Mazungumzo ya Marekani na Korea ya Kaskazini yatoa ratiba ya kuondoa silaha za nyukilia za Korea ya Kaskazini 2007/09/03 Mkutano wa pili wa Marekani na Korea ya Kaskazini ulimalizika alasiri ya tarehe 2 mwezi Septemba huko Geneva, Uswisi. Mwakilishi wa kwanza wa Marekani kwenye mazungumzo ya pande sita ambaye ni msaidizi wa waziri wa mambo ya nje Bw. Christopher Hill alisema, Korea ya Kaskazini imekubali kuripoti mpango wake wa nyukilia na kuondoa uwezo wa zana zake zote za nyukilia kabla ya mwishoni mwa mwaka huu
|
Nchi za Afrika zashirikiana kususia hatua ya Marekani ya kuanzisha makao makuu ya jeshi lake barani Afrika 2007/08/31 Waziri wa ulinzi wa Afrika ya kusini Bwana Mosiuoa Lekota tarehe 29 Agosti alisema kwenye Mkutano uliofanyika huko Cape Town, mji mkuu wa Afrika ya kusini kuwa, Bara la Afrika halifurahii kuwepo kwa jeshi la nchi za nje, hasa kupinga Marekani kujenga makao makuu ya jeshi lake barani Afrika yaliyo kama kituo chake cha kijeshi.
|
Suala la mateka wa Korea ya Kusini latazamiwa kutatuliwa kabisa 2007/08/30 Tarehe 29 kundi la Taliban kwa vikundi vitatu liliwaachia huru mateka 12 wa Korea ya Kusini. Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa tarehe 28kati ya serikali ya Korea ya Kusini na kundi la Taliban, tarehe 30 mateka saba waliobaki wataachiwa huru. Hadi sasa suala la mateka wote wa Korea ya Kusini walioshikiliwa kwa wiki saba linatazamiwa kutatuliwa kabisa.
|
Viongozi wa Palestina na Israel wajadili kwa mara ya kwanza hatma ya Palestina 2007/08/29 Mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert tarehe 28 walikutana huko Jerusalem na kujadili masuala kuhusu hatma ya Palestina ikiwa ni pamoja na masuala ya mipaka, haki ya wakimbizi wa Palestina kurudi nyumbani na udhibiti wa mji wa Jerusalem.
|
Kwa nini waziri mkuu wa Iraq ajibu vikali ukosoaji wa Marekani? 2007/08/28 Hivi karibuni kauli ya kumkosoa waziri mkuu wa Iraq Bw. Nouri al-Maliki imekuwa inasikika sana nchini Marekani, na hata baadhi ya wanachama wa Chama cha Democrat wanataka afukuzwe madarakani
|
Serikali ya Maliki yakumbwa na matatizo ya kutawala na kidiplomasia 2007/08/27 Waziri mkuu wa Iraq Bw. Nouri al-Maliki kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 26 mwezi Agosti, aliwakosoa mbunge wa baraza la juu la bunge la Marekani wa chama cha Democrat cha Marekani na Bw. Carl Levin, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mambo ya kijeshi ya baraza la juu la bunge la Marekani, akiwalaali kwa kuchukulia Iraq kama ni kijiji kimoja cha Marekani na kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo.
|
China na Costa Rica zazidisha urafiki 2007/08/24 Tarehe 23 Agosti kwa saa za Costa Rica, ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Jamhuri ya Costa Rica ilizinduliwa rasmi, ambapo kwa mara ya kwanza bendera ya taifa la Jamhuri ya Watu wa China ikapandishwa juu kwenye mlingoti nchini Costa Rica
|
Kwa nini Iran imeonesha ishara nzuri katika suala la nyuklia? 2007/08/22 Mazungumzo ya duru la tatu kati ya Iran na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki yalimalizika tarehe 21 jioni huko Tehran. Baada ya mazungumzo pande zote mbili zilisema mazungumzo hayo yamepata maendeleo, na zimefikia makubaliano kuhusu masuala yaliyotakiwa kutatuliwa katika muda maalum kwenye mpango wa nyuklia wa Iran.
|
Jeshi la anga la Russia laonesha tena nguvu zake 2007/08/21 Tarehe 19 ndege za kivita za Russia zilipaa angani kutoka kwenye manowari ya "Jemadari Kuzniezov". Hii inamaanisha kuwa jukumu la ndege za kivita zinazoruka na kurudi kwenye manowari yenye ndege limerudi tena. Kabla ya hapo, ndege 14 zikiwemo ndege za makombora, ndege za kulinda safari ya manowari na ndege za kuongeza mafuta angani, zimeanza tena kufanya doria baada ya kuacha kufanya hivyo kwa miaka 15.
|
Nchi tatu za Amerika ya kaskazini zatumai kuharakisha mchango wa utandawazi wa uchumi wa kikanda 2007/08/20 Mkutano wa 3 wa siku mbili wa "wenzi wa ushirikiano wa nchi za Amerika ya kaskazini kuhusu usalama na ustawi" unatazamiwa kufunguliwa tarehe 20 Agosti huko Chateau Montebello ya Quebec ya kaskazini nchini Canada
|
Ukurasa mpya muhimu katika mchakato wa maendeleo ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai 2007/08/17 Mkutano wa 7 wa Baraza la wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ulifanyika tarehe 16 huko Bishkek, mji mkuu wa Kyrgyzstan. Rais Hu Jintao wa China na viongozi wengine wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo walihudhuria Mkutano huo na kusaini "Mkataba wa ujirani mwema, urafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai' na nyaraka nyingine muhimu.
|
Siku nyingine ya umwagaji damu yatokea nchini Iraq 2007/08/16 Tarehe 14 kwenye maeneo kadhaa wanakoishi wafuasi wa dhehebu la Yazidi kaskazini mwa mkoa wa Neineva ilitokea milipuko minne ya mabomu yaliyofichwa ndani ya gari ilitokea kwa mfululizo na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 250 na wengine 300 kujeruhiwa. Haya ni mauaji makubwa kabisa tangu ya vita vya Iraq kutokea mwaka 2003.
|
Lebanon na Israel bado zinasumbuliwa na masuala yaliyobaki ya mgogoro kati yao 2007/08/15 Tarehe 14 Agosti ilikuwa ni siku ya kutimia kwa mwaka mmoja tangu mgogoro kati ya Lebanon na Israel umalizike, lakini pande hizo mbili bado zinasumbuliwa na masuala yaliyobaki ya mgogoro huo
|
Rais Hu Jintao aanza ziara yake ya Asia ya Kati 2007/08/14 Rais Hu Jintao wa China tarehe 14 Agosti ameanza ziara katika sehemu ya Asia ya Kati. Katika ziara hiyo ya siku 5, rais Hu Jintao atafanya ziara rasmi nchini Kyrgyzstan, ambapo atahudhuria mkutano wa wakuu wa jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai, pia atatizama luteka ya jumuiya hiyo inayolenga kupambana na ugaidi na kufanya ziara rasmi nchini Kazakhstan.
|
Chama cha leba cha Uingereza chapata uungaji mkono zaidi siku hadi siku, huenda Brown ataitisha uchaguzi mkuu kabla ya wakati uliowekwa 2007/08/13 Gazeti la The Sunday Times la Uingereza tarehe 12 lilichapisha matokeo ya uchunguzi wa maoni ya raia uliofanyika hivi karibuni yakionesha kuwa, uungaji mkono wa raia kwa chama cha Leba kinachoongozwa na waziri mkuu Gordon Brown umefikia asilimia 42 na umezidi kwa asilimia 10 kuliko ule wa chama kikubwa cha upinzani cha wahafidhina, kiwango hiki kimefikia kile cha kabla ya vita vya Iraq.
|
Kazi ya kutetea haki na maslahi ya watu wa jamii za kiasili duniani ni ngumu 2007/08/10 Tarehe 9 Agosti ni siku ya kimataifa ya watu wa jamii za kiasili. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon alitoa hotuba ya maandishi akitaka jumuyia ya kimataifa ichukue hatua ili kuhakikisha haki na maslahi yao yanalindwa. Bw. Ban Ki-moon alisema, hivi leo watu wa jamii za kiasili bado wanakabiliwa na hali ya kubaguliwa na kupuuzwa, ardhi yao na njia yao ya kujipatia maisha inazuiwa, na utamaduni wao utaharibiwa na pengine utatoweka kabisa. Bw. Ban Ki-moon anaona kuwa jumuyia ya kimataifa inatakiwa kuchukua hatua za kushughulika na masuala hayo.
|
Jumuiya ya kimataifa yafanya juhudi nyingine kwa ajili ya utatuzi wa suala la usalama wa Iraq 2007/08/09 Kamati ya ushirikiano na uratibu wa usalama wa nchi jirani za Iraq tarehe 8 iliitisha Mkutano huko Damascus, mji mkuu wa Syria, kujadili hali ya usalama wa Iraq na usalama wa sehemu za mipaka kati ya Iraq na nchi jirani zake.
|
Tukio la ndege zisizojulikana laleta utatanishi zaidi kwenye uhusiano kati ya Russia na Georgia 2007/08/08 Wizara ya mambo ya ndani ya Georgia tarehe 7 ilitoa taarifa ikilaani kitendo cha ndege za kivita za Russia kuvamia anga ya nchi hiyo na kupiga kombora kwenye kijiji cha Tsitelubani nchini humo. Wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo pia ilitoa taarifa ikilaani vikali tukio hilo na kuitaka Russia itoe maelezo mapema iwezekanavyo.
|
Mazungumzo kati ya Marekani na Iran hayawezi kuboresha hali ya Iraq katika muda mfupi 2007/08/07 Baada ya maduru mawili ya mazungumzo ya ngazi ya kibalozi yaliyofanyika kati ya Marekani na Iran mwezi Mei na Julai, tarehe 6 Agosti wajumbe wa nchi mbili walikutana mjini Baghdad na kufanya mazungumzo ya pande tatu, ikiwa ni pamoja na wajumbe wa Iraq.
|
Umoja wa Asia ya kusini mashariki umekuwa nguvu ya kikanda isiyopuuzika kwenye jukwaa la kimataifa 2007/08/06 Tarehe 8 Agosti mwaka huu itakuwa siku ya maadhimisho ya miaka 40 tangu kuundwa kwa Umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki. Mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa mambo ya Asia na Pasifiki katika idara ya utafiti wa masuala ya kimataifa Bwana Shen Shishun alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, Umoja wa Asia ya kusini mashariki umekuwa nguvu ya kikanda isiyopuuzika kwenye jukwaa la kimataifa.
|
Bi. Rice afanya ziara kwenye sehemu ya Palestina na Israel kwa ajili ya Mkutano wa kimataifa kuhusu suala la mashariki ya kati 2007/08/03 Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice tarehe 2 Agosti alimaliza ziara yake fupi kwenye sehemu ya Palestina na Israel. Vyombo vya habari vimesema katika zaidi ya miaka miwili iliyopita tangu Rice ashike wadhifa wa waziri wa mambo ya nje, amefanya ziara mara kwa mara kwenye sehemu ya Palestina na Israel.
|
Kenya yavutiwa na bidhaa kutoka China 2007/08/02 Katika maonesho ya biashara ya kimataifa yaliyofanyika mwezi Oktoba mwaka jana huko Nairobi, nchini Kenya, watu wengi wakiwemo wafanyabiashara wa huko walijazana kwenye banda la bidhaa la China, na wengi wao walipotoka walibeba mifuko mikubwa na midogo iliyojaa bidhaa kutoka China.
|
Kwa nini katika siku za karibuni Marekani imekuwa inahubiri sana amani ya Mashariki ya Kati? 2007/08/01 Tarehe 31 Julai waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice huko Sharm El-sheikh nchini Misri alikutana na mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Jordan na nchi wanachama wa Kamati ya Ushirikiano ya Nchi za Ghuba, na kwenye taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo aliahidi kujishughulisha na amani na utulivu wa Mashariki ya Kati.
|
Cote d'ivoire yakaribisha mwanga wa amani 2007/07/31 Baada ya mazungumzo magumu na juhudi zisizolegea kwa pande mbalimbali zinazohusika katika miaka mitano iliyopita, wananchi wa Cote d'ivoire waliochoshwa na balaa la vita, sasa wanakaribisha mwanga wa amani waliokuwa wakiusubiri kwa muda mrefu. Sherehe ya kuanzisha mchakato wa kunyang'anya silaha ambayo ni ishara ya muungano mpya wa sehemu za kusini na kaskazini ilifanyika tarehe 30 Julai huko Bouake, kaskazini ya nchi hiyo.
|
Umuhimu wa kupata ubingwa kwa timu ya Iraq ni mkubwa zaidi kuliko mchezo wa soka 2007/07/30 Katika fainali ya soka ya kombe la Asia la mwaka 2007 iliyofanyika tarehe 29 mwezi Julai mjini Jakarta Indonesia, timu ya Iraq iliishinda timu ya Saudi Arabia kwa bao moja kwa bila, na kupata ubingwa wa kombe la Asia katika historia, kwa kuishinda timu ya Saudi Arabia, ambayo ilipata ubingwa kwa mara tatu.
|
Russia yawa na msimamo imara siku hadi siku kuhusu suala la "Mkataba wa nguvu za majeshi ya kawaida ya Ulaya" 2007/07/27 Rais Vladimir Putin wa Russia tarehe 25 alisema, mwaka ule wakati "Mkataba wa nguvu za majeshi ya kawaida ya Ulaya" ulipokuwa unasainiwa kulikuwa na makundi makubwa mawili ya kijeshi yaani Jumuiya ya NATO na Jumuiya ya Mkataba wa Warsaw
|
Watu wa Korea ya Kusini waliotekwa nyara na Taliban wako hatarini 2007/07/26 Polisi wa mkoa wa Ghazni tarehe 25 walithibitisha kuwa mmoja kati ya watu 23 wa Korea ya Kusini waliotekwa nyara na kundi la Taliban wiki iliyopita aliuawa kando ya barabara baada ya kupigwa risasi, na wanadiplomasia wa nchi za magharibi walidokeza kuwa mateka wanane wameachiwa huru. Ingawa kuna habari nyingi tofauti kuhusu mateka hao wa Korea ya Kusini, lakini hali ilivyo ni kuwa bado wako hatarini.
|
Marekani na Iran zafanya mazungumzo ya ngazi ya kibalozi kwa mara ya pili 2007/07/25 Marekani na Iran tarehe 24 zilifanya mazungumzo ya ngazi ya kibalozi kwa mara ya pili kuhusu usalama wa Iraq mjini Baghdad. Mazungumzo ya mara ya kwanza yalifanyika tarehe 28 mwezi Mei.
|
Sudan yatakiwa kutatua suala la Darfur kwa lengo la kujiendeleza 2007/07/25 Rais Omar Al Bashir wa Sudan kuanzia tarehe 21 hadi 23 Julai alifanya ukaguzi kwenye sehemu ya Darfur, magharibi mwa Sudan, na kufanya mazungumzo na mawaziri wa serikali na maofisa wenyeji kuhusu namna ya kutatua suala la Darfur. Ukaguzi na uchunguzi umethibitisha kwa mara nyingine tena kuwa, suala la Darfur haliwezi kutatuliwa bila kuzingatia maendeleo ya huko, na usalama na amani ni masharti ya lazima ya kuleta maendeleo kwenye sehemu hiyo.
|
Mazungumzo ya pande nne kuhusu suala la Mashariki ya Kati yafanyika mjini Lisbon 2007/07/24 Mazungumzo ya pande nne kuhusu suala la Mashariki ya Kati yalifnyika tarehe 19 mjini Lisbon, mji mkuu wa Ureno, na kujadili pendekezo la Marekani la "kuitisha mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati". Huu ni mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu kufanyika baada ya kundi la Hamas kuudhibiti ukanda wa Gaza na baada ya waziri wa zamani wa Uingereza Bw. Blair kuteuliwa kuwa mjumbe maalumu wa pande nne anayeshughulikia suala la Mashariki ya Kati. Kwa hiyo mkutano huo unafuatiliwa sana.
|