehe tano Julai Umoja wa Mataifa ulifanya mkutano mkubwa wa kilele kwenye kasri la Umoja wa Mataifa katika makao makuu yake mjini Geneva.
|
Kwa mara nyingine tena Rais George Bush atetea vita dhidi ya Iraq 2007/07/05 Tarehe 4 rais George Bush wa Marekani alisema, ushindi wa vita dhidi ya Iraq "unahitaji subira, ushupavu na mihanga mingi zaidi". Wachambuzi wanaona kuwa maneno hayo aliyosema katika sherehe ya kuadhimisha siku ya uhuru wa Marekani yanaonesha kuwa serikali ya Marekani imekuwa na shinikizo kubwa zaidi la vita vya Iraq kutoka ndani na nje ya nchi.
|
Bara la Afrika litaendelea kusukuma mbele utandawazi 2007/07/04 Mkutano wa 9 wa wakuu wa Umoja wa Afrika uliofunguliwa tarhe mosi Julai, ulifungwa tarehe 3 huko Accra, mji mkuu wa Ghana. Usiku wa siku hiyo presidium ya Mkutano huo ilitoa Taarifa ya Accra ikisema kuwa, Afrika itaendelea kusukuma mbele utandawazi wa Afrika.
|
Tamasha la filamu za Hong Kong lafanyika kwenye kasri la mataifa la Umoja wa Mataifa 2007/07/04 Tarehe mosi Julai ilikuwa ni siku ya kuadhimisha mwaka wa kumi tokea Hong Kong irudishwe nchini China. Tarehe 3 jioni tamasha la filamu za Hong Kong lilizinduliwa katika kasri la mataifa la Umoja wa Mataifa, katika tamasha hilo la siku tatu filamu tatu mpya za Hong Kong zitaoneshwa na pia yatafanywa maonesho ya picha zinazoonesha maisha wa wakazi wa Hong Kong kutoka pande mbalimbali.
|
Mkutano wa marais wa Russia na Marekani utakuwaje? 2007/07/03 Tarehe mosi Julai rais George Bush wa Marekani na rais Vladimir Putin wa Russia walikutana nyumbani kwa rais Bush kwenye jimbo la Maine nchini Marekani, na walifanya mazungumzo kuhusu mpango wa Marekani wa kuweka mfumo wa kukinga makombora Ulaya ya Mashariki na suala la Iran. Vyombo vya habari vinaona kuwa, hii ni mara ya mwisho kwa marais hao kukutana kuboresha uhusiano wa wasiwasi kati ya nchi mbili, kabla ya wao kuondoka madarakani.
|
Hali ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa 2007/07/02 Baraza la uchumi na jamii la Umoja wa Mataifa tarehe 2 Julai huko Geneva limetoa ripoti likijumuisha hali ya kipindi cha katikati cha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa katika miaka saba iliyopita. Ripoti hiyo imesema nchi mbalimbali duniani, hasa nchi na sehemu zilizo nyuma kabisa kimaendeleo zimepata maendeleo mazuri, lakini kama malengo ya maendeleo ya milenia yanatakiwa kutimizwa kikamilifu ifikapo mwaka 2015, nchi mbalimbali zinatakiwa kufanya juhudi kubwa zaidi.
|
Umoja wa Mataifa watoa mwito kuzisaidia nchi zilizo za nyuma kimaendeleo kuongeza uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa 2007/06/29 "Ripoti ya mabadiliko ya hali ya hewa ya mwaka 2007" iliyotolewa tarehe 28 Juni na Umoja wa Mataifa inasema kuwa, nchi zenye nguvu dhaifu kabisa duniani hutoa hewa chache kabisa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani
|
Umoja wa Mataifa wataka uwepo mpango wa kupunguza athari zinazoletwa na mchakato wa ujenzi wa miji 2007/06/28 "Taarifa kuhusu idadi ya watu duniani mwaka 2007" iliyotolewa na shirika la utoaji misaada kuhusu idadi ya watu la Umoja wa Mataifa tarehe 27 mwezi Juni kwenye makao makuu yake mjini New York inasema, idadi ya wakazi wa mijini itafikia bilioni 3.3 ifikapo mwaka 2008
|
Russia na NATO hazijafikia makubaliano kuhusu suala la usalama 2007/06/27 Mkutano wa ngazi ya kibalozi kati ya Russia na NATO ulimalizika tarehe 26 mjini Moscow, pande mbili zilifanya mazungumzo kuhusu masuala ya usalama, likiwemo suala la mfumo wa kukinga makombora barani Ulaya na "Mkataba wa kupunguza nguvu za kijeshi barani Ulaya", lakini mazungumzo hayo hayakupata mafanikio.
|
Mjumbe maalumu wa serikali ya China azungumzia suala la Darfur 2007/06/26 Mkutano wa kimataifa kuhusu suala la Darfur, Sudan ulifanyika tarehe 25 Juni huko Paris, Ufaransa. Watu waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na wajumbe kutoka Marekani, Uingereza, Ufaransa, China na mashirika ya kimataifa yakiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Umoja wa nchi za kiarabu, benki ya dunia na benki ya maendeleo ya Afrika.
|
Mkutano wa Asia ya mashariki wafuatilia umuhimu wa kuongoza na mwelekeo wa maendeleo ya Asia 2007/06/25 Mkutano wa 16 wa Asia ya mashariki wa baraza la uchumi, unaofanyika kwa siku mbili ulifunguliwa tarehe 24 mjini Singapore. Kauli-mbiu ya mkutano huo ni "kuimarisha uwezo wa kuongoza, na kuanzisha karne ya Asia".
|
Marekani yaharakisha hatua za kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea 2007/06/22 Mkuu wa ujumbe wa Marekani wa mazungumzo ya pande sita kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea Bw. Christopher Hill ambaye pia ni msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, tarehe 21 alifanya ziara nchini Korea ya Kaskazini, hii ni ziara ya kwanza kwa ofisa mwandamizi wa Marekani kuzuru Korea ya Kaskazini katika muda wa miaka mitano iliyopita.
|
Shughuli za Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu zaingia katika kipindi kipya 2007/06/20 Mkutano wa 6 wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ulifanyika tarehe 19 huko Geneva. Mkutano huo umepitisha mpango wa uundaji wa utaratibu wa baraza hilo jipya na kuthibitisha kanuni mpya za kufanya ukaguzi na mazungumzo baada ya kila muda maalumu. Hii inaonesha kuwa shughuli za haki za binadamu za Umoja wa Mataifa zimeingia katika kipindi kipya.
|
Palestina na Israel zakabiliwa na fursa mpya ya kurudisha mazungumzo ya amani 2007/06/19 Mwenyekiti wa Mamlaka ya utawala wa Palestina Bwana Mahmoud Abbas tarehe 18 aliongea kwa njia ya simu na rais Bush wa Marekani akidai kurudisha mara moja mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati. Na waziri mkuu wa Israel Bwana Ehud Olmert ambaye yuko ziarani nchini Marekani tarehe 17 alisema, Israel inapenda kufanya mawasiliano na serikali ya Palestina iliyoanzishwa hivi karibuni. Wachambuzi wanaona kuwa, viongozi wa pande hizo mbili wana haraka ya kuanzisha mazungumzo ya amani katika hali ya hivi sasa.
|
Mapambano ya kisiasa kati ya Abbas na kundi la Hamas yapamba moto 2007/06/18 Serikali ya dharura ya Palestina tarehe 17 adhuhuri huko Ramallah, magharibi ya Mto Jordan iliapishwa kwa mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Mahmoud Abbas ili kushika madaraka badala ya serikali ya muungano wa kitaifa ya Palestina ambayo imevunjwa na Bwana Abbas usiku wa tarehe 14 Juni.
|
Bw. Abbas atangaza kuvunja serikali ya muungano wa kitaifa ya Palestina 2007/06/15 Ili kukabiliana na mabadiliko makubwa ya hali ya sehemu ya Gaza, mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas tarehe 14 usiku alisaini amri tatu za mwenyekiti: kuvunja serikali ya muungano wa kitaifa ya Palestina; kutangaza sehemu zote za Palestina zikiwemo sehemu za magharibi ya Mto Jordan na Gaza ziingie katika hali ya hatari; kuunda serikali ya dharura mapema kushughulikia mambo ya serikali ya muungano wa kitaifa ya Palestina
|
Je, Palestina itafarakana? 2007/06/14 Jioni tarehe 13, kundi la Hamas lilifanya mashambulizi dhidi ya vituo vitatu muhimu vya jeshi la ulinzi la taifa linaloongozwa na kundi la Fatah katika mji wa Gaza, mgogoro kati ya makundi hayo mawili umeingia katika kipindi kipya cha mapambano. Hivi sasa kundi la Hamas limedhibiti ukanda wa Gaza. Hali hiyo imedhihirisha wazi zaidi hatari ya kutokea kwa mfarakano nchini Palestina kama wataalamu walivyobashiri.
|
Mapigano yamezuka katika ukanda wa Gaza kati ya makundi mawili makubwa nchini Palestina 2007/06/13 Tarehe 12 alasiri, chama cha Hamas nchini Palestina kilitoa onyo la mwisho la kutaka jeshi la usalama la Palestina linaloongozwa na chama cha Fatah, liondoke kwenye ukanda wa Gaza, kisha kilianzisha mashambulizi dhidi ya shabaha kadhaa yakiwemo makao makuu ya jeshi la usalama la Palestina yaliyoko sehemu ya kaskazini mwa Gaza.
|