Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Israel ina kiwango gani cha udhati katika kurejesha mazungumzo ya amani
  •  2007/01/16
    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bibi Condoleezza Rice, ambaye hivi sasa anaitembelea sehemu ya mashariki ya kati, na waziri mkuu wa Israel Bw. Ehud Olmert wamekubali kuwa na mazungumzo tarehe 15 mwezi Januari pamoja na mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas.
  • Ziara ya mara ya kwanza ya Rais wa Iraq nchini Syria yafuatiliwa na watu
  •  2007/01/15
    Rais Jalal Talabani wa Iraq tarehe 14 Januari alifika Damascus kufanya ziara rasmi nchini Syria ambayo ni nchi jirani ya Iraq. Hii ni mara ya kwanza kwa rais Talabani kufanya ziara nchini humo tangu nchi hizo mbili zirudishe uhusiano wa kibalozi mwezi Novemba mwaka jana, pia ni ziara ya kwanza ya rais wa Iraq nchini Syria tangu miaka 27 iliyopita.
  • Kujitahidi kujenga ukoo mkbuwa kuwa nufaishana pamoja na matokeo ya ushirikiano
  •  2007/01/12
    Mkutano wa 12 wa wakuu wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki, Mkutano wa10 wa wakuu wa nchi 10 za Umoja wa Asia ya kusini na China, Japan na Korea ya kusini, Mkutano wa 10 wa wakuu wa nchi 10 za Umoja wa Asia ya kusini mashariki na China pamoja na Mkutano wa pili wa wakuu wa nchi 16 za Asia ya mashariki itafanyika huko Cebu, katikati ya Philippines kuanzia tarehe 13 hadi 15 mwezi huu.
  • Rais George Bush wa Marekani atangaza marekebisho ya sera za Marekani kuhusu Iraq
  •  2007/01/11
    Tarehe 10 Rais Bush wa Marekani alitangaza kwa njia ya televisheni sera mpya za Marekani kuhusu Iraq ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya askari na kusaidia ukarabati wa Iraq, akitumai kuwa sera hizo mpya zitatuliza vurugu zinazoongezeka nchini humo
  • Kwanini Marekani imepiga mabomu tena dhidi ya Somalia?
  •  2007/01/10
    Tarehe 8 helikopta za Marekani zilipiga mabomu dhidi ya watuhumiwa wa kundi la Al-Qaida walioko sehemu ya kusini ya Somalia zikasababisha watu kumi kadhaa kuuawa au kujeruhiwa, kati ya hao wengi ni askari wa vikosi vya makundi ya upinzani ya Somalia.
  • Kupandishwa ngazi kwa Idara kuu ya ulinzi ya Japan kutatingisha msingi wa amani na utulivu wa Japan baada ya vita vikuu vya dunia
  •  2007/01/09
    Kuanzia tarehe 9 Januari, 2007, Idara kuu ya ulinzi ya Japan itapandishwa ngazi na kuwa Wizara ya ulinzi, ambapo Wizara mpya ya ulinzi ya Japan itainuliwa hadhi yake ya kisheria, kuongezwa madaraka ya utoaji maamuzi na kuongezwa madaraka ya kifedha, na mabadiliko mbalimbali yatatokea mfululizo
  • Mwaka muhimu kwa waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe
  •  2007/01/05
    Januari mosi kwenye hotuba ya "mawazo yangu mwanzoni mwa mwaka mpya" waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe alisisitiza, "katiba imekuwa na miaka 60, sasa ni wakati wa kubadilisha katiba hiyo ili iende na wakati". Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 4 waziri mkuu huyo alisisitiza tena kuwa kurekebisha katiba ni lengo lake anapokuwa madarakani.
  • Margaret Chan ashika rasmi madaraka ya mkurugenzi mkuu wa Shirika la afya duniani
  •  2007/01/04
    Tarehe 4 Januari,2007 ni siku isiyo ya kawaida kwa Bibi Margaret Chan, kwani siku hiyo ameanza kazi ya Mkurugenzi mkuu mpya wa Shirika la afya duniani WHO. Akiwa mkurugenzi mkuu wa WHO, atafanyeje kazi yake na ataonesha umuhimu gani? 
  • Kwa nini Iran kuchukua msimamo mkali katika suala la nyuklia
  •  2007/01/03
    Rais Mahmud Ahmadinejad wa Iran tarehe 2 Januari alisema Iran itaendelea na mpango wake wa nyuklia, na azimio lililopitishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo Iran ni la haramu. Siku hiyo msemaji wa serikali ya Iran alisema kama nchi za magharibi zinashikilia kuishinikiza Iran katika suala la nyuklia, huenda Iran itajitoa kutoka kwenye mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia.
  • Wamarekani wamechoka na vita
  •  2007/01/02
    mwanzo mwa mwaka 2007 wizara ya ulinzi ya Marekani imethibitisha kuwa, idadi ya vifo vya askari wa Marekani nchini Iraq imefikia 3,000. Licha ya kusherehekea siku ya mwaka mpya, Wamarekani wanaonesha kuwa wamechoka na vita. Katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa 2007, mvua ilinyesha kwenye sehemu ya Washington.
  • Jeshi la serikali ya mpito ya Somalia laingia mjini Mogadishu
  •  2006/12/29
    Tarehe 28 hali ya vita nchini Somalia ilibadilika, kwamba jeshi la serikali ya mpito ya Somalia liliingia mjini Mogadishu bila upinzani na kutangaza kuwa serikali hiyo itahamia mjini humo kutoka Baidoa, mji uliopo kusini mwa nchi hiyo.
  • Iran yakataa katakata azimio la baraza la usalama
  •  2006/12/28
    Tarehe 27 bunge la Iran lilipitisha azimio la kuihimiza serikali ya Iran "itimize mapema mpango wa nyuklia na kurekebisha mara moja sera kuhusu ushirikiano wake na shirika la kimataifa la nishati ya atomiki".
  • Idadi ya askari wa Marekani waliouawa katika vita vya Iraq imezidi idadi ya watu waliokufa katika "tukio la Septemba 11"
  •  2006/12/27
    Jeshi la Marekani tarehe 26 lilitangaza kuwa askari wengine sita waliuawa nchini Iraq, na kuifanya idadi ya askari wa Marekani waliouawa katika vita vya Iraq vilivyoanzishwa mwaka 2003 ifikie 2,977, ambayo ni watu wane zaidi kuliko idadi ya watu waliokufa katika "tukio la Septemba 11".
  • Nchi za Asia zakumbuka miaka miwili tangu kutokea kwa tsunami kwenye bahari ya Hindi
  •  2006/12/26
    Tsunami kubwa iliyotokea tarehe 26 mwezi Desemba mwaka 2004 kwenye bahari ya Hindi karibu na Asia ya kusini mashariki na Asia ya kusini, ilisababisha vifo vya kiasi cha watu laki 2.2 wa nchi 11 za huko.
  • Mabishano kuhusu suala la nyuklia la Iran yaingia katika kipindi kipya
  •  2006/12/25
    Baada ya nchi sita za Russia, Marekani, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kufanya majadiliano kwa miezi miwili, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 23 Desemba lilipitisha kwa kauli moja azimio No. 1737 kuhusu suala la nyuklia la Iran.
  • Mapambano ya kisilaha yapamba moto nchini Somalia
  •  2006/12/22
    Mapambano katika siku zilizopita yalisababisha vifo na majeruhi ya watu wengi, miili mingi ilikuwa imesambaa kwenye barabara ya tarafa ya Idale. wakazi wa huko sasa wamekimbia makazi yao ili kujiepusha na vita.
  • China yaona kuwa mazungumzo ya pande 6 yamepata maendeleo fulani
  •  2006/12/21
    Kitu muhimu zaidi kwa hivi sasa ni kwa pande zote kutekeleza ahadi zilizotoa katika taarifa ya pamoja na kushikilia msimamo wa 'vitendo kwa vitendo'.
  • Serikali ya Bush yazingatia kuongeza askari nchini Iraq
  •  2006/12/21
    Rais George Bush wa Marekani tarehe 20 kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ikulu ya Marekani alisisitiza kuwa, Marekani inapaswa kuongeza nguvu ya jeshi linalofanya mapambano nchini Iraq, na kumwagiza waziri wa ulinzi wa Marekani Bwana Robert Gates atoe mapendekezo kuhusu jinsi ya kuongeza askari nchini Iraq
  • Mwaka mwingine tena wa wasiwasi ulioigubika Mashariki ya Kati
  •  2006/12/20
    Mwaka 2006 karibu unamalizika, mwaka huu hali ya eneo la mashariki ya kati lililokuwa na hali ya wasiwasi imezidi kuwa mbaya, mgogoro kati ya Lebanon na Israel ulitokea kabla ya mgogoro kati ya Palestina na Israel kutatuliwa, suala la nyuklia la Iran limekuwa donda ndugu, na mapambano kati ya makundi ya madhehebu ya kidini nchini Iraq yamekuwa makali siku hadi siku, migogoro hiyo imewatia watu wasiwasi kuhusu mustakabali wa sehemu hiyo.
  • Nchi za Ulaya na Marekani zarekebisha sera za uhamiaji
  •  2006/12/19
    Hivi sasa hapa duniani kuna wahamiaji kiasi cha milioni 200, na wahamiaji hao karibu wote wanaishi katika nchi zilizoendelea. Ghasia zilizotokea mwezi Oktoba mwaka jana huko Paris zilisababisha nchi za magharibi kutafakari suala la wahamiaji. Baada ya mwaka 2006 kuanza, nchi nyingi za Ulaya na Marekani zilianza kurekebisha sera zao kuhusu uhamiaji.
  • Utaratibu wa kimataifa wa kutosambazwa kwa silaha za nyuklia wakabiliwa na changamoto kubwa
  •  2006/12/18
    Mwaka wa 2006 unaokaribia kumalizika, ni mwaka ambao suala kuhusu silaha za nyuklia lilifuatiliwa mara kwa mara. Vitendo vya nchi kadhaa katika sekta ya nyuklia vilichochea utaratibu wa kimataifa wa kutosambazwa kwa silaha za nyuklia na kuwapa watu wasiwasi kuhusu mustakbali wa utaratibu huo.
  • Uchumi wa dunia unapiga hatua ukiwa na fursa na changamoto
  •  2006/12/15
    Ripoti Kuhusu Makadirio ya Uchumi Duniani kwa Mwaka 2007 iliyotangazwa na Benki ya Dunia tarehe 13 Desemba imesema, kwa ujumla hali ya uchumi duniani kwa mwaka 2006 ilikuwa nzuri, na kwa makadirio ongezeko la uchumi litafikia 5.1% ambalo ni kubwa kuliko ongezeko la 3.2% la mwaka 2005
  • Waziri mkuu wa Israel kudokeza kuhusu silaha za nyuklia nchini Israel kwasababisha mtafaruku
  •  2006/12/13
    Waziri mkuu wa Israel Bw. Ehud Olmert tarehe 11 alipozungumza na waandishi wa habari aliorodhesha Israel kwenye nchi zinazomiliki silaha za nyuklia. Hii ni mara ya kwanza kwa waziri mkuu wa Israel kuashiria hadharani kuwa Israel inamiliki silaha za nyuklia katika nusu karne iliyopita
  • Jumuyia ya kimataifa yasifu juhudi za China baada ya kujiunga na WTO
  •  2006/12/12
    Miaka mitano imepita tangu China ijiunge na WTO. Katika muda wa miaka mitano iliyopita, je China imekuwa ni nchi mwanachama anayewajibika kwa WTO? Na je jumuyia ya kimataifa inaionaje China baada ya kujiunga na WTO? Hivi karibuni waandishi wetu wa habari walizungumza na maofisa wa WTO na wasomi wa Umoja wa Ulaya na Marekani.
  • Kwa nini rais wa Iraq anaipinga sana taarifa iliyotolewa na "kikundi cha utafiti wa masuala ya Iraq" cha Marekani
  •  2006/12/11
    Rais Jalal Talabani wa Iraq kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika huko Baghdad tarehe 10 mwezi Desemba, alikosoa taarifa iliyotolewa na "kikundi cha utafiti wa masuala ya Iraq" cha bunge la Marekani akisema, taarifa hiyo si ya haki na usawa
  • Ripoti ya uchunguzi wa suala la Iraq ya Marekani yaibua maoni tofauti
  •  2006/12/08
    Baada ya kikundi cha uchunguzi wa suala la Iraq cha Marekani kukabidhi ripoti yake ya uchunguzi kwa rais George Bush tarehe 6 Desemba, nchi husika za Iraq, Iran, Syria na Israel zimetoa maoni tofauti kuhusu ripoti hiyo kutokana na maslahi yao mbalimbali.
  • Mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki wafanyika katika mji wa Khartoum
  •  2006/12/07
    Mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki unafunguliwa tarehe 7 mjini Khartoum, mji mkuu wa Sudan. Viongozi wakuu kutoka nchi 79 za Afrika, Caribbean na Pasifiki wakiwemo marais 16 watahudhuria mkutano huo, mada ya mkutano huo ni ushirikiano kwa ajili ya amani, umoja na maendeleo endelevu.
  • Je, Iran, Uturuki na Syria zinaweza kutatua suala la Iraq kwa ushirikiano?
  •  2006/12/05
    Mwenyekiti wa Kamati ya Maslahi ya Taifa ya Iran Bw. Rafsanjani tarehe 3 jioni alipokutana na waziri mkuu wa Uturuki Bw. Erdogan aliyekuwa ziarani nchini Iran alisema, ushirikiano wa nchi tatu za Iran, Uturuki na Syria utaisaidia Iraq kutimiza usalama na ukamilifu wa ardhi.
  • Jumuiya ya Afrika Mashariki yapiga hatua kubwa
  •  2006/12/04
    Kwenye mkutano wa 8 wa wakuu uliofanyika tarehe 30 Novemba huko Arusha, wakuu wa nchi tatu wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki Tanzania, Kenya na Uganda waliamua kuzipokea Burundi na Rwanda kuwa nchi wanachama wapya wa jumuiya hiyo
  • Mkutano wa kwanza wa wakuu wa nchi za Afrika na Amerika ya Kusini wamalizika
  •  2006/12/01
    Mkutano wa kwanza wa wakuu wa nchi za Afrika na Amerika ya Kusini ulimalizika tarehe 30 Novemba mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria. Wajumbe kutoka nchi 47 za Afrika na nchi 11 za Amerika ya Kusini wakiwemo marais wa nchi 23 walihudhuria mkutano huo.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44