Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Wachina waishio nchini Kenya washerehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China
  •  2007/02/19
    Tarehe 18 Februari ilikuwa Tarehe 1 Januari ya mwaka mpya wa jadi wa China kwa kalenda ya kilimo ya China, siku hiyo shamrashamra zilionekana kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa huko Nairobi Kenya
  • Mahmoud Abbas amteua rasmi Ismail Haniyeh kuunda serikali mpya
  •  2007/02/16
    Serikali ya kundi la Hamas iliyodumu kwa miezi 11, tarehe 15 ilitangaza kujiuzulu, kisha mwenyekiti wa mamlaka la utawala wa Palestina Bw. Abbas amemteua rasmi waziri mkuu wa muda Bw. Ismail Haniyeh aunde serikali mpya ya muungano. Hii inamaanisha kuwa Palestina imepiga hatua ya kuelekea kwenye maafikiano ya kitaifa na kujinasua kutoka kwenye vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa.
  • Hali ya Lebanon baada ya miaka miwili tokea waziri mkuu wa nchi hiyo wa zamani Rafiq Hariri auawe
  •  2007/02/15
    Tarehe 14 watu elfu kumi kadhaa walikusanyika kwenye sehemu ya katikati ya mji wa Beirut kukumbuka miaka miwili tokea waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Bw. Rafiq Hariri auawe.
  • Mashambulizi yatokea tena nchini Lebanon
  •  2007/02/14
    Milipuko miwili ya mabomu yaliyotegwa kwenye mabasi ilitokea karibu na mji wa Beirut nchini Lebanon, na kusababisha vifo vya watu watatu, na wengine 23 kujeruhiwa.
  • Hatua kubwa na imara imepigwa kwa mchakato wa kuifanya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na nyuklia
  •  2007/02/13
    Baada ya kufanya kwa makini majadiliano ya siku 6, mkutano wa kipindi cha tatu cha Duru la tano la mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea umefungwa tarehe 13.
  • Kuundwa kwa serikali mpya ya Palestina kutakumbwa na matatizo kadhaa
  •  2007/02/13
    Ofisa wa Palestina tarehe 12 alitangaza kuwa serikali ya sasa ya Palestina inayoongozwa na kundi la Hamas itavunjwa katika siku za karibuni na kuundwa kwa serikali mpya. Viongozi wa Hamas na Fatah watajadiliana kuhusu kuundwa kwa serikali mpya.
  • Je, amirijeshi mpya wa jeshi la Marekani anaweza kutuliza vurugu nchini Iraq?
  •  2007/02/12
    Hivi karibuni amirijeshi mpya wa jeshi la Marekani lililopo nchini Iraq Bw. David Petraeus alitumwa huko Iraq kuwa amirijeshi wa awamu ya tatu. Kwenye sherehe ya kushika madaraka iliyofanyika kwenye kituo cha jeshi la Marekani mjini Baghdad alisema, ataongoza jeshi lake kwa mkakati mpya, mbinu mpya za kivita na fikra mpya, na kujitahidi kutumia "fursa" ili kubadilisha hali ya kisiasa nchini Iraq. Lakini watu wana wasiwasi kama amirijeshi huyo ataweza kutimiza ahadi zake.
  • Rais Hu Jintao wa China amaliza ziara ya urafiki na ushirikiano barani Afrika
  •  2007/02/11
    Rais Hu Jintao wa China amemaliza ziara rasmi katika nchi 8 za Afrika, na kuondoka Shelisheli usiku wa tarehe 10 kurudi nyumbani China. Rais Hu Jintao ameeleza kufurahia mafanikio yaliyopatikana na ziara hiyo.
  • Ziara ya Rais Hu Jintao wa China barani Afrika yamepata mafanikio
  •  2007/02/11
    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Li Zhaoxing aliwaambia waandishi wa habari kuwa, ziara hiyo barani Afrika ni ziara ya urafiki na ushirikiano, ni tukio kubwa linalohusu uhusiano kati ya China na Afrika kufuatia kufanyika kwa mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika huko Beijing.
  • Ziara ya rais Hu Jintao wa China nchini Shelisheli
  •  2007/02/10
    Kutokana na mwaliko wa rais James Alex Michel wa Shelisheli, tarehe 9 rais Hu Jintao wa China alifika Victoria, mji mkuu wa Shelisheli na kuanza ziara rasmi nchini humo. Shelisheli ni nchi inayozungukwa na bahari ya Hindi inayoundwa na visiwa 115. Nchi hiyo ina eneo la ardhi la kilomita 455 za mraba na watu zaidi ya elfu 80.
  • Rais Hu Jintao wa China aanza ziara yake nchini Msumbiji
  •  2007/02/09
    Kutokana na mwaliko wa rais Armando Guebuza wa Msumbiji, rais Hu Jintao wa China tarehe 8 aliwasili Maputo, mji mkuu wa Msumbiji na kuanza ziara ya kiserikali nchini humo.
  • Utamaduni wa China na utamaduni wa Afrika wasonga mbele kwa pamoja
  •  2007/02/08
    Rais Hu Jintao wa China ambaye yuko ziarani barani Afrika tarehe 7 alitembelea mabaki ya ustaarabu wa Maropeng nchini Afrika Kusini ambayo ni urithi wa utamaduni duniani yaliyorodheshwa na UNESCO, na kutangaza kuwa China itasaidia mfuko wa hifadhi ya urithi wa utamaduni barani Afrika kwa kutoa dola za kimarekani milioni moja, ili kuonesha urafiki wa watu wa Afrika na kuunga mkono hifadhi ya urithi wa utamaduni wa Afrika.
  • Kuimarisha mshikamano na ushirikiano na kuhimiza ujenzi wa dunia yenye masikilizano
  •  2007/02/07
    Rais Hu Jintao wa China anayefanya ziara nchini Afrika ya kusini, tarehe 7 ametoa hotuba kwenye Chuo Kikuu cha Pretoria akifafanua mapendekezo ya China ya kuimarisha urafiki wa vizazi baada ya vizazi kati ya China na Afrika na kuhimiza ujenzi wa dunia yenye masikilizano
  • Rais Hu Jintao ahudhuria mazungumzo na wawakilishi wa kampuni za China zilizoko barani Afrika
  •  2007/02/07
    Kabla ya kuwasili nchini Afrika ya Kusini, rais Hu Jintao wa China tarehe 6 mwezi Februari huko Namibia alishiriki kwenye mazungumzo na wawakilishi wa kampuni zenye mitaji ya China zilizoko barani Afrika
  • Rais Hu Jintao wa China afanya ziara nchini Namibia
  •  2007/02/06
    Kutokana na mwaliko wa rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia, rais wa China Hu Jintao tarehe 5 alifika Windhoek, mji mkuu wa Namibia kuanza ziara yake ya kiserikali nchini humo.
  • China yaanzisha eneo la kwanza la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara barani Afrika
  •  2007/02/05
    Eneo la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara ambalo ni la kwanza kuanzishwa na China barani Afrika limezinduliwa tarehe 4, Januari huko Lusaka, mji mkuu wa Zambia. Rais Hu Jintao wa China ambaye yupo nchini Zambia kwa ziara na rais Levy Mwanawasa wa Zambia walihudhuria uzinduzi huo.
  • Hu Jintao atembelea Kampuni ya kusafisha mafuta ya Khartoum Sudan
  •  2007/02/03
    Alasiri ya Tarehe 2 Februari Rais Hu Jintao ambaye yuko Sudan kwa ziara akiambatana na rais Omar Al Bashir wa Sudan alitembelea Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Khartoum
  • Tukio la Uingereza kutupa takataka nchini China lafuatiliwa na kulaumiwa
  •  2007/01/31
    Hivi karibuni takataka nyingine zenye uzito wa tani laki mbili hivi zimesafirishwa na kufika nchini China kutoka Uingereza, takataka hizo zimesababisha uchafuzi kwa mazingira ya sehemu ya China. Vitendo vya Uingereza kutupa takataka zake mara kwa mara nchini China vimelaumiwa vikali na watu wa jamii ya China.
  • Pande husika zakaribisha mazungumzo ya pande sita yatakayorejeshwa
  •  2007/01/31
    Tarehe 30 msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Jiang Yu alitangaza kuwa baada ya kufanyika kwa majadiliano, mkutano wa kipindi cha tatu wa duru la tano la mazungumzo ya pande sita utaanza kufanyika tena tarehe 8 Februari mjini Beijing, pande husika zimeonesha msimamo wa kuukaribisha mkutano huo.
  • Ushirikiano kati ya China na Cameroon wazaa matunda tele
  •  2007/01/30
    Kutokana na mwaliko kutoka kwa na rais Paul Biya wa Cameroon, rais Hu Jintao wa China atafanya ziara rasmi nchini Cameroon mwishoni mwa mwezi huu. Hii ni fursa nyingine tena ya kusukuma mbele uhusiano kati ya pande mbili hizo.
  • Mkutano wa mwaka wa baraza la uchumi duniani wafungwa
  •  2007/01/29
    Mkutano wa mwaka wa 37 wa baraza la uchumi duniani ulifungwa tarehe 28 mjini Davos, Uswisi. Kwenye mkutano huo wa siku tano viongozi wa sekta za siasa, biashara, utamaduni na jamii duniani walijadili kwa kina masuala kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya uchumi duniani, mabadiliko ya hali ya hewa, hali ya Mashariki ya Kati, na mazungumzo ya raundi ya Doha.
  • Kuimarisha urafiki wa jadi, kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana na kutimiza maendeleo ya pamoja
  •  2007/01/29
    Kutokana na mwaliko wa marais wa nchi nane za Cameron, Liberia, Sudan, Zambia, Namibia, Afrika ya kusini, Msumbiji na visiwa vya Shelisheli, Rais Hu Jintao wa China anatazamiwa kufanya ziara ya kiserikali katika nchi hizo kuanzia tarehe 30 Januari hadi tarehe 10 Februari.
  • Vijana wanaojitolea wa China waenda kutoa huduma barani Afrika
  •  2007/01/25
    Tarehe 24 Januari huko Harare, mji mkuu wa Zimbabwe ilifanyika sherehe moja ya kuwalaki vijana wanaojitolea kutoka China, katika kipindi cha mwaka mmoja vijana hao watafanya shughuli zinazohusiana na mifugo, kilimo, elimu na matibabu nchini Zimbabwe.
  • Kwa nini Israel inataka kujiunga na NATO?
  •  2007/01/24
    Gazeti la Israel Jerusalem Post tarehe 23 lilichapisha makala ikisema, serikali ya Israel inatunga mpango wa kujiunga na Jumuiya ya NATO.
  • Mkutano wa mwaka wa Baraza la uchumi duniani kufanyika Uswisi
  •  2007/01/23
    Mkutano wa 37 wa mwaka wa Baraza la uchumi duniani unatazamiwa kufanyika tarehe 24 hadi 28 huko Davos, Uswisi. Kauli mbiu ya mkutano huo ni "Miundo ya nguvu katika mabadiliko"
  • Iran yakabiliwa na shinikizo kutokana na kufanya luteka
  •  2007/01/22
    Televisheni ya Iran tarehe 21 mwezi Januari ilitangaza kuwa, kuanzia siku hiyo jeshi la Iran litafanya luteka kwa siku 3. Hiyo ni luteka ya kwanza kuifanya na jeshi la Iran tangu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lipitishe azimio No. 1737 la kuiwekea vikwazo Iran, ambayo watu wanaichukulia kuwa ni jibu kali kuhusu azimio hilo.
  • Mazungumzo ya pande sita kuhusu suala la nyuklia ya peninsula ya Korea yatarajiwa kurudishwa
  •  2007/01/19
    Mkutano kati ya viongozi wa ujumbe wa Marekani na Korea ya Kaskazini ulioshiriki kwenye mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia ya peninsula ya Korea, ulimalizika tarehe 18 huko Berlin, nchini Ujerumani. Hapo baadaye kiongozi wa ujumbe wa Marekani ambaye pia ni msaidizi wa waziri wa mambo ya nje Bw. Christopher Hill alielekea ziarani nchini Korea ya Kusini, China na Japan kuziarifu nchi hizo tatu maendeleo ya mkutano huo na kusawazisha misimamo yao.
  • Waziri mkuu wa Israel akabiliwa na shinikizo kubwa la kisiasa
  •  2007/01/18
    Tarehe 12 Jumanne ilikuwa ni "siku ya mkosi" kwa waziri mkuu Ehud Olmert wa Israel, kwani siku hiyo jioni kamanda mkuu wa jeshi la Israel Bw. Dan Halutz alitangaza kujiuzulu, ambaye ni ofisa wa ngazi ya juu kabisa aliyejiuzulu kutokana na mgogoro uliotokea kati ya Israel na Lebanon katika majira ya joto mwaka jana, kisha watu wengi wa Israel walitaka Olmert na waziri wa ulinzi Amir Peretz pia wajiuzulu. Waziri huyo anakabiliwa shinikizo kubwa la kisiasa.
  • Condoleezza Rice amevuna nini katika ziara yake ya Mashariki ya Kati?
  •  2007/01/17
    Bi. Codoleezza Rice alianza ziara yake ya Mashariki ya Kati kuanzia tarehe 13. Inasemekana kwamba ziara yake ina nia mbili, moja ni kutaka kusukuma mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel, nyingine ni kuzishawishi nchi za Kiarabu ziunge mkono sera mpya za Marekani kuhusu Iraq. Lakini dalili zote zinaonesha kuwa Bi. Rice hajavuna chochote alichotaka katika ziara yake.
  • Condoleezza Rice amevuna nini katika ziara yake ya Mashariki ya Kati?
  •  2007/01/17
    Tarehe 16 waziri wa mambo ya nje wa Marekani Codoleezza Rice alifika Kuwait, kituo chake cha mwisho katika ziara yake ya Mashariki ya Kati, na alifanya mazungumzo na wajumbe wa nchi sita za Kamati ya Ushirikiano wa Nchi za Ghuba na mawaziri wa mambo ya nje wa Misri na Jordan, na kujadili masuala kuhusu hali mbaya ya usalama na namna ya kurudisha amani na utulivu nchini Iraq na kusukuma mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44