Lengo la ziara ya Condoleezza Rice barani Asia 2008/10/07 Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice alimaliza ziara yake nchini India na nchini Kazakhstan. Ingawa lengo lake muhimu la kusaini makubaliano ya ushirikiano wa nishati ya nyukilia kwa matumizi ya kiraia kati ya Marekani na India katika ziara yake ya India halikuweza kutimizwa, lakini alijitahidi kufanya vizuri kazi ya mshawishi kwa ajili ya makampuni ya tekenolojia ya nyukilia ya Marekani.
|
Mkutano wa Shirika la IAEA wafuatilia usalama wa nyuklia 2008/10/06 Mkutano wa 52 wa Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA ulifungwa tarehe 4 huko Vienna, Austria. Kwenye mkutano huo wa siku 6, masuala yaliyofuatiliwa zaidi ni jinsi ya kutumia nishati ya nyuklia kwa amani na namna ya kuhakikisha usalama wa nyuklia.
|
Kujiuzulu kwa Thabo Mbeki kumesababisha mtafaruku wa kisiasa nchini Afrika Kusini 2008/09/25 Tarehe 25 bunge la Afrika Kusini litafanya mkutano na kupitisha ombi la rais Thabo Mbeki kujiuzulu, na pia kupitisha maombi ya kujiuzulu kwa makamu wa rais Phumzile Mlambo-Ngcuka na mawaziri 11 pamoja na manaibu mawaziri wanne. Kujiuzulu kwa Thabo Mbeki na mawaziri walio karibu nusu kumesababisha mtafaruku wa kisiasa nchini Afrika Kusini, hata hivyo mwenyekiti wa chama tawala ANC Bw. Jacob Zuma alisema chama chake kimejiandaa kwa kazi zote baada ya rais Thabo Mbeki kuondoka madarakani na watu wa fani zote wasiwe na wasiwasi.
|
Dunia nzima yatakiwa kuchangia maendeleo ya Afrika 2008/09/23 Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya maendeleo ya Afrika ulifanyika tarehe 22 huko New York. Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 160, wakiwemo wakuu na viongozi wa serikali zaidi ya 40 walihudhuria mkutano huo. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Ban Ki-Moon, alitoa wito kwa nchi mbalimbali duniani, hususan nchi zilizoendelea zitekeleze ahadi ziliyoitoa ya kuongeza misaada kwa bara la Afrika na kuzisaidia nchi mbalimbali za Afrika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia.
|
Rais Thabo Mbeki ajiuzulu na siasa nchini Afrika Kusini kuingia katika awamu mpya 2008/09/22 Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini alitangaza kujiuzulu usiku wa tarehe 21 alipohutubia taifa kwa kupitia televisheni. Kwenye hotuba yake, alikanusha madai kwamba aliingilia kesi ya ufisadi dhidi ya mwenyekiti wa chama cha ANC Bw. Jacob Zuma, hata hivyo aliamua kujiuzulu kwa ajili ya kulinda mshikamano ndani ya chama cha ANC.
|
Ripoti ya Umoja wa Mataifa yatoa mwito wa kutimiza ahadi za kuhakikisha na kuboresha haki na maslahi ya wanawake 2008/09/19 Kabla ya kufanyika kwa mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia, Shirika la kusaidia maendeleo ya wanawake la Umoja wa Mataifa tarehe 18 lilitoa ripoti kuhusu maendeleo ya hali ya wanawake duniani wa mwaka 2008 hadi mwaka 2009, ripoti hiyo imezitaka nchi mbalimbali na mashirika mbalimbali ya Kimataifa yaanzishe taratibu za kubeba wajibu kwa nguvu zaidi, na kutimiza vizuri zaidi ahadi zao kuhusu kuhakikisha na kuboresha haki na maslahi ya wanawake
|
Baraza la Tokyo-Beijing lajenga daraja la uaminifu kati ya watu wa China na Japan 2008/09/18 Mkutano wa pili wa Baraza la Tokyo-Beijing ulifungwa tarehe 17 huko Tokyo, nchini Japan. Mkutano huo wa siku nne uliwashirikisha wajumbe 110 kutoka sekta mbalimbali za China na Japan, na masuala mengi zaidi yalijadiliwa.
|
Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Mataifa ataka umoja huo uwe umoja wenye udhati 2008/09/17 Mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 16 ulifunguliwa katika makao makuu ya umoja huo huko New York. Mwenyekiti mpya wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Miguel d'Escoto Brockman aliyekuwa waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Nicaragua kwenye ufunguzi wa mkutano huo alieleza matumaini yake kuwa baraza kuu la awamu hii la Umoja wa Mataifa litakuwa baraza lenye udhati na kufanya kazi kwa juhudi kwa ajili ya kutimiza amani na kutokomeza umaskini na njaa duniani.
|
Vyama mbalimbali vya Zimbabwe vyasaini makubaliano ya ugawaji wa madaraka 2008/09/16 Viongozi wa vyama mbalimbali vya Zimbabwe tarehe 15 huko Harare walisaini makubaliano ya ugawaji wa madaraka na kutangaza kuunda serikali ya maafikiano ya taifa. tukio hilo ni alama ya kuelekea kumalizika kwa mgogoro wa kisiasa uliosababishwa mwezi Machi na uchaguzi mkuu nchini humo, na Zimbabwe imeingia kwenye kipindi kipya cha utawala wa pamoja wa vyama viwili.
|
Kimbunga "Ike" chaleta hasara kubwa jimboni Texas, Marekani 2008/09/15 Katika mwisho wa juma lililopita, kimbunga"Ike" kilikumba sehemu ya pwani jimboni Texas, Marekani na kusababisha vifo vya watu 9 pamoja na hasara kubwa. Shughuli za uokoaji ambazo ni kubwa zaidi katika historia ya jimbo hilo zimeanza, na maofisa wa huko walikadiria kuwa, itachukua muda mrefu kabla ya maisha kurejea katika hali ya kawaida.
|
Makubaliano ya kugawa madaraka yamefikiwa kwenye mazungumzo kati ya vyama mbalimbali vya Zimbabwe 2008/09/12 Msuluhishi wa msukosuko wa kisiasa nchini Zimbabwe ambaye ni rais wa Afrika kusini Thabo Mbeki tarehe 11 huko Harare alisema, makubaliano ya kugawa madaraka yamefikiwa kwenye mazungumzo kati ya vyama mbalimbali vya Zimbabwe, makubaliano hayo yatasainiwa rasmi tarehe 15 huko Harare, ambapo serikali ya umoja wa kitaifa ya Zimbabwe pia itatangazwa kuanzishwa.
|
New York yawakumbuka watu waliokufa kwenye tukio la "Septemba 11" 2008/09/11 Kama ilivyokuwa miaka iliyopita, tarehe 11 Septemba serikali ya mji wa New York ilifanya maadhimisho ya miaka saba tangu tukio la "Septemba 11" litokee kuwakumbuka watu waliokufa katika tukio hilo. Usiku wa siku hiyo kwa saa za huko, kama kila mwaka ilivyofanywa, kurunzi mbili zitawaka na kutoa mwali mbili za mwangaza kwenye mahali kilipokuwa Kituo cha Biashara Duniani kwa kumithilisha majengo marefu mawili ya kituo hicho yaliyobomolewa katika tukio hilo ili watu wawakumbuke marehemu.
|
Hali ya mvutano wa kisiasa nchini Zimbabwe bado haijaondolewa 2008/09/10 Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya kusini tarehe 8 alikwenda tena Harare, mji mkuu wa Zimbabwe ili kufanya juhudi za mwisho kwa ajili ya kuondoa hali ya mvutano wa kisiasa kati ya vyama mbalimbali vya Zimbabwe. Lakini hadi kufikia usiku wa tarehe 9, mazungumzo kati ya pande mbalimbali bado hayajapata maendeleo, ambapo pande hizo hazijafikia makubaliano kuhusu kugawa madaraka.
|
Mkutano wa maji duniani wafanyika Vienna 2008/09/09 Mkutano wa maji duniani unafanyika huko Vienna toka tarehe 7 hadi tarehe 12, wajumbe 3,000 kutoka nyanja za sayansi na tenkolojian, siasa, viwanda, huduma za maji na shughuli za kushughulikia majitaka wanajadiliana uhifadhi wa mazingira ya asili, uchumi na afya.
|
Miradi ya nishati safi barani Afrika yatarajiwa kupata vitega uchumi vingi 2008/09/05 Mkutano wa kwanza wa Baraza la carbon dioxide la Afrika unatazamiwa kufungwa tarehe 5 huko Dakar, mji mkuu wa Senegal baada ya kufanyika kwa siku tatu. Mkutano huo unalenga kuhimiza nchi zilizoendelea kuwekeza kwenye miradi ya "Mfumo wa kujipatia maendeleo bila uchafuzi" barani Afrika, ili kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani
|
Georgia yavunja uhusiano wa kibalozi na Russia 2008/09/03 Wizara ya mambo ya nje ya Georgia tarehe 2 ilitoa taarifa kwa ubolozi wa Russia nchini humo na kutangaza rasmi kuvunja uhusiano wa kibalozi na Russia. Wizara hiyo siku hiyo pia ilitangaza rasmi kuwa, Georgia inajitoa kwenye makubaliano yaliyosainiwa kati ya nchi hiyo na Russia kuhusu utatuzi wa mgogoro wa Ossetia ya kusini.
|
Jeshi la Marekani laikabidhi Iraq mamlaka ya ulinzi wa mkoa wa Anbar 2008/09/02 Jeshi la Marekani nchini Iraq tarehe 1 Septemba asubuhi huko Ramadi, mji mkuu wa mkoa wa Anbar, lilifanya sherehe ya kuikabidhi rasmi serikali ya Iraq mamlaka ya ulinzi wa mkoa wa Anbar. Hadi sasa, Iraq imekabidhiwa mamlaka ya ulinzi wa mikoa 11 kati ya mikoa 18.
|
Mkutano wa Baraza la marais wa nchi wanachama wa Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai wafuatiliwa na watu 2008/08/29 Mkutano wa 8 wa Baraza la marais wa nchi wanachama wa Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai ulifanyika tarehe 28 huko Dushanbe, mji mkuu wa Tajikstan. Kwenye mkutano huo, marais wa nchi 6 wanachama walisaini Taarifa ya Dushanbe ya Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai na nyaraka nyingine, na mkutano huo pia ulitoa taarifa ya pamoja ya mkutano, masuala mbalimbali yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo yamefuatiliwa zaidi na watu.
|
Nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki na nchi marafiki zake zafanya majadiliano kuhusu kuimarisha ushirikiano 2008/08/29
Mkutano wa 40 wa mawaziri wa uchumi wa nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki na mikutano husika imefanyika mfululizo nchini Singapor. Mawaziri wa uchumi wa nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki wamejadili na mawaziri wa uchumi wa nchi zinazofanya mazungumzo na umoja huo, ili kuimarisha zaidi ushirikiano na kusukuma mbele maendeleo ya uchumi wa sehemu hiyo. 
|
Ubalozi wa China nchini Kenya wafanya sherehe kuwaaga wanafunzi wa Kenya watakaosoma nchini China 2008/08/27 Tarehe 26 ubalozi wa China nchini Kenya ulifanya sherehe ya kuwaaga wanafunzi 42 wa Kenya watakaosoma nchini China ambao wamepata udhamini wa masomo na serikali ya China.
|
Mkutano wa 15 wa harakati zisizofungamana na upande wowote wafikia maoni mengi ya pamoja 2008/08/01 Mkutano wa 15 wa mawaziri wa Harakati zisizofungamana na upande wowote ulifungwa tarehe 30 Julai huko Tehran. "Waraka wa mwisho" uliopitishwa kwenye mkutano huo umeona kuwa, mkutano huo unasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya kusini na kusini, kuzihimiza nchi zinazoendelea zifikie makubaliano kuhusu mambo ya kisiasa, na kusaidia kufanya ushirikiano kwa kujiendeleza na kustawisha tena Harakati zisizofungamana na upande wowote.
|
Je hali ya kupungua kwa bei ya mafuta ni ya muda? 2008/07/31 Baada ya bei ya mafuta kupanda na kufikia kiwango cha juu kabisa mwanzoni mwa mwezi Julai, bei hiyo ilianza kupungua kwa mfululizo. Tarehe 29 mwezi Julai bei ya mafuta ilikuwa dola za Marekani 122.19 kwa pipa ambayo ilishuka kwa 2.5% ikilinganishwa na siku ya biashara iliyotangulia, na bei hiyo ilikuwa ni chini kabisa tokea mwezi wa Mei na ilipungua kwa zaidi ya dola za Marekani 23 ikilinganishwa na bei ya mwanzoni mwa mwezi huo Julai.
|
Sababu mbalimbali zachangia janga la kibinadamu katika pembe ya Afrika 2008/07/30 Takwimu mpya zilizotolewa na Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, hivi sasa upungufu mkubwa wa chakula unawatishia watu wapatao milioni 15 wanaoishi nchini Somalia, Ethiopia, Djibouti na kaskazini mwa Kenya, sehemu inayojulikana kama pembe ya Afrika. Msemaji wa shirika hilo Bw. Peter Smerdon ametoa onyo kuwa, janga la kibinadamu linaweza kuikumba sehemu hiyo kama hatua za kutoa msaada hazitachukuliwa haraka.
|
Jumuiya ya kimataifa yapokea kwa pamoja michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008/07/28 kadiri inavyokaribia ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Beijing, shughuli nyingi zenye kauli-mbiu ya michezo ya Olimpiki zinafanyika katika sehemu mbalimbali za dunia, watu wanatumia nafasi hiyo kuonesha matarajio na kuitakia kila la heri michezo ya Olimpiki ya Beijing.
|
Baraza la sehemu ya Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini Mashariki lasisitiza kuimarisha ushirikiano 2008/07/25
Mkutano wa 15 wa baraza la sehemu ya Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini Mashariki tarehe 24 ulitoa "Taarifa ya Mwenyekiti" huko Singapore ikisisitiza kuimarisha mazungumzo na ushirikiano, kulinda amani na usalama wa sehemu hiyo. 
|
Mazungumzo kuhusu suala la nyuklia yafanyika Singapore 2008/07/24 Mazungumzo yasiyo rasmi ya mawaziri wa mambo ya nje wa pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea yalifanyika tarehe 23 huko Singapore. Waziri wa mambo ya nje wa nchi mwenyekiti wa mazungumzo ya pande 6 Bw. Yang Jiechi aliendesha mkutano, waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Bw. Pak Ui Chun, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice, waziri wa mambo ya nje wa Japan Bw. Komura Masahiko, waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergey Lavrov na waziri wa mambo ya nje na biashara wa Korea ya Kusini Bw. Liu Ming-hwan walishiriki kwenye mazungumzo hayo
|
Serikali ya Singh yapata kura ya uungaji mkono 2008/07/23 Mkutano maalumu wa baraza la chini la bunge la India ulimalizika mjini New Delhi saa mbili usiku ya tarehe 22. mkutano huo ulifanya upigaji kura za uaminifu kuhusu serikali ya chama cha UPA inayoongozwa na waziri mkuu Manmohan Singh wa chama cha Congress, serikali hiyo itaendelea na utawala wake kwa kura 275 za ndiyo, na kura 256 za hapana
|
Mazungumzo ya Doha yakabiliwa na changamoto pamoja na fursa 2008/07/22 Mawaziri kutoka nchi kubwa 35 wanachama wa Shirika la Biashara la Kimataifa (WTO) tarehe 21 Julai huko Geneva kwenye makao makuu ya shirika hilo walianza kufanya mkutano wa wiki moja, na kujaribu kufanya mazungumzo ya Doha yaliyoendelea kwa miaka saba yamalizike kwa mafanikio. Sasa mazungumzo ya doha yako mbele ya kivuko kingine muhimu.
|
Bw. Obama afanya ziara nchini Afghanistan na kutangaza sera zake kuhusu nchi hiyo 2008/07/21 Mgombea wa urais wa Marekani kutoka chama cha Demokrasia Bw. Barack Obama tarehe 20 alifanya mazungumzo na rais Hamid Karzai wa Afghanistan huko Kabul, mji mkuu wa nchi hiyo, viongozi hao walijadiliana kuhusu hali ya nchini humo na ya kanda hiyo, na masuala mengi kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi na biashara ya dawa za kulevya, ukarabati wa Afghanistan na ushirikiano wa usalama na wa kiuchumi kati ya Marekabni na Afghanistan.
|
Marekani yalegeza msimamo wake kuhusu suala la nyuklia la Iran 2008/07/18 Tarehe 16 serikali ya Marekani ilitangaza kuwa naibu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Williams Burns anayeshughulikia mambo ya siasa atahudhuria mazungumzo ya mwanzo ya suala la nyuklia yatakayofanyika tarehe 19 huko Geneva kati ya mjumbe mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya kidiplomasia na usalama Bw. Solana na mwakilishi mkuu wa Iran kwenye mazungumzo ya suala la nyuklia Bw. Saeed Jalili. Hii inadhihirisha kwamba Marekani imelegeza msimamo wake katika suala la nyuklia la Iran.
|