Vyombo vya habari vya nchi za magharibi na sura ya Afrika 2005/05/23 Rais Kagame alisema kuwa habari mbaya zilizotolewa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi kuhusu Afrika zimeathiri uwekezaji wa nchi za nje katika Afrika, hii ni moja ya chanzo kinachofanya Afrika kuwa nyuma kimaendeleo.
|
Ziara ya Jia Qinglin yatia nguvu mpya kwa maendeleo ya urafiki na ushirikiano kati ya China na Latin Amerika katika sekta zote 2005/05/23 Mwenyekiti wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bwana Jia Qinglin tarehe 20 alimaliza ziara yake rasmi ya kirafiki katika nchi 4 za Latin Amerika.
|
Mabadiliko ya hali ya hewa duniani huenda yatasababisha kuongezeka kwa sehemu zinazokumbwa na ugonjwa wa malaria nchini Afrika ya Kusini 2005/05/20 Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi ya utafiti wa aina nyingi za viumbe ya Afrika ya Kusini inaona kuwa, mabadiliko ya hali ya hewa duniani huenda yatasababisha kupanuka kwa sehemu zinazokumbwa na ugonjwa wa malaria nchini humo. Jambo hilo si kama tu litatishia afya za wananchi, bali pia litaathiri sekta ya utalii ya huko.
|
Bw Faure Gnassingbe achaguliwa kuwa rais, hali ya Togo yatazamiwa kuwa tulivu siku hadi siku 2005/05/19 Mahakama ya katiba ya Togo tarehe 26 usiku ilitangaza kuwa, katika uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 24, mgombea kutoka Shirikisho la umma la Togo Bwana Faure Gnassingbe amepata kura nyingi za ndiyo na kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Togo.
|
Hali ya kusimamisha vita kati ya Palestina na Israel iko hatarini 2005/05/19 Hali ya hatari ilionekana tena tarehe 18 katika sehemu ya Gaza. Siku hiyo, watu wenye silaha wa Palestina walirusha mabomu kadhaa kwenye makazi ya Wayahudi yaliyoko katika sehemu ya Gaza na jeshi la Israel liliwajibu watu hao wa Palestina kwa makombora kwa mara ya kwanza tangu mwezi Februari mwaka huu
|
Hali ya kisiasa nchini Ethiopia yavurugika tena 2005/05/19 Ethiopia ilifanya uchaguzi wa tatu wa bunge la umma na uchaguzi wa mabunge ya majimbo 8 ya nchi hiyo tarehe 15 mwezi huu. Huo ni uchaguzi wa tatu wa vyama vingi ulioshirikisha wapigaji kura wengi zaidi katika historia. Kwa mujibu wa katiba ya Ethiopia, chama kinachopata viti vingi zaidi kwenye bunge la nchi hiyo kina haki ya kuunda serikali.
|
Mkutano wa nchi za Afrika kuhusu suala la Darfur wafanyika 2005/05/18 Mkutano mdogo wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu suala la Darfur nchini Sudan ulifunguliwa jana usiku huko Tripoli, mji mkuu wa Libya. Viongozi wa nchi walioshiriki kwenye mkutano wanatoka Libya, Sudan, Ethiopia, Nigeria, Chad na Eritrea pamoja na maofisa kutoka Umoja wa Afrika na Umoja wa Nchi za Kiarabu.
|
Kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Latin Amerika na kusukuma mbele maendeleo kwa pamoja 2005/05/18 Mwenyekiti wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bwana Jia Qinglin ambaye yuko ziarani nchini Colombia tarehe 17 alasiri alitoa hotuba kwenye Baraza la juu la bunge la Colombia akisema kuwa, kuimarisha ushirikiano kati ya China na Latin Amerika si kama tu kunasaidia kuinua hadhi ya kila upande duniani, bali pia kunasaidia zaidi amani, utulivu na maendeleo ya dunia.
|
Mageuzi ya Umoja wa Mataifa yangefanyika hatua kwa hatua 2005/05/18 Katika hali ambayo pande mbalimbali zina maoni tofauti kabisa, "Umoja wa Nchi Nne" unaoundwa na Japan, Ujerumani, Brazil na India tarehe 16 ulifanya harakati ya kusambaza kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mswada wa azimio la mageuzi ya baraza la usalama.
|
Vyama vya upinzani nchini Misri vyapinga upigaji kura za maoni kuhusu marekebisho ya kifungu cha 76 cha katiba 2005/05/18 Chama cha Ndugu wa Kiislamu, Ikhwan, pamoja na vyama vingine vitatu nchini Misri tarehe 17 vilitangaza kupinga upigaji kura za maoni dhidi ya marekebisho ya kifungu cha 76 cha katiba.
|
Ziara ya Jia Qinglin nchini Cuba yapata mafanikio makubwa 2005/05/17 Mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa ya China Bw. Jia Qinglin tarehe 15 alimaliza ziara rasmi ya kirafiki nchini Cuba, na kuelekea Bogotá, kuanza ziara yake nchini Colombia.
|
Mazungumzo kati ya serikali ya Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini yameanza tena 2005/05/17 Mazungumzo yaliyosimamishwa kwa karibu mwaka mmoja kati ya serikali ya Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini yameanza tena tarehe 16 katika mji wa Gaesong nchini Korea ya Kaskazini.
|
Nchi za Afrika zafanya majadiliano tena ili kuondoa mgogoro wa Darfur wa Sudan 2005/05/16 Viongozi wa nchi 6 za Afrika za Libya, Sudan, Misri, Nigeria, Chad na Gabon pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa nchi za kiarabu Amr Musaa tarehe 16 wamekutana huko Tripoli, mji mkuu wa Libya wakifanya majadiliano kuhusu suala la Darfur la Sudan.
|
Upunguzaji wa vituo vya kijeshi wasababisha malalamiko 2005/05/16 Bw. Rumsfeld ana lengo lake kuhusu hatua hizo anazochukua. Katika taarifa moja alisema kuwa nia ya jeshi la Marekani kujenga vituo vingi vya kijeshi hapo awali ilitokana na kukabiliana na vita baridi. Lakini hali ya hivi sasa imekuwa na mabadiliko makubwa.
|
Upigaji kura wa uchaguzi mkuu nchini Ethiopia wamalizika 2005/05/16 Upigaji kura wa uchaguzi wa baraza la wajumbe wa umma la bunge la shirikisho la Ethiopia na mabunge ya mikoa minane ulimalizika tarehe 15. Huu ni uchaguzi wa tatu wa kidemokrasia wa vyama vingi katika historia ya Ethiopia.
|
Iran haitaacha nia yake ya kutumia nyuklia kwa matumizi ya amani 2005/05/16 Hivi karibuni suala la nyuklia la Iran limepata maendeleo kidogo. Ofisa wa Iran alidokeza kuwa mazungumzo kati ya Iran na nchi tatu za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zinazowakilisha Umoja wa Ulaya yamekaribia kufikia makubaliano.
|
Maandamano makubwa ya kupinga Marekani yazuka nchini Afghanistan 2005/05/13 Tarehe 12 maandamano makubwa ya kuipinga Marekani yalifanyika huko Kabul, mji mkuu wa Afghanistan. Wanafunzi karibu elfu moja walifanya maandamano barabarani wakilipinga jeshi la Marekani kuikashifu Kurani na kuwaua wapinzani. Kuanzia tarehe 10, wanafunzi na raia wa Afghanistan wamefanya maandamano ya kuipinga Marekani katika sehemu mbalimbali nchini humo, na mgogoro ulitokea kati yao na polisi, na kusababisha vifo vya watu 7 na wengine 76 kujeruhiwa. Maandamano hayo ni makubwa kabisa tangu jeshi la Marekani lianzishe vita nchini humo mwezi Desemba mwaka 2001.
|
Watu wa fani mbalimbali wa Italia waikumbuka vita dhidi ya ufashisti. 2005/05/13 Baada ya miaka 60 kupita, vita kuu ya pili ya dunia si kama tu haijasahaulika, bali pia imeongezewa maana mpya na wapenda amani. Lakini hadi leo, ufashisti bado upo, hasa nchini Italia ambako ndiyo chanzo chake...
|
Suala la nyuklia la Iran limefikia kwenye ukingo wa hatari 2005/05/13 Katibu wa Kamati ya Usalama ya Iran ambaye pia ni mjumbe wa kwanza wa mazungumzo Bw. Hassan Rowhan tarehe 12 kwenye kituo cha televisheni alisisitiza kuwa hivi karibuni Iran hakika itaanza tena shughuli za kusafisha uranium
|
Hali ya nyuklia ya pennisula ya Korea yawe ya utatanishi 2005/05/12 Korea ya Kaskazini hivi karibuni imemaliza kazi ya kuondoa fimbo 8000 zilizokwisha kutumika kuzalisha nishati ya nyuklia kutoka kwenye zana za nyuklia huko Ongbyon, na kusema kuwa itaendelea kuchukua hatua za lazima ili kupanua ghala la silaha za nyuklia kwa lengo la kujilinda kutokana na hali ya hivi sasa.
|
Kazi za kulazimishwa bado hazijakomeshwa duniani 2005/05/12 Shirika la Kazi la Kimataifa, ILO, tarehe 11 lilitoa ripoti ikisema kuwa hali mbaya ya kulazimishwa kufanya kazi inaendelea kuwepo duniani, kwa hiyo kukomesha kulazimisha kufanya kazi ni changamoto kubwa inayoikabili jumuyia ya kimataifa.
|
Mabishano yatokea tena ndani ya serikali ya Israel kuhusu "mpango wa upande mmoja" 2005/05/11 Hivi karibuni, waziri wa mambo ya nje wa Israel Bw. Shalom alisema kuwa kama Hamas itashinda katika uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria ya Palestina utakaofanyika mwezi Julai mwaka huu, Israel itafikiria upya utekelezaji wa mpango wa upande mmoja.
|
Hatua za Marekani na Umoja wa Ulaya zaenda kinyume na biashara huria 2005/05/10 Hivi karibuni umetokea mkwaruzano kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya kwa upande mmoja na China kwa upande mwingine kuhusu biashara ya nguo.
|
Kukumbuka historia, kutosahau mambo ya zamani, kuthamini amani na kupigania mustakbali mzuri 2005/05/09 Tarehe 8 rais Hu Jintao wa China alikutana na wajumbe na jamaa waliofiwa na askari wa Urusi walioshiriki katika vita dhidi ya wavamizi wa Japan nchini China na vita vya kulinda taifa la Urusi na alitoa hotuba katika ubalozi wa China nchini Russia.
|
Kukumbuka historia na kuanzisha mustakabali mzuri 2005/05/09 Historia ni kama kioo kwa hali halisi ya hivi sasa, na pia ni kitabu kizuri cha kiada. Bw. Hu Jintao alisema kuwa kukumbuka mafunzo ya historia na kuanzisha mustakabali mzuri ni chaguo sahihi la binadmau kwa historia.
|
Nchi mbalimbali za Ulaya zaadhimisha miaka 60 ya ushindi wa vita ya pili ya dunia 2005/05/09 Tarehe 8 mwezi Mei mwaka 1945, Wanazi wa Ujerumani walisalimu amri kwa majeshi ya muungano. Tukio hilo liliashiria kumalizika rasmi kwa vita vya pili vya dunia katika medani ya Ulaya. Siku hiyo baada ya miaka 60
|
Russia kuadhimisha kwa shangwe miaka 60 ya ushindi wa vita vya kulinda taifa 2005/05/06 Huu ni mwaka wa 60 tangu ushindi upatikane katika vita vya kupambana na ufashisti duniani, na tarehe 9 Mei itakuwa siku ya maadhimisho miaka 60 ya ushindi wa vita vya kulinda taifa la Russia. Russia itafanya sherehe kubwa tarehe 9 huko Moscow.
|
Mgogoro wa kisiasa wa Togo watazamiwa kutatuliwa 2005/05/05 Mgombea wa rais wa chama tawala cha "Shirikisho la umma la Togo" Bwana Faure ambaye ni mtoto wa rais wa zamani wa Togo Gnasisingbe Eyadema tarehe 4 huko Lome, mji mkuu wa Togo aliapishwa kuwa rais mpya wa Jamhuri ya Togo. Rais mpya Faure anatazamiwa kuweza kuunda serikali ya muungano na vyama vingine katika muda mfupi, na kushinda mgogoro wa kisiasa wa hivi sasa.
|
Serikali ya mpito ya Iraq yaapishwa 2005/05/04 Serikali ya mpito ya Iraq iliapishwa tarehe 3 huko Bagdad, hii imeonesha kuwa serikali ya kwanza ya Iraq iliyochaguliwa na raia imeanzishwa rasmi, na mchakato wa ukarabati wa kisiasa wa Iraq umepiga hatua kubwa.
|
Mkutano wa kuthibitisha "Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia" wafunguliwa 2005/05/03 Mkutano wa mwaka 2005 wa kuthibitisha "Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia" ulifunguliwa tarehe 2 huko New York katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
|