Mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel bado yakabiliwa na changamoto 2008/01/11 Rais wa Marekani George Bush tarehe 9 na tarehe 10 alifanya ziara nchini Israel na Palestina akijaribu kufufua mazungumzo yaliyosimama kwa karibu mwezi mmoja kati ya Israel na Palestina.
|
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika aanza kusuluhisha mgogoro wa kisiasa nchini Kenya 2008/01/10 Msuluhishi wa mgogoro wa kisiasa nchini Kenya ambaye pia ni rais wa Ghana na mwenyekiti wa muda wa Umoja wa Afrika Bw. John Kufour, tarehe 9 alifanya mazungumzo na rais wa Kenya Mwai Kibaki na kiongozi wa Chama cha ODM Bw. Raila Odinga kwa nyakati tofauti, lakini kila upande haukutoa taarifa yoyote baada ya mazungumzo
|
Uwekezaji kwa mwaka 2007 duniani ulikuwa mkubwa kuliko miaka yote iliyopita 2008/01/09 Shirika la Maendeleo na Biashara la Umoja wa Mataifa, UNCTAD, tarehe 8 lilitoa taarifa ikisema, thamani ya uwekezaji duniani kwa mwaka jana ilifikia dola za Kimarekani trilioni 1.538, huu ni uwekezaji mkubwa kabisa kupataikana kuliko wa miaka yote iliyopita.
|
Ghasia nchini Kenya zatazamiwa kutulia 2008/01/08 Kutokana na usuluhishi wa kimataifa, tarehe 7 kiongozi wa chama cha ODM Bw. Raila Odinga alitangaza kufuta maandamano yaliyopangwa kufanyika tarehe 8, na hali ya Kenya inaelekea kuwa ya utulivu. Hapo kabla, Rais Mwai Kibaki aliyeshinda uchaguzi mkuu tarehe 3 alitoa hotuba akisema, ghasia zikitulia atafanya mazungumzo na chama cha upinzani. Ingawa Bw. Odinga alijibu kwa hasira lakini alitoa masharti mawili ya kufanya mazungumzo, moja ni kuwa Rais kibaki ajiuzulu, pili ni kufanya usuluhisho kupitia upande wa tatu.
|
Mkutano wa dharura wajadili msukosuko wa kisiasa wa Lebanon na hali ya Palestina na Israel 2008/01/07 Mkutano wa dharura wa Umoja wa nchi za kiarabu ulifanyika tarehe 6 huko Cairo, ambapo mawaziri wa mambo ya nje au wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa nchi za kiarabu, walijadili msukosuko wa kisiasa wa Lebanon na kuanzisha upya mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel.
|
Machafuko nchini Kenya 2008/01/04
Tarehe 3 Januari maandamano makubwa ya kushirikisha watu milioni moja hayakufanyika huko Nairobi kama yalivyopangwa, na hakuna dalili yoyote ya kupungua kwa machafuko yanayoikumba Kenya. 
|
Kwa nini bei ya mafuta imezidi dola 100 za Kimarekani? 2008/01/03 Tarehe 2 mwezi Januari mwaka 2008 ilikuwa siku ya kwanza kwa biashara ya mafuta ya petroli yatakayozalishwa kwenye soko la mafuta ya petroli duniani. Bei ya mafuta ya asili ya petroli yatakayozalishwa katika mwezi Februari katika siku hiyo ilipanda sana kwa kiasi cha kushangaza, hata ilizidi dola za kimarekani 100 kwa pipa, ambayo ni mara ya kwanza kutokea kwenye historia ya biashara ya mafuta yatakayozalishwa.
|
Mwanadiplomasia wa Marekani auawa nchini Sudan 2008/01/02 Mwanadiplomasia mmoja wa Marekani tarehe mosi Januari aliuawa nchini Sudan. Hili ni tukio la kwanza kwa mwanadiplomasia wa nchi za nje kuuawa nchini Sudan katika miaka ya karibuni. Tukio hilo lilitokea saa kumi alfajiri, wakati huo gari la ubalozi wa Marekani nchini Sudan lilipokuwa likipita kwenye barabara kuu mjini Khartoum lilishambuliwa kwa risasi na watu wenye silaha.
|
Mwai Kibaki achaguliwa kuwa rais wa Kenya katika kipindi kijacho 2007/12/31 Tume ya uchaguzi ya Kenya tarehe 30 mwezi Desemba ilitangaza, rais wa sasa wa Kenya Bw Mwai Kibaki ameshinda katika upigaji kura wa uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 27 mwezi Desemba. Kisha Bw. Kibaki aliapishwa kuwa rais wa kipindi kijacho.
|
Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Bibi Benazir Bhutto auawa 2007/12/28 Waziri mkuu wa zamani ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Umma cha Pakistan Bibi Benazir Bhutto tarehe 27 aliuawa katika mji wa Rawalpindi, mji ulio karibu na Islamabad, mji mkuu wa Pakistan. Jumuyia ya kimataifa imelaani vikali kitendo hicho. Wachambuzi wanaona kuwa kuuawa kwake ni pigo kubwa kwa hali inayoelekea kuwa tulivu nchini Pakistan.
|
Kwa nini Russia yaonesha nguvu zake za kijeshi? 2007/12/27 Kikosi cha ulinzi wa anga cha jeshi la Russia tarehe 25 mwezi Desemba kilitangaza kuwa, kuanzia mwaka 2009jeshi la nchi kavu la Russia litaanza kujizatiti kwa mfumo mpya wa kutungulia ndege wa makombora ya masafa mafupi ya aina ya "Tor-M2".
|
Serikali ya China yatoa waraka "Hali na Sera ya Nishati ya China" 2007/12/26 Ofisi ya habari ya baraza la serikali ya China tarehe 26 mwezi Desemba ilitoa waraka "Hali na Sera ya Nishati ya China" ukieleza hali, mkakati na lengo la maendeleo ya nishati ya China. Waraka wa serikali unasema, katika miaka ya hivi karibuni harakati za kuokoa nishati zilipata ufanisi mkubwa, vitu vya uchafuzi vinavyotolewa vimeweza kudhibitiwa
|
Waziri mkuu wa Japan anata kusukuma uhusiano kati ya Japan na China kwenye kipindi kipya 2007/12/26 Waziri mkuu wa Japan Bw. Yasuo Fukuda atakayefanya ziara nchini China, tarehe 25 alipokutana na waandishi wa habari wa China nchini Japan alisema, anataka kusukuma mbele uhusiano kati ya Japan na China kwenye kipindi kipya na kuufanya mwaka wa kesho uwe wa kupiga hatua kubwa ya maendeleo kwenye uhusiano kati ya Japan na China.
|
Askari wa jeshi la Marekani nchini Iraq hawathubutu kusema "Heri ya Krismasi" 2007/12/25 Alasiri ya tarehe 24 kabla ya sikukuu ya Krismasi, askari wa rejimenti ya pili ya jeshi la Marekani nchini Iraq walijizatiti na kuwa tayari kuondoka kambini. Lakini hawakwenda kwenye sherehe ya Krismasi kama kawaida yao, bali walijipenyeza ndani ya madereya na kwenda kufanya doria mjini Baghdad.
|
Kwa nini wakuu watatu wamefanya ziara ghafla nchini Afghanistan 2007/12/24 Rais Hamid Karzai wa Afghanistan alikuwa na shughuli nyingi katika wikiendi iliyopita, tarehe 22 na 23 mwezi Desemba alikuwa na wageni watatu waheshimiwa wa nchi za magharibi ambao nni rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa, waziri mkuu wa Australia Bw, Kevin Rudd na waziri mkuu wa Italia Bw Romano Prodi.
|
Mwenyekiti mpya wa Chama cha ANC asema ataendelea na sera za hivi sasa 2007/12/21 Bw. Jacob Zuma asema Chama cha ANC kitajitahidi kuondoa tofauti za ndani, kushikilia siasa iliyopo, kulinda maslahi ya wawekezaji, kupunguza umaskini, kupambana na uhalifu, kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa UKIMWI na kulinda haki za wanawake.
|
Umoja wa Ulaya ujiondoe kutoka msukosuko wa kutunga katiba 2007/12/20
Mwaka 2007 ni mwaka muhimu kwa ujenzi wa Umoja wa Ulaya. Baada ya kufanya mazungumzo magumu ya muda mrefu, tarehe 13 Desemba, viongozi wa nchi mbalimbali za Umoja wa Ulaya walisaini "Mkataba wa Lisbon" utakaotekelezwa badala ya mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya.
|
Binadamu wafanya juhudi kwa pamoja ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa 2007/12/19 Kutokana na maendeleo ya jamii, mazingira ya hali ya hewa duniani yanazidi kuwa mabaya siku hadi siku, hivi sasa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kumekuwa somo kubwa linalowakabili binadamu. Baada ya kufanya mazungumzo magumu ya siku 13, tarehe 15 Desemba, Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa uliofanyika nchini Indonesia ulipitisha "Mpango wa Bali" wenye umuhimu wa kufungua ukurasa mpya.
|
Hali ya uchaguzi mkuu unaobadilika badilika nchini Korea ya Kusini 2007/12/18 Uchaguzi mkuu wa Korea ya Kusini utafanyika tarehe 19. matokeo ya uchaguzi huo yataamua mwelekeo wa utawala na mambo ya ndani na ya nje katika kipindi cha miaka mitano ijayo, na ni uchaguzi ambao unahusu amani na utulivu wa peninsula ya Korea.
|
Mwaka wa kupata maendeleo makubwa ya utatuzi wa suala la nyuklia la peninsula ya Korea 2007/12/17 Suala la nyuklia la peninsula la Korea bado ni suala linalofuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Kutokana na pande mbalimbali kufanya juhudi nyingi, mazungumzo ya pande sita kuhusu suala hilo yamepata maendeleo makubwa.
|
Ukungu uliotanda suala la nyuklia la Iran waanza kupungua 2007/12/14 Tarehe 24 mwezi Machi mwaka huu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio jipya la kuiwekea Iran vikwazo dhidi ya mradi wa kutengeneza silaha za nyuklia, lakini Iran haikutishika badala yake inaendelea na mpango wake wa nyuklia
|
Baada ya Mkutano wa Annapolis, sehemu ya mashariki ya kati inakaribia na amani? 2007/12/13 Katika mwaka 2007, kwenye sehemu ya mashariki ya kati, mbali na mapambano kati ya Israel na Palestina, migongano mikali kati ya makundi ya Palestina imeleta utatanishi zaidi kwa mgogoro kati ya Israel na Palestina. Na Mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya mashariki ya kati uliofanyika tarehe 27 Novemba, mwaka 2007 huko Annapolis
|
Sera ya mambo ya nje ya Marekani inarekebishwa kwa mujibu wa hali ilivyo 2007/12/12 Wakati mwaka 2007 unapokaribia kumalizika, Marekani inaendelea kuwa kwenye matope ya Iraq. Serikali ya George Bush inaendelea kutanguliza mbele mapambano yake dhidi ya ugaidi kwenye sera yake ya mambo ya nje. Kutokana na shinikizo kutoka ndani na nje, serikali ya George Bush ambayo kipindi chake kinakaribia kwisha imeanza kurekebisha sera yake ya mambo ya nje, ili iweze kutatua matatizo kwa njia ya kidiplomasia
|
Ulaya na Afrika zaanzisha uhusiano kiwenzi na kimkakati 2007/12/10 Mkutano wa pili wa siku mbili wa viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya na Afrika ulifungwa tarehe 9 huko Lisbon, mji mkuu wa Ureno, nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya. Kwenye mkutano huo viongozi kutoka nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya na nchi 53 za Afrika walijadiliana waraka wa "Uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya Afrika na Umoja wa Ulaya" na kuandaa "Mpango wa Utekelezaji Mwaka 2008-2010".
|
Matarajio kuhusu mkutano wa viongozi wa Ulaya na Afrika 2007/12/07 Mkutano wa pili wa viongozi wakuu wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya na nchi 53 za Afrika utafanyika kuanzia tarehe 8 hadi 9 huko Lisbon, mji mkuu wa Ureno, nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya. Kufanyika kwa mkutano huo ulioahirishwa mara kadhaa kumeonesha kuwa sera za Umoja wa Ulaya kwa Afrika zimebadilika kuwa busara.
|
OPEC yaamua kutoongeza uzalishaji wa mafuta 2007/12/06 Mkutano wa mawaziri wa jumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta duniani, OPEC, ambao ulifanyika tarehe 5 mwezi Desemba mjini Abu Dhabi, uliamua kutoongeza kwa muda uzalishaji wa mafuta. Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo kumalizika inasema, hivi sasa kwa jumla hakuna mabadiliko katika pande mbili za mahitaji na utoaji wa mafuta kwenye soko la kimataifa, mafuta yaliyopo kwenye soko la kimataifa ni mengi ya kutosha.
|
Mkutano wa Kamati ya Ushirikiano ya nchi za Ghuba wafungwa 2007/12/05 Mkutano wa 28 wa siku mbili wa Kamati ya Ushirikiano ya nchi za Ghuba ulifungwa tarehe 4 huko Doha, mji mkuu wa Qatar. Mkutano huo umetoa "Taarifa ya Doha" na kufikia makubaliano kuhusu uchumi na usalama wa kikanda. Kutokana na kuwa mkutano huo wa viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Kamati ya Ushirikiano wa Nchi za Kiarabu za Ghuba utatangaza soko la pamoja la nchi za Ghuba.
|
Nani atahudhuria mkutano wa viongozi wakuu wa Ulaya na Afrika? 2007/12/04 Mkutano wa pili wa viongozi wakuu wa Ulaya na Afrika ulioahirishwa kwa miaka minne utafanyika tarehe 8 hadi 9 katika Lisbon, mji mkuu wa Ureno, nchi mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya. Kadiri mkutano huo unavyokaribia, waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown anaendelea kushikilia msimamo wa kutohudhuria mkutano huo kama rais Robert Mugabe wa Zimbabwe atahudhuria, kwa hiyo bado kuna tatizo kama mkutano huo utakuwa kweli ni mkutano wa viongozi wakuu.
|
Bw. Pervez Musharraf kuondoa amri ya hatari nchini Pakistan 2007/11/30 Rais Pervez Musharraf wa Pakistan tarehe 29 baada ya kuapishwa kuwa rais wa Pakistan bila wadhifa wa kijeshi, alisema tarehe 16 Desemba ataondoa amri ya hali ya hatari nchini Pakistan, na kuacha kufuata katiba ya muda iliyotangazwa kabla ya hapo.
|
Manowari ya jeshi la China yafanya ziara ya kirafiki nchini Japan 2007/11/29 Wasikilizaji wapendwa, manowari yenye makombora iitwayo "Shenzhen" ya jeshi la China iliwasili Tokyo, Japan tarehe 28 asubuhi, na kuanza ziara ya kirafiki ya siku 4 nchini humo. Hii ni mara ya kwanza kwa manowari ya jeshi la baharini la ukombozi la watu wa China kutembelea Japan, ambayo inafungua ukurasa mpya wa maingiliano kati ya China na Japan katika eneo la ulinzi.
|