Kujenga dunia ya masikilizano 2008/07/17 Maofisa na askari 172 kwa jumla waliobaki wa kikosi cha kwanza cha askari wahandisi cha China kinachotakiwa kwenda Darfur nchini Sudan kutekeleza jukumu la kulinda amani, tarehe 16 usiku walifunga safari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zhengzhou, mkoani Henan.
|
Sudan yakataa mashitaka ya mahakama ya kimataifa 2008/07/16 Mwendesha mashitaka wa mahakama ya kesi za jinai ya kimataifa iliyowekwa The Hague, nchini Uholanzi, Bw. Luis Moreno Ocampo Tarehe 14 alimfungulia mashitaka rais Omar al-Bashir wa Sudan kwa hatia ya kuanzisha vita kwenye sehemu ya Darfur nchini Sudan, na kuiomba mahakama kutoa amri ya kumkamata.
|
Umoja wa Mediterranean wakabiliwa na changamoto mbalimbali 2008/07/14 Umoja wa Mediterranean umeanzishwa kwenye mkutano wa wakuu wa kanda ya bahari ya Mediterranean uliofanyika tarehe 13 huko Paris. Wachambuzi wanaona kuwa, umoja huo umeanzishwa baada ya pande mbalimbali kufanya mazungumzo kwa muda mrefu na kutoa maamuzi ya kurudi nyuma, lakini umoja huo bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na hali ya utatanishi katika kanda ya bahari ya Mediterranean.
|
Makubaliano kati ya India na Marekani yaanza kuleta mkoroganyo kwenye jukwaa la kisiasa la India 2008/07/11 Tovuti ya wizara ya mambo ya nje ya India tarehe 10 ilitangaza mswada wa makubaliano ya uhakikisho yaliyofikiwa kati ya India na Shirika la nishati ya atomiki la Kimataifa kuhusu kuhimiza utekelezaji wa makubaliano kati ya India na Marekani kuhusu mambo ya nyuklia. Wakati huo huo serikali ya India ilisema, India imewasilisha nyaraka za mswada huo kwenye Baraza la Shirika la nishati ya atomiki la Kimataifa, na itasaini rasmi makubaliano ya uhakikisho na Shirika hilo mapema zaidi
|
Mkutano wa wakuu wa nchi nane wafungwa 2008/07/10 Mkutano wa wakuu wa nchi nane, ambao ulifanyika kwa siku 3 kwenye ziwa la Toyoko, Hokkaido nchini Japan, ulifungwa tarehe 9 alasiri, waziri mkuu wa Japan Bw. Yasuo Fukuda alitangaza kuwa mkutano umefanikiwa. Lakini vyombo vya habari vinaona kuwa, mkutano huo haukupata maendeleo halisi, kufungwa hivi hivi kwa kawaida kunaonesha mgongano kati ya maslahi ya nchi hizo nane. Kwa upande mwingine, athari za kundi la nchi nane la viwanda kwa dunia inatiliwa mashaka kwa mara nyingine tena, ambapo athari ya nchi zinazoendelea inainuka kila siku ipitayo
|
Mazungumzo ya pande sita kuaanza tena baada ya kusimama kwa miezi 9 2008/07/09 Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Qin Gang tarehe 8 alitangaza kuwa, kutokana na juhudi za pande zote mazungumzo ya pande sita kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea yamepata maendeleo muhimu. Ili kusukuma mbele mazungumzo hayo, pande sita zimeamua kufanya mkutano wa siku tatu wa viongozi wa ujumbe mjini Beijing kuanzia tarehe 10 Julai. Hayo ni mazungumzo ambayo yamerejeshwa tena baada ya kusimama kwa miezi 9.
|
Viongozi wa kundi la nchi 8 zinazoendelea watajadili masuala ya uchumi 2008/07/08 Viongozi wa kundi la nchi 8 zinazoendelea D-8 tarehe 8 wanafanya mkutano huko Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia, ambapo wanajadili kwa kina masuala ya uchumi yanayokumba nchi hizo. Mkuktano wa viongozi wa D-8 unafanyika kila baada ya miaka miwili. Mada ya mkutano huo ni "kufanya ushirikiano mpya kwa ajili ya kukabiliana pamoja na changamoto". Washiriki wa mkutano huo watajadili maendeleo ya kundi lenyewe, kuandaa mpango wa ushirikiano wa kiuchumi na kuanzisha ofisi ya sekretarieti na kujadili suala la kupanda kwa bei ya mafuta na chakula duniani.
|
Shambulizi la bomu la kujiua latokea tena mjini Islamabad 2008/07/07 Shambulizi la bomu la kujiua lilitokea tena tarehe 6 mjini Islamabad, ambapo zaidi ya watu 10 waliuawa na zaidi ya watu 40 walijeruhiwa, watu wengi kati ya waliouawa katika shambulizi hilo ni polisi. Mlipuko huo ulitokea karibu na mskiti wa Lal Masjid, ambao ulifuatiliwa sana na watu wa duniani katika kipindi fulani. Katika siku hiyo maelfu ya watu walikuwa wakishiriki kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika nje ya mskiti huo kuadhimisha mwaka mmoja tangu tukio la "mskiti wa Lal Masjid" lilipotokea.
|
Lebanon na Israel kubadilishana mateka 2008/07/04 Katibu mkuu wa Chama cha Hezbollah cha Lebanon Bw. Hassan Nasrallah tarhe 2 alipozungumza na waandishi wa habari alithibitisha kuwa chama chake kitabadilishana mateka na Israel ndani ya wiki mbili zijazo. Kwenye mkutano na waandishi wa habari Bw. Nasrallah alitangaza kuwa Israel itawaachia huru mateka wa kivita wa Lebanon walioongozwa na Samir Kantar na kukabidhi miili ya mateka wa Lebanon na nchi nyingine za Kiarabu.
|
Jumuiya ya kimataifa yajadili namna ya kukabiliana na mgogoro wa nafaka duniani 2008/07/03 Maofisa wa ngazi ya juu pamoja na watafiti wa baadhi ya jumuiya za kimataifa wapatao zaidi ya 200, walikuwa na kongamano tarehe 2 huko Washington kujadili namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazotokana na kupanda kwa bei za nafaka duniani kwa hivi sasa.
|
IMF yatoa ripoti kuhusu kupanda kwa bei ya chakula na mafuta 2008/07/02 Shirika la Fedha la Kimataifa IMF tarehe mosi Julali kwenye makao makuu yake mjini Washington, lilitoa ripoti ya ufafanuzi kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta na chakula duniani. Ripoti hiyo inasema hivi sasa kazi za haraka zinazozikabili nchi zote ni kutatua tatizo la chakula na huku zikihakikisha utulivu wa uchumi duniani ambao haukupatikana kwa urahisi.
|
Mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika wajadili masuala ya maji na usafi 2008/07/01 Mkutano wa 11 wa wakuu wa Umoja wa Afrika ulifunguliwa tarehe 30 Juni huko Sharm el Sheikh, nchini Misri. Rais Hosni Mubarak wa Misri, ambayo ni nchi mwenyeji wa mkutano huo, akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, alisema "Hivi sasa dunia nzima inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo msukosuko wa chakula, kupanda kwa bei ya nishati, pamoja na athari za nishati ya kiviumbe na mabadiliko ya hali ya hewa.
|
Masuala yanayofuatiliwa zaidi kwenye mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika 2008/06/30 Mkutano wa 11 wa wakuu wa Umoja wa Afrika unafanyika tarehe 30 Juni na tarehe 1 Julai huko Sharm el Sheikh, nchini Misri. Masuala yanayofuatiliwa zaidi kwenye mkutano huo ni suala la maji na afya, msukosuko wa chakula na hali ya kisiasa nchini Zimbabwe.
|
Mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea yatazamiwa kuingia katika kipindi kipya 2008/06/27 Tarehe 26 Mei Korea ya kaskazini ilikabidhi mpango wake wa nyuklia kwa China ambayo ni nchi mwenyekiti wa mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea. Rais Bush wa Marekani siku hiyo alitangaza kuwa Marekani inataka kufuta jina la Korea ya kaskazini kutoka kwenye "orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi" na kusimamisha vikwazo vyake dhidi ya nchi hiyo.
|
"Wiki ya Maji ya Kimataifa" inafanyika nchini Singapore 2008/06/26 Mkutano wa "Wiki ya Maji ya Kimataifa" unaofanyika sasa nchini Singapore umewapatia wajumbe wa nchi mbalimbali nafasi za kujadiliana kuhusu matatizo ya maliasili ya maji, kubadilishana uzoefu wa usimamizi na kuonesha teknolojia mpya zinazotumika katika nyanja ya maji.
|
Makubaliano ya kusimamisha vita kati ya Israel na Palestina yakumbwa na changamoto mpya 2008/06/25 Tarehe 23 na 24 mapambano kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa Palestina yalitokea tena katika sehemu ya kusini ya Israel na ukanda wa Ghaza. Haya ni mapambano yaliyotokea baada ya kusimamisha vita kwa miezi 6 tokea makubaliano yalipoanza kutekelezwa. Tarehe 23 jioni, kombora moja lililopigwa kutoka ukanda wa Ghaza lililipuka katika sehemu ya kusini ya Israel. Hili ni tukio la kwanza baada ya makubaliano ya kusimamisha vita kuanza kutekelezwa.
|
Umoja wa Ulaya waichukulia Iran vikwazo vipya 2008/06/24 Ofisa mmoja wa Umoja wa Ulaya ambaye hakutaka kutaja jina lake tarehe 23 alidokeza kwamba mkutano wa mawaziri wa Umoja wa Ulaya umekubali kuiwekea Iran vikwazo vipya ikiwa ni pamoja na kuzuia mali za Benki ya Taifa ya Iran na kupiga marufuku watu wanaohusika na mpango wa nyuklia wa Iran kuingia kwenye nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya au kufanya biashara katika nchi hizo
|
Kiongozi wa chama cha upinzani atangaza kujitoa kwenye duru la pili la uchaguzi nchini Zimbabwe 2008/06/23 Kiongozi wa chama cha upinzani Movement for Democratic Changge MDC Bw. Morgan Tsvangirai tarehe 22 alitangaza kujitoa kwenye duru la pili la uchaguzi utakaofanyika tarehe 27 mwezi huu. Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Zimbabwe, kama mgombea mmoja akijitoa kwenye uchaguzi, mgombea mwingine anakuwa rais bila kupigiwa kura.
|
China na nchi za Afrika zitafanya ushirikiano halisi kwenye sekta ya hakimiliki ya ubunifu 2008/06/20 Mkutano wa siku 5 wa wakurugenzi wa idara za hakimiliki ya ubunifu za China na nchi za Afrika umefungwa Tarehe 20 Juni hapa Beijing. Maofisa wa nchi za Afrika waliohudhuria mkutano huo wameeleza matumaini ya kuimarisha ushirikiano na China katika kazi ya kulinda hakimiliki ya ubunifu kwenye sekta ya utamaduni wa jadi, matibabu na dawa.
|
Historia ya mazungumzo ya mkakati wa kiuchumi kati ya China na Marekani 2008/06/16 Mazungumzo ya nne ya mkakati wa kiuchumi kati ya China na Marekani yatafanyika tarehe 17 na 18 huko Annapolis, nchini Marekani, ambapo naibu waziri mkuu wa China Bw. Wang Qishan na waziri wa fedha wa Marekani Bw. Henry Paulson wataendesha mazungumzo hayo kwa pamoja.
|
Umoja wa Nchi za Kiarabu na Umoja wa Afrika wataka Eritrea na Djibouti zitatue mgogoro wa mpakani kwa njia ya mazungumzo 2008/06/13 Tarehe 12 Umoja wa Nchi za Kiarabu na Umoja wa Afrika ulizitaka Eritrea na Djibouti zitatue mgogoro wa mpakani kwa njia ya mazungumzo. Wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Nchi za Kiarabu tarehe 12 walifanya mkutano wa dharura, azimio lililopitishwa kwenye mkutano huo lilizitaka Eritrea na Djibouti ziondoe majeshi yao kutoka mpakani.
|
Balozi Sun Zhenyu achambua sera za biashara za Marekani 2008/06/12 Shirika la biashara duniani, WTO, tarehe 11 lilimaliza majadiliano ya siku mbili kuhusu sera za biashara za Marekani. Marekani ikiwa nchi inayochukua nafasi ya kwanza katika shughuli za kiuchumi na kibiashara duniani, sera zake za biashara zina athari kubwa kuhusu mazingira ya biashara ya dunia
|
Makubaliano ya usalama kati ya Marekani na Iraq yakabiliwa na matatizo 2008/06/11 Mshauri mwandamizi anayeshughulikia masuala ya Iraq katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani tarehe 10 huko Baghdad alisisitiza kuwa, Marekani na Iraq zitafikia makubaliano ya usalama mwishoni mwa Julai. Hivi sasa mazungumzo hayo kuhusu makubaliano yaliyoanzishwa mwezi Februari yanaendelea faraghani, masuala kuhusu hadhi ya jeshi la Marekani nchini Iraq na mamlaka ya Iraq yanafuatiliwa zaidi na pande mbalimbali
|
Waziri mkuu wa Iraq asema ziara yake nchini Iran imefanikiwa 2008/06/10 Waziri mkuu wa Iraq Bw Nouri Al-Maliki tarehe 9 alimaliza ziara yake nchini Iran, na kabla ya kuondoka mjini Teheran alisema ziara yake imepata mafanikio makubwa,na ana matumaini kuwa mafanikio hayo yatasukuma mbele maendeleo ya urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili
|
Bw Maliki ataka kuiondoa wasiwasi wa Iran 2008/06/09 Waziri mkuu wa Iraq Bw. Nouri al-Maliki tarehe 8 alipokuwa na mazungumzo na rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran alisisitiza kuwa, Iraq yenye hali tulivu itachangia kuwepo kwa usalama wa sehemu hiyo na hata wa dunia nzima. Bw. Maliki aliiahidi Iran kuwa, Iraq haitatoa nafasi ya kuiathiri Iran. Wachambuzi wanaona kuwa ziara hiyo ya Bw Maliki inahusiana sana na "mkataba kuhusu hadhi ya jeshi la Marekani lililoko nchini Iraq" ambao unajadiliwa katika mazungumzo.
|
Fursa mpya ya kuhakikisha usalama wa chakula duniani 2008/06/06 Mkutano mkuu wa kujadili usalama wa chakula duniani ulimalizika tarehe 5 Juni huko Rome, Italia. Mkutano huo ulioitishwa na Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO ulishindwa kuondoa maoni tofauti ya pande mbalimbali kuhusu masuala nyeti, lakini ulitoa fursa nzuri kwa jumuiya ya kimataifa kubadilishana maoni kuhusu malengo ya milenia ya Umoja wa Mataifa ambayo yanazingatia maendeleo ya kilimo kwa lengo la kuhakikisha kila mtu anapata chakula.
|
Mazungumzo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa yajadili "mpango wa Bali" 2008/06/05 Mazungumzo ya duru la pili ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa yatakayofanyika kwa wiki mbili yalianza tarehe 2 huko Bonn, Ujerumani, wajumbe zaidi ya 2,400 kutoka nchi na sehemu 172 wanashiriki kwenye mazungumzo hayo, wajumbe wa mkutano watajadili zaidi utekelezaji wa "mpango wa Bali" uliopitishwa kwenye mkutano wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwezi Desemba mwaka jana huko Bali, Indonesia, na kufanya maandalizi ya uidhinishaji wa mkataba wa kulinda hali ya hewa ya dunia wa baada ya mwaka 2012.
|
Jumuiya ya kimataifa yajadili usalama wa chakula duniani 2008/06/04 Mkutano wa viongozi kuhusu usalama wa chakula duniani ulianza kufanyika tarehe 3 kwenye makao makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo FAO huko Rome. Kutokana na kupanda kwa juu kwa bei ya chakula, mkutano huo umekuwa unafuatiliwa sana. Ajenda ya mkutano huo ni "changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa na matumizi ya nafaka katika kutengeneza nishati".
|
Mkutano mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo FAO wafanyika 2008/06/03 Mkutano wa siku tatu wa viongozi wakuu kuhusu usalama wa chakula duniani unaoandaliwa na Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO unafanyika kuanzia tarehe 3 huko Rome. Wajumbe wa ngazi ya juu kutoka nchi na jumuiya za kimataifa zaidi ya 150 wanahudhuria mkutano huo. Ajenda kuu ya mkutano huo ni usalama wa chakula kutokana na changamoto za kupanda haraka kwa bei ya chakula, mabadiliko ya hali ya hewa na utengenezaji wa nishati kwa kutumia nafaka.
|
"Mazungumzo ya Shangri-La" yatoa mapendekezo kuhusu usalama wa kikanda 2008/06/02 Mkutano wa 7 wa usalama wa Asia unaojulikana kama "Mazungumzo ya Shangri-La", ulifungwa tarehe 1 mwezi Juni huko Singapore. Katika muda wa siku tatu za mkutano huo, mawaziri wa ulinzi, wakuu wa majeshi, maofisa wa usalama na wataalamu kutoka nchi na sehemu 27 za Asia na Pasifiki walifanya mazungumzo kuhusu changamoto, mapambano dhidi ya ugaidi, mabadiliko ya hali ya hewa na mfumo wa usalama wa sehemu ya Asia na Pasifiki, na kutoa mapendekezo yao kuhusu usalama wa kikanda.
|