Milipuko mfululizo yatokea nchini Bangladesh 2005/08/18 Milipuko mfululizo ya mabomu zaidi ya 300 ya mabomu ilitokea ndani ya saa moja tarehe 17 huko Dacca na wilaya 58 katika wilaya zote 64 nchini Bangladesh, na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine zaidi ya 130 kujeruhiwa.
|
Mchakato wa kisiasa wa Iraq wazuiliwa na mashambulizi makali 2005/08/18 Mashambulizi makali yameongezeka hivi karibuni nchini Iraq. Tarehe 17, Matukio ya kuwashambulia raia yalitokea mjini Baghdad, Iraq.
|
Mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC wajadili mikakati ya maendeleo ya kikanda 2005/08/17 Mkutano wa mwaka wa wakuu wa Umoja wa maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC umefunguliwa tarehe 17 huko Gaborone, mji mkuu wa Botswana. Marais na wakuu wa serikali kutoka nchi wanachama wa SADC wamehudhuria mkutano huo wa siku mbili
|
Israel yaanza kuwaondoa kwa nguvu wayahudi wanaoishi kwenye sehemu ya Gaza 2005/08/17 Askari elfu kadhaa wa Israel walianza operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu Wayahudi kutoka katika sehemu ya Gaza kuanzia saa sita usiku wa manane tarehe 17
|
Uhusiano kati ya China na Kenya waendelea kwa utulivu 2005/08/16 Katika miaka ya hivi karibuni uhusiano kati ya China na Kenya unaendelea vizuri na kwa utulivu katika sekta mbalimbali, ambapo pande hizo mbili zimeimarisha siku hadi siku maingiliano na ushirikiano katika sekta za siasa , uchumi, utamaduni na elimu na utalii.
|
Siku ya kwanza kwa Israel kuondoka kutoka Gaza 2005/08/16 Tarehe 15 ilikuwa siku ya kwanza kwa Israel kutekeleza mpango wake wa kuondoka kutoka Gaza. Siku hiyo ingawa vitendo vyake vya kuondoka huko vilisusiwa na wakazi fulani, lakini jeshi la Israel lilisema kuwa, kwa ujumla mpango ulitekelezwa vizuri.
|
Israel na Palestina zafanya maandalizi ya mwisho kwa kuondoka Israel 2005/08/15 Israel imeanza kutekeleza mpango wa upande mmoja wa kuondoka kutoka sehemu ya Gaza na kando ya magharibi ya mto Jordan kuanzia tarehe 15 alfajiri.
|
Baraza la Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani laitaka Iran isimamishe shughuli za kusafisha Uranium 2005/08/12 Baada ya majadiliano, baraza la Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani tarehe 11 huko Vienna lilipitisha azimio likionesha ufuatiliaji mkubwa kwa Iran kuanzisha tena shughuli za kusafisha uranium, na kuitaka Iran isimamishe shughulizo zote, lakini azimio hilo halitaji kama shirika hilo litaliwasilisha suala hilo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
|
Mchakato wa amani wa Sudan wakabiliwa na changamoto na kuendelea kusonga mbele 2005/08/12 Kiongozi wa chama cha ukombozi wa umma cha Sudan Salva Kiir Mayardit tarehe 11 huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan aliapishwa kuwa makamu wa kwanza wa Sudan ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali ya kusini ya nchi hiyo badala ya John Garang aliyefariki dunia katika ajali ya ndege mwishoni mwa mwezi uliopita.
|
Suala la nyuklia la Iran laendelea kupamba moto 2005/08/11 Tarehe 10, chini ya usimamizi wa shirika la nishati ya atomiki la kimataifa, wataalamu wa Iran walifungua lakiri zote zilizobandikwa kwenye zana za nyuklia huko Isfahan, na kuanzisha tena shughuli za kusafisha uranium.
|
Utawala wa kijeshi wa Mauritania waanzisha serikali ya mpito 2005/08/11 "Kamati ya kijeshi ya demokrasia na haki" ya Mauritania iliyoshika hatamu za kiserikali tarehe 3 baada ya kufanya mapinduzi, tarehe 10 ilianzisha rasmi serikali ya mpito ya Mauritania ambayo waziri mkuu wake ni Sidy Mohamed Ould Boubacar.
|
Makundi mbalimbali ya Iraq yafanya mazungumzo ya "marathon" juu ya mswada wa katiba 2005/08/11 Kuanzia tarehe 7, viongozi wa madhehebu ya Shia na ya Suni pamoja na kundi la vyama vya wakurd waliendelea na mkutano kujadili suala la katiba ya kudumu ili kuondoa migongano na kujitahidi kupata maoni ya pamoja juu ya mswada wa katiba. Lakini baada ya majadiliano ya "kimarathon" ya siku kadhaa, makundi hayo bado hayajaweza kuondoa migongano husika.
|
Rais wa zamani wa Guinea Bissau Joao Bernardo Vieira athibitishwa kuwa rais mteule wa nchi hiyo 2005/08/11 Tume ya uchaguzi mkuu wa Guinea Bissau tarehe 10 ilitoa hadharani matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu, na kuthibitisha mgombea huru ambaye pia alikuwa rais wa nchi hiyo Bw. Joao Bernardo Vieira kuwa rais mteule.
|
Misimamo ya watu wa nchini Mauritania na nje ya nchi hiyo juu ya utawala wa kijeshi wabadilika kidogo 2005/08/10 Ujumbe wa ngazi wa mawaziri uliotumwa na Umoja wa Afrika tarehe 9 ulifika Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania kufanya mazungumzo na utawala wa kijeshi ulioshika hatamu za kiserikali baada ya uasi kuhusu kufufua utaratibu wa katiba wa Mauritania.
|
Mkutano wa kuamua mambo kuhusu suala la nyuklia la Iran 2005/08/10 Kutokana na ombi la Umoja wa Ulaya, baraza la shirika la nishati ya atomiki duniani liliitisha mkutano wa dharura tarehe 9 mjini Vienna, kujadili hasa suala la nyuklia la Iran.
|
Chombo cha "Discovery" cha Marekani charejea duniani salama 2005/08/10 Baadhi ya wataalamu wamelalamika kuwa vituo vya angani vya kimataifa vinahitaji vyombo vya aina hiyo, hususan katika muda wa kabla ya kutumika kwa vyombo vya aina mpya. Hivyo kurejea kwa usalama kwa "Discovery" huenda kutaanzisha kipindi kipya cha utafiti wa mambo ya anga ya juu.
|
Nchi za Afrika zapoteza watu wengi wenye ujuzi 2005/08/10 Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na shirika la uhamiaji duniani zinaonesha kuwa, kila mwaka watu zaidi ya elfu 20 wenye ujuzi wa nchi za Afrika wanaondoka makwao, na kwenda kutafuta kazi kwenye nchi zilizoendelea za Ulaya na Marekani.
|
Iran yashikilia kushughulikia uranium 2005/08/09 Iran tarehe 8 ilianzisha tena kazi za zana za uzalishaji wa uranium ya gesi, na ilichagua siku moja kabla ya kufanyika kwa mkutano wa dharura wa baraza la uratibu la shirika la atomiki duniani, jambo ambalo limefuatiliwa sana na vyombo vya habari vya nchi za magharibi.
|
Duru la 4 la mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea lapumzika kwa muda 2005/08/08 Duru la 4 la mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea tarehe 7 liliamua kupumzika kwa muda. Mazungumzo hayo yataingia katika kipindi chake cha pili katika wiki itakayoanzia tarehe 29 mwezi huu.
|
Duru la nne la mazungumzo ya pande 6 lapiga hatua 2005/08/08 Wachambuzi wanaona kuwa mazungumzo ya duru hilo yamethibitisha lengo la pamoja la kufanya peninsula ya Korea kuwa sehemu isiyo na silaha za nyuklia, kuimarisha maelewano na kupunguza tofauti ya maoni.
|
Suala la nyuklia la Iran laibuka tena 2005/08/08 Hivi karibuni, suala la nyuklia ya Iran limeibuka tena, ambapo Iran ilikataa mapendekezo yaliyotolewa na Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kutatua suala la nyuklia la Iran na kusisitiza kuanzisha upya shughuli za uranium.
|
Marekani na Uingereza zakabiliana na tishio la mashambulizi ya kigaidi ya Kundi la Al-Qaeda 2005/08/05 Katika video iliyooneshwa tarehe 4 na kituo cha televisheni cha Al-Jazeera, kiongozi wa pili wa kundi la Al-Qaeda Ayman al-Zawahri alitishia kuwa, kundi hilo litaanzisha mashambulizi mengi zaidi dhidi ya Marekani na Uingereza.
|
Mazungumzo kuhusu suala la nyukilia la penisula ya Korea yaingia wakati muhimu 2005/08/04 Habari zinasema kuwa endapo pande zote zitaweza kuafikiana kuhusu mswada wa waraka wa pamoja, basi waraka huo wa pamoja utaweza kutolewa kama taarifa ya pamoja. Hiyo itakuwa ni taarifa ya kwanza ya pamoja kutolewa tangu kuanzishwa kwa mazungumzo ya pande 6.
|
Uasi wa kijeshi watokea nchini Mauritania 2005/08/04 Tarehe 3 alfajiri kwa saa za huko, askari walioongozwa na kikosi cha ulinzi wa rais na idara ya usalama wa taifa wa Mauritania walifanya uasi wa kijeshi. Alasiri ya siku hiyo, askari hao walitangaza kuundwa kwa kamati ya kijeshi ya "Demokrasia na Haki" badala ya madaraka ya Rais Taya wa nchi hiyo.
|
Suala la nyuklia ya Iran lafuatiliwa tena 2005/08/03 Umoja wa Ulaya umejibu kwa hatua kali kitendo kilichofanywa na Iran tarehe mosi mwezi Agosti kuhusu kuanzisha upya kwa kazi za zana za kushughulikia mabadiliko ya uranium.
|
Mchakato wa amani ya Sudan wakabiliwa changamoto kutokana na kifo cha Bw John Garang 2005/08/02 Chama cha ukombozi cha Sudan kilitoa taarifa ikitaka watu wasisikilize uvumi na kuisaidia serikali kupita katika wakati mgumu kwa uvumilivu na kusema kuwa chama hicho kitaendelea kutekeleza mkataba wa amani uliofikiwa pamoja na serikali ya Sudan mwezi Januari mwaka huu.
|
Suala la nyuklia ya Iran lafuatiliwa tena 2005/08/01 Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Hamid-reza Asefi tarehe 31 mjini Teheran aliuhimiza Umoja wa Ulaya utoe mapendekezo ya kutatua suala la nyuklia ya Iran kabla ya tarehe mosi, ama sivyo, Iran itaanzisha tena shughuli za mabadiliko ya uranium katika kipindi cha maandalizi ya shughuli za uranium nzito.
|
Mazungumzo ya pande 6 yaendelea katika hali ya utulivu na yenye matumaini 2005/07/29 Duru la 4 la mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea yanayofanyika hapa Beijing tarehe 28 yaliingia katika siku yake ya 3, ambapo pande mbili za Korea ya kaskazini na Marekani zilifanya majadiliano, mazungumzo ya siku hiyo yaliendelea katika hali ya utulivu sana, wachambuzi wanaona kuwa hali hiyo ya utulivu inaonesha matumaini.
|
Marekani yataka kubwaga mzigo wa kulinda usalama wa Iraq 2005/07/28 Waziri wa ulinzi wa Marekani Bwana Donald Rumsfeld tarehe 27 aliizuru Iraq kwa ghafla, na kufanya mazungumzo na viongozi wa Iraq kuhusu Marekani kuikabidhi Iraq jukumu la kulinda usalama nchini humo na kuondoa jeshi lake kutoka Iraq.
|
Mkutano wa baraza kuu la WTO wafuatilia mazungumzo ya raundi ya Doha 2005/07/28 Baraza kuu la WTO tarehe 27 liliitisha mkutano tarehe 27 mjini Geneva. Mada kuu ya mkutano huo ni kujadili suala kuhusu mazungumzo ya raundi ya Doha na kujitahidi kuendeleza mazungumzo ya raundi ya Doha kabla ya likizo ya mwezi Agosti.
|