Mohmoud Abbas afikia makubaliano na makundi mbalimbali ya Palestina kuhusu kulinda hali ya usimamishaji vita kati ya Palestina na Israel 2005/06/10 Mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mohamoud Abbas tarehe 9 alifanya mazungumzo na viongozi wa makundi mbalimbali yenye silaha ya Palestina katika sehemu ya Gaza
|
Waislamu wa madhehebu ya Sunni wa Iraq wataka kuongezewa idadi ya wajumbe kwenye kamati ya utungaji katiba 2005/06/09 Wajumbe 150 wa vyama vya madhehebu ya Sunni vya Iraq tarehe 8 huko Baghdad walifanya mkutano, wakitaka kuongezewa idadi ya wajumbe wa madhehebu ya Sunni kwenye kamati ya utungaji katiba ya nchi hiyo.
|
Kuna matumaini ya kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea 2005/06/09 Wawakilishi wa Korea ya kusini na Marekani hivi karibuni walifanya mawasiliano mara mbili kwa kupitia "njia ya New York". Ingawa pande hizo mbili bado hazikupata maendeleo makubwa katika kufikia maoni ya pamoja kuhusu kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea
|
Usimamishaji wa vita kati ya Palestina na Israel vyakabiliwa na changamoto 2005/06/08 Watu wenye silaha wa Palestina tarehe 7 walipiga mizinga dhidi ya makazi ya wayahudi kwenye ukanda wa Gaza, mfanyakazi wa China na mwingine wa Palestina waliuawa kutokana na mashambulizi hayo, na wengine 6 wa Palestina walijeruhiwa. Siku hiyo, watu wenye silaha wa Palestina walipambana vikali na jeshi la Israel, na wapalestina wawili waliuawa katika mapambano hayo. Matukio hayo yaliyofanyika mfululizo yanafanya usimamishaji vita kati ya Palestina na Isarel ukabiliwe na matatizo.
|
Mahakama maalum ya Iraq itamhukumu Saddam ndani ya miezi miwili ijayo 2005/06/07 Mahakama maalum ya Iraq inayoshughulikia hukumu ya rais wa zamani wa Iraq Saddam tarehe 6 ilitangaza kuwa, mahakama yake itamhukumu Saddam ndani ya miezi miwili ijayo, na mashitaka kwake ni pamoja na kuwaua wakurd, kutoa hukumu za vifo kwa wakuu wa dini, kuwaua raia kwa kutumia silaha za kemikali, na kuivamia Kuwait.
|
Ni vigumu kwa Tony Blair kupata uungaji wa Marekani kuhusu masuala ya utoaji msaada kwa Afrika na kupunguza utoaji wa hewa ya carbon dioxide 2005/06/06 Kutokana na mpango uliowekwa, waziri mkuu wa Uingereza Bw. Tony Blair angewasili leo huko Washington kuwa na mazungumzo na rais Bush wa Marekani, ili kutafuta uungaji mkono wa Marekani kuhusu mpango wake wa kusaidia Afrika na kupunguza utoaji wa hewa ya carbon dioxide.
|
Kwa nini Abbas ametangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa tume ya utungaji sheria ya Palestina 2005/06/06 Mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas tarehe 4 alisaini amri ya kutangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa tume ya utungaji sheria ya Palestina uliopangwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu.
|
Mkutano wa wakuu wa COMESA wataka kuimarisha umoja wa kanda hiyo 2005/06/03 Mkutano wa 10 wa wakuu wa COMESA ulifunguliwa jana huko Kigali, mji mkuu wa Rwanda. Wakuu waliohudhuria mkutano huo kwa kauli moja walizitaka nchi mbalimbali za COMESA ziharakishe mchakato wa umoja wa kanda hiyo, ili kupambana na changamoto zilizosababishwa na utandawazi
|
Umoja wa Ulaya wachukua hatua ya dharura kukabiliana na tatizo la kutopitsha mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya 2005/06/03 Chansela wa Ujerumani Bw. Gerhard Schroeder tarehe 2 mwezi Juni alikwenda Luxembourg ambayo ni nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya kujadiliana na waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Jean-Claude Junchker, pia ameamua kufanya mkutano na Rais Jacques Chirac wa Ufaransa huko Berlin.
|
Hali ya wasiwasi kati ya Palestina na Israel yapungua 2005/06/03 Kutokana na makubaliano ya viongozi wa Palestina na Israel kwenye mkutano uliofanyika mwezi Februari mwaka huu mjini Sharm el-Sheikh, Misri, tarehe pili Juni wafungwa 398 wa Palestina waliachiwa huru.
|
Shughuli za kuadhimisha siku ya mazingira duniani zafanyika mjini San Francisco 2005/06/02 Mameya wa miji zaidi ya 60 duniani wanakusanyika mjini San Francisco, Marekani kuanzia tarehe mosi mwezi Juni kushiriki shughuli za kuadhimisha siku ya mazingira duniani zinazofanywa na Umoja wa Mataifa. Katika shughuli za siku tano, mameya hao watabadilishana maoni kwa undani kuhusu suala la maendeleo ya miji na hifadhi ya mazingira na kusaini azimio la miji ya kijani linalohusiana na hifadhi ya mazingira.
|
Mlipuko watokea katika msikiti nchini Afghanistan na kusababisha vifo na majeruhi ya watu makumi kadhaa 2005/06/02 Tarehe 1 mwezi Juni, mlipuko ulitokea kwenye msikiti mmoja ulioko huko Kandahar, mji wa kusini wa Afghanistan, na kusababisha vifo vya watu 19 na watu wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa. Mlipuko huo ni shambulizi kikatili kabisa la kimabavu lililotokea nchini humo katika mwaka huu, na tukio hilo limewafanya watu waingiliwe na wasiwasi tena kuhusu hali ya usalama nchini humo.
|
Haifai kutumia vigezo viwili katika biashara ya kimataifa. 2005/06/02 Kuanzia mwezi Aprili mwaka huu, Marekani na Umoja wa Ulaya zilitangaza kufanya uchunguzi wa "dhamana maalum" na hatua maalum za vizuizi kwa bidhaa za nguo za China zinazouzwa katika nchi za nje kutokana na kifungu cha 242 cha ripoti ya kikundi cha kazi cha China kujiunga na WTO
|
Mkuu mpya wa benki ya dunia asema lengo la benki hiyo la hivi sasa ni kusaidia Afrika 2005/06/02 Mkuu mpya wa benki ya dunia anayeshika madaraka kuanzia tarehe mosi Juni Bw. Paul Wolfowitz alisema kuwa, lengo la benki hiyo ni kulisaidia bara la Afrika kuwa "bara lenye matumaini".
|
Bado kuna njia ndefu hadi kufikia lengo la kutokomeza uvutaji wa tumbaku duniani 2005/06/01 Hivi sasa duniani kuna wavutaji wa tumbaku bilioni 1.3, wakati idadi ya wavutaji tumbaku imechukua 20% kati ya jumla ya idadi ya watoto wenye umri wa miaka ya kutoka 13 hadi 15, na kila mwaka kuna idadi ya watu milioni 5 wanaofariki dunia kutokana na maradhi yanayohusika na uvutaji wa tumbaku.
|
Watoto wa Afrika wanatamani familia 2005/06/01 Watoto duniani wanapozama katika furaha ya sikukuu yao duniani, mtoto wa kike Sushan mwenye umri wa miaka minane, kama kawaida yake anakaa kando ya dampo akinyoosha mikono midogo akiomba msaada.
|
Athari zinazoletwa na kura ya turufu ya Ufaransa kuhusu "mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya" 2005/05/31 Kabla ya upigaji kura za maoni ya raia nchini Ufaransa, viongozi wa Umoja wa Ulaya na Ufaransa walitoa wito wa kutaka watu wa Ufaransa wapige kura ya ndiyo kuunga mkono "mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya",
|
Wafanyakazi wa afya na udhibiti wa uvutaji wa sigara 2005/05/30 Tarehe 31 mwezi Mei mwaka huu ni siku ya 18 ya kupiga marufuku ya uvutaji sigara. Kaulimbiu ya siku hiyo ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara mwaka huu ni wafanyakazi wa afya na udhibiti wa uvutaji sigara.
|
Ziara ya Mahmood Abbas nchini Marekani ina mafanikio gani? 2005/05/27 Tarehe 26, mwenyekiti wa mamlaka ya Palestina Bw. Mahmood Abbas alikutana na rais George Bush wa Marekani na kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Marekani.
|
Umoja wa Afrika waomba misaada ya fedha na vitu kwa ajili ya utekelezaji wa kusimamisha vita huko Darfur 2005/05/27 Mkutano wa siku moja wa Umoja wa Afrika ulifanyika huko Addis Ababa tarehe 26. Huu ni mkutano wa kutafuta misaada ya fedha na vitu kwa ajili ya vikosi vya Umoja huo kusimamia utekelezaji wa mkataba wa kusimamisha vita katika sehemu ya Darfur.
|
Kwa nini Marekani haipingi tena mazungumzo kuhusu Iran kushiriki kwenye Shirika la Biashara Duniani. 2005/05/27 Kutokana na Marekani kutopinga tena kuanzisha mazungumo kuhusu Iran kushiriki kwenye Shirika la Biashara Duniani, baraza la shirika hilo tarehe 26 lilikubali kuanzisha mchakato wa Iran kushiriki kwenye shirika hilo.
|
Mkutano wa 58 wa afya duniani wafungwa 2005/05/26 Mkutano wa 58 wa afya duniani uliofanyika kwa siku 10 ulifungwa tarehe 25 huko Geneva baada ya kupitisha nyaraka mbili kuhusu "Azimio la kinga na tiba ya saratani" na "Mikakati ya dunia nzima ya kutoa chanjo".
|
Jeshi la Marekani laendelea kuyasaka makundi yanayoipinga Marekani kaskazini magharibi mwa Iraq 2005/05/26 Jeshi la Marekani lililoko nchini Iraq tarehe 25 liliendelea kuyasaka makundi yanayoipinga Marekani mjini Haditha, magharibi mwa Iraq.
|
Maonesho ya kimataifa-Maonesho ya mavumbuzi ya kisasa 2005/05/26 Tokea mwaka 1851 maonesho ya kwanza ya kimataifa yafanyike mjini London hadi mwaka 2005 maonesho ya kimataifa ya Aichi yanayofanyika nchini Japan, miaka 154 imepita.
|
Kwa nini mazungumzo kuhusu suala la nyuklia la Iran bado hayajavunjika? 2005/05/26 Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bw. Michel Barnier, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Bw. Joschka Fischer na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw. Jack Straw tarehe 25 walifanya mazungumzo na mwakilishi mkuu wa mazungumzo wa Iran kuhusu suala la nyuklia la nchi hiyo Bw. Hassan Rohani kwa muda wa saa 3 huko Geneva, na kuamua kuwa mazungumzo kuhusu suala hilo yataendelea.
|
Mazungumzo ni njia bora ya utatuzi wa mgogoro wa biashara 2005/05/25 Kwa ujumla, kutokea kwa baadhi ya matatizo katika ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya china na Ulaya ni hali ya kawaida. Pande zote husika zingefahamu na kufanya uchambuzi kuhusu chanzo chake na kutafuta njia nzuri ya utatuzi.
|
Upigaji kura kuhusu mswada wa marekebisho wa katiba ya taifa ya Misri hautakuwa na wasiwasi 2005/05/25 Rais Hosni Mubarak wa Misri tarehe 24 alitoa hotuba mjini Cairo, akiwataka raia wajitokeze kushiriki kwenye upigaji kura kuhusu mswada wa marekebisho ya katiba utakaofanyika tarehe 25.
|
Makadirio kuhusu mazungumzo ya mwisho ya suala la nyuklia la Iran 2005/05/25 Tarehe 25 Irani itafanya mazungumzo na nchi tatu za Umoja wa Ulaya kwa mara ya mwisho kuhusu suala la nyuklia la Iran mjini Geneva. Viongozi waandamizi wa pande mbili walifanya maadalizi tarehe 24 kwa ajili ya mazungumzo hayo.
|
Ziara moja yenye pilikapilika iliyofanikiwa vizuri 2005/05/25 Spika wa bunge la umma la China Bwana Wu Bangguo alifanya ziara rasmi ya siku 7 nchini Australia kuanzia tarehe 19 hadi 25 Mei. Katika ziara yake hiyo, spika Wu si kama tu alikutana na viongozi wa serikali ya Australia, kuhudhuria ufunguzi wa Baraza la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Australia, na kutangaza kuanzisha duru la kwanza la mazungumzo kati ya China na Australia kuhusu mkataba wa biashara huru.
|
Watu wa Iraq wapinga hatua za jeshi la Marekani nchini humo 2005/05/24 Kutokana na milipuko mfululizo inayotokea nchini Iraq, jeshi la Marekani nchini Iraq tarehe 23 lilitoa taarifa likisema kuwa, kuanzia tarehe 22, majeshi ya muungano ya Marekani na Iraq yameanza kusaka watu wenye silaha huko Baghdad. Katika kitendo hicho cha usakaji, watuhumiwa 285 wa makundi ya kijeshi walikamatwa. Msemaji wa jeshi la Marekani amesema kuwa, hiki ni kitendo kikubwa zaidi kinachoanzishwa kwa pamoja na jeshi la Marekani na jeshi la usalama la Iraq.
|