ECOWAS washindwa kwa muda katika kusuluhisha mgogoro wa kisiasa nchini Togo 2005/05/02 Ofisa wa Umoja wa ECOWAS tarehe 1 Mei alithibitisha kuwa, Shirikisho la vyama vya upinzani la Togo siku hiyo lilikataa pendekezo lililotolewa na ECOWAS kuhusu chama tawala na vyama vya upinzani kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
|
Kuzidisha ujirani mwema na ushirikiano na kuenzi Moyo wa Bandung 2005/04/29 Kuanzia tarehe 20 hadi 28 Aprili, Rais Hu Jintao wa China alifanya ziara nchini Brunei, Indonesia na Philippines, kuhudhuria mkutano wa wakuu wa Asia na Afrika wa mwaka 2005 na kushiriki shughuli za kuadhimisha miaka 50 ya mkutano wa Bandung.
|
Umoja wa Mataifa wafanya uchunguzi huru kuhusu kuuawa kwa Bw. Rafik Hariri 2005/04/29 Waziri wa mambo ya nje wa Lebanon Bw. Mahamoud Hamoud tarehe 28 alisema huko Beirut kuwa, Lebanon itashirikiana katika pande zote na kikundi cha utangulizi cha tume ya uchunguzi ya kimataifa kuhusu tukio la kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Bw. Rafik Hariri.
|
Orodha ya majina ya mawaziri wa baraza la serikali yapitishwa 2005/04/29 Majukumu muhimu ya Bw. Jafari na serikali mpya ni kutunga katiba rasmi ya nchi na kuufanyia upigaji kura katiba hiyo mpya. Kutokana na kuwa serikali mpya ya Iraq ni dhaifu tangu ilipoanzishwa, hivyo itakabiliwa na shida na changamoto nyingi.
|
Russia yaweka sura mpya ya kidiplomasia katika suala la Mashariki ya Kati 2005/04/28 arehe 27 rais Vladimir Putin wa Russia alimaliza ziara yake nchini Misri na kwenda Israel kuendelea na ziara yake katika Mashariki ya Kati. Alipokuwa nchini Misri alipendekeza kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa amani ya Mashariki ya Kati.
|
Uchaguzi wa katibu mkuu wa shirika la nishati ya atomiki la kimataifa waahirishwa tena 2005/04/28 Baraza la shirika la nishati ya atomiki la kimataifa tarehe 27 huko Geneva liliitikisha mkutano maalum kuhusu Bw. Mohamed Elbaradei kuendelea kuwa katibu mkuu wa shirika hilo, na kuamua kuahirisha tena uchaguzi wa katibu mkuu wa shirika hilo.
|
Ibrahim Al-Jafari awasilisha orodha ya majina ya baraza la mawaziri kwa tume ya urais ya Iraq 2005/04/27 Msemaji wa Bw. Ibrahim Al-Jafari aliyeteuliwa kuwa waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Iraq tarehe 26 alithibitisha kuwa, Bw Jafari ametoa orodha ya majina ya baraza la mawaziri na kumpa rais Jalal Talabani.
|
Mgogoro wa kisiasa wa Togo watazamiwa kuondolewa 2005/04/26 Tarehe 25, mgombea wa rais kutoka chama tawala cha Togo Bw. Faure Gnassingbe na kiongozi wa chama muhimu cha upinzani Bw. Gilchrist Olympio walikubali kwa kauli moja kuwa, endapo chama chochote kitashinda kwenye uchaguzi wa rais, Togo itaunda serikali ya umoja wa kitaifa itakayowakilisha maslahi ya wananchi wote.
|
Iraq yaahirisha tena kuunda serikali mpya 2005/04/26 Vyama vikubwa mbalimbali vya Iraq tarehe 25 bado havijaafikiana kuhusu ugawaji wa nyadhifa kwenye baraza la mawaziri, hivyo vimeahirisha tena kuunda serikali mpya iliyotazamiwa kuundwa siku hiyo.
|
Mkutano wa 11 wa Umoja wa Mataifa dhidi ya makosa ya jinai wafungwa 2005/04/26 Mkuktano wa 11 wa siku nane wa Umoja wa Mataifa dhidi ya makosa ya jinai ulifungwa tarehe 25 mjini Bangkok, Thailand. Mkutano huo ulipitisha Taarifa ya Bangkok
|
Ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya Asia na Afrika wafunguliwa 2005/04/25 Mkutano wa wakuu wa Asia na Afrika wa mwaka 2005 na shughuli za kuadhimisha miaka 50 tangu Mkutano wa Bandung ufanyike zimemalizika tarehe 24 nchini Indonesia.
|
Kukumbuka historia na kutupia macho siku za mbele 2005/04/25 Shughuli za kuadhimisha miaka 50 ya mkutano wa Bandung zilifanyika tarehe 24 huko Bandung, Indonesia. Rais Hu Jintao wa China na viongozi au wawakilishi wa nchi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa wakuu wa Asia na Afrika walishiriki kwenye shughuli zilizofanyika huko.
|
Upigaji kura katika uchaguzi wa uais wa Togo wamalizika 2005/04/25 Upigaji kura katika uchaguzi wa uais wa Togo ulimalizika tarehe 24, Aprili. Hivi sasa kazi ya kuhesabu kura inafanyika, na matokeo yanatazamiwa kujulikana ndani ya siku mbili zijazo.
|
Ushirikiano wa Afia na Afrika waingia zama mpya 2005/04/25 Mkutano wa Bandung wenye maana ya kihistoria umepita miaka 50, tarehe 24 viongozi wakuu wa nchi za Asia na Afrika walikutana mjini Djakarta kushiriki sherehe ya kuadhimisha miaka 50 ya mkutano huo baada ya mkutano wa viongozi hao kumalizika kwa mafanikio.
|
Rais wa Zambia akutana na ujumbe wa kutoa mkono wa pole wa serikali ya China 2005/04/25 Rais Levy Patrick Mwanawasa alikutana na ujumbe wa kutoa mkono wa pole wa serikali ya China unaoongozwa na Bw. Chen Jian ambaye ni msaidizi wa waziri wa biashara ya China na Bw. Wu Xiaohua ambaye ni naibu mkurugenzi wa tume ya usimamizi wa raslimali za taifa ya baraza la serikali la China tarehe 24 huko Ndola, mji mkuu wa mkoa wa Copperbelt, nchini Zambia.
|
Mkutano wa wakuu wa Asia na Afrika wa mwaka 2005 wafunguliwa, Rais wa China Hu Jintao atoa hotuba muhimu 2005/04/22 Mkutano wa wakuu wa Asia na Afrika wa mwaka 2005 umefunguliwa tarehe 22 huko Jakarta, mji mkuu wa Indonesia. Viongozi wa nchi au wawakilishi wa serikali wa nchi 88 za Asia na Afrika akiwemo rais Hu Jintao wa China pamoja na wachunguzi wa mabara mengine wamehudhuria mkutano huo.
|
Makadirio kwa mkutano wa viongozi wakuu wa nchi za Asia na Afrika 2005/04/21 Mkutano wa pili wa viongozi wakuu wa nchi za Asia na Afrika utafanyika tarehe 22 hadi 23 huko Djakarta, mji mkuu wa Indonesia. Rais Hu Jintao wa Chinapamoja na viongozi au wajumbe wa serikali za nchi 87 za Asia na Afrika watahudhuria mkutano huo.
|
Mwanadiplomasia mzoefu wa India azungumzia mkutano wa Bandung 2005/04/21 Mkutano wa pili wa Asia na Afrika utafunguliwa tarehe 22 mwezi Aprili, huko Jakarta, mji mkuu wa Indonesia. Huu ni mkutano mkubwa mwingine utakaoitishwa na nchi nyingi zinazoendelea barani Asia na Afrika baada ya mkutano wa kwanza wa Asia na Afrika yaani mkutano wa Bandung uliofanyika mwaka 1955.
|
Nchi za Afrika zawania maendeleo kwa ushirikiano 2005/04/19 Viongozi na wawakilishi kutoka nchi karibu 30 za Afrika wamekutana leo huko Sharm el-sheikh nchini Misri, kushiriki mkutano wa 13 wa kamati ya utendaji ya viongozi wa nchi kuhusu "ushirikiano mpya wa maendeleo ya uchumi barani Afrika NEPAD".
|
Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Pakistan azungumzia mkutano wa Bandung 2005/04/19 Tokea tarehe 18 hadi 24 Aprili, mwaka 1955 wajumbe wa nchi 29 za Asia na Afrika walifanya mkutano huko Bandung, Indonesia.
|
"Diplomasia ya mchezo wa kriketi" yasukuma mbele mchakato wa amani ya India na Pakistan 2005/04/18 Waziri mkuu wa India Bwana Manmohan Singh jana huko New Dheli alifanya mazungumzo na rais Pervez Musharaf wa Pakistan ambaye yuko nchini India kutazama mchezo wa kriketi na kufanya ziara isiyo rasmi.
|
Moyo wa mkutano wa Bandung wadumu milele 2005/04/18 Kuanzia tarehe 18 hadi tarehe 24 mwezi Aprili mwaka 1955, mkutano wa kwanza wa Asia na Afrika ulifanyika mjini Bandung, Indonesia, mkutano huo ulizishirikisha nchi na sehemu zipatazo 29.
|
Kwa nini matukio mengi ya milipuko kutokea tena nchini Iraq 2005/04/15 Tarehe 14 ilikuwa siku ya umwagaji damu nchini Iraq. Kwa mujibu wa matangazo ya kituo cha televisheni cha Al Jazeera, cha Qatar milipuko miwili ya mabomu yaliyowekwa katika magari ilitokea siku hiyo karibu na jengo la wizara ya mambo ya ndani mjini Baghdad
|
Mahmoud Abbas atoa amri ya kufanyika kwa mageuzi ya jeshi la usalama 2005/04/15 Mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Mahmoud Abbas tarehe 14 alitoa amri ya kufanyika kwa mageuzi ya jeshi la usalama ili kuimarisha uongozi. Hii ni hatua kubwa nyingine ya mageuzi ya usalama nchini Palestina.
|
Ujumbe wa Baraza la Usalama waitembelea Haiti 2005/04/14 Ujumbe unaoundwa na wanadiplomasia kutoka nchi 15 wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana ulifika huko Port-au-Prince, mji mkuu wa Haiti, na kuanza ziara ya siku tatu nchini humo. huo ni ujumbe wa kwanza kutumwa na Baraza la Usalama kwa nchi za Caribbean. Katika ziara hiyo, ujumbe huo utakutana na viongozi wa serikali ya muda ya Haiti na mkuu wa tume maalum ya Umoja wa Mataifa nchini humo, na kuwasiliana na vyama mbalimbali na wananchi wa nchi hiyo. Wachambuzi wanaona kuwa, ziara hiyo inabeba majukumu mengi.
|
Mkutano wa kimataifa wa kuichangia Sudan misaada yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 4.5 2005/04/14 Mkutano wa kimataifa wa kuipatia Sudan misaada ulifungwa tarehe 12 huko Oslo, mji mkuu wa Norway. Pande mbalimbali zilizohudhuria mkutano huo ziliahidi kuchangia dola za kimarekani bilioni 4.5 kwa ajili ya ukarabati na maendeleo ya Sudan baada ya vita kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2007.
|
Umoja wa Mataifa wapitisha mkataba wa kimataifa wa kuzuia vitendo vya ugaidi vya nyuklia 2005/04/14 Mkutano mkuu wa 59 wa Umoja wa Mataifa tarehe 13 ulipitisha Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Vitendo vya Ugaidi vya Nyuklia (International Convention for the Suppression of Acts of Nuclear Terrorism). Haya ni matokeo ya juhudi za miaka minane zilizofanywa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.
|
Ziara ya waziri mkuu wa China italeta athari kubwa nzuri katika kusukuma mbele urafiki na ushirikiano kati ya China na nchi za Asia ya kusini 2005/04/13 Waziri mkuu wa China Wen Jiabao alifanya ziara rasmi kutokana na mwaliko wa Pakistan, Bangladesh, Sri Lanka na India kuanzia tarehe 5 hadi 12 Aprili.
|
Umoja wa Mataifa wasisitiza kutunza dunia, maskani pekee ya binadamu 2005/04/12
Hivi karibuni Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika yake yametoa ripoti kadhaa mfululizo zikieleza tishio kubwa kwa mfumo wa ikolojia kutokana na shughuli za binadamu, zikitaka nchi zote ziamke na kuchukua hatua za kutunza dunia, maskani pekee ya binadamu.
|
Ofisa wa Ubalozi wa Pakistan atekwa nyara nchini Iraq 2005/04/12 Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan Bw. Jalail Abbas Jilani tarehe 11 alisema kuwa, hali ya hivi sasa inaonesha kuwa, madhumuni ya kundi la Iraq la kumteka nyara ofisa wa ubalozi wa Pakistan nchini Iraq ni kupata fedha. Mpaka sasa mateka huyo yuko salama, na serikali ya Pakistan inafanya juhudi zote kumwokoa mateka huyo.
|