Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Mkutano wa 6 wa wakuu wa Asia na Umoja wa Ulaya wafunguliwa
  •  2006/09/11
    Mkutano wa 6 wa wakuu wa Asia na Umoja wa Ulaya ulifunguliwa tarehe 10 alasiri huko Helsinki, mji mkuu wa Finland. Kwenye mkutano wa siku mbili, viongozi wa nchi 39 wanachama wa Baraza la Asia na Umoja wa Ulaya ikiwemo China watajadili masuala mbalimbali yanayohusu kauli mbiu ya mkutano huo "Kushirikiana ili kukabiliana na changamoto kote duniani". 
  • Ziara muhimu itakayosukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya China na nchi za Umoja wa Ulaya
  •  2006/09/08
    Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao tarehe 9 Septemba atakwenda Ulaya kuhudhuria Mkutano wa 9 wa wakuu wa China na Umoja wa Ulaya na mkutano wa wakuu wa Asia na Umoja wa Ulaya, pia atafanya ziara katika nchi 3 za Ulaya ikiwemo Fenland.
  • Ushirikiano wa kimkakati na kiwenzi kati ya China na Umoja wa Ulaya waendelea kwa hatua madhubuti
  •  2006/09/07
    Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao tarehe 9 atafanya ziara nchini Finland na kuhudhuria mkutano wa 9 wa wakuu wa China na Umoja wa Ulaya.
  • Bw Annan ahimiza suala la nyukilia la Iran litatuliwe kwa njia ya mazungumzo
  •  2006/09/04
    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Kofi Annan tarehe 3 mwezi huu alimaliza ziara ya siku 2 nchini Iran. Bw. Annan ameitembelea Iran baada ya kupita tarehe iliyowekwa katika azimio la baraza la usalama la kuitaka Iran kusimamisha shughuli za kusafisha uranium.
  • Baraza la Usalama laamua kutuma jeshi la Umoja wa Mataifa kwenye sehemu ya Darfur
  •  2006/09/01
    Tarehe 31 Agosti Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio No. 1076 la kutuma jeshi a Umoja wa Mataifa kwenye sehemu ya Darfur mwishoni mwa mwezi Septemba, wakati ambapo jeshi la Umoja wa Afrika litakamilisha kipindi chake
  • Bw. Kofi Annan hakupata mafanikio makubwa katika ziara yake nchini Lebanon na Israel
  •  2006/08/31
    Hivi karibuni katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan alifanya ziara nchini Lebanon na Israel akitaka kuhimiza Hezbollah na Israel kuafikiana kwenye usimamishaji mapigano wa kudumu. Lakini kutokana na matatizo yenye utata mwingi kati ya Lebanon na Israel, hivyo Bw. Annan alikutana na shida kubwa katika shughuli za usuluhishi na hakupata mafanikio makubwa katika ziara yake kwenye nchi hizo mbili.
  • China na Marekani zakubali kuhimiza mazungumzo ya biashara ya pande nyingi duniani
  •  2006/08/30
    Hivi karibuni China na Marekani ziliafikiana kuhusu namna ya kuhimiza mazungumzo ya biashara ya pande nyingi duniani, zikieleza kuwa zitahimiza urejeshaji wa raundi ya Doha ya mazungumzo ya Shirika la Biashara Duniani, WTO, ingawa bado kuna tofauti kubwa kati ya pande hizo mbili.
  • Israel yachunguza makosa ya maofisa wa ngazi ya juu wa serikali na jeshi kuhusu mapambano kati ya Israel na Lebanon
  •  2006/08/29
    Waziri mkuu wa Israel Bw. Ehud Olmert tarehe 28 usiku alitangaza kuwa, serikali imeamua kuunda tume mbili kufanya uchunguzi kuona kama hatua walizochukua maofisa wa ngazi ya juu wa serikali na jeshi kuhusu mapambano kati ya Lebanon na Israel ni sahihi au la.
  • Mgogoro kati ya Iran na Marekani wapamba moto siku hadi siku
  •  2006/08/28
    Azimio No. 1696 lililopitishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linaitaka Iran iache shughuli za kusafisha uranium kabla ya tarehe 31 mwezi Agosti. Kutokana na kukaribia kwa siku hiyo, mvutano kati ya Marekani na Iran unapamba moto siku hadi siku.
  • Mazungumzo ni njia pekee ya kutatua suala la nyuklia la Iran
  •  2006/08/25
    Baada ya Iran kujibu mapendekezo ya nchi sita za Marekani, Russia, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani tarehe 22 Agosti, Russia na China kwa nyakati tofauti zimesema zinatumai suala la nyuklia la Iran litatatuliwe kwa njia ya mazungumzo kwa msingi wa mfumo wa kimataifa wa kutoeneza silaha za nyuklia, na hili pia ni tumaini la nchi nyingi na maoni yanayotawala katika jamii ya kimataifa.
  • Mazungumzo ni njia pekee ya kutatua suala la nyuklia la Iran
  •  2006/08/25
    Baada ya Iran kujibu mapendekezo ya nchi sita za Marekani, Russia, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani tarehe 22 Agosti, Russia na China kwa nyakati tofauti zimesema zinatumai suala la nyuklia la Iran litatatuliwe kwa njia ya mazungumzo kwa msingi wa mfumo wa kimataifa wa kutoeneza silaha za nyuklia, na hili pia ni tumaini la nchi nyingi na maoni yanayotawala katika jamii ya kimataifa.
  • Shirika la chakula na kilimo cha Umoja wa Mataifa lazingatia udhibiti wa matumizi ya maji kwa ajili ya kilimo
  •  2006/08/24
    Hivi sasa matumizi ya maji kwa ajili ya ya kilimo yanachukua sehemu kubwa zaidi katika matumizi ya maji ya baridi duniani.
  • Suala la nyuklia wa Iran litaelekea wapi?
  •  2006/08/23
    Tarehe 22 Agosti Iran ilitoa rasmi waraka wa majibu kwa pendekezo la kutatua suala la nyuklia la Iran lililotolewa na nchi 6 za Marekani, Russia, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.
  • Kauli mpya ya Ayatollah Khamenei ina maana gani?
  •  2006/08/22
    Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei tarehe 21 alisema, Iran imetunga mpango wa kinyuklia na itaendelea kuutekeleza kwa uthabiti. Alisema nchi kadhaa ikiwemo Marekani zina hofu na Iran kuendeleza teknolojia ya nyuklia, kwa hiyo zinaiwekea Iran shinikizo kubwa ingawa zina ufahamu kwamba Iran haina nia ya kutengeneza silaha za nyuklia.
  • Ni kwa nini Iran imeamua kufanya luteka kubwa kwa wakati huu?
  •  2006/08/21
    Tarehe 19 Agosti Iran ilianza kufanya luteka kubwa itakayodumu kwa wiki tano, ambayo inawashirikisha wanajeshi wa majeshi ya nchi kavu, majini na anga. Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha taifa cha Iran, katika luteka iliyofanyika tarehe 20 jeshi la Iran lilirusha kwa majaribio kombora la masafa kati ya kilomita 80 na 250 dhidi ya shabaha ya ardhini, na majaribio mengine ya kurusha makombora dhidi ya manowari pia yatafanywa. Lakini ni kwa nini Iran inafanya luteka hiyo kubwa kwa wakati huu?
  • Watu wa hali mbalimbali wa Japan wana matarajio na pia wana wasiwasi kuhusu serikali ya awamu ijayo kuboresha uhusiano na China na Korea ya kusini
  •  2006/08/18
    Baada ya kwenda kwenye Hekalu la Yasukuni kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita tarehe 15, waziri mkuu wa Japan Koizumi Junichiro alikaa nyumbani akipumzika bila kutoka nje.
  • Wagonjwa wa Ukimwi wapewe haki ya kutumia dawa
  •  2006/08/17
    Miongoni mwa wagonjwa wa Ukimwi karibu milioni 40 duniani, ni wagonjwa karibu 10% tu ambao wanapata fursa ya kutumia dawa, na wengi wa wagonjwa hao wanaishi katika nchi zilizoendelea. Mkutano wa 16 kuhusu ugonjwa wa Ukimwi duniani, ambao unaendelea kufanyika huko Toronto, Canada, umetoa wito wa kutaka nchi zilizoendelea kutekeleza ahadi zao za kutoa dawa na misaada ya fedha kwa nchi zinazoendelea, na kupunguza bei za dawa za Ukimwi ili kuwawezesha wagonjwa wote wapate dawa.
  • Waalimu wa China, Japan na Korea ya kusini wafikia maoni ya pamoja kuhusu elimu ya historia ya Asia ya mashariki ya zama za karibu
  •  2006/08/17
    Wajumbe wa waalimu wa historia kutoka shule za sekondari na za msingi za China, Japan na Korea ya kusini hivi karibuni kwa mara ya kwanza wamefanya mkutano hapa Beijing, ambapo walibadilishana maoni kuhusu uzoefu wa mafunzo ya elimu ya historia, na kujadili masuala kadhaa yenye migongano kuhusu elimu ya historia katika nchi hizo tatu.
  • Hali ya sasa na matumaini ya kupatikana kwa chanjo ya Ukimwi
  •  2006/08/16
    Utafiti wa wanasayansi kuhusu chanjo ya ugonjwa wa Ukimwi ulianza miaka 20 iliyopita. Mwaka 1987 chanjo ya kwanza ya Ukimwi duniani ilifikia hatua ya kutumika kwa binadamu, lakini hadi hivi leo hakuna aina moja kati ya aina zaidi ya elfu moja za chanjo za Ukimwi, inayoweza kukinga maambukizi ya Ukimwi.
  • Waziri mkuu wa Japan ameharibu sura ya Japan duniani
  •  2006/08/15
    Tarehe 15 Agosti, waziri mkuu wa Japan Bw Junichiro Koizumi alifikia hatua ya kwenda tena kwenye hekalu la Yasukuni bila kujali upinzani wa watu wengi wa nchini Japan na duniani, na kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita.
  • Mkutano kuhusu ugonjwa wa Ukimwi duniani wafunguliwa Toronto
  •  2006/08/14
    Mkutano wa 16 kuhusu ugonjwa wa Ukimwi duniani ulifunguliwa tarehe 13 huko Toronto, nchini Canada. Wataalamu, wasomi na maofisa watapao zaidi ya elfu 20 kutoka sehemu mbalimbali duniani wanahudhuria mkutano huo, wakijadili kwa pamoja masuala yanayohusu kinga na tiba ya Ukimwi.
  • Kongo Kinshasa itatulia baada ya uchaguzi huu?
  •  2006/08/10
    Tarehe 30 mwezi julai mwaka huu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliingia katika uchaguzi wake mkuu, ukiwa ni uchaguzi huru wa kwanza kufanyika katika nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 46 toka nchi hiyo ilipopata uhuru wake.
  • Bw Gedi afanya juhudi kutatua msukosuko wa serikali ya mpito ya Somalia
  •  2006/08/09
    Waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia Ali Mohamed Gedi tarehe 8 huko Baidoa, alikutana na watemi wa huko wenye nguvu na ushawishi ili kutafuta uungaji mkono wao kwa baraza jipya la mawaziri litakaloundwa. Wachambuzi wanasema hii ni sehemu ya juhudi za Bw. Gedi za kutatua msukosuko wa serikali ya mpito.
  • Mswada wa azimio uliotolewa na Marekani na Ufaransa wapokelewa kwa maoni tofauti
  •  2006/08/07
    Wajumbe wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa usiku wa tarehe 5 mwezi huu zilifanya mjadala wa kwanza kuhusu mswada wa azimio linalohusu mgogoro kati ya Lebanon na Israel. Israel na nchi kadhaa za magharibi zimeeleza kuufurahia mswada huo
  • Jumuiya ya nchi za kiislamu yalaani vitendo vya uvamizi vya Israel
  •  2006/08/04
    Nchi kadhaa wanachama wa Jumuiya ya nchi za kiislamu tarehe 3 mwezi huu zilifanya mkutano wa dharura huko Putrajaya, Malaysia, baadaye zilitoa taarifa zikilaani vikali vitendo vya uvamizi vya Israel.
  • Hali ya siku za baadaye ya Iran inayotatizwa na suala la nyukilia
  •  2006/08/03
    Tarehe 3 mwezi Agosti ni siku ya kutimiza mwaka mmoja tangu Bw Mohamed Ahamednejad aapishwe kuwa rais wa Iran. Ni siku chache tu zilizopita baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio No. 1696 kuhusu suala la nyukilia la Iran, likiitaka Iran isimamishe shughuli zote za utafiti kuhusu usafishaji wa uranium kabla ya tarehe 31 mwezi Agosti.
  • Maoni tofuati yaoneokana kwenye uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
  •  2006/08/02
    Uchaguzi wa rais na baraza la chini la bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ulifanyika tarehe 30 mwezi Julai na matokeo ya uchaguzi yatatolewa baada ya wiki kadhaa. Tarehe mosi mwezi Agosti, mmoja wa wagombea urais Bw. Azarias Ruberwa alieleza kuwa atakataa matokeo ya uchaguzi huo, ambapo maoni tofauti yameonekana kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia wa nchi hiyo uliokuwa unasubiriwa na watu kwa miaka zaidi ya 40 iliyopita.
  • "Sehemu kubwa ya mashariki ya kati" na "sehemu mpya ya mashariki ya kati" inayotarajia Marekani
  •  2006/08/01
    Tangu kuzuka mapigano ya kisilaha kati ya Israel na jeshi la chama cha Hezbollah nchini Lebanon, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bibi Condoleezza Rice amefanya usuluhisho mara mbili kwenye sehemu ya mashariki ya kati. Jambo linalostahili kutupiwa macho ni kuwa bibi Rice hakuihimiza Israel kusimamisha vitendo vya kijeshi, wala hakubali kusimamisha mapigano mara moja, bali alitoa wazo la "sehemu mpya ya mashariki ya kati".
  • Radio China Kimataifa kukutana na wasikilizaji wake wa Russia huko Ulan-Ute
  •  2006/08/01
    Tarehe 31 Julai Mkutano kati ya Radio China kimataifa na wasikilizaji wake wa Russia ulifanyika huko Ulan-Ute, mji mkuu wa Jamhuri ya Buriat ya Russia, mkutano huo uliandaliwa na ujumbe wa waandishi wa habari wa "Safari ya Urafiki wa China na Russia".
  • Uchaguzi mkuu Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wafanyika katika hali ya shwari nchini
  •  2006/07/31
    Uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ulifanyika tarehe 30, huu ni uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia kufanyika nchini humo tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1960. Siku hiyo wananchi wa nchi hiyo walimiminika kwenye vituo vya kupigia kura wakiwa na matarajio makubwa juu ya demokrasia na amani ya nchi hiyo katika siku za usoni, wakipiga kura kumchagua rais na bunge la taifa la nchi hiyo.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44