Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Hatua za pamoja zatakiwa kuchukuliwa ili kukabiliana na suala la kuongezeka kwa joto duniani
  •  2007/11/28
    Shirika la maendeleo na mipango la Umoja wa Mataifa tarehe 27 lilitoa mwito wa kuzitaka nchi mbalimbali duniani zichukue hatua za dharura, ili kukabiliana kwa pamoja na suala la kuongezeka kwa joto duniani, kwani suala hilo limezidi kuleta shinikizo kubwa kwa binadamu siku hadi siku
  • Bw. Pervez Musharraf atakuwa rais wa Pakistan
  •  2007/11/27
    Mwendeshaji mkuu wa mahakama ya Pakistan Bw Malik Muhammad Qayyum tarehe 26 alisema, rais wa sasa Pervez Musharraf tarehe 29 atajiuzulu wadhifa wake wa jenerali na kuwa rais wa kiraia katika kipindi kipya cha miaka mitano
  • Mkutano wa Jumuiya ya Madola wafungwa nchini Uganda
  •  2007/11/26
    Mkutano wa 36 wa wakuu wa Jumuiya ya Madola ulifungwa tarehe 25 huko Kampala nchini Uganda. Taarifa ya Kampala iliyotolewa kwenye mkutano huo wa siku tatu imesistiza kulinda amani ya dunia, kusukuma mbele maendeleo ya demokrasia na uchumi, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kufuatilia maendeleo ya vijana na kuhimiza maendeleo ya shughuli mbalimbali za elimu, afya na nyinginezo
  • Mikutano yenye mafanikio makubwa kati ya viongozi wa nchi za Asia ya mashariki
  •  2007/11/23
    Waziri mkuu wa Singapore Bw. Lee Hsien Loong aliitisha Mkutano na waandishi wa habari akifanya majumuisho ya mikutano hiyo. Alisema mikutano mbalimbali kati ya viongozi wa nchi za Asia ya mashariki imepata mafanikio makubwa. Bw. Lee Hsien Loong alisema, kwenye mikutano hiyo viongozi wa nchi mbalimbali za Asia ya mashariki walisaini taarifa na mikataba kadha wa kadha, na mikutano hiyo imepata matunda kemkem.
  • Ni vigumu kwa makao makuu ya uongozi ya jeshi la Marekani kudumu barani Afrika
  •  2007/11/22
    Hivi karibuni serikali ya Nigeria ilikataa makao makuu ya uongozi ya jeshi la Marekani yaliyoanzishwa majuzi kuweko nchini humo, hatua ambayo inafanya shughuli za kutafuta sehemu mpya ya kuweka makao makuu hayo kukumbwa na matatizo tena.
  • Ushirikiano wa nishati kati ya Uturuki na Iran ni mahitaji ya kila upande
  •  2007/11/21
    Uturuki na Iran tarehe 20 zilisaini mkataba wa ushirikiano wa kuzalisha umeme huko Ankara. Huu ni mkataba wa pili wa ushirikiano wa kinishati tokea mwezi Julai. Wachambuzi wanaona kuwa wakati Marekani inapotaka kuiwekea Iran vikwazo vipya, Uturuki na Iran bado zinaendelea na ushirikiano wa kinishati, hakika hii ni nia ya kila upande.
  • Kabla ya kufanyika kwa mkutano wa amani wa Mashariki ya Kati pande husika zajitahidi kuleta mazingira bora ili kuufanikisha
  •  2007/11/20
    Mkutano wa kimataifa wenye lengo la kusukuma mchakato wa mazungumzo kati ya Palestina na Israel na amani ya Mashariki ya Kati, utafanyika mwishoni mwa mwezi huu huko Annapolis, Marekani. Kabla ya mkutano huo kufanyika pande husika zinajitahidi kuleta mazingira mazuri ili kuufanikisha mkutano huo.
  • Mawaziri wakuu wa China na Singapore wafanya mazungumzo kuhusu kujenga mji wa mazingira ya viumbe
  •  2007/11/19
    Waziri mkuu wa Singapore Bw. Lee Hsien Loong alasiri ya tarehe 18 mwezi Novemba alikuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa China Bw. Wen jiabao, ambaye hivi sasa yuko ziarani nchini Singapore. Pande hizo mbili zilifikia makubaliano kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili, na kusaini makubaliano kati ya serikali za nchi hizo mbili kuhusu kuujenga mji wa Tianjin wa China uwe mji wenye mapatano na mazingira ya viumbe.
  • Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kimataifa la nishati ya Atomiki asema Iran imefanya ushirikiano wa kutosha na Shirika hilo, lakini haikufanya juhudi ipasavyo
  •  2007/11/16
    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Bw. Mohamed El Baradei tarehe 15 aliwasilisha ripoti mpya kuhusu suala la nyuklia la Iran kwa nchi 35 wajumbe wa baraza la shirika hilo, kwenye makao makuu ya shirika hilo mjini Vienna.
  • Nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki zataka kuunda umoja wao wa usalama
  •  2007/11/15
    Mkutano wa pili wa mawaziri wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki ulianza tarehe 14 huko Singapore. Kwenye mkutano huo mawaziri wa ulinzi wa nchi kumi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki walisisitiza kuwa, nchi zote za umoja huo zitajitahidi kuimarisha ushirikiano wa amani na usalama wa sehemu hiyo
  • Kauli ya Bibi Benazir Bhutto yasababisha wasiwasi wa kisiasa nchini Pakistan
  •  2007/11/14
    Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Umma cha Pakistan Bibi Benazir Bhutto, tarehe 13 huko Lahore alisema huenda Chama cha Umma anachokiongoza hakitashiriki kwenye uchaguzi wa bunge. Kauli hiyo imesababisha hali ya wasiwasi wa kisiasa nchini Pakistan.
  • Misri na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zajitahidi kufanikisha mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati
  •  2007/11/13
    Waziri wa mambo ya nje wa Misri tarehe 12 alisema Misri itajitahidi kufanikisha mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati. Siku hiyo katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Bw. Amr Moussa pia alisisitiza kuwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ina matumaini kuwa mkutano huo kuhusu amani ya Mashariki ya Kati, unaweza kufanyika na kupata matokeo yanayotarajiwa katika muda uliowekwa
  • Hali ya usalama nchini Iraq bado mbaya
  •  2007/11/12
    Tarehe 11 waziri mkuu wa Iraq alitoa tathmini kwa furaha kuhusu hali ya usalama nchini Iraq akisema, milipuko ya mabomu na ya kujiua nchini Iraq imepungua sana, na migogoro kati ya madhehebu ya kidini imemalizika. Kadhalika jeshi la Marekani nchini Iraq pia lina mtazamo huo huo.
  • Hali mpya imetokea katika uhusiano kati ya nchi tatu za Marekani, Iran na Iraq
  •  2007/11/09
    Hivi karibuni hali mpya imetokea katika uhusiano kati ya nchi tatu za Marekani, Iran na Iraq. Tarehe 6 msemaji wa jeshi la Marekani Bw. Greg Smith alithibitisha kuwa watu tisa wa Iran waliokuwa wanashikiliwa na jeshi la Marekani nchini Iraq, wataachiwa huru katika siku za karibuni. Kati ya watu hao, wawili walikamatwa na jeshi la Marekani katika sehemu ya kaskazini ya Iraq.
  • Maendeleo ya hali nchini Pakistan yanafuatiliwa na watu duniani
  •  2007/11/08
    Baraza la chini la bunge la Pakistan kwenye mkutano uliofanyika huko Islamabad tarehe 7 mwezi Novemba, lilipitisha uamuzi wa kuthibitisha uamuzi wa rais Pervez Musharraf wa Pakistan ambaye pia ni mkuu wa jeshi la nchi hiyo, kutangaza hali ya hatari kote nchini na kutekeleza katiba ya muda.
  • Kuimarisha ujirani mwema na urafiki na kuhimiza ushirikiano halisi
  •  2007/11/07
    Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao amerudi Beijing tarehe 7 asubuhi baada ya kumaliza ziara yake katika nchi 4 za Ulaya na Asia. Wakati wa kumaliza ziara yake katika nchi hizo, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Yang Jiechi ambaye alifuatana na waziri mkuu katika ziara yake hiyo alipohojiwa na waandishi wa habari alisema, ziara ya waziri mkuu Bw. Wen Jiabao imeimarisha uhusiano wa ujirani mwema na urafiki kati ya China na Uzbekistan, Turkmenistan, Belarus na Russia.
  • "Mwaka wa China" uliofanyika nchini Russia wamalizika kwa mafanikio
  •  2007/11/07
    "Mwaka wa China" uliofanyika nchini Russia kwa mwaka mzima ulimalizika tarehe 6, hadi kufikia hapo miaka miwili ya taifa ya China na Russia imemalizika. Siku hiyo waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao na waziri mkuu wa Russia Bw. Viktor Zubkov walihudhuria sherehe ya kufungwa kwa mwaka huo wa China kwenye Ikulu ya Kremlin mjini Moscow.
  • Maendeleo ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika yafikia kiwango kipya
  •  2007/11/06
    Mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ulifanyika mjini Beijing tarehe 4 hadi tarehe 5 mwezi Novemba mwaka 2006. Mkutano huo uliamua uhusiano wa kimkakati wa kiwenzi kati ya China na Afrika, hasa ushirikiano wa kiuchumi wa kunufaishana kati ya pande hizo mbili.
  • Utekelezaji makubaliano ya Mkutano wa wakuu wa Beijing na kuhimizaa uhusiano wa aina mpya kati ya China na Afrika uendelezwe siku hadi siku
  •  2007/11/05
    Tafrija ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu Mkutano wa wakuu wa Beijing wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ufanyike, ilifanyika tarehe 4 usiku hapa Beijing, ambapo mjumbe wa taifa wa China Bwana Tang Jiaxuan, na mabalozi wa nchi za Afrika nchini China wapatao 200 walihudhuria tafrija hiyo.
  • Ushirikiano kati ya China na Afrika waongeza uchangamfu wa shughuli za mawasiliano ya habari barani Afrika
  •  2007/11/05
    Mmkutano wa wakuu wa "kuunganisha Afrika" ulioandaliwa na mashirikisho kadhaa likiwemo Shirikisho la Mawasiliano ya Habari Duniani (ITU) lilifungwa hivi karibuni huko Kigali, Rwanda. Lengo la mkutano huo ni kustawisha shughuli za mawasiliano ya habari barani Afrika, kuondoa pengo katika mawasiliano ya kitarakimu, na kuboresha mazingira ya uwekezaji.
  • Mkutano wa nishati wa Umoja wa Ulaya, Afrika na Mashariki ya Kati wasisitiza ushirikiano na mazungumzo
  •  2007/11/02
    Mkutano wa nishati wa Umoja wa Ulaya, Afrika na Mashariki ya Kati ulifunguliwa tarehe mosi huko Sharm el-Sheik, nchini Misri. Mkutano huo ulitoa taarifa ikisisitiza kuwa, pande mbalimbali zinatakiwa kuimarisha ushirikiano na mazungumzo katika mambo ya nishati
  • Mahakama ya Hispania yatoa hukumu kuhusu tukio la "Machi 11"
  •  2007/11/01
    Mahakama ya taifa ya Hispania tarehe 31 Oktoba ilitoa hukumu kuhusu milipuko iliyotokea "Machi 11" mwaka 2004 ambayo ililipua magarimoshi manne mfululizo, wahalifu wakuu watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka zaidi ya elfu 30 na miaka zaidi ya elfu 40.
  • China kuwa nchi kubwa kibiashara inayotoa fursa nyingi zaidi kwa dunia nzima
  •  2007/10/31
    Baada ya kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango karibu miaka 30 iliyopita, China imeingia kwenye safu ya nchi tatu zenye nguvu kubwa kabisa katika mambo ya biashara duniani. Kwenye kongamano maalum kuhusu "Umuhimu wa China katika biashara kote duniani"
  • Mkutano wa Doha kuhusu matumizi ya gesi wahimiza maendeleo ya nishati safi
  •  2007/10/30
    Mkutano wa sita kuhusu matumizi ya gesi ulifunguliwa tarehe 29 mjini Doha, maofisa na wataalamu karibu elfu moja kutoka sekta mbalimbali walihudhuria mkutano huo. Kauli mbiu ya mkutano huo ni "Gesi--nishati ya karne ya 21", mkutano huo unasisitiza umuhimu wa matumizi ya nishati safi katika siku za baadaye
  • Je Marekani itashambulia Iran?
  •  2007/10/29
    Hivi karibuni, msimamo wa serikali ya George Bush dhidi ya Iran umekuwa mkali zaidi, na maneno ya kuitishia kwa kutaka kuishambulia Iran yanasikika mara kwa mara. Watu wengi wanajiuliza, je kweli Marekani itaishambulia Iran?
  • Nchi mbalimbali zatakiwa kujenga na kuimarisha mfumo wa ushirikiano wa pande nyingi chini ya kiini cha Umoja wa Mataifa
  •  2007/10/25
    Tarehe 24 Oktoba ni siku ya maadhimisho ya miaka 62 tangu Katiba ya Umoja wa Mataifa ianze kufanya kazi na tangu Umoja wa Mataifa uanzishwe. Siku hiyo shughuli za maadhimisho zilifanyika huko New York, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na katika miji mikuu ya nchi nyingi duniani.
  • Kuzifanya nchi zote ziwe na maendeleo ni jukumu la pamoja la jumuiya ya kimataifa
  •  2007/10/24
    Mkutano wa 62 wa mawaziri kuhusu ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya maendeleo ya uchumi ulifanyika tarehe 23 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, wajumbe kutoka nchi zaidi ya 100 na mashirika ya kimataifa walishiriki kwenye mkutano huo wa siku mbili.
  • Uswisi nchi inayodumisha hali ya kutopendelea upande wowote, inaweza kuwa ya mrengo wa kulia?
  •  2007/10/23
    Idara ya takwimu ya Shirikisho la Uswisi tarehe 22 ilitangaza matokeo ya mwisho kuhusu uchaguzi wa bunge uliofanyika tarehe 21, kwamba Chama cha umma cha Uswisi kilipata kura nyingi zaidi kuliko vyama vingine. Kwa kuwa chama hicho kina msimamo mkali wa kutetea kuzuia vikali wahamiaji kutoka nchi za nje kuingia nchini Uswisi, na kuwafukuza vijana wahalifu pamoja na wazazi wao, ushindi wa chama hicho unawafanya watu wafuatilie kama mwelekeo wa kisiasa wa Uswisi katika siku zijazo, utakuwa wa mrengo wa kulia au la.
  • Mlipuko watokea wakati waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto akirudi nchini
  •  2007/10/19
    Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Bibi Benazir Bhutto ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha upinzani, Chama cha Umma, tarehe 18 alirudi mjini Karachi Pakistan baada ya kuishi Uingereza kwa miaka minane. Baada ya yeye kufika tu ilitokea milipuko miwili dhidi ya waziri huyo wa zamani. Habari kutoka polisi ya Pakistan zinasema, milipuko hiyo ilisababisha vifo vya watu 124 na watu karibu 400 kujeruhiwa, na idadi hiyo pengine sio ya mwisho.
  • Dunia yatangaza vita dhidi ya umaskini
  •  2007/10/18
    Tarehe 17 mwezi Oktoba ni siku ya kutokomeza umaskini duniani. Makao makuu ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa lililoko mjini New York, Marekani yalifanya shughuli za maadhimisho alasiri ya siku hiyo.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44